Zaburi 150

Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake

1 MsifuniBwana.

Msifuni Mungu katika patakatifu pake,

msifuni katika mbingu zake kuu.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu,

msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,

msifuni kwa kinubi na zeze,

4 Msifuni kwa matari na kucheza,

msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

5 Msifuni kwa matoazi yaliayo,

msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila chenye pumzi na kimsifuBwana.

MsifuniBwana. Haleluya!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/150-cc95c5b1e920e3320c0de853056acb58.mp3?version_id=1627—

Ayubu 1

Ayubu Na Jamaa Yake

1 Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye jina lake aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu, alimcha Mungu na kuepuka ubaya.

2 Alikuwa na wana saba na binti watatu,

3 naye alikuwa na kondoo 7,000, ngamia 3,000, jozi 500 za maksai, punda 500, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki.

4 Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika ndugu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao.

5 Wakati kipindi cha karamu kimemalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu.

Jaribu La Kwanza La Ayubu

6 Siku moja wana wa Munguwalikwenda kujionyesha mbele zaBwana. Shetaninaye akaja pamoja nao.

7 Bwanaakamwambia Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibuBwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

8 NdipoBwanaakamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Mtu ambaye hakuna mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.”

9 Shetani akajibu, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure?

10 Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima.

11 Lakini nyosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

12 Bwanaakamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.”

Ndipo Shetani akatoka mbele zaBwana.

13 Siku moja watoto wa Ayubu walipokuwa wakifanya karamu wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,

14 akaja mjumbe kwa Ayubu na kusema, “Maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakilisha karibu nao,

15 Waseba wakawashambulia na kuchukua mifugo. Kisha wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

16 Wakati alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Moto wa Mungu ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kondoo na watumishi, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

17 Wakati alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.”

18 Wakati alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wana wako na binti zako walipokuwa wakifanya karamu, wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,

19 ghafula upepo wenye nguvu ukavuma kutoka jangwani, nao ukaipiga nyumba hiyo pembe zake nne. Ikawaangukia hao watoto nao wamekufa, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

20 Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu

21 na kusema:

“Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,

# nami nitaondoka uchi,

Bwanaalinipa, nayeBwanaameviondoa,

jina laBwanalitukuzwe.”

22 Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi, wala kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/1-f86d4ff6207168828cc8bcb99d7b9655.mp3?version_id=1627—

Ayubu 2

Jaribu La Pili La Ayubu

1 Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele zaBwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake.

2 Bwanaakamwuliza Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibuBwana“Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

3 Bwanaakamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Mtu ambaye hakuna mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado mpaka sasa anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”

4 Shetani akajibu, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake.

5 Lakini nyosha mkono wako na kuipiga nyama yake na mifupa yake, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

6 Bwanaakamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, yeye yumo mikononi mwako, lakini lazima umuachie uhai wake.”

7 Basi Shetani akatoka mbele zaBwananaye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa.

8 Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu.

9 Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”

10 Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavuye yote angelinena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kusema kwake.

Marafiki Watatu Wa Ayubu

11 Basi marafiki watatu wa Ayubu, Elifazi, Mtemani na Bildadi, Mshuhi na Sofari, Mnaamathi waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka majumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji.

12 Walipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua, wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao.

13 Kisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba mchana na usiku. Hakuna ye yote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/2-fc6d18042f3d3806c85f9523944f0fb0.mp3?version_id=1627—

Ayubu 3

Hotuba Ya Kwanza Ya Ayubu

1 Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.

2 Akasema:

3 “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali,

nao usiku ule iliposemekana,

‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’

4 Siku ile na iwe giza,

Mungu juu na asiiangalie,

nayo nuru isiiangazie.

5 Giza na kivuli kikuu kiikalie tena,

wingu na likae juu yake,

weusi na uifunike nuru yake.

6 Usiku ule na ushikwe na giza kuu,

usihesabiwe katika siku za mwaka,

wala usihesabiwe katika siku

za mwezi wo wote.

7 Usiku ule na uwe tasa,

sauti ya furaha na isisikike ndani yake.

8 Wale wazilaanio siku, wailaani hiyo siku,

wale walio tayari

# kumwamsha Lewiathani.

9 Nyota zake za alfajiri na ziwe giza,

nao ungojee mwanga bila mafanikio,

wala usiuone muonzi wa kwanza

wa mapambazuko,

10 kwa sababu huo usiku haukunifungia

mlango wa tumbo la mama yangu,

ili kuyaficha macho yangu

kutokana na taabu.

11 “Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa?

Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?

12 Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea

na matiti ili nipate kunyonyeshwa?

13 Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani,

ningekuwa nimelala na kupumzika

14 pamoja na wafalme na washauri wa dunia,

waliojijengea kwa ajili yao mahali

ambapo sasa ni magofu,

15 pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu,

waliozijaza nyumba zao kwa fedha.

16 Au kwa nini sikufichwa ardhini

kama mtoto aliyezaliwa mfu,

kama mtoto mchanga ambaye

kamwe hakuuona mwanga?

17 Huko waovu huacha kusumbua

na huko waliochoka hupumzika.

18 Wafungwa nao hufurahia utulivu wao,

hawasikii tena sauti ya kukemea

ya kiongozi wa watumwa.

19 Wadogo na wakubwa wamo humo,

na mtumwa ameachiwa huru

kutoka kwa bwana wake.

20 “Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni

na hao wenye uchungu kupewa uhai?

21 Kwa nini wale wanaotamani kufa hilo haliji,

wale watafutao kufa

zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa,

22 ambao hujawa na furaha

na shangwe wafikapo kaburini?

23 Kwa nini uhai hupewa mtu

ambaye njia yake imefichika,

ambaye Mungu amemzungushia boma?

24 Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu

kwanijia badala ya chakula;

mlio wangu wa kusononeka

unamwagika kama maji.

25 Lile nililokuwa naliogopa limenijia;

lile nililokuwa ninalihofia limenipata.

26 Sina amani, wala utulivu;

sina pumziko, bali taabu tu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/3-2b7b03cbd95c9324befdebee068f04d2.mp3?version_id=1627—

Ayubu 4

Elifazi Anazungumza: Ayubu Ametenda Dhambi

1 Ndipo Elifazi, Mtemani akajibu:

2 “Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe,

kutakukasirisha?

Lakini ni nani awezaye

kujizuia asiseme?

3 Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi,

jinsi ambavyo umeitia nguvu

mikono iliyokuwa dhaifu.

4 Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa,

umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.

5 Lakini sasa hii taabu imekujia wewe,

nawe unashuka moyo,

imekupiga wewe,

nawe unafadhaika.

6 Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa

ndiyo matumaini yako

na njia zako kutokuwa na lawama

ndilo taraja lako?

7 “Fikiri sasa: Ni mtu yupi, asiye na hatia,

ambaye aliwahi kuangamia?

Ni wapi ambapo wanyofu

waliwahi kuangamizwa?

8 Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza,

wale walimao ubaya

na wale hupanda uovu,

huvuna yayo hayo.

9 Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa,

kwa mshindo wa hasira zake huangamia.

10 Simba anaweza kunguruma na kukoroma,

lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika.

11 Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo,

nao wanasimba wa simba jike hutawanyika.

12 “Neno lililetwa kwangu kwa siri,

masikio yangu yakasikia mnong’ono wake.

13 Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku,

hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu,

14 hofu na kutetemeka kulinishika

na kufanya mifupa yangu yote itetemeke.

15 Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu,

nazo nywele za mwili wangu zikasimama.

16 Yule roho akasimama,

lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani.

Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu,

kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti:

17 ‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu?

Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?

18 Kama Mungu hawaamini watumishi wake,

kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,

19 ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba

za udongo wa mfinyanzi,

ambazo misingi yake ipo mavumbini,

ambao wamepondwa kama nondo!

20 Kati ya maawio na machweo

huvunjwa vipande vipande,

bila ye yote kutambua,

huangamia milele.

21 Je, kamba za hema yao hazikung’olewa,

hivyo hufa bila hekima?’

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/4-86b253121a8a1580812f68757ea04d7d.mp3?version_id=1627—

Ayubu 5

Elifazi Anaendelea

1 “Ita kama unataka, lakini ni nani atakayekujibu?

Ni yupi kati ya hao watakatifu utakayemgeukia?

2 Kuweka uchungu moyoni humwua mpumbavu,

nao wivu humchinja mjinga.

3 Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akistawi,

lakini ghafula nyumba yake ikawa imelaaniwa.

4 Watoto wake wako mbali na usalama,

hushindwa mahakamani bila mtetezi.

5 Wenye njaa huyala mavuno yake,

wakiyatoa hata katikati ya miiba,

nao wenye kiu huitamani sana mali yake.

6 Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo,

wala udhia hauchipui kutoka ardhini.

7 Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika,

kwa hakika kama cheche ya moto

irukayo kuelekea juu.

8 “Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu,

ningeliweka shauri langu mbele zake.

9 Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa,

miujiza isiyoweza kuhesabika.

10 Yeye huipa nchi mvua,

huyapeleka maji kunyesha mashamba.

11 Huwainua juu wanyonge,

nao wale waombolezao

huinuliwa wakawa salama.

12 Huipinga mipango ya wenye hila,

ili mikono yao isifikie ufanisi.

13 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao,

nayo mipango ya wadanganyifu

huifagilia mbali.

14 Giza huwapata wakati wa mchana,

wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku.

15 Humwokoa mhitaji kutokana

na upanga ulioko kinywani mwao,

huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu.

16 Kwa hiyo maskini analo tarajio,

nao udhalimu hufumba kinywa chake.

17 “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi,

# kwa hiyo usidharau marudi yake Mwenyezi.

18 Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga,

huumiza, lakini mikono yake pia huponya.

19 Kutoka katika majanga sita yeye atakuokoa,

naam, hata katika saba hakuna dhara

litakalokupata wewe.

20 Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo,

naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.

21 Utalindwa kutokana na kuchapa kwa ulimi,

wala hutakuwa na sababu ya kuogopa

maangamizi yatakapokujia.

22 Utayacheka maangamizo na njaa,

wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa

wanyama wakali wa mwituni.

23 Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba,

nao wanyama wa mwitu

watakuwa na amani nawe.

24 Utajua ya kwamba hema lako li salama,

utahesabu mali zako

wala hutakuta cho chote kilichopungua.

25 Utajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi,

nao wazao wako wengi kama majani ya nchi.

26 Utaingia kaburini ukiwa na umri wa uzee mtimilifu,

kama masuke ya ngano yakusanywapo kwa wakati wake.

27 “Tumelichunguza hili, nalo ni kweli,

hivyo lisikie na ulitendee kazi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/5-6d8359bc47546ef08b10cdb0bbcfb694.mp3?version_id=1627—

Ayubu 6

Ayubu Anajibu: Malalamiko Yangu Ni Ya Haki

1 Kisha Ayubu akajibu:

2 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa,

nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani!

3 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote,

kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka.

4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu,

roho yangu inakunywa sumu yake,

vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.

5 Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani,

au ng’ombe dume hulia akiwa na chakula?

6 Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi,

au upo utamu katika ute mweupe wa yai?

7 Ninakataa kuvigusa,

vyakula vya aina hii hunichukiza.

8 “Laiti ningepata haja yangu,

kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,

9 kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda,

kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali!

10 Ndipo bado ningekuwa na hii faraja,

bado ningekuwa na furaha katika maumivu makali:

kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu.

11 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini?

Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu?

12 Je, mimi nina nguvu za jiwe?

Je, mwili wangu ni shaba?

13 Je, ninao uwezo wo wote wa kujisaidia mimi mwenyewe,

wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami?

14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,

hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.

15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,

ni kama vijito vya msimu,

ni kama vijito ambavyo hufurika

16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo

ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,

17 lakini hukauka majira ya ukame,

na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.

18 Misafara hugeuka kutoka katika njia zake,

hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia.

19 Misafara ya Tema inatafuta maji,

wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri

hutazama kwa matarajio.

20 Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini,

walipofika huko, wakahuzunika

kwa kukosa walichotarajia.

21 Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wo wote,

mnaona jambo la kutisha nanyi mnaogopa.

22 Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu,

au mnilipie fidia kutoka katika mali zenu,

23 au niokoeni mikononi mwa adui,

au nikomboeni kutoka kwenye makucha

ya wasio na huruma’?

24 “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya,

nionyesheni nilikokosea.

25 Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli!

Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini?

26 Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema,

na kuyafanya maneno ya mtu

anayekata tamaa kama upepo?

27 Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima

na kubadilishana rafiki yenu na mali.

28 “Lakini sasa iweni na huruma mkaniangalie mimi.

Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu?

29 Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu;

# angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu.

30 Je, pana uovu wo wote midomoni mwangu?

Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila?

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/6-a917806091f902715f12b0b700f6fcc5.mp3?version_id=1627—

Ayubu 7

Ayubu: Mateso Yangu Hayana Mwisho

1 “Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani?

Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa?

2 Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni,

au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake,

3 ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili,

nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku.

4 Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’

Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko.

5 Mwili wangu umevikwa mabuu na uchafu,

ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha.

Ayubu Anamlilia Mungu

6 “Siku zangu zinapita upesi kuliko pia ya mashine ya kufuma,

nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini.

7 Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi,

macho yangu kamwe hayataona tena raha.

8 Lile jicho linaloniona sasa halitaniona tena,

utanitafuta, wala sitakuwapo.

9 Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka,

# vivyo hivyo yeye ashukaye kaburiniharudi tena.

10 Kamwe harudi tena kwenye nyumba yake,

wala mahali pake hapatamjua tena.

11 “Kwa hiyo sitanyamaza;

nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu,

nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.

12 Je, mimi ni bahari au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini,

hata uniweke chini ya ulinzi?

13 Ninapofikiri kwamba kitanda changu kitanifariji,

nacho kiti changu cha fahari kitapunguza malalamiko yangu,

14 ndipo wanitisha kwa ndoto

na kunitia hofu kwa maono,

15 hivyo ninachagua kujinyonga na kufa,

kuliko huu mwili wangu.

16 Ninayachukia maisha yangu, nisingetamani kuendelea kuishi.

Niache, siku zangu ni ubatili.

17 “Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki,

kwamba unamtia sana maanani,

18 kwamba unamwangalia kila asubuhi

na kumjaribu kila wakati?

19 Je, hutaacha kamwe kunitazama,

au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?

20 Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini,

Ewe mlinzi wa wanadamu?

Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako?

Je, nimekuwa mzigo kwako?

21 Kwa nini husamehi makosa yangu

na kuachilia dhambi zangu?

Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini,

nawe utanitafuta, wala sitakuwapo.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/7-b81b95687814edd432a2870bc7b0273f.mp3?version_id=1627—

Ayubu 8

Bildadi Anasema: Yampasa Ayubu Atubu

1 Kisha Bildadi, Mshuhi akajibu:

2 “Hata lini wewe utasema mambo kama haya?

Maneno yako ni kama upepo mkuu.

3 Je, Mungu hupotosha hukumu?

Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?

4 Watoto wako walipomtenda dhambi,

aliwapa adhabu ya dhambi yao.

5 Lakini ukimtafuta Mungu,

nawe ukamsihi Mwenyezi,

6 ikiwa wewe ni safi na mnyofu,

hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako

na kukurudisha katika mahali pako pa haki.

7 Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo,

lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.

8 “Ukaulize vizazi vilivyotangulia

na uone baba zao walijifunza nini,

9 kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lo lote,

nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.

10 Je, hawatakufundisha na kukueleza?

Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?

11 Je, mafunjoyaweza kumea mahali pasipo na matope?

Matete yaweza kustawi bila maji?

12 Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa,

hunyauka haraka kuliko majani mengine.

13 Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu,

vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.

14 Lile analolitumainia huvunjika upesi,

lile analolitegemea ni utando wa buibui.

15 Huutegemea utando wake, lakini hausimami,

huung’ang’ania, lakini haudumu.

16 Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua,

ukieneza machipukizi yake bustanini,

17 huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe

na kutafuta nafasi katikati ya mawe.

18 Unapong’olewa kutoka mahali pake,

ndipo mahali pale huukana na kusema,

‘Mimi kamwe sikukuona.’

19 Hakika uhai wake hunyauka

na kutoka udongoni mimea mingine huota.

20 “Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia

wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya.

21 Bado atakijaza kinywa chako na kicheko

na midomo yako na kelele za shangwe.

22 Adui zako watavikwa aibu,

nazo hema za waovu hazitakuwapo tena.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/8-8e5202493c50f57ae42df252e4d54581.mp3?version_id=1627—

Ayubu 9

Hakuna Mpatanishi

1 Kisha Ayubu akajibu:

2 “Naam, najua hili ni kweli.

Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?

3 Ingawa mtu angetaka kushindana naye,

asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.

4 Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno.

Ni nani aliyempinga naye akawa salama?

5 Aiondoa milima bila yenyewe kujua

na kuipindua kwa hasira yake.

6 Aitikisa dunia kutoka mahali pake

na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.

7 Husema na jua nalo likaacha kuangaza,

naye huizima mianga ya nyota.

8 Yeye peke yake huzitandaza mbingu

na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.

9 Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubuna Orioni,

# Kilimiana kundi la nyota za kusini.

10 Hutenda maajabu yasiyopimika,

miujiza isiyoweza kuhesabiwa.

11 Anapopita karibu nami, siwezi kumwona,

apitapo mbele yangu, simtambui.

12 Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia?

Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’

13 Mungu hataizuia hasira yake,

# hata jeshi kubwa la Rahabulenye nguvu

linajikunyata miguuni pake.

14 “Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye?

Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye?

15 Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu;

ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.

16 Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali,

siamini kama angenisikiliza.

17 Yeye angeniangamiza kwa dhoruba

na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.

18 Asingeniacha nipumue

bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.

19 Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu!

Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?

20 Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu;

kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.

21 “Ingawa mimi sina kosa,

haileti tofauti katika nafsi yangu;

nauchukia uhai wangu.

22 Hayo yote ni sawa, ndiyo sababu nasema,

‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’

23 Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula,

yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa.

24 Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu,

yeye huwafunga macho mahakimu wake.

Kama si yeye, basi ni nani?

25 “Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji,

zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo tu.

26 Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo,

mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.

27 Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu,

nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’

28 bado ninahofia mateso yangu yote,

kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.

29 Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia,

kwa nini basi nitaabishwe bure?

30 Hata kama ningejiosha kwa sabuni

na kutakasa mikono yangu kwa magadi,

31 wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi

kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

32 “Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu,

ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.

33 Laiti angelikuwapo mtu wa kutupatanisha kati yetu,

aweke mkono wake juu yetu sote wawili,

34 mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu,

ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.

35 Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa,

lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/9-13876cc46d0e381c17459d52de98778f.mp3?version_id=1627—