Isaya 37

Kuokolewa Kwa Yerusalemu Kunatabiriwa

1 Wakati Mfalme Hezekia aliposikia hili, alirarua nguo zake na kuvaa nguo ya gunia, naye akaenda hekaluni mwaBwana.

2 Akawatuma Eliakimu msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu na makuhani viongozi, wote wakiwa wamevaa nguo ya gunia, waende kwa nabii Isaya mwana wa Amozi.

3 Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama vile wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa.

4 YamkiniBwana, Mungu wako atayasikia maneno ya Amirijeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayoBwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako hai.”

5 Watumishi wa Mfalme Hezekia walipomjia Isaya,

6 Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Usiogope kwa ajili ya yale uliyoyasikia, yale maneno ambayo kwayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana mimi.

7 Sikiliza! Nitatia roho ndani yake ili kwamba atakaposikia taarifa fulani, atarudi katika nchi yake mwenyewe, nami huko nitafanya auawe kwa upanga.’ ”

8 Amirijeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi akamkuta mfalme anapigana dhidi ya Libna.

9 Basi Senakeribu akapata taarifa kwamba Tirhaka, Mkushi mfalme wa Misri, alikuwa anatoka kupigana dhidi yake. Aliposikia jambo hili akatuma wajumbe kwa Hezekia kwa neno hili:

10 “Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda: Usikubali Mungu unayemtumainia akudanganye wakati anaposema, ‘Yerusalemu haitatiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’

11 Hakika umesikia yale ambayo wafalme wa Ashuru wametenda kwa nchi zote, wakiwaangamiza kabisa. Je, wewe utaokolewa?

12 Je, miungu ya yale mataifa ambayo yaliangamizwa na baba zangu iliwaokoa, miungu ya Gozani, Harani, Resefu na watu wa Edeni ambao walikuwa katika Telasari?

13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa mji wa Sefarvaimu, au wa Hena au wa Iva?”

Maombi Ya Hezekia

14 Hezekia alipokea barua kutoka kwa wale wajumbe naye akaisoma. Kisha akapanda hekaluni mwaBwanaakaikunjua mbele zaBwana.

15 Naye Hezekia akamwombaBwanaakisema:

16 “EeBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Umeumba mbingu na nchi.

17 EeBwana, tega sikio na usikie, fungua macho yako, EeBwana, uone, sikiliza maneno yote Senakeribu aliyotuma ili kumtukana Mungu aliye hai.

18 “Ni kweli, EeBwanakwamba wafalme wa Waashuru wameyaangamiza mataifa haya yote pamoja na nchi zao.

19 Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiteketeza, kwani haikuwa miungu bali ni miti na mawe tu, iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

20 EeBwana, Mungu wetu, sasa utuokoe toka mkononi mwake ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kwamba wewe peke yako, EeBwana, ndiwe Mungu.”

Kuanguka Kwa Senakeribu

21 Kisha Isaya mwana wa Amozi akapeleka ujumbe kwa Hezekia akisema: “Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli: Kwa sababu umeniomba kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru,

22 hili ndilo neno ambaloBwanaamesema dhidi yake:

“Bikira binti Sayuni

anakudharau na kukudhihaki.

Binti Yerusalemu

anatikisa kichwa chake ukimbiapo.

23 Wewe ni nani uliyenitukana na kunikufuru?

Ni dhidi ya nani umeinua sauti yako

na kuinua macho yako kwa kiburi?

Ni dhidi ya yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!

24 Kwa kutumia wajumbe wako

umelundika matukano juu ya Bwana.

Nawe umesema,

‘Kwa magari yangu mengi ya vita,

nimekwea kwenye vilele vya milima,

kwenye vilele vya juu kabisa vya Lebanoni.

Nimeikata mierezi yake iliyo mirefu kuliko yote,

misonobari yake iliyo bora sana.

Nimefika mahali pake palipoinuka palipo mbali sana,

katika msitu wake ulio mzuri kuliko yote.

25 Nimechimba visima katika nchi za kigeni

na kuyanywa maji huko.

Kwa nyayo za miguu yangu

nimevikausha vijito vyote vya Misri.’

26 “Je, hukusikia?

Zamani sana nililisimika.

Katika siku za zamani nililipanga,

na sasa nimelitimiza,

kwamba umeigeuza miji yenye maboma

kuwa malundo ya mawe.

27 Watu wa miji hiyo, wakiwa wameishiwa nguvu,

wanatiwa hofu na kuaibishwa.

Wao ni kama mimea katika shamba,

kama machipukizi mororo ya kijani,

kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba,

ambayo hukauka kabla ya kukua.

28 “Lakini ninajua mahali ukaapo,

kutoka kwako na kuingia kwako

na jinsi unavyoghadhibika dhidi yangu.

29 Kwa sababu unaghadhibika na ufedhuli dhidi yangu

na kwa sababu ufidhuli wako umefika masikioni mwangu,

nitaweka ndoana yangu kwenye pua yako

na hatamu yangu kinywani mwako,

nami nitakufanya urudi kwa njia uliyoijia.

30 “Hii itakuwa ndiyo ishara kwako, Ee Hezekia:

“Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe

na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake.

Lakini katika mwaka wa tatu panda na kuvuna,

panda shamba la mizabibu

na ule matunda yake.

31 Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda

yataeneza mizizi chini na kuzaa matunda.

32 Kwa kuwa kutoka Yerusalemu yatatokea mabaki,

na kutoka Mlima Sayuni kikosi cha wale walionusurika.

Wivu waBwanaMwenye Nguvu Zote,

utatimiza hili.

33 “Kwa hiyo hili ndiloBwanaasemalo kuhusu mfalme wa Ashuru:

“Hataingia katika mji huu

wala hatapiga mshale hapa.

Hatakuja mbele yake na ngao

wala kupanga majeshi kuzunguka dhidi yake.

34 Kwa njia ile aliyoijia ndiyo atakayorudi kwayo;

hataingia katika mji huu,”

asemaBwana.

35 “Nitaulinda mji huu na kuuokoa,

kwa ajili yangu mwenyewe

na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu!”

36 Ndipo malaika waBwanaakaondoka na kuwaua watu mia themanini na tano elfu katika kambi ya Waashuru. Watu walipoamka asubuhi yake, wote huko walikuwa maiti!

37 Kwa hiyo Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Alirudi Ninawi na kukaa huko.

38 Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza walimwua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme badala yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/37-d4d0dc7573517cdf553c345d2888fe39.mp3?version_id=1627—

Isaya 38

Kuugua Kwa Mfalme Hezekia

1 Katika siku hizo Hezekia akaugua naye akawa karibu na kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea na kumwambia, “Hili ndilo asemaloBwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

2 Hezekia akageuza uso wake kuelekea ukutani na kumwombaBwana,

3 “EeBwana, kumbuka, jinsi nilivyotembea mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wote nami nimefanya lile lililo jema machoni pako.” Naye Hezekia akalia sana sana.

4 Ndipo neno laBwanalikamjia Isaya:

5 “Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimesikia maombi yako na nimeona machozi yako, nitaiongeza miaka kumi na mitano katika maisha yako.

6 Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

7 “ ‘Hii ndiyo ishara yaBwanakwako ya kwambaBwanaatafanya kile alichoahidi:

8 Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.

9 Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona:

10 Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu

# je, ni lazima nipite katika malango ya mauti

na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

11 Nilisema, “Sitamwona tenaBwana,

Bwanakatika nchi ya walio hai,

wala sitamtazama tena mwanadamu,

wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu.

12 Kama hema la mchunga mifugo,

nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu.

Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu,

naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi,

mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

13 Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,

lakini kama simba alivunja mifupa yangu yote,

mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

14 Nililia kama mbayuwayu au korongo,

niliomboleza kama hua aombolezaye.

Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni.

Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!”

15 Lakini niseme nini?

Amesema nami,

naye yeye mwenyewe amelitenda hili.

Nitatembea kwa unyenyekevu

katika miaka yangu yote

kwa sababu ya haya maumivu makali

ya nafsi yangu.

16 Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,

nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia.

Uliniponya

na kuniacha niishi.

17 Hakika ilikuwa kwa ajili ya faida yangu ndiyo maana nikapata maumivu makali.

Katika upendo wako ukaniokoa

kutoka katika shimo la uharibifu;

umeziweka dhambi zangu zote

nyuma yako.

18 Kwa maana kaburihaliwezi kukusifu,

mauti haiwezi kuimba sifa zako;

wale washukao chini shimoni

hawawezi kuutarajia uaminifu wako.

19 Walio hai, walio hai, wanakusifu,

kama ninavyofanya leo;

baba huwaambia watoto wao

habari za uaminifu wako.

20 Bwanaataniokoa,

nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi

siku zote za maisha yetu

katika Hekalu laBwana.

21 Isaya alikuwa amesema, “Uandae mkate wa tini uubandike juu ya jipu, naye atapona.”

22 Hezekia alikuwa ameuliza, “Ni ishara ipi kwamba nitapanda kwenda hekaluni mwaBwana?”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/38-e25042c08218db7f0aab76070ad3053b.mp3?version_id=1627—

Isaya 39

Wajumbe Kutoka Babeli

1 Wakati huo Merodaki-Baladani mwana wa Baladani mfalme wa Babeli alimpelekea Hezekia barua na zawadi, kwa kuwa alikuwa amesikia habari za kuugua na kupona kwake.

2 Hezekia akawapokea wajumbe hao kwa furaha na kuwaonyesha kile kilichokuwa ndani ya ghala zake: Fedha, dhahabu, vikolezo, mafuta safi, silaha zake zote za vita na kila kitu kilichopo katika hazina zake. Hapakuwepo kitu cho chote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.

3 Ndipo nabii Isaya akaenda kwa Mfalme Hezekia na kumwuliza, “Watu wale walisema nini, nao wametoka wapi?”

Hezekia akajibu, “Kutoka nchi ya mbali. Walikuja kwangu kutoka Babeli.”

4 Nabii akauliza, “Waliona nini katika jumba lako la kifalme?”

Hezekia akajibu, “Waliona kila kitu katika jumba langu la kifalme. Hakuna kitu cho chote katika hazina yangu ambacho sikuwaonyesha.”

5 Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno laBwanaMwenye Nguvu Zote:

6 Hakika wakati unakuja ambapo kila kitu katika jumba lako la kifalme, navyo vyote ambavyo baba zako waliweka akiba mpaka siku hii, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna cho chote kitakachosalia, asemaBwana.

7 Tena baadhi ya wazao wako, watu wa nyama na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa, nao watakuwa matowashi katika jumba la kifalme la mfalme wa Babeli.”

8 Hezekia akajibu, “Neno laBwanaulilosema ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, “Patakuwepo amani na salama katika siku za maisha yangu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/39-e218a60b2018a0ff6536e76ed482bc99.mp3?version_id=1627—

Isaya 40

Faraja Kwa Watu Wa Mungu

1 Wafarijini, wafarijini watu wangu,

asema Mungu wenu.

2 Sema na Yerusalemu kwa upole,

umtangazie

kwamba kazi yake ngumu imekamilika,

kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia,

kwamba amepokea kutoka mkononi mwaBwana

maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote.

3 Sauti ya mtu aliaye:

“Itengenezeni jangwani njia yaBwana,

nyosheni njia kuu nyikani

kwa ajili ya Mungu wetu.

4 Kila bonde litainuliwa,

kila mlima na kilima kitashushwa;

ardhi yenye mabonde patasawazishwa,

mahali palipoparuza patanyooshwa.

5 Utukufu waBwanautafunuliwa,

nao wanadamu wote kwa pamoja watauona.

Kwa maana kinywa chaBwanakimenena.”

6 Sauti husema, “Piga kelele.”

Nami nikasema, “Nipige kelele gani?”

“Wanadamu wote ni kama majani,

nao utukufu wao wote

ni kama maua ya kondeni.

7 Majani hunyauka na maua huanguka,

kwa sababu pumzi yaBwanahuyapuliza.

Hakika wanadamu ni majani.

8 Majani hunyauka na maua huanguka,

lakini neno la Mungu wetu lasimama milele.”

9 Wewe uletaye habari njema Sayuni,

panda juu ya mlima mrefu.

Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,

inua sauti yako kwa kupiga kelele,

inua sauti, usiogope;

iambie miji ya Yuda,

“Yuko hapa Mungu wenu!”

10 Tazameni,BwanaMwenyezi anakuja na nguvu,

nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake.

Tazameni, ujira wake u pamoja naye,

nayo malipo yake yanafuatana naye.

11 Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:

Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake

na kuwachukua karibu na moyo wake,

huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao.

12 Ni nani aliyepima maji ya bahari

kwenye konzi ya mkono wake,

# au kuzipima mbingu kwa shibiriyake?

Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,

au kupima milima kwenye kipimio

na vilima kwenye mizani?

13 Ni nani aliyeyafahamu mawazo yaBwana,

au kumfundisha kama mshauri wake?

14 Ni nani ambayeBwanaametaka shauri kwake ili kumwelimisha,

naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?

Ni nani aliyemfundisha maarifa

au kumwonyesha mapito ya ufahamu?

15 Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo,

ni kama vumbi jembamba juu ya mizani,

huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.

16 Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni,

wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa.

17 Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu,

yanaonekana yasio na thamani

na zaidi ya bure kabisa.

18 Basi, utamlinganisha Mungu na nani?

Utamlinganisha na kitu gani?

19 Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,

naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu

na kuitengenezea mikufu ya fedha.

20 Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii

huuchagua mti usiooza.

Humtafuta fundi stadi

wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.

21 Je, hujui?

Je, hujasikia?

Je, hujaambiwa tangu mwanzo?

Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia?

22 Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia,

nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi.

Huzitandaza mbingu kama chandarua

na kuzitandaza kama hema la kuishi.

23 Huwafanya wakuu kuwa si kitu

na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure.

24 Mara baada ya kupandwa,

mara baada ya kutiwa ardhini

mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini,

ndipo huwapulizia nao wakanyauka,

nao upepo wa kisulisuli

huwapeperusha kama makapi.

25 “Utanilinganisha mimi na nani?

Au ni nani anayelingana nami?”

Asema yeye Aliye Mtakatifu.

26 Inueni macho yenu mtazame mbinguni:

Ni nani aliyeumba hivi vyote?

Yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine

na kuziita kila moja kwa jina lake?

Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu,

hakuna hata mojawapo inayokosekana.

27 Kwa nini unasema, Ee Yakobo,

nanyi Ee Israeli, kulalamika,

“Njia yangu imefichwaBwanaasiione,

Mungu wangu hajali shauri langu?”

28 Je wewe, hufahamu?

Je wewe, hujasikia?

Bwanani Mungu wa milele,

Muumba wa miisho ya dunia.

Hatachoka wala kulegea,

wala hakuna hata mmoja

awezaye kuupima ufahamu wake.

29 Huwapa nguvu waliolegea

na huongeza nguvu za wadhaifu.

30 Hata vijana huchoka na kulegea,

nao vijana wanaume kujikwaa na kuanguka,

31 bali wale wamtumainioBwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/40-3461f7e73668810625cba05ce7394d8c.mp3?version_id=1627—

Isaya 41

Msaidizi Wa Israeli

1 “Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa!

Mataifa na wafanye upya nguvu zao!

Wao na wajitokeze, kisha waseme,

tukutane pamoja mahali pa hukumu.

2 “Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki,

akimwita katika haki kwa utumishi wake?

Huyatia mataifa mikononi mwake

na kuwatiisha wafalme mbele zake.

Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake,

huwafanya makapi yapeperushwayo

na upepo kwa upinde wake.

3 Huwafuatia na kuendelea salama,

katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita.

4 Ni nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza,

akiita vizazi tangu mwanzo?

Mimi,Bwana, ni wa kwanza

nami nitakuwa pamoja na wa mwisho:

mimiBwanandiye.”

5 Visiwa vimeliona na kuogopa,

miisho ya dunia inatetemeka.

Wanakaribia na kuja mbele,

6 kila mmoja humsaidia mwingine

na kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!”

7 Fundi humtia moyo sonara,

yeye alainishaye kwa nyundo

humhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe,

Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.”

Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike.

8 “Lakini wewe, Ee Israeli, mtumishi wangu,

Yakobo, niliyemchagua,

ninyi wazao wa Abrahamu rafiki yangu,

9 Nilikuchukua toka miisho ya dunia,

nilikuita kutoka pembe zake za mbali.

Nilisema, ‘Wewe ni mtumishi wangu’;

nimekuchagua, wala sikukukataa.

10 Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

11 “Wote walioona hasira dhidi yako

hakika wataaibika na kutahayarika,

wale wakupingao

watakuwa kama vile si kitu na kuangamia.

12 Ingawa utawatafuta adui zako,

hutawaona.

Wale wanaopigana vita dhidi yako

watakuwa kama vile si kitu kabisa.

13 Kwa maana Mimi ndimiBwana, Mungu wako,

nikushikaye mkono wako wa kuume

na kukuambia, Usiwe na hofu,

nitakusaidia.

14 Usiogope, Ee Yakobo uliye mdudu,

Ee Israeli uliye mdogo,

kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,” asemaBwana,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

15 “Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria,

kipya na chenye makali, chenye meno mengi.

Utaipura milima na kuiponda

na kuvifanya vilima kuwa kama makapi.

16 Utaipepeta, nao upepo utaichukua,

dhoruba itaipeperushia mbali.

Bali wewe utajifurahisha katikaBwana

na katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

17 “Maskini na wahitaji wanatafuta maji,

lakini hayapo,

ndimi zao zimekauka kwa kiu.

Lakini MimiBwananitawajibu,

Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.

18 Nitaifanya mito itiririke juu ya vilima vilivyo kame,

nazo chemchemi ndani ya mabonde.

Nitaligeuza jangwa liwe mabwawa ya maji,

nayo ardhi iliyokauka kuwa chemchemi za maji.

19 Katika jangwa nitaotesha

mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni.

Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku

pamoja huko nyikani,

20 ili kwamba watu wapate kuona na kujua,

wapate kufikiri na kuelewa,

kwamba mkono waBwanaumetenda hili,

kwamba yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ndiye aliyelifanya.”

21 Bwanaasema, “Leta shauri lako.

Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo.

22 “Leteni sanamu zenu zituambie

ni nini kitakachotokea.

Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini,

ili tupate kuyatafakari

na kujua matokeo yake ya mwisho.

Au tutangazieni mambo yatakayokuja,

23 tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye,

ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu.

Fanyeni jambo lo lote zuri au baya,

ili tupate kutishika na kujazwa na hofu.

24 Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa

na kazi zenu hazifai kitu kabisa;

yeye awachaguaye ni chukizo sana.

25 “Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,

naye yuaja, mmoja toka maawio ya jua aliitaye Jina langu.

Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,

kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.

26 Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua,

au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’?

Hakuna aliyenena hili,

hakuna aliyetangulia kusema hili,

hakuna ye yote aliyesikia maneno kutoka kwenu.

27 Nilikuwa wa kwanza kumwambia Sayuni,

‘Tazama, wako hapa!’

Nilimpa Yerusalemu mjumbe wa habari njema.

28 Ninatazama lakini hakuna ye yote:

hakuna ye yote miongoni mwao awezaye kutoa shauri,

hakuna ye yote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza.

29 Tazama, wote ni ubatili!

Matendo yao ni bure;

vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/41-f33740067275a72627924a0505b905d0.mp3?version_id=1627—

Isaya 42

Mtumishi Wa Bwana

1 “Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza,

mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye;

nitaweka Roho yangu juu yake,

naye ataleta haki kwa mataifa.

2 Hatapaza sauti wala kupiga kelele,

wala hataiinua sauti yake barabarani.

3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja

na utambi ufukao moshi hatauzima.

Kwa uaminifu ataleta haki,

4 hatazimia roho wala kukata tamaa

mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia.

Visiwa vitaweka tumaini lake katika sheria yake.”

5 Hili ndilo asemalo Mungu,Bwana,

yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda,

aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo,

awapaye watu wake pumzi

na uzima kwa wale waendao humo:

6 “Mimi,Bwana, nimekuita katika haki;

nitakushika mkono wako.

Nitakulinda na kukufanya

kuwa Agano kwa ajili ya watu

na nuru kwa Mataifa,

7 kuwafungua macho wale wasioona,

kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela,

na kuwafungua kutoka gerezani

wale wanaokaa gizani.

8 “Mimi ndimiBwana; hilo ndilo Jina langu!

Sitampa mwingine utukufu wangu

wala sanamu sifa zangu.

9 Tazama, mambo ya kwanza yametokea,

nami natangaza mambo mapya;

kabla hayajatokea

nawatangazia habari zake.”

Wimbo Wa Kumsifu Bwana

10 MwimbieniBwanawimbo mpya,

sifa zake toka miisho ya dunia,

ninyi mshukao chini baharini,

na vyote vilivyomo ndani yake,

enyi visiwa na wote wakaao ndani yake.

11 Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao;

makao anamoishi Kedari na yashangilie.

Watu wa Sela waimbe kwa furaha

na wapige kelele kutoka vilele vya milima.

12 WampeBwanautukufu

na kutangaza sifa zake katika visiwa.

13 Bwanaataenda kama mtu mwenye nguvu,

kama shujaa atachochea shauku yake,

kwa kelele ataamsha kilio cha vita

naye atashinda adui zake.

14 “Kwa muda mrefu nimenyamaza kimya,

nimekaa kimya na kujizuia.

Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua,

ninapiga kelele, ninatweta

na kushusha pumzi.

15 Nitaharibu milima na vilima

na kukausha uoto wake wote;

nitafanya mito kuwa visiwa

na kukausha mabwawa.

16 Nitawaongoza vipofu kwenye njia ambayo hawajaijua,

kwenye mapito wasiyoyazoea nitawaongoza;

nitafanya giza kuwa nuru mbele yao

na kufanya mahali palipoparuza kuwa laini.

Haya ndiyo mambo nitakayofanya;

mimi sitawaacha.

17 Lakini wale wanaotumaini sanamu,

wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’

watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa.

Israeli Kipofu Na Kiziwi

18 “Sikieni, enyi viziwi;

tazameni, enyi vipofu, mpate kuona!

19 Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu,

na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?

Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu,

aliye kipofu kama mtumishi waBwana?

20 Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia;

masikio yenu yako wazi lakini hamsikii cho chote.”

21 IlimpendezaBwana

kwa ajili ya haki yake

kufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu.

22 Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara,

wote wamenaswa katika mashimo,

au wamefichwa katika magereza.

Wamekuwa nyara,

wala hapana ye yote awaokoaye.

Wamefanywa mateka,

wala hapana ye yote asemaye, “Warudishe.”

23 Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili

au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao?

24 Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka,

na Israeli kwa wateka nyara?

Je, hakuwaBwana,

ambaye tumetenda dhambi dhidi yake?

Kwa kuwa hawakufuata njia zake,

hawakutii sheria zake.

25 Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka,

ukali wa vita.

Ikawazunguka kwa miali ya moto,

hata hivyo hawakuelewa;

ikawateketeza,

lakini hawakuyatia moyoni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/42-788fb4b293f8b7e54626fd900a3a74bd.mp3?version_id=1627—

Isaya 43

Mwokozi Pekee Wa Israeli

1 Lakini sasa hili ndilo asemaloBwana,

yeye aliyekuumba, Ee Yakobo,

yeye aliyekuhuluku, Ee Israeli:

“Usiogope kwa maana nimekukomboa,

nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu.

2 Unapopita kwenye maji makuu,

nitakuwa pamoja nawe,

unapopita katika mito ya maji,

hayatakugharikisha.

Utakapopita katika moto,

hutaungua,

miali ya moto haitakuunguza.

3 Kwa kuwa Mimi ndimiBwana, Mungu wako,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako,

ninaitoa Misri kuwa fidia yako,

Kushi na Seba badala yako.

4 Kwa kuwa wewe ni wa thamani na wa kuheshimiwa machoni pangu,

nami kwa kuwa ninakupenda,

nitatoa watu badala yako

na mataifa badala ya maisha yako.

5 Usiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe,

nitawaleta watoto wako kutoka mashariki

na kukukusanya kutoka magharibi.

6 Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’

nayo kusini, ‘Usiwazuie.’

Walete wana wangu kutoka mbali

na binti zangu kutoka miisho ya dunia:

7 kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu,

niliyemwumba kwa utukufu wangu,

niliyemhuluku na kumfanya.”

8 Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni,

wenye masikio lakini hawasikii.

9 Mataifa yote yanakutanika pamoja

na mataifa wanakusanyika.

Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya

na kututangazia mambo yaliyopita?

Walete mashahidi wao ili kuthibitisha kuwa walikuwa sahihi,

ili kwamba wengine waweza kusikia na kusema, “Ni kweli.”

10 “Ninyi ni mashahidi wangu,” asemaBwana,

“na mtumishi wangu niliyemchagua,

ili mpate kunijua na kuniamini

na kutambua kwamba Mimi ndiye.

Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa,

wala hatakuwepo mwingine baada yangu.

11 Mimi, naam mimi, ndimiBwana,

zaidi yangu hakuna mwokozi.

12 Nimedhihirisha, kuokoa na kutangaza:

Mimi, wala si mungu mgeni katikati yenu.

Ninyi ni mashahidi wangu,” asemaBwana,

“kwamba Mimi ndimi Mungu.

13 Naam, tangu siku za kale, Mimi ndiye.

Hakuna hata mmoja awezaye kuokoa

kutoka katika mkono wangu.

Mimi ninapotenda,

ni nani awezaye kutangua?”

Huruma Za Mungu Na Kukosa Uaminifu Kwa Israeli

14 Hili ndiloBwanaasemalo,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa ajili yenu nitatumana Babeli

na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi,

katika meli walizozionea fahari.

15 Mimi ndimiBwana, yeye Aliye Mtakatifu wako,

Muumba wa Israeli, Mfalme wako.”

16 Hili ndilo asemaloBwana,

yeye aliyefanya njia baharini,

mahali pa kupita kwenye maji mengi,

17 aliyeyakokota magari ya vita na farasi,

jeshi pamoja na askari wa msaada,

nao wakalala huko, wala hawatainuka tena kamwe,

wamekomeshwa, wakazimika kama utambi:

18 “Msiyakumbuke mambo yaliyopita,

wala msiyatafakari mambo ya zamani.

19 Tazama, nitafanya jambo jipya!

Sasa litachipuka, je, hamtalitambua?

Nitafanya njia jangwani

na vijito vya maji katika nchi kame.

20 Wanyama wa mwituni wataniheshimu,

mbweha na bundi,

kwa sababu ninawapatia maji jangwani,

na vijito katika nchi kame,

ili kuwapa watu wale maji, ambao ni chaguo langu.

21 Watu wale niliowaumba kwa ajili yangu,

ili wapate kutangaza sifa zangu.

22 “Hata hivyo hukuniita mimi, Ee Yakobo,

hujajitaabisha kwa ajili yangu, Ee Israeli.

23 Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa,

wala kuniheshimu kwa dhabihu zako.

Sikukulemea kwa sadaka za nafaka

wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba.

24 Hukuninunulia uvumba wo wote wenye manukato,

wala hukunipa kwa ukarimu

mafuta ya wanyama wa dhabihu zako.

Lakini umenilemea kwa dhambi zako

na kunitaabisha kwa makosa yako.

25 “Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako,

kwa ajili yangu mwenyewe,

wala sizikumbuki dhambi zako tena.

26 Tafakari mambo yaliyopita,

njoo na tuhojiane,

leta shauri lako, uweze kupewa haki yako.

27 Baba yako wa kwanza, alitenda dhambi,

wasemaji wako wameasi dhidi yangu.

28 Kwa hiyo nitawaaibisha wakuu wa Hekalu lako,

nami nitamtoa Yakobo aangamizwe

na Israeli adhihakiwe.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/43-9fe976cb0192986d267c1965feb29cf4.mp3?version_id=1627—

Isaya 44

Israeli Aliyechaguliwa

1 “Lakini sasa sikiliza, Ee Yakobo, mtumishi wangu,

Israeli, niliyemchagua.

2 Hili ndilo asemaloBwana,

yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni,

yeye atakayekusaidia:

Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu,

# Yeshuruni, niliyekuchagua.

3 Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu

na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka;

nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako,

nayo baraka yangu juu ya wazao wako.

4 Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani,

kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo.

5 Mmoja atasema, ‘Mimi ni waBwana’;

mwingine atajiita kwa jina la Yakobo;

vile vile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘WaBwana,’

na kujiita kwa jina la Israeli.

Ni Bwana, Siyo Sanamu

6 “Hili ndilo asemaloBwana,

Mfalme wa Israeli na Mkombozi,

BwanaMwenye Nguvu Zote:

Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho;

zaidi yangu hakuna Mungu.

7 Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na aseme.

Yeye na aseme na kuweka mbele yangu

ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale,

tena ni nini kitakachotokea,

naam, yeye na atoa unabii ni nini kitakachokuja.

8 Msitetemeke, msiogope.

Je, sikutangaza hili na kutoa unabii tangu zamani?

Ninyi ni mashahidi wangu.

Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi?

Hasha, hakuna Mwamba mwingine;

mimi simjui mwingine.”

9 Wote wachongao sanamu ni ubatili,

navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu.

Wale ambao wangesema juu yao ni vipofu,

ni wajinga, ili wao waaibike.

10 Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu,

ambayo haiwezi kumfaidia kitu cho chote?

11 Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa,

mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu.

Wote na wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao,

watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha.

12 Muhunzi huchukua kifaa

na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto,

hutengeneza sanamu kwa nyundo,

huifanyiza kwa nguvu za mkono wake.

Huona njaa na kupoteza nguvu zake,

asipokunywa maji huzimia.

13 Seremala hupima kwa kutumia kamba

na huuchora mstari kwa kalamu;

huchonga kwa patasi

na kutia alama kwa bikari.

Huifanyiza katika umbo la binadamu,

la mwanadamu katika utukufu wake wote,

ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.

14 Hukata miti ya mierezi,

huchukua mteashuri au mwaloni.

Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni,

au hupanda msunobari, mvua huufanya ukue.

15 Ni kuni kwa ajili ya binadamu,

huchukua baadhi yake na kuota moto,

huwasha moto na kuoka mkate.

Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu,

huitengeneza sanamu na kuisujudia.

16 Sehemu ya kuni huziweka motoni,

akapikia chakula chake,

hubanika nyama na kula hadi ashibe.

Huota moto na kusema,

“Aha! Ninahisi joto, ninaona moto.”

17 Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake;

yeye huisujudia na kuiabudu.

Huiomba na kusema,

“Niokoe; wewe ni mungu wangu.”

18 Hawajui cho chote, hawaelewi cho chote,

macho yao yamefungwa hivyo hawawezi kuona,

akili zao zimefungwa hivyo hawawezi kufahamu.

19 Wala hakuna anayefikiri,

hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema,

“Sehemu yake nilitumia kwa kuni;

hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake,

nilibanika nyama na kuila.

Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki?

Je, nisujudie gogo la mti?”

20 Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha;

hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema,

“Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?”

21 “Ee Yakobo, kumbuka mambo haya,

Ee Israeli, kwa kuwa wewe ni mtumishi wangu.

Nimekuumba wewe, wewe ni mtumishi wangu,

Ee Israeli, sitakusahau.

22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu,

dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.

Nirudie mimi,

kwa kuwa nimekukomboa wewe.”

23 Enyi mbingu, imbeni kwa furaha,

kwa maanaBwanaamefanya jambo hili,

Ee vilindi vya dunia, piga kelele.

Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,

enyi misitu na miti yenu yote,

kwa maanaBwanaamemkomboa Yakobo,

ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.

Yerusalemu Kukaliwa

24 “Hili ndilo asemaloBwana,

Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni:

“Mimi niBwana,

yeye aliyeumba vitu vyote,

yeye peke yake aliyezitanda mbingu,

yeye aliyeitandaza nchi mwenyewe,

25 “yeye huzipinga ishara za manabii wa uongo,

na kuwatia upumbavu waaguzi,

ayapinduaye maarifa ya wenye hekima,

na kuyafanya kuwa upuzi,

26 ayathibitishaye maneno ya watumishi wake,

na kutimiza utabiri wa wajumbe wake,

“yeye aiambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’

aiambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’

na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’

27 akiambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka,

nami nitakausha vijito vyako,’

28 amwambiaye Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu,

naye atatimiza yote yanipendezayo;

atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,”

na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/44-b52439c0d00bf031343b941f4d9a938c.mp3?version_id=1627—

Isaya 45

Koreshi Chombo Cha Mungu

1 “Hili ndilo asemaloBwanakwa mpakwa mafuta wake,

Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume

kutiisha mataifa mbele yake

na kuwavua wafalme silaha zao,

kufungua milango mbele yake

ili kwamba malango yasije yakafungwa:

2 Nitakwenda mbele yako

na kusawazisha milima;

nitavunjavunja malango ya shaba

na kukatakata mapingo ya chuma.

3 Nitakupa hazina za gizani,

mali zilizofichwa mahali pa siri,

ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimiBwana,

Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.

4 Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu,

Israeli niliyemchagua,

nimekuita wewe kwa jina lako

na kukupa jina la heshima,

ingawa wewe hunitambui.

5 Mimi ndimiBwana, wala hakuna mwingine,

zaidi yangu hakuna Mungu.

Nitakutia nguvu,

ingawa wewe hukunitambua,

6 ili kwamba kutoka maawio ya jua

mpaka machweo yake,

watu wapate kujua kwamba

hakuna Mungu mwingine ila Mimi.

Mimi ndimiBwanawala hakuna mwingine.

7 Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza,

ninaleta mafanikio na kusababisha maafa,

Mimi,Bwana, hufanya vitu hivi vyote.

8 “Enyi mbingu juu, nyesheni haki,

mawingu na yaidondoshe.

Dunia na ifunguke sana,

wokovu na uchipuke,

haki na ikue pamoja nao;

mimi,Bwana, ndiye niliyeiumba.

9 “Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake,

yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi.

Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi,

‘Unatengeneza nini wewe?’

Je, kazi yako husema,

‘Hana mikono’?

10 Ole wake amwambiaye baba yake,

‘Umezaa nini?’

Au kumwambia mama yake,

‘Umezaa kitu gani?’

11 “Hili ndilo asemaloBwana,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na Muumba wake:

Kuhusu mambo yatakayokuja,

je, unaniuliza habari za watoto wangu,

au kunipa amri kuhusu kazi za mikono yangu?

12 Mimi ndiye niliyeumba dunia

na kumwumba mwanadamu juu yake.

Mikono yangu mwenyewe ndiyo iliyozitanda mbingu,

nikayapanga majeshi yake yote ya angani.

13 Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu:

Nitazinyosha njia zake zote.

Yeye atajenga kwa upya mji wangu

na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni,

lakini si kwa kima cha fedha wala kwa kupewa zawadi,

asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.”

14 Hili ndilo asemaloBwana:

“Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi,

nao wale Waseba warefu,

watakujia na kuwa wako,

watakujia wakijikokota nyuma yako,

watakujia wamefungwa minyororo.

Watasujudu mbele yako

wakikusihi na kusema,

‘Hakika Mungu yu pamoja nawe,

wala hakuna mwingine;

hakuna Mungu mwingine.’ ”

15 Hakika wewe u Mungu unayejificha,

Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli.

16 Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika;

watatahayarika kwa pamoja.

17 Lakini Israeli ataokolewa naBwana

kwa wokovu wa milele;

kamwe hutaaibika wala kutatahayarika,

milele yote.

18 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana,

yeye aliyeumba mbingu,

ndiye Mungu;

yeye aliyeifanya dunia na kuiumba,

yeye ndiye aliyeiwekea misingi imara,

hakuiumba ili iwe tupu,

bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake,

anasema:

“Mimi ndimiBwana,

wala hakuna mwingine.

19 Sijasema sirini,

kutoka mahali fulani katika nchi ya giza;

sijawaambia wazao wa Yakobo,

‘Nitafuteni bure.’

Mimi,Bwana, nasema kweli;

ninatangaza lile lililo sahihi.

20 “Kusanyikeni pamoja mje,

enyi wakimbizi kutoka katika mataifa.

Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili,

Wale waombao miungu ile isiyoweza kuokoa.

21 Tangazeni lile litakalokuwapo, lisemeni hilo,

wao na wafanye shauri pamoja.

Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani,

aliyetangaza tangu zamani za kale?

Je, haikuwa Mimi,Bwana?

Wala hapana Mungu mwingine

zaidi yangu mimi,

Mungu mwenye haki na Mwokozi;

hapana mwingine ila mimi.

22 “Nigeukieni mimi nanyi mkaokolewe,

enyi miisho yote ya dunia;

kwa maana mimi ndimi Mungu,

wala hapana mwingine.

23 Nimeapa kwa nafsi yangu,

kinywa changu kimenena katika uadilifu wote

neno ambalo halitatanguka:

Kila goti litapigwa mbele zangu,

kwangu mimi kila ulimi utaapa.

24 Watasema kuhusu mimi,

‘KatikaBwanapeke yake

ndiko kuna haki na nguvu.’ ”

Wote ambao wamemkasirikia Mungu

watamjia yeye nao watatahayarika.

25 Lakini katikaBwanawazao wote wa Israeli

wataonekana wenye haki na kutukuka.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/45-b9b962d8a5efc8e5b8c2437ec3e2c6a4.mp3?version_id=1627—

Isaya 46

Miungu Ya Babeli

1 Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama;

sanamu zao hubebwa na wanyama wa mizigo.

Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea,

mzigo kwa waliochoka.

2 Vinyago pamoja na wale wanaovibeba wanainama chini;

hiyo miungu haiwezi kuwaokoa watu,

wote wanakwenda utumwani pamoja.

3 “Nisikilizeni mimi, Ee nyumba ya Yakobo,

ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli,

ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba,

nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.

4 Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi Mimi ndiye,

Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

Nimewahuluku nami nitawabeba,

nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.

5 “Mtanilinganisha na nani

au mtanihesabu kuwa sawa na nani?

Ni nani mtakayenifananisha naye

ili tuweze kulinganishwa?

6 Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao

na kupima fedha kwenye mizani;

huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu,

kisha huisujudia na kuiabudu.

7 Huiinua kuiweka mabegani na kuichukua;

huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo,

wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale.

Ingawa mtu huililia, haijibu;

haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.

8 “Kumbukeni hili, mkajionyesha kuwa waume,

litieni akilini, liwekeni moyoni, enyi waasi.

9 Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale;

mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine;

mimi ndimi Mungu,

wala hakuna mwingine aliye kama mimi.

10 Ni mimi tangazaye mwisho tangu mwanzo,

naam, tangu zamani za kale,

mambo ambayo hayajatendeka.

Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama,

nami nitatenda mapenzi yangu yote.

11 Kutoka mashariki ninaita ndege awindaye;

kutoka nchi ya mbali,

mtu atakayetimiza kusudi langu.

Lile ambalo nimelisema, ndilo nitakalolitimiza;

lile nililolipanga, hilo ndilo nitakalolitenda.

12 Nisikilizeni, ninyi wenye mioyo migumu,

ninyi mlio mbali na haki.

13 Ninaleta haki yangu karibu,

haiko mbali;

wala wokovu wangu hautachelewa.

Nitawapa Sayuni wokovu,

Israeli utukufu wangu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/46-eac1d24dd960b072cef119ad4ac2543f.mp3?version_id=1627—