Mithali 11

1 Bwanahuchukia sana mizani za udanganyifu,

bali vipimo sahihi ni furaha yake.

2 Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,

bali unyenyekevu huja na hekima.

3 Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,

bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.

4 Utajiri haufaidii kitu katika siku ya ghadhabu,

bali haki huokoa kutoka mautini.

5 Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka,

bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.

6 Haki ya wanyofu huwaokoa,

bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.

7 Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka,

yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.

8 Mtu mwenye haki huokolewa kutoka katika taabu,

naye mtu mwovu huingia humo badala yake.

9 Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu

humwangamiza jirani yake,

bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.

10 Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi,

mwovu atowekapo, huwa kuna kelele za furaha.

11 Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa,

bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.

12 Mtu asiye na akili humdharau jirani yake,

bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.

13 Masengenyo husaliti tumaini,

bali mtu mwaminifu hutunza siri.

14 Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka,

bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.

15 Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka,

bali ye yote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.

16 Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima,

bali wanaume wakorofi hupata mali tu.

17 Mwanaume mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe,

bali mwanaume katili hujiletea taabu mwenyewe.

18 Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu,

bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.

19 Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima,

bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.

20 Bwanahuwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu,

bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.

21 Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa,

bali wale wenye haki watakuwa huru.

22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe

ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.

23 Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema,

bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.

24 Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi,

mwingine huzuia, lakini huwa maskini.

25 Mtu mkarimu atastawi;

yeye awaburudishaye wengine

ataburudishwa mwenyewe.

26 Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka,

bali baraka itamkalia kichwani kama taji

yeye aliye radhi kuiuza.

27 Yeye atafutaye mema hupata ukarimu,

bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.

28 Ye yote ategemeaye utajiri wake ataanguka,

bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.

29 Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo,

naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.

30 Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima,

naye mwenye hekima huvuta roho za watu.

31 Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani,

si zaidi sana wasiomcha Mungu na wenye dhambi!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/11-81584545fab6ddaa41d75fc3209ba4c1.mp3?version_id=1627—

Mithali 12

Mafundisho Ya Kifamilia Na Ya Kijamii

1 Ye yote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa,

bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.

2 Mtu mwema hupata kibali kutoka kwaBwana,

baliBwanahumhukumu mwenye hila.

3 Mtu hathibitiki kutokana na uovu,

bali mwenye haki hataondolewa.

4 Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe,

bali aaibishaye ni kama uozo

katika mifupa ya mumewe.

5 Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki,

bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.

6 Maneno ya mwovu huotea kumwaga damu,

bali maneno ya mwadilifu huwaokoa.

7 Watu waovu huondolewa na kutoweka,

bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.

8 Mtu husifiwa kulingana na hekima yake,

bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa.

9 Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi,

kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.

10 Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake,

bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili.

11 Yeye alimaye ardhi yake atakuwa na chakula tele,

bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.

12 Waovu hutamani mateka ya watu wabaya,

bali shina la mwenye haki hustawi.

13 Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi,

bali mwenye haki huepuka taabu.

14 Kutokana na tunda la midomo yake

mtu hujazwa na mambo mema,

hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza.

15 Njia ya mpumbavu huonekana sawa

machoni pake mwenyewe,

bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri.

16 Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara,

bali mtu wa busara hupuuza matukano.

17 Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika,

bali shahidi wa uongo husema uongo.

18 Maneno ya ushupavu huchoma kama upanga,

bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

19 Midomo isemayo kweli hudumu milele,

bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.

20 Upo udanganyifu katika mioyo

ya wale ambao hupanga mabaya,

bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.

21 Hakuna dhara linalompata mwenye haki,

bali waovu wana taabu nyingi.

22 Bwanaanachukia sana midomo idanganyayo,

bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.

23 Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe,

bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.

24 Mikono yenye bidii itatawala,

bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.

25 Moyo wa wasiwasi humlemea mtu,

bali neno la huruma humfurahisha.

26 Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki,

bali njia ya waovu huwapotosha.

27 Mtu mvivu haoki mawindo yake,

bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.

28 Katika njia ya haki kuna uzima;

katika mapito hayo kuna maisha ya milele.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/12-c450a442ab8087f82a1232c137345f3a.mp3?version_id=1627—

Mithali 13

Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu

1 Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye,

bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

2 Kutoka katika tunda la midomo yake

mtu hufurahia mambo mema,

bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri.

3 Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake,

bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia.

4 Mvivu hutamani sana na hapati kitu,

bali nafsi ya mwenye bidii

hutoshelezwa kikamilifu.

5 Mwenye haki huchukia uongo,

bali waovu huleta aibu na fedheha.

6 Haki humlinda mtu mwadilifu,

bali uovu humwangusha mwenye dhambi.

7 Mtu mmoja hujifanya tajiri,

kumbe hana kitu cho chote

mwingine hujifanya maskini,

kumbe ana utajiri mwingi.

8 Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake,

bali mtu maskini hasikii kitisho.

9 Nuru ya mwenye haki hung’aa sana,

bali taa ya mwovu itazimishwa.

10 Kiburi huzalisha magomvi tu,

bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

11 Fedha isiyo ya halali hupungua,

bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.

12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua,

bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.

13 Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi,

bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo.

14 Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima,

yamgeuzayo mtu kutoka mitego ya mauti.

15 Ufahamu mzuri hupata upendeleo,

bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.

16 Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa,

bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake.

17 Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu,

bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji.

18 Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu,

bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa.

19 Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi,

bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.

20 Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima,

bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.

21 Balaa humwandama mtenda dhambi,

bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki.

22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi,

bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa

kwa ajili ya wenye haki.

23 Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi,

bali dhuluma hukifutilia mbali.

24 Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe,

bali yeye ampendaye

huwa mwangalifu kumwadibisha.

25 Mwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake,

bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/13-060611124ec74cca55cfae5f484edb94.mp3?version_id=1627—

Mithali 14

1 Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,

bali mpumbavu huibomoa nyumba yake

kwa mikono yake mwenyewe.

2 Yeye ambaye njia zake ni nyofu humchaBwana,

bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.

3 Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake,

bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake.

4 Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,

bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.

5 Shahidi wa kweli hadanganyi,

bali shahidi wa uongo humimina uongo.

6 Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,

bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.

7 Kaa mbali na mtu mpumbavu,

kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.

8 Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake,

bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.

9 Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka katika dhambi,

bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.

10 Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe,

wala hakuna ye yote awezaye kushiriki furaha yake.

11 Nyumba ya mwovu itaangamizwa,

bali hema la mnyofu litastawi.

12 Iko njia ionekanayo sawa kwa mtu,

bali mwishoni huelekea mautini.

13 Hata katika kicheko moyo waweza kuuma,

nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.

14 Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao,

naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake.

15 Mtu mjinga huamini kila kitu,

bali mwenye busara hufikiria hatua zake.

16 Mtu mwenye hekima humchaBwanana kuepuka mabaya,

bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.

17 Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu,

naye mtu wa hila huchukiwa.

18 Mjinga hurithi upumbavu,

bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji.

19 Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema,

nao waovu kwenye malango ya wenye haki.

20 Maskini huepukwa hata na majirani zao,

bali matajiri wana marafiki wengi.

21 Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi,

bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji.

22 Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki?

Bali wale wanaopanga kilicho chema

hupata upendo na uaminifu.

23 Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida,

bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.

24 Utajiri wa wenye hekima ni taji yao,

bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu.

25 Shahidi wa kweli huokoa maisha,

bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu.

26 Yeye amchayeBwanaana ngome salama,

na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.

27 KumchaBwanani chemchemi ya uzima,

ikimwepusha mtu na mitego ya mauti.

28 Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme,

bali pasipo watu mkuu huangamia.

29 Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi,

bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu.

30 Moyo wenye amani huupa mwili uzima,

bali wivu huozesha mifupa.

31 Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao,

bali ye yote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.

32 Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu,

bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio.

33 Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu

bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu.

34 Haki huinua taifa,

bali dhambi ni aibu kwa watu wote.

35 Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima,

bali ghadhabu yake humwangukia

mtumishi mwenye kuaibisha.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/14-5194feb12439eb26dccdd9476ad8a5b1.mp3?version_id=1627—

Mithali 15

1 Jawabu la upole hugeuza ghadhabu,

bali neno liumizalo huchochea hasira.

2 Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa,

bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.

3 Macho yaBwanayako kila mahali,

yakiwaangalia waovu na wema.

4 Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima,

bali ulimi udanganyao huponda roho.

5 Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake,

bali ye yote akubaliye maonyo huonyesha busara.

6 Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa,

bali mapato ya waovu huwaletea taabu.

7 Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa,

bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.

8 Bwanahuchukia sana dhabihu za waovu,

bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu.

9 Bwanahuchukia sana njia ya waovu,

bali huwapenda wale wafuatao haki.

10 Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia,

yeye achukiaye maonyo atakufa.

11 Mauti na Uharibifuviko wazi mbele zaBwana,

je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu!

12 Mwenye mzaha huchukia maonyo,

hatataka shauri kwa mwenye hekima.

13 Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke,

bali maumivu ya moyoni huponda roho.

14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa,

bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu.

15 Siku zote za wanaoonewa ni za taabu,

bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu.

16 Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumchaBwana,

kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.

17 Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo

kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.

18 Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi,

bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.

19 Njia ya mvivu imezibwa na miiba,

bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu.

20 Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake,

bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.

21 Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili,

bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka.

22 Mipango hushindwa kufanikiwa kwa ajili ya kukosa ushauri,

bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa.

23 Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa,

ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake.

24 Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima

kumwepusha asiende chini kaburini.

25 Bwanahubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi,

bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

26 Bwanahuchukia sana mawazo ya mwovu,

bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye.

27 Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu,

bali yeye achukiaye rushwa ataishi.

28 Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake,

bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya.

29 Bwanayuko mbali na waovu,

bali husikia maombi ya wenye haki.

30 Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni,

nazo habari njema huipa mifupa afya.

31 Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima

atakuwa miongoni mwa wenye hekima.

32 Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe,

bali ye yote anayekubali maonyo hupata ufahamu.

33 KumchaBwanahumfundisha mtu hekima,

nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/15-c52a2eca0d6221c0df5a89dde7f38b77.mp3?version_id=1627—

Mithali 16

1 Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,

bali jibu la ulimi hutoka kwaBwana.

2 Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,

bali makusudi hupimwa naBwana.

3 MkabidhiBwanalo lote ufanyalo,

nayo mipango yako itafanikiwa.

4 Bwanahufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe,

hata waovu kwa siku ya maangamizi.

5 Bwanahuwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo.

Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.

6 Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa,

kwa kumchaBwanamtu hujiepusha na ubaya.

7 Njia za mtu zinapompendezaBwana,

huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.

8 Afadhali kitu kidogo pamoja na haki

kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.

9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake,

baliBwanahuelekeza hatua zake.

10 Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu,

wala kinywa chake hakipotoshi haki.

11 Vipimo na mizani za halali hutoka kwaBwana,

mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.

12 Wafalme huchukia sana kutenda maovu,

kwa maana kiti cha kifalme hufanywa imara kwa njia ya haki.

13 Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu,

humthamini mtu asemaye kweli.

14 Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti,

bali mtu mwenye hekima ataituliza.

15 Uso wa mfalme ung’aapo, ina inamaanisha uhai,

upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli.

16 Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu,

kuchagua ufahamu kuliko fedha!

17 Njia kuu ya wanyofu huepa ubaya,

yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.

18 Kiburi hutangulia maangamizi,

roho ya majivuno hutangulia maanguko.

19 Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho

miongoni mwa walioonewa

kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.

20 Ye yote anayekubali mafundisho hustawi,

tena amebarikiwa yeye anayemtumainiBwana.

21 Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu

na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho.

22 Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao,

bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu.

23 Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake,

na midomo yake huchochea mafundisho.

24 Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali,

ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,

bali mwisho wake huongoza mautini.

26 Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi,

njaa yake humsukuma aendelee.

27 Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya,

maneno yake ni kama moto uunguzao.

28 Mtu mpotovu huchochea ugomvi,

nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.

29 Mtu mkali humvuta jirani yake

na kumwongoza katika mapito yale mabaya.

30 Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu;

naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.

31 Mvi ni taji ya utukufu,

hupatikana kwa maisha ya uadilifu.

32 Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa,

mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.

33 Kura hupigwa kwa siri,

lakini kila uamuzi wake hutoka kwaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/16-6ee4b639d5294b7e69535e60cff92e21.mp3?version_id=1627—

Mithali 17

1 Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu

kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.

2 Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye,

naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.

3 Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu,

baliBwanahuujaribu moyo.

4 Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya,

mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.

5 Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake;

ye yote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.

6 Wana wa wana ni taji la wazee,

nao wazazi ni fahari ya watoto wao.

7 Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu,

ni mibaya kiasi gani midomo ya uongo kwa mtawala!

8 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho,

ko kote kigeukiapo, hufanikiwa.

9 Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,

bali ye yote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.

10 Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua

kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.

11 Mtu mbaya hupenda kuasi tu,

mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.

12 Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyang’anywa watoto wake,

kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.

13 Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema,

kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.

14 Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji,

kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.

15 Yeye asemaye asiye na haki ana haki,

naye asemaye mwenye haki hana haki,

Bwanahuwachukia sana wote wawili.

16 Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu,

wakati yeye hana haja ya kupata hekima?

17 Rafiki hupenda wakati wote

naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.

18 Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani

naye huweka dhamana kwa jirani yake.

19 Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi,

# naye ainuaye sana lango lakehutafuta uharibifu.

20 Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa;

naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu

huangukia kwenye taabu.

21 Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni,

hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.

22 Moyo wenye furaha ni dawa nzuri,

bali roho iliyonyong’onyea hukausha mifupa.

23 Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri,

ili kupotosha njia ya haki.

24 Mtu wa ufahamu huitazama hekima,

lakini macho ya mpumbavu huhangaika

hadi kwenye miisho ya dunia.

25 Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake

na uchungu kwa yeye aliyemzaa.

26 Sio vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia,

au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.

27 Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia,

naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.

28 Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza,

na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/17-a994f3777eb3a1d41931d0312be762c3.mp3?version_id=1627—

Mithali 18

1 Mtu ajitengaye na wengine

hufuata matakwa yake mwenyewe;

hupiga vita kila shauri jema.

2 Mpumbavu hafurahii ufahamu,

bali hufurahia kutangaza

maoni yake mwenyewe.

3 Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia,

pamoja na aibu huja lawama.

4 Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji,

bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.

5 Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu,

au kumnyima asiye na hatia haki.

6 Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi

na kinywa chake hualika kipigo.

7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake

na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.

8 Maneno ya uchongezi ni kama vyakula vitamu,

huingia sehemu za ndani sana za mtu.

9 Mtu aliye mlegevu katika kazi yake

ni ndugu na yule anayeharibu.

10 Jina laBwanani ngome imara,

wenye haki huikimbilia na kuwa salama.

11 Mali ya matajiri ni mji wao wa ngome,

wanaudhania kuwa ni ukuta usioweza kurukwa.

12 Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,

bali unyenyekevu hutangulia heshima.

13 Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza,

huo ni upumbavu wake na aibu yake.

14 Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa

bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?

15 Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa,

masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.

16 Zawadi humfungulia njia mtoaji,

nayo humleta mbele ya wakuu.

17 Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi,

hadi mwingine ajitokezapo na kumwuliza maswali.

18 Kupiga kura hukomesha mashindano

na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.

19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika

kuliko mji uliozungushiwa ngome,

nayo mabishano ni kama malango

ya ngome yenye makomeo.

20 Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,

atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.

21 Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,

nao waupendao watakula matunda yake.

22 Apataye mke apata kitu chema

naye ajipatia kibali kwaBwana.

23 Mtu maskini huomba kuhurumiwa

bali tajiri hujibu kwa ukali.

24 Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,

bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/18-d3e050454d824e01ec02c50d2a6a2997.mp3?version_id=1627—

Mithali 19

1 Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,

kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.

2 Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa,

wala kufanya haraka na kuikosa njia.

3 Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake

pamoja na hivyo moyo wake humkasirikiaBwana.

4 Mali huleta marafiki wengi,

bali rafiki wa mtu maskini humwacha.

5 Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,

naye amwagaye uongo hataachwa huru.

6 Wengi hujipendekeza kwa mtawala

na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi.

7 Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote:

Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani!

Ingawa huwafuata kwa kuwaomba,

hawapatikani po pote.

8 Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,

yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.

9 Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,

naye amwagaye uongo ataangamia.

10 Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa,

itakuwa vibaya kiasi gani

kwa mtumwa kuwatawala wakuu.

11 Hekima ya mtu humpa uvumilivu,

ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.

12 Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba,

bali wema wake ni kama umande juu ya majani.

13 Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye,

naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

14 Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi,

bali mke mwenye busara hutoka kwaBwana.

15 Uvivu huleta usingizi mzito,

naye mtu mzembe huona njaa.

16 Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake,

bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.

17 Yeye amhurumiaye maskini humkopeshaBwana,

naye atamtuza kwa aliyotenda.

18 Mrudi mwanao, wakati bado liko tumaini,

wala nafsi yako isifadhaike kwa kulia kwake.

19 Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake,

kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena.

20 Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho,

nawe mwishoni utakuwa na hekima.

21 Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,

lakini kusudi laBwanandilo litakalosimama.

22 Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,

afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.

23 KumchaBwanahuongoza kwenye uzima,

kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,

bila kuguswa na shida.

24 Mtu mvivu huuzamisha mkono wake kwenye sahani,

lakini hawezi hata kuurudisha kwenye kinywa chake!

25 Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara,

mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa.

26 Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake

ni mwana aletaye aibu na fedheha.

27 Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho,

utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.

28 Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu

na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi.

29 Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka

na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/19-2f7e927166d3a73c11878213239c7df2.mp3?version_id=1627—

Mithali 20

1 Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi;

ye yote apotoshwaye navyo hana hekima.

2 Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;

yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake.

3 Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi,

bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.

4 Mvivu halimi kwa majira;

kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama

lakini hapati cho chote.

5 Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina,

lakini mtu mwenye ufahamu huyachota.

6 Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma,

bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?

7 Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,

wamebarikiwa watoto wake baada yake.

8 Wakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu,

hupepeta ubaya wote kwa macho yake.

9 Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi;

mimi ni safi na sina dhambi?”

10 Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti,

Bwanahuchukia vyote viwili.

11 Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,

kama tabia yake ni safi na adili.

12 Masikio yasikiayo na macho yaonayo,

Bwanandiye aliyevifanya vyote viwili.

13 Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini,

uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.

14 “Haifai, haifai!” asema mnunuzi,

kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.

15 Kuna dhahabu na marijani kwa wingi,

lakini midomo inenayo maarifa

ni kito cha thamani kilicho adimu.

16 Chukua vazi la yule amdhaminiye mgeni;

lishike kuwa rehani kama atafanya hivyo

kwa mwanamke mgeni.

17 Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu,

bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.

18 Fanya mipango kwa kutafuta mashauri,

ukipigana vita, tafuta maelekezo.

19 Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika,

kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.

20 Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake,

taa yake itazimwa katika giza nene.

21 Urithi upatikanao haraka mwanzoni,

hautabarikiwa mwishoni.

22 Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!”

MngojeeBwana, naye atakuokoa.

23 Bwanaanachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu,

nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.

24 Hatua za mtu huongozwa naBwana.

Anawezaje basi mtu ye yote kuelewa njia yake mwenyewe?

25 Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka

na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.

26 Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu,

hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.

27 Taa yaBwanahuchunguza roho ya mwanadamu,

huchunguza utu wake wa ndani.

28 Upendo na uaminifu humweka mfalme salama,

kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama.

29 Utukufu wa vijana ni nguvu zao,

mvi ni fahari ya uzee.

30 Mapigo na majeraha huusafisha ubaya,

nayo michapo hutakasa utu wa ndani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PRO/20-07e2a2ebb2a83ee79afd3453be8d1db7.mp3?version_id=1627—