Isaya 27

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli

1 Katika siku ile,

Bwanaataadhibu kwa upanga wake,

upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu,

# ataadhibu Lewiathaniyule nyoka apitaye mbio kwa mwendo laini,

Lewiathani yule nyoka mwenye kupindapinda;

atamwua joka huyo mkubwa sana wa baharini.

2 Katika siku ile:

“Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:

3 Mimi,Bwana, ninalitunza,

nitalinyweshea maji mfululizo.

Ninalichunga mchana na usiku ili mtu ye yote asije akalidhuru.

4 Mimi sijakasirika.

Hata kama pangekuwepo michongoma

na miiba inayonikabili!

Ningepambana dhidi yake katika vita,

ningeliichoma moto yote.

5 Au niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,

wao na wafanye amani nami,

naam, wafanye amani nami.”

6 Katika siku zijazo Yakobo atatia mizizi,

Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,

naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.

7 Je,Bwanaamempiga kama alivyowapiga wale waliompiga?

Je, yeye ameuawa

kama wale waliouawa

ambao walimwua yeye?

8 Kwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye,

kwa mshindo wake mkali anamfukuza,

kama siku uvumapo upepo wa mashariki.

9 Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho,

hili litakuwa ndiyo matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake:

Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu

kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande,

hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia

uvumba zitakazobaki zimesimama.

10 Mji ulio na boma umebaki ukiwa,

makao yaliyotelekezwa yameachwa kama jangwa,

huko ndama hulisha,

huko hujilaza,

wanakwanyua matawi yake.

11 Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa

nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.

Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,

kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,

Muumba wao hawaonyeshi fadhili.

12 Katika siku ileBwanaatapura kutoka matiririko ya mto wa Eufrati hadi Kijito cha Misri, nanyi, Ee Waisraeli mtakusanywa pamoja mmoja mmoja.

13 Katika siku ile tarumbeta kubwa italia. Wale waliokuwa wakiangamia katika nchi ya Ashuru, nao wale waliokuwa uhamishoni katika nchi ya Misri watakuja na kumwabuduBwanakatika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/27-11d9a8e1a22a0bf89939a171a02d608c.mp3?version_id=1627—

Isaya 28

Ole Wa Efraimu

1 Ole wa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,

kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,

kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!

2 Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.

Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,

kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,

atakiangusha chini kwa nguvu.

3 Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,

kitakanyagwa chini ya nyayo.

4 Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,

litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:

mara mtu aionapo, huichuma na kuila.

5 Katika siku ile,BwanaMwenye Nguvu Zote

atakuwa taji la utukufu,

taji zuri la maua

kwa mabaki ya watu wake.

6 Atakuwa roho ya haki

kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu,

chanzo cha nguvu

kwa wale wazuiao vita langoni.

7 Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo,

wanayumbayumba kwa sababu ya kileo:

Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo,

wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo;

wanapepesuka wanapoona maono,

wanajikwaa wanapotoa maamuzi.

8 Meza zote zimejawa na matapishi

wala hakuna sehemu hata ndogo

isiyokuwa na uchafu.

9 “Yeye anajaribu kumfundisha nani?

Yeye anamwelezea nani ujumbe wake?

Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya?

Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini?

10 Kwa maana ni:

Amri juu ya amri, amri juu ya amri,

kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;

hapa kidogo, kule kidogo.”

11 Basi, vyema kabisa, kwa midomo migeni

na kwa lugha ngeni,

Mungu atasema na watu hawa,

12 wale ambao aliwaambia,

“Hapa ni mahali pa kupumzika,

waliochoka na wapumzike,”

na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,”

lakini hawakutaka kusikiliza.

13 Hivyo basi, neno laBwanakwao litakuwa:

Amri juu ya amri, amri juu ya amri,

kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni,

hapa kidogo, kule kidogo:

ili waende na kuanguka chali,

wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa.

14 Kwa hiyo sikieni neno laBwana,

enyi watu wenye dharau

mnaotawala watu hawa wa Yerusalemu.

15 Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti,

tumefanya mapatano na kuzimu.

Wakati pigo lifurikalo litakapopita,

haliwezi kutugusa sisi,

kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu

na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.”

16 Kwa hiyo hivi ndivyoBwanaMwenyezi asemavyo:

“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni,

jiwe lililojaribiwa,

jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti,

yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.

17 Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia

na uadilifu kuwa timazi;

mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo,

nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha.

18 Agano lenu na kifo litabatilishwa,

patano lenu na kuzimu halitasimama.

Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba,

litawaangusha chini.

19 Kila mara lijapo litawachukua,

asubuhi baada ya asubuhi,

wakati wa mchana na wakati wa usiku,

litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.”

Kuuelewa ujumbe huu

utaleta hofu tupu.

20 Kitanda ni kifupi mno kujinyosha juu yake,

nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno

mtu asiweze kujifunikia.

21 Bwanaatainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu,

ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni:

ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu,

ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni.

22 Sasa acheni dharau zenu,

la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi,

Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote, ameniambia

habari za maangamizi yaliyoamuriwa dhidi ya nchi yote.

23 Sikilizeni na msikie sauti yangu,

tegeni masikio na msikie niyasemayo.

24 Wakati mkulima alimapo ili apande,

je, hulima siku zote?

Je, huendelea kubomoa ardhi

na kusawazisha udongo?

25 Akiisha kusawazisha shamba,

je, hasii mbegu za bizari na kutawanya jira?

Je, hapandi ngano katika sehemu yake,

shayiri katika eneo lake

na nafaka nyingine katika shamba lake?

26 Mungu wake humwelekeza

na kumfundisha njia iliyo sahihi.

27 Iliki haitwangwi kwa nyundo kubwa,

wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira;

iliki hutwangwa kwa mtwangio,

na jira kwa fimbo.

28 Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate,

kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima.

Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake,

farasi wake hawasagi.

29 Haya yote pia hutoka kwaBwanaMwenye Nguvu Zote,

mshauri wa ajabu na anayepita wote kwa hekima.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/28-5e666061cae65be3720839d2b88c5b6d.mp3?version_id=1627—

Isaya 29

Ole Wa Mji Wa Daudi

1 Ole wako, wewe Arieli, Arieli,

mji alimokaa Daudi!

Ongezeni mwaka kwa mwaka

na mzunguko wa sikukuu zenu uendelee.

2 Hata hivyo nitauzunguka Arieli kwa jeshi,

utalia na kuomboleza,

utakuwa kwangu kama mahali

pa kuwashia moto madhabahuni.

3 Nitapiga kambi pande zote dhidi yako,

nitakuzunguka kwa minara

na kupanga mazingiwa yangu dhidi yako.

4 Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini,

utamumunya maneno yako kutoka mavumbini.

Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu,

utanong’ona maneno yako toka mavumbini.

5 Lakini adui zako wengi watakuwa kama vumbi laini,

kundi la wakatili watakuwa

kama makapi yapeperushwayo.

Naam, ghafula kwa mara moja,

6 BwanaMwenye Nguvu Zote atakuja

na ngurumo, tetemeko la ardhi na kwa sauti kuu,

atakuja na dhoruba, tufani na miali ya moto iteketezayo.

7 Kisha makundi ya mataifa yote yale yapiganayo dhidi ya Arieli,

yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzunguka kwa jeshi,

watakuwa kama ilivyo ndoto,

kama maono wakati wa usiku:

8 kama vile wakati mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula,

lakini huamka, bado njaa yake ingalipo,

kama vile wakati mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji,

lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu.

Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa,

yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.

9 Duwaa na kushangaa,

jifanyeni vipofu wenyewe na msione,

leweni, lakini si kwa mvinyo,

pepesukeni lakini si kwa kileo.

10 Bwanaamewaleteeni juu yenu usingizi mzito:

Ameziba macho yenu (ninyi manabii);

amefunika vichwa vyenu (ninyi waonaji).

11 Kwa maana kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa lakiri katika kitabu. Kama mkimpa mtu ye yote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa lakiri.”

12 Au kama mkimpa mtu ye yote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”

13 Bwana anasema:

“Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao

na kuniheshimu kwa midomo yao,

lakini mioyo yao iko mbali nami.

Huniabudu bure,

mafundisho yao ni sheria tu

walizofundishwa na wanadamu.

14 Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa,

kwa ajabu juu ya ajabu,

hekima ya wenye hekima itapotea,

akili ya wenye akili itatoweka.”

15 Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu

kumfichaBwanamipango yao,

wafanyao kazi zao gizani na kufikiri kuwa,

“Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”

16 Mnapindua mambo juu chini,

kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi!

Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga,

“Wewe hukunifinyanga mimi?”

Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi,

“Wewe hujui cho chote?”

17 Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa

kuwa shamba lenye rutuba

na shamba lenye rutuba liwe kama msitu?

18 Katika siku ile viziwi watasikia maneno ya kitabu

na katika utusitusi na giza macho ya kipofu yataona.

19 Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katikaBwana,

wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

20 Wakatili watatoweka na wenye kudhihaki watatokomea,

nao wote wenye jicho la uovu watakatiliwa mbali,

21 wale ambao kwa neno humfanya mtu kuwa mwenye hatia,

wamtegeao mtego mtetezi katika mahakama

na kwa ushuhuda wa uongo humnyima haki

yeye asiye na hatia.

22 Kwa hiyo hili ndiloBwana, aliyemkomboa Abrahamu, analosema kwa nyumba ya Yakobo:

“Yakobo hataaibishwa tena,

wala nyuso zao hazitabadilika sura tena.

23 Wakati watakapoona watoto wao miongoni mwao,

kazi ya mikono yangu,

watalitakasa Jina langu takatifu;

wataukubali utakatifu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Yakobo,

nao watamcha Mungu wa Israeli.

24 Wale wanaopotoka rohoni watapata ufahamu,

wale wanaolalamika watayakubali mafundisho.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/29-25bc0f6f04f24099dd6bf61881500972.mp3?version_id=1627—

Isaya 30

Ole Wa Taifa Kaidi

1 Bwanaasema,

“Ole wa watoto wakaidi,

kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,

wakifanya umoja, lakini si kwa Roho wangu,

wakilundika dhambi juu ya dhambi,

2 wale washukao kwenda Misri

bila kutaka shauri langu,

wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,

watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.

3 Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,

kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.

4 Ingawa wana maafisa katika Soani

na wajumbe wamewasili katika Hanesi,

5 kila mmoja ataaibishwa

kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu,

ambalo haliwaletei msaada wala faida,

bali aibu tu na fedheha.”

6 Neno kuhusu wanyama wa Negebu:

Katika nchi ya taabu na shida,

ya simba waume na wake,

ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao,

wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda,

hazina zao juu ya nundu za ngamia,

kwa lile taifa lisilokuwa na faida,

7 kuvipeleka Misri,

ambaye msaada wake haufai kabisa.

Kwa hiyo nimemwita “Rahabu, yaani, yeye aketiye

kimya bila kufanya cho chote.”

8 Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao,

liandike kwenye kitabu,

ili kwa ajili ya siku zijazo

liweze kuwa shahidi milele.

9 Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,

watoto ambao hawataki

kusikiliza mafundisho yaBwana.

10 Wanawaambia waonaji,

“Msione maono tena!”

Nako kwa manabii wanasema,

“Msiendelee kutupatia maono

ambayo ni ya kweli!

Tuambieni mambo ya kupendeza,

tabirini mambo ya uongo.

11 Acheni njia hii,

ondokeni katika mapito haya,

nanyi acheni kutukabili pamoja

na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”

12 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,

mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu,

13 dhambi hii itakuwa kwenu

kama ukuta mrefu,

wenye ufa na wenye kubetuka,

ambao unaanguka ghafula,

kwa mara moja.

14 Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo

ukipasuka pasipo huruma

ambapo katika vipande vyake

hakuna kipande kitakachopatikana

kwa kuukulia makaa kutoka mekoni

au kuchotea maji kisimani.”

15 Hili ndiloBwanaMwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:

“Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,

katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,

lakini hamkutaka.

16 Mlisema, ‘Hapana, tutakimbia kwa farasi.’

Kwa hiyo mtakimbia!

Mlisema, ‘Tutakimbia kwa farasi waendao kasi.’

Kwa hiyo wanaowafukuza watakwenda kasi!

17 Watu 1,000 watakimbia

kwa ajili ya kitisho cha mtu mmoja,

kwa vitishio vya watu watano

wote mtakimbia,

hadi mtakapoachwa

kama mlingoti wa bendera

juu ya kilele cha mlima,

kama bendera juu ya kilima.”

18 Hata hivyoBwanaanatamani kutupatia neema,

anainuka ili kuwaonyesha huruma.

Kwa kuwaBwanani Mungu wa haki.

Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

19 Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazama jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu.

20 Ingawa Bwana huwapa chakula cha shida na maji ya taabu, walimu wenu hawatafichwa tena, kwa macho yenu wenyewe mtawaona.

21 Kwamba mtageuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu, ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.”

22 Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu, mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!”

23 Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana tena kwa wingi. Katika siku ile ng’ombe wenu watalisha katika shamba pana la majani.

24 Maksai na punda walimao watakula majani makavu na vyakula vilivyotengenezwa, vinavyotandazwa kwa uma na sepeto.

25 Katika siku ile ya mauaji makuu, wakati minara itakapoanguka, vijito vya maji vitatiririka juu ya kila milima mirefu na kila kilima kilichoinuka sana.

26 Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utang’aa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakatiBwanaatakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.

27 Tazama, hilo Jina laBwanalinakuja kutoka mbali,

likiwa na hasira kali inayowaka

pamoja na wingu zito la moshi,

midomo yake imejaa ghadhabu

na ulimi wake ni moto ulao.

28 Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi,

yakipanda hadi shingoni.

Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu,

huweka lijamu katika mataya ya mataifa

ambayo huwaongoza upotevuni.

29 Nanyi mtaimba kama usiku mnaoadhimisha

sikukuu takatifu,

mioyo yenu itashangilia

kama vile watu wanapokwea na filimbi

kwenye mlima waBwana,

kwa Mwamba wa Israeli.

30 Bwanaatawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,

naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka

pamoja na hasira yake kali na moto ulao,

kukiwa na tufani ya mvua,

ngurumo za radi na mvua ya mawe.

31 Sauti yaBwanaitaivunjavunja Ashuru,

kwa fimbo yake ya utawala atawapiga.

32 Kila pigoBwanaatakaloliweka juu yao

kwa fimbo yake ya kuadhibu,

litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi,

anapopigana nao katika vita

kwa mapigo ya mkono wake.

33 Tofethi imeandaliwa toka zamani,

imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme.

Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu

na kwa upana mkubwa,

likiwa na moto na kuni tele;

pumzi yaBwana,

kama kijito cha kiberiti,

huuwasha moto.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/30-0fdc42da734d063b43738287f9512bc2.mp3?version_id=1627—

Isaya 31

Ole Wa Wale Wanaotegemea Misri

1 Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada,

wale wategemeao farasi,

wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita

na katika nguvu nyingi za wapanda farasi,

lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

wala hawatafuti msaada kwaBwana.

2 Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa,

wala hayatangui maneno yake.

Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu,

dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya.

3 Lakini Wamisri ni wanadamu wala si Mungu,

farasi wao ni nyama wala si roho.

WakatiBwanaatakaponyosha Mkono wake,

yeye anayesaidia atajikwaa,

yeye anayesaidiwa ataanguka,

wote wawili wataangamia pamoja.

4 Hili ndiloBwanaanaloniambia:

“Kama vile simba angurumavyo,

simba mkubwa juu ya mawindo yake:

hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo

huitwa pamoja dhidi yake,

hatiwi hofu na kelele zao

wala kusumbuliwa na ghasia zao;

ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote atakavyoshuka

kufanya vita juu ya Mlima Sayuni

na juu ya vilele vyake.

5 Kama ndege warukao,

BwanaMwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu;

ataukinga na kuuokoa,

atapita juu yake na kuufanya salama.”

6 Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana.

7 Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.

8 “Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu;

upanga, ambao si wa kibinadamu,

utawaangamiza.

Watakimbia mbele ya upanga

na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.

9 Ngome zao zitaanguka kwa sababu ya hofu,

kwa kuona bendera ya vita,

majemadari wao watashikwa na hofu ya ghafula,”

asemaBwana,

ambaye moto wake uko Sayuni,

nayo tanuru yake iko Yerusalemu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/31-5cfb50d7e1913a2e11ccab7e3b674f51.mp3?version_id=1627—

Isaya 32

Ufalme Wa Haki

1 Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu

na watawala watatawala kwa haki.

2 Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo

na kimbilio kutokana na dhoruba,

kama vijito vya maji jangwani

na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu.

3 Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena,

nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.

4 Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa,

nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha.

5 Mpumbavu hataitwa tena muungwana

wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.

6 Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu,

moyo wake hushughulika na uovu:

Hutenda mambo yasiyo ya uchaji Mungu,

na hueneza habari za makosa kuhusuBwana;

yeye huwaacha wenye njaa bila kitu

na wenye kiu huwanyima maji.

7 Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,

hufanya mipango miovu

ili kumwangamiza maskini kwa uongo,

hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.

8 Lakini mtu mwungwana hufanya mipango ya kiungwana

na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa.

Wanawake Wa Yerusalemu

9 Enyi wanawake wenye kuridhika sana,

amkeni na mnisikilize,

enyi binti mnaojisikia kuwa salama,

Sikieni lile ninalotaka kuwaambia!

10 Kwa zaidi kidogo ya mwaka

ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,

mavuno ya zabibu yatakoma

na mavuno ya matunda hayatakuwepo.

11 Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,

tetemekeni, kwa hofu enyi binti mnaojisikia salama!

Vueni nguo zenu,

vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.

12 Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri,

kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri

13 na kwa ajili ya nchi ya watu wangu,

nchi ambayo miiba na michongoma imemea:

naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha

na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe.

14 Ngome itaachwa,

mji wenye kelele nyingi utahamwa,

ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,

mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,

15 mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu,

nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba

na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.

16 Haki itakaa katika jangwa

na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.

17 Matunda ya haki yatakuwa amani,

matokeo ya haki yatakuwa utulivu

na matumaini milele.

18 Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,

katika nyumba zilizo salama,

katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.

19 Hata mvua ya mawe iangushe msitu

na mji ubomolewe kabisa,

20 tazama jinsi utakavyobarikiwa,

ukipanda mbegu yako katika kila kijito,

na kuwaacha ng’ombe wako

na punda wajilishe kwa uhuru.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/32-3621b8ccce0d1fe34d61cabc87da26c8.mp3?version_id=1627—

Isaya 33

Taabu Na Msaada

1 Ole wako wewe, Ee mharabu,

wewe ambaye hukuharibiwa!

Ole wako, Ee msaliti,

wewe ambaye hukusalitiwa!

Utakapokwisha kuharibu,

utaharibiwa;

utakapokwisha kusaliti,

utasalitiwa.

2 EeBwana, uturehemu,

tunakutamani.

Uwe nguvu yetu kila asubuhi

na wokovu wetu wakati wa taabu.

3 Kwa ngurumo ya sauti yako, mataifa yanakimbia;

unapoinuka, mataifa hutawanyika.

4 Mateka yako, Enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu,

kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.

5 Bwanaametukuka, kwa kuwa anakaa mahali palipoinuka,

ataijaza Sayuni kwa haki na uadilifu.

6 Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu,

ghala za wokovu tele, hekima na maarifa;

kumchaBwanani ufunguo wa hazina hii.

7 Angalia, watu wake mashujaa wanapiga kelele kwa nguvu barabarani,

wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.

8 Njia kuu zimeachwa,

hakuna wasafiri barabarani.

Mkataba umevunjika,

# mashahidi wake wamedharauliwa,

hakuna ye yote anayeheshimiwa.

9 Ardhi inaombolezana kuchakaa,

Lebanoni imeaibika na kunyauka,

Sharoni ni kama Araba,

nayo Bashani na Karmeli

wanapukutisha majani yao.

10 “Sasa nitainuka,” asemaBwana.

“Sasa nitatukuzwa;

sasa nitainuliwa juu.

11 Mlichukua mimba ya makapi,

mkazaa mabua,

pumzi yenu ni moto uwateketezao.

12 Mataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa,

kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.”

13 Ninyi mlio mbali sana, sikieni lile nililofanya;

ninyi mlio karibu, tambueni uweza wangu!

14 Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu,

kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:

“Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?

Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”

15 Yeye aendaye kwa uadilifu

na kusema lile lililo sawa,

yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma

na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,

yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji

na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:

16 huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,

ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.

Atapewa mkate wake,

na maji yake hayatakoma.

17 Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake

na kuiona nchi inayoenea mbali.

18 Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita:

“Yuko wapi yule afisa mkuu?

Yuko wapi yule aliyechukua ushuru?

Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?”

19 Hutawaona tena wale watu wenye kiburi,

wale watu wenye usemi wa mafumbo,

wenye lugha ngeni, isiyoeleweka.

20 Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu;

macho yenu yatauona Yerusalemu,

mahali pa amani pa kuishi,

hema ambalo halitaondolewa,

nguzo zake hazitang’olewa kamwe,

wala hakuna kamba yake yo yote itakayokatika.

21 HukoBwanaatakuwa Mwenye Nguvu wetu.

Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito.

Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko,

wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko.

22 Kwa kuwaBwanani mwamuzi wetu,

Bwanandiye mtoa sheria wetu,

Bwanani mfalme wetu,

yeye ndiye atakayetuokoa.

23 Kamba zenu za merikebu zimelegea:

Mlingoti haukusimama imara,

tanga halikukunjuliwa.

Wingi wa mateka yatagawanywa,

hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara.

24 Hakuna ye yote aishiye Sayuni atakayesema, “Mimi ni mgonjwa”;

nazo dhambi za wale waishio humo zitasamehewa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/33-266cf71af09405eec759a6e358662e17.mp3?version_id=1627—

Isaya 34

Hukumu Dhidi Ya Mataifa

1 Njoni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize;

sikilizeni kwa makini,

enyi kabila za watu!

Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake,

ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake!

2 Bwanaameyakasirikia mataifa yote;

ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote.

Atawaangamiza kabisa,

atawatia mikononi mwa wachinjaji.

3 Waliouawa watatupwa nje,

maiti zao zitatoa uvundo,

milima itatota kwa damu zao.

4 Nyota zote za mbinguni zitayeyuka

na anga litasokotwa kama kitabu,

jeshi lote la angani litaanguka

kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu,

kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini.

5 Upanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni,

tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu,

wale watu ambao nimeshawahukumu,

kuwaangamiza kabisa.

6 Upanga waBwanaumeoga katika damu,

umefunikwa na mafuta ya nyama:

damu ya kondoo na mbuzi,

mafuta kutoka katika figo za kondoo waume.

Kwa maanaBwanaana dhabihu huko Bosra

na machinjo makuu huko Edomu.

7 Nyati wataanguka pamoja nao,

ndama waume na mafahali wakubwa.

Nchi yao italowana kwa damu,

nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.

8 Kwa sababuBwanaanayo siku ya kulipiza kisasi,

mwaka wa malipo,

siku ya kushindania shauri la Sayuni.

9 Vijito vya Edomu vitageuka kuwa lami,

mavumbi yake yatakuwa kiberiti kiunguzacho,

nchi yake itakuwa lami iwakayo!

10 Haitazimishwa usiku wala mchana,

moshi wake utapaa juu milele.

Kutoka kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa,

hakuna mtu ye yote atakayepita huko tena.

11 Bundi wa jangwani na bundi mwenye sauti nyembamba wataimiliki,

bundi wakubwa na kunguru wataweka viota humo.

Mungu atanyosha juu ya Edomu

kamba ya kupimia ya machafuko matupu

na timazi ya ukiwa.

12 Watu wake wa kuheshimiwa hawatakuwa na cho chote

huko kitakachoitwa ufalme,

wana wao wa kifalme wote watatoweka.

13 Miiba itaenea katika ngome za ndani,

viwawi na michongoma itaota

kwenye ngome zake.

Itakuwa maskani ya mbweha,

makao ya bundi.

14 Viumbe vya jangwani vitakutana na fisi,

nao mbuzi-mwitu watalia wakiitana;

huko viumbe vya usiku vitastarehe pia

na kujitafutia mahali pa kupumzika.

15 Bundi wataweka viota huko na kutaga mayai,

atayaangua na kutunza makinda yake

chini ya uvuli wa mbawa zake;

pia huko vipanga watakusanyika,

kila mmoja na mwenzi wake.

16 Angalieni katika gombo laBwanana msome:

Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana,

hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake.

Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza,

na Roho wake atawakusanya pamoja.

17 Huwagawia sehemu zao,

mkono wake huwagawanyia kwa kipimo.

Wataimiliki hata milele

na kuishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/34-c881929f04f8be4b62c70e56bce73c70.mp3?version_id=1627—

Isaya 35

Furaha Ya Waliokombolewa

1 Jangwa na nchi kame vitafurahi;

nyika itashangilia na kuchanua maua.

Kama waridi,

2 litachanua maua,

litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha.

Litapewa utukufu wa Lebanoni.

Fahari ya Karmeli na Sharoni;

wataona utukufu waBwana,

fahari ya Mungu wetu.

3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu,

yafanyeni imara magoti yaliyolegea,

4 waambieni wale wenye mioyo ya hofu,

“Iweni hodari, msiogope;

tazama, Mungu wenu atakuja,

pamoja na malipo ya Mungu,

atakuja na kuwaokoa ninyi.”

5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa

na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

6 Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu,

nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe.

Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika

na vijito katika jangwa.

7 Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji,

ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi.

Maskani ya mbweha walikolala hapo awali

# patamea majani, matete na mafunjo.

8 Nako kutakuwa na njia kuu,

nayo itaitwa Njia ya Utakatifu.

Wasio safi hawatapita juu yake;

itakuwa kwa ajili ya wale

watembeao katika Njia ile;

yeye asafiriye juu yake,

ajapokuwa mjinga, hatapotea.

9 Huko hakutakuwepo na simba,

wala mnyama mkali hatapita njia hiyo,

wala hawatapatikana humo.

Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko,

10 waliokombolewa naBwanawatarudi.

Wataingia Sayuni wakiimba;

furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.

Watapata furaha na shangwe;

huzuni na majonzi vitakimbia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/35-96b8b13a1ac9d2d57620cc3bb28ea101.mp3?version_id=1627—

Isaya 36

Senakeribu Anatishia Yerusalemu

1 Katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwa Mfalme Hezekia, Mfalme Senakeribu wa Ashuru alishambulia miji yote ya Yuda yenye maboma na kuiteka.

2 Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma Amirijeshi kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Amirijeshi aliposimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu lililojengwa, katika njia iendayo kwenye uwanda wa Dobi,

3 Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna aliyekuwa katibu na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wakamwendea.

4 Amirijeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia,

“ ‘Hili ndilo asemalo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru: Ni wapi ulikoweka hili tumaini lako?

5 Unasema mnayo mikakati na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Je, wewe unamtegemea nani, hata kwamba unaniasi mimi?

6 Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huutoboa na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea.

7 Kama ukiniambia, “TunamtumainiaBwana, Mungu wetu,” si ni yeye ambaye mahali pake pa juu na madhabahu zake Hezekia ameziondoa, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima msujudu mbele ya madhabahu hii”?

8 “ ‘Njoni sasa, fanyeni patano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi 2,000, kama wewe unaweza kuwapandisha watu juu yao!

9 Wawezaje basi kurudisha nyuma mmoja wa maafisa wangu wadogo wa bwana wangu, hata kama unaitegemea Misri kwa ajili ya magari ya vita na wapanda farasi?

10 Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza nchi hii bilaBwana?Bwanamwenyewe aliniambia niingie niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’ ”

11 Ndipo Eliakimu, Shebna na Yoa wakamwambia Amirijeshi, “Tafadhali, zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania watu walioko juu ya ukuta wakiwa wanasikia.”

12 Lakini Amirijeshi akajibu, “Kwani ni kwa bwana wenu na ninyi peke yenu ambao bwana wangu amenituma kusema mambo haya, wala si kwa watu walioketi juu ya ukuta, ambao, kama ninyi, itawapasa kula mavi yao na kunywa mkojo wao wenyewe?”

13 Ndipo Amirijeshi akasimama na kuita kwa lugha ya Kiebrania, “Sikilizeni maneno ya mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru!

14 Hili ndilo mfalme asemalo: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa!

15 Msikubali Hezekia awashawishi kumtumainiBwanawakati anaposema, ‘HakikaBwanaatatuokoa sisi, mji huu hautatiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’

16 “Msimsikilize Hezekia. Hili ndilo mfalme wa Ashuru asemalo: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka katika mzabibu wake na mtini wake mwenyewe na kunywa maji kutoka katika kisima chake mwenyewe,

17 mpaka nije nikawachukue mwende kwenye nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na ya mashamba ya mizabibu.

18 “Msikubali Hezekia awapotoshe wakati asemapo, ‘Bwanaatatuokoa.’ Je, mungu wa taifa lo lote ameshawahi kuokoa nchi yake kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru?

19 Wako wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Wako wapi miungu ya Sefarvaimu? Je, wameokoa Samaria kutoka katika mkono wangu?

20 Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya nchi hizi aliyeweza kuokoa nchi yake kutoka kwangu? Inawezekanaje basiBwanakuiokoa Yerusalemu kutoka katika mkono wangu?”

21 Lakini watu wakakaa kimya wala hawakujibu lo lote, kwa kuwa mfalme aliamuru kuwa, “Msimjibu.”

22 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia kiongozi wa jumba la kifalme, Shebna katibu na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa na kumwambia yale Amirijeshi aliyosema.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/36-86f666f221ff9e6fa78ee36635bd0d1b.mp3?version_id=1627—