Ayubu 40

1 Bwanaakamwambia Ayubu:

2 “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha?

Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”

3 Ndipo Ayubu akamjibuBwana:

4 “Mimi sistahili kabisa, ninawezaje kukujibu wewe?

Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.

5 Nimesema mara moja, lakini sina jibu;

naam, nimesema mara mbili,

lakini sitasema tena.”

6 NdipoBwanaakasema na Ayubu kutoka katika upepo wa kisulisuli:

7 “Jikaze kama mwanaume;

nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.

8 “Je, utabatilisha hukumu yangu?

Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?

9 Je, una mkono kama wa Mungu,

nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?

10 Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari,

nawe uvae heshima na enzi.

11 Fungulia ukali wa ghadhabu yako,

mtafute kila mwenye kiburi umshushe,

12 mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze,

waponde waovu mahali wasimamapo.

13 Wazike wote mavumbini pamoja,

wafunge nyuso zao kaburini.

14 Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa

mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.

15 “Mwangalie kiboko, niliyemwumba kama nilivyokuumba wewe,

ambaye anajilisha kwa majani kama ng’ombe.

16 Tazama basi, nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake,

uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!

17 Mkia wake hutikisika kama mwerezi,

mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.

18 Mifupa yake ni bomba za shaba,

maungo yake ni kama fito za chuma.

19 Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu,

lakini Muumba wake anaweza

kumsogelea kwa upanga wake.

20 Vilima humletea yeye mazao yake,

nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.

21 Hulala chini ya mimea ya yungiyungi,

katika maficho ya matete kwenye matope.

22 Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake;

miti mirefu karibu na kijito humzunguka.

23 Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu;

yeye yu salama, hata kama Yordani

ingefurika hadi kwenye kinywa chake.

24 Je, mtu ye yote anaweza kumkamata yeye akiwa macho,

au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/40-9a82a235af97c35ef4e9bdfbd9bb1399.mp3?version_id=1627—

Ayubu 41

1 “Je, waweza kumvua Lewiathanikwa ndoano ya samaki

au kufunga ulimi wake kwa kamba?

2 Waweza kupitisha kamba puani mwake

au kutoboa taya lake kwa kulabu?

3 Je, ataendelea kukuomba umhurumie?

Atasema nawe maneno ya upole?

4 Je, atafanya agano nawe ili umtwae

awe mtumishi wako maisha yake yote?

5 Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege,

au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?

6 Je, wafanya biashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake?

Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?

7 Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali,

au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?

8 Kama ukiweka mkono wako juu yake,

utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena!

9 Tumaini lo lote la kumtiisha ni kujidanganya,

kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.

10 Hakuna ye yote aliye mkali athubutuye kumchokoza.

Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu Mimi?

11 Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa?

Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.

12 “Sitashindwa kunena juu ya maungo yake,

nguvu zake na umbo lake zuri.

13 Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje?

Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?

14 Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake,

kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?

15 Mgongo wake una safu za ngao

zilizoshikamanishwa imara pamoja,

16 kila moja i karibu sana na mwenzake

wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.

17 Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine,

zimeng’ang’aniana pamoja

wala haziwezi kutenganishwa.

18 Akipiga chafya mwanga humetameta,

macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.

19 Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake,

cheche za moto huruka nje.

20 Moshi hufuka kutoka puani mwake,

kama kutoka kwenye chungu

kinachotokota kwa moto wa matete.

21 Pumzi yake huwasha makaa ya mawe,

nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.

22 Nguvu hukaa katika shingo yake,

utisho hutangulia mbele yake.

23 Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja,

iko imara na haiwezi kuondolewa.

24 Kifua chake ni kigumu kama mwamba,

kigumu kama jiwe la chini la kusagia.

25 Ainukapo, wenye nguvu wanaogopa,

wenye nguvu hurudi nyuma mbele yake

anapokwenda kwa kishindo.

26 Upanga unaomfikia haumdhuru,

wala mkuki au mshale wala fumo.

27 Chuma hukiona kama unyasi

na shaba kama mti uliooza.

28 Mishale haimfanyi yeye akimbie;

mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.

29 Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu;

hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.

30 Sehemu zake za chini kwenye tumbo

zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu,

zikiacha mburuzo kwenye matope

kama chombo chenye meno cha kupuria.

31 Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo

na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu.

32 Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta;

mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi.

33 Hakuna cho chote duniani kinacholingana naye,

kiumbe kisicho na woga.

34 Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna;

yeye ni mfalme juu ya wale wote wenye kiburi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/41-b80ee188812911100ed0a7552396d5a7.mp3?version_id=1627—

Ayubu 42

Ayubu Anamjibu Bwana

1 Ndipo Ayubu akamjibuBwana:

2 “Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,

wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

3 Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’

Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi,

mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.

4 “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;

nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’

5 Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,

lakini sasa macho yangu yamekuona.

6 Kwa hiyo najidharau mwenyewe

na kutubu katika mavumbi na majivu.”

Mwisho: Marafiki Wa Ayubu Wanafedheheshwa

7 Baada yaBwanakusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi, Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.

8 Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo waume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.”

9 Kwa hiyo Elifazi, Mtemani, Bildadi, Mshuhi na Sofari, Mnaamathi wakafanya kamaBwanaalivyowaambia; nayeBwanaakayakubali maombi ya Ayubu.

10 Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake,Bwanaakamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo kabla.

11 Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu kabla, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yoteBwanaaliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.

12 Bwanaakaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo 14,000, ngamia 6,000, jozi za mafahali 1,000 na punda wa kike 1,000.

13 Tena alikuwa na wana saba na binti watatu.

14 Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki.

15 Hapakuwepo mahali po pote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao.

16 Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne.

17 Hivyo Ayubu akafa, mzee sana naye ameshiba siku.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/42-f4f15620604b73cc5f955b360bb8d163.mp3?version_id=1627—

Esta 1

Malkia Vashti Aondolewa

1 Hili ndilo lililotokea wakati wa utawala wa Mfalme Ahusuero ambaye alitawala juu ya majimbo mia na ishirini na saba tangu Bara Hindi mpaka Kushi.

2 Wakati huo Mfalme Ahusuero alipotawala katika kiti chake cha enzi kilikuwa katika ngome ya mji wa Shushani,

3 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo.

4 Kwa siku zote 180 mfalme alionyesha utajiri mwingi wa ufalme wake, fahari na utukufu wa enzi yake.

5 Siku hizo zilipopita, ndipo mfalme alifanya karamu kwa muda wa siku saba, katika bustani ya ndani katika jumba la kifalme, kwa ajili ya watu wote kuanzia mdogo hadi mkubwa, ambao walikuwa katika ngome ya mji wa Shushani.

6 Bustani iliyokuwa na mapazia ya kitani nyeupe na buluu, yaliyofungiwa kamba za kitani nyeupe na kitambaa cha zambarau, kwenye pete za fedha juu ya nguzo za marmar. Kulikuwepo viti vya dhahabu na vya fedha vilivyokuwa vimewekwa kwenye ile sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi, marmar, lulumizi na mawe mengine ya thamani.

7 Vyombo vya dhahabu vilitumika kwa watu kunywea mvinyo, kila kimoja tofauti na kingine, naye mfalme akatoa mvinyo kwa wingi kwa kadiri ya ukarimu wake.

8 Kwa amri ya mfalme kila mgeni aliruhusiwa kunywa alichotaka, kwa kuwa mfalme alitoa maagizo kwa watumishi wote wa kuhudumu mvinyo kumhudumia kila mtu kwa jinsi alivyotaka.

9 Malkia Vashti pia akawafanyia wanawake karamu katika jumba la kifalme la Mfalme Ahusuero.

10 Siku ya saba, wakati Mfalme Ahusuero alipokuwa amesisimka roho yake kwa mvinyo, aliamuru matowashi saba ambao walikuwa wakimhudumia, yaani, Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi,

11 kumleta Malkia Vashti mbele ya mfalme akiwa amevaa taji lake la kifalme, ili aonyeshe uzuri wake kwa watu na wakuu, kwa kuwa alikuwa ni mzuri wa kupendeza.

12 Lakini wakati watumishi walipotoa amri ya mfalme, Malkia Vashti alikataa kuja. Ndipo mfalme alighadhibika na hasira ikawaka.

13 Kwa kuwa ilikuwa desturi ya mfalme kupata ushauri kwa wataalamu katika mambo ya sheria na haki, alizungumza na watu wenye busara, ambao walijua nyakati,

14 nao waliokuwa karibu na mfalme ni Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Meresi, Marsena na Memukani, wakuu saba wa Uajemi na Umedi ambao walikuwa na nafasi ya pekee kwa mfalme nao walikuwa na vyeo vya juu kabisa katika utawala wake.

15 Mfalme akauliza, “Kulingana na sheria, Malkia Vashti anapaswa atendewe nini? Malkia hakutii amri ya Mfalme Ahusuero ambayo matowashi walimpelekea.”

16 Kisha Memukani akajibu mbele ya mfalme na wakuu, “Malkia Vashti si kwamba amemkosea mfalme tu bali pia amewakosea wakuu wote na watu wa himaya yote ya Mfalme Ahusuero.

17 Kwa maana tendo hili la malkia litajulikana kwa wanawake wote, kwa hiyo watawadharau waume zao na kusema, ‘Mfalme Ahusuero aliagiza Malkia Vashti aletwe mbele yake, lakini alikataa.’

18 Leo hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi ambao wamesikia juu ya tabia ya malkia watawatendea wakuu wote wa mfalme vivyo hivyo. Hapatakuwepo na mwisho wa dharau na magomvi.

19 “Kwa hiyo, kama itampendeza mfalme, atoe amri ya kifalme na iandikwe katika sheria ya Uajemi na Umedi, ambayo haitakaa ibadilike, kwamba Vashti kamwe asije tena mbele ya Mfalme Ahusuero. Pia mfalme na atoe hiyo nafasi yake ya umalkia kwa mwanamke mwingine aliye bora kuliko yeye.

20 Kisha wakati mbiu hii ya mfalme itakapotangazwa katika himaya yake iliyo kubwa sana, wanawake wote watawaheshimu waume zao, kuanzia mdogo hadi mkubwa.”

21 Mfalme na wakuu wake walipendezwa na shauri hili, mfalme akafanya kama Memukani alivyopendekeza.

22 Alipeleka barua katika sehemu zote za ufalme wake, kwa kila jimbo kwa maandishi yake mwenyewe na kwa kila watu katika lugha yao wenyewe, akitangaza kwa msemo wa kila watu kwamba inampasa kila mwanaume kuwa mtawala wa nyumba yake mwenyewe.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EST/1-0266356e88d9c1ec20e94ae51896bee8.mp3?version_id=1627—

Esta 2

Esta Afanywa Malkia

1 Baadaye, wakati hasira ya Mfalme Ahusuero ilipokuwa imetulia, alimkumbuka Vashti na kile alichokuwa amekifanya na alilokuwa ameamuru juu yake.

2 Kisha watumishi waliomhudumia mfalme walipendekeza, “Na ufanyike utafiti kwa ajili ya wanawali mabikira wazuri wa sura kwa ajili ya mfalme.

3 Mfalme na ateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake kuwaleta hao wanawali wote wazuri wa sura katika nyumba ya wanawake na masuria katika ngome ya mji wa Shushani. Kisha wawekwe chini ya utunzaji wa Hegai, towashi wa mfalme, ambaye ndiye kiongozi wa wanawake, na wapewe matunzo yote ya urembo.

4 Kisha yule ambaye atampendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti.” Shauri hili likampendeza mfalme, naye akalifuata.

5 Basi katika mji wa ngome ya Shushani palikuwa na Myahudi wa kabila ya Benyamini, jina lake Mordekai mwana wa Yairi, mwana wa Shimei, mwana wa Kishi,

6 ambao walichukuliwa uhamishoni kutoka Yerusalemu na Mfalme Nebukadneza wa Babeli, wakiwa miongoni mwa waliochukuliwa mateka pamoja na Mfalme Yekonia wa Yuda.

7 Mordekai alikuwa na binamu yake msichana aliyeitwa Hadasa, ambaye alimlea kwa kuwa hakuwa na baba wala mama. Msichana huyu, ambaye pia alijulikana kwa jina la Esta, alikuwa na umbo na sura ya kupendeza, naye Mordekai alimtunza kama binti yake mwenyewe baada ya baba yake na mama yake kufariki.

8 Wakati agizo na amri ya mfalme lilipotangazwa, wanawali wengi waliletwa kwenye ngome ya mji wa Shushani na kuwekwa chini ya uangalizi wa Hegai. Pia Esta alipelekwa katika jumba la mfalme na akakabidhiwa Hegai, ambaye alikuwa mkuu wa nyumba ya wanawake na masuria.

9 Msichana huyu alimpendeza mfalme na kupata kibali mbele zake. Mara moja akaanza kumpa matunzo ya uzuri na chakula maalum. Alimpa Esta vijakazi saba waliochaguliwa kutoka katika jumba la kifalme na kumhamishia yeye pamoja na vijakazi wake katika sehemu bora zaidi katika nyumba ya wanawake na masuria.

10 Esta alikuwa hajadhihirisha uraia wala kabila lake, kwa sababu Mordekai alikuwa amemkataza.

11 Kila siku Mordekai alikuwa akitembea tembea karibu na ua wa nyumba ya wanawake na masuria kuona jinsi Esta anavyoendelea na kuona yaliyokuwa yakitendeka kwake.

12 Kabla zamu ya msichana haijafika ya kwenda kwa Mfalme Ahusuero, ilimbidi atimize miezi kumi na miwili ya matunzo ya urembo kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa miezi sita walikuwa wajipake mafuta ya manemane na miezi sita ya kujipaka manukato na vipodozi.

13 Basi hivi ndivyo ambavyo Esta angeingia kwa mfalme: Kila kitu alichohitaji aliruhusiwa kuchukua kutoka katika nyumba ya wanawake na masuria na kwenda navyo katika jumba la mfalme.

14 Jioni angekwenda pale na asubuhi kurudi sehemu nyingine ya nyumba ya wanawake na masuria katika utunzaji wa Shaashgazi, towashi wa mfalme ambaye alikuwa mkuu wa masuria. Hangeweza kurudi kwa mfalme mpaka apendezwe naye na kuagiza aitwe kwa jina lake.

15 Wakati zamu ya Esta ilipofika kwenda kwa mfalme (msichana ambaye Mordekai alikuwa amemlea, naye ni binti wa Abihaili mjomba wake) Esta hakutaka vitu zaidi ya vile ambavyo Hegai towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake na masuria alivyokuwa ameshauri. Naye Esta alipata kibali kwa kila mtu aliyemwona.

16 Alipelekwa kwa Mfalme Ahusuero katika makao ya kifalme katika mwezi wa kumi, mwezi wa Tebethi, katika mwaka wake wa saba wa kutawala.

17 Basi ikawa mfalme alivutiwa na Esta zaidi kuliko wanawake wengine wote, naye akapata upendeleo na kibali kuliko mabikira wengine. Kisha akamvika taji la kifalme kichwani mwake na kumfanya malkia badala ya Vashti.

18 Mfalme akafanya karamu kubwa, karamu ya Esta, kwa wakuu wake wote na maafisa. Mfalme alitangaza mapumziko katika majimbo yake yote na kugawa zawadi kwa ukarimu wa kifalme.

Mordekai Afunua Hila

19 Wakati mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa ameketi katika lango la mfalme.

20 Lakini Esta alikuwa ameficha siri ya kabila lake na uraia wake kama Mordekai alivyokuwa amemwambia, kwa maana aliendelea kufuata maelekezo ya Mordekai kama alivyokuwa akifanya alipokuwa akimlea.

21 Wakati Mordekai alipokuwa ameketi kwenye lango la mfalme, Bigthana na Tereshi maafisa wawili wa mfalme waliokuwa walinzi wa lango, walikasirika na kupanga njama ya kumwua Mfalme Ahusuero.

22 Lakini Mordekai aligundua juu ya hila hii na kumwambia Malkia Esta, ambaye baadaye alimwarifu mfalme huku akimsifu Mordekai.

23 Kisha wakati taarifa hiyo ilipochunguzwa na kuonekana kuwa kweli, maafisa hao wawili waliangikwa juu ya miti ya kunyongea. Haya yote yaliandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EST/2-a8dec7e2535eab1bd32f41a689873e2d.mp3?version_id=1627—

Esta 3

Hila Ya Hamani Kuwaangamiza Wayahudi

1 Baada ya matukio haya, Mfalme Ahusuero alimheshimu Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akampandisha na kumpa kiti chake cha heshima cha juu sana kuliko wakuu wengine wote.

2 Maafisa wote wa kifalme waliokaa langoni mwa mfalme walipiga magoti na kumpa Hamani heshima, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru hili kuhusu Hamani. Lakini Mordekai hakumpigia magoti wala kumheshimu.

3 Kisha maafisa wa kifalme waliokuwa langoni mwa mfalme walimuuliza Mordekai, “Kwa nini hutii agizo la mfalme?”

4 Siku baada ya siku walizungumza naye lakini hakukubali. Kwa hiyo walimweleza Hamani kuona kama tabia ya Mordekai itaweza kuvumiliwa, kwa maana alikuwa amewaambia kuwa yeye ni Myahudi.

5 Wakati Hamani alipoona kuwa Mordekai hampigii magoti wala kumpa heshima alighadhibika.

6 Hata hivyo baada ya kujulishwa watu wa Mordekai ni akina nani, alibadili wazo la kumwua Mordekai peke yake. Badala yake Hamani alitafuta njia ya kuwaangamiza watu wote wa Mordekai, yaani, Wayahudi, walio katika ufalme wote wa Ahusuero.

7 Katika mwaka wa kumi na mbili wa kutawala Mfalme Ahusuero, katika mwezi wa kwanza uitwao Nisani, walipiga puri (yaani kura) mbele ya Hamani kuchagua siku na mwezi. Kura ikaangukia kwenye mwezi wa kumi na mbili, yaani Adari.

8 Kisha Hamani alimwambia Mfalme Ahusuero, “Wako watu fulani wameenea na kutawanyika miongoni mwa watu katika majimbo yote ya ufalme wako, ambao desturi zao ni tofauti na zile za watu wengine wote, nao hawatii sheria za mfalme. Haifai mfalme kuwavumilia watu hawa.

9 Kama inampendeza mfalme, itolewe amri kuwaangamiza, nami nitaweka talanta 10,000za fedha katika hazina ya mfalme kwa ajili ya watu watakaoshughulikia jambo hili.”

10 Basi mfalme alichukua pete yake ya muhuri kutoka kwenye kidole chake na kumpa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui wa Wayahudi.

11 Mfalme akamwambia Hamani, “Baki na fedha yako na uwatendee hao watu utakavyo.”

12 Kisha siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza waandishi wa mfalme waliitwa. Wakaandika barua kwa kila jimbo na katika kila lugha ya watu kama agizo la Hamani lilivyotoka kwa mfalme, kwa watawala wa majimbo mbalimbali, na wakuu wa watu mbalimbali. Hizi ziliandikwa kwa jina la Mfalme Ahusuero mwenyewe na kutiwa muhuri wa pete yake mwenyewe.

13 Barua zilipelekwa na tarishi katika majimbo yote ya mfalme zikiwa na amri ya kuharibu, kuua na kuangamiza Wayahudi wote wadogo kwa wakubwa, wanawake na watoto wadogo kwa siku moja. Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, walipaswa pia kuteka nyara vitu vyao.

14 Nakala ya andiko la amri ilipaswa kutolewa kama sheria katika kila jimbo na kufahamishwa kwa watu wa kila taifa ili waweze kuwa tayari kwa siku ile.

15 Kwa kuharakishwa na amri ya mfalme, matarishi walikwenda na andiko lilitolewa katika mji wa ngome ya Shushani. Mfalme na Hamani waliketi na kunywa, lakini mji wa Shushani ulifadhaika.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EST/3-23ed20a0f6d821ef9f1d8123c27b17f1.mp3?version_id=1627—

Esta 4

Mordekai Amshawishi Esta Kusaidia

1 Wakati Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini, akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu.

2 Alikwenda akasimama nje ya lango la mfalme, kwa sababu hakuna ye yote aliyeruhusiwa kuingia akiwa amevaa nguo za magunia.

3 Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya nguo za magunia na majivu.

4 Wakati wajakazi wa Esta na matowashi walipokuja na kumwambia kuhusu Mordekai, alipatwa na huzuni kuu. Alimtumia nguo avae badala ya nguo za magunia, lakini Mordekai hakuzikubali.

5 Ndipo Esta akamwita Hathaki, mmojawapo wa matowashi wa mfalme ambaye alikuwa amewekwa kumhudumia Esta, akamwagiza kutafuta ni nini kilikuwa kikimtaabisha Mordekai na ni kwa nini.

6 Basi Hathaki alitoka nje kumwendea Mordekai kwenye uwanja ulio wazi wa mji mbele ya lango la mfalme.

7 Mordekai akamwambia kila kitu ambacho kimempata, pamoja na hesabu kamili ya fedha Hamani alizoahidi kulipa katika hazina ya kifalme kwa ajili ya maangamizi ya Wayahudi.

8 Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonyesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.

9 Hathaki akarudi kwa Esta na kumwarifu lile Mordekai alilosema.

10 Kisha Esta akamwamuru amweleze Mordekai,

11 “Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya kifalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke ye yote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyoshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.”

12 Wakati maneno ya Esta yalipotaarifiwa kwa Mordekai,

13 Mordekai alirudisha jibu hili: “Usifikiri kwamba kwa sababu uko katika nyumba ya mfalme wewe mwenyewe katika Wayahudi wote utapona.

14 Kwa kuwa kama utakaa kimya wakati huu, msaada na ukombozi kwa Wayahudi utatoka mahali pengine, lakini wewe na jamaa ya baba yako mtaangamia. Nani ajuaye kwamba hukuja kwenye nafasi ya kifalme kwa ajili ya wakati kama huu?”

15 Kisha Esta alituma jibu hili kwa Mordekai:

16 “Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, fungeni kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.”

17 Kwa hiyo Mordekai alikwenda zake na kutekeleza maagizo yote ya Esta.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EST/4-07010ffad0a1842a0d8892c2aa42319d.mp3?version_id=1627—

Esta 5

Ombi La Esta Kwa Mfalme

1 Siku ya tatu Esta alivaa mavazi yake ya kimalkia, naye akasimama katika ua wa ndani wa jumba la mfalme, mbele ya ukumbi wa mfalme. Naye mfalme alikuwa akiketi katika kiti chake cha kifalme katika ukumbi, akielekea langoni.

2 Alipomwona Malkia Esta amesimama uani alipendezwa naye, akamnyoshea fimbo ya utawala ya dhahabu ile iliyokuwa mkononi mwake. Kwa hiyo Esta alikaribia na kuigusa ncha ya fimbo ya mfalme.

3 Kisha mfalme aliuliza, “Malkia Esta, ni nini? Ombi lako ni nini? Hata kama ni nusu ya ufalme, utapewa.”

4 Esta akajibu, “Kama itampendeza mfalme, mfalme pamoja na Hamani waje leo katika karamu ambayo nimeiandaa kwa ajili yake.”

5 Mfalme akasema, “Mleteni Hamani mara moja, ili tupate kufanya lile Esta analoomba.”

Kwa hiyo mfalme na Hamani walihudhuria karamu aliyoiandaa Esta.

6 Walipokuwa wakinywa mvinyo mfalme akamwuliza Esta tena, “Sasa haja yako ni nini? Utapewa. Ombi lako ni nini? Hata nusu ya ufalme, utapewa.”

7 Esta akajibu, “Haja yangu na ombi langu ni hili:

8 Kama mfalme ameona vyema, nami nimepata kibali kwake na kama ikimpendeza mfalme kunipa ombi langu na kunitimizia haja yangu, mfalme na Hamani waje kwangu kesho katika karamu nitakayowaandalia. Kisha nitajibu swali la mfalme.”

Ghadhabu Ya Hamani Dhidi Ya Mordekai

9 Hamani alitoka siku hiyo kwa furaha na moyo mchangamfu. Lakini alipomwona Mordekai langoni mwa mfalme na kuona kwamba hakusimama wala hakuonyesha hofu mbele yake, alijawa na ghadhabu dhidi ya Mordekai.

10 Hata hivyo, Hamani alijizuia akaenda zake nyumbani.

Akawaita pamoja rafiki zake na Zereshi, mkewe.

11 Hamani akajisifia kwao juu ya utajiri wake mwingi, wanawe wengi na kwa njia zote ambazo mfalme amemheshimu kwazo na jinsi alivyomweka juu ya wakuu na maafisa wengine.

12 Hamani akaongeza, “Si hayo tu. Mimi ndiye mtu pekee ambaye Malkia Esta amemwalika kumsindikiza mfalme kwenye karamu aliyomwandalia. Naye amenialika pamoja na mfalme kesho.

13 Lakini haya yote hayanipi kuridhika iwapo ninaendelea kumwona yule Myahudi Mordekai akiketi kwenye lango la mfalme.”

14 Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, “Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini, kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha.” Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EST/5-f5c94411dad1d569eb16740f3abff92c.mp3?version_id=1627—

Esta 6

Mordekai Anapewa Heshima

1 Usiku ule mfalme hakupata usingizi, hivyo akaagiza aletewe kitabu cha kumbukumbu za matukio ya utawala wake, asomewe.

2 Kitabu hicho kilikutwa na kumbukumbu kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumwua Mfalme Ahusuero.

3 Mfalme akauliza, “Je, ni heshima na shukrani gani Mordekai alipokea kwa ajili ya jambo hili?”

Watumishi wake wakajibu, “Hakuna lo lote alilofanyiwa.”

4 Mfalme akasema, “Ni nani yuko uani?” Wakati uo huo Hamani alikuwa ameingia ua wa nje wa jumba la mfalme kusema na mfalme kuhusu kumwangika Mordekai katika mahali pa kuangikia watu alipokuwa amepajenga kwa ajili yake.

5 Watumishi wake wakamjibu, “Hamani amesimama uani.”

Mfalme akaamuru, “Mleteni ndani.”

6 Hamani alipoingia, mfalme alimwuliza, “Afanyiwe nini mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu?”

Basi Hamani akawaza moyoni mwake, “Ni nani mwingine ambaye mfalme angemheshimu kuliko mimi?”

7 Kwa hiyo akamjibu mfalme, “Kwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu,

8 aletewe joho la kifalme ambalo mfalme ameshalivaa na farasi ambaye mfalme alishampanda, ambaye amevikwa taji ya kifalme kichwani mwake.

9 Kisha joho na farasi vikabidhiwe kwa mmojawapo wa wakuu wa mfalme anayeheshimika sana. Nao wamvike mtu yule ambaye mfalme anapenda kumheshimu, na aongozwe akiwa juu ya farasi kupitia barabara za mji, wakitangaza mbele yake, ‘Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu!’ ”

10 Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu cho chote ulichoshauri.”

11 Hivyo Hamani akachukua joho na farasi.

Akamvika Mordekai, na kumpandisha juu ya farasi akamtembeza katika barabara za mji akitangaza mbele yake, “Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme anapenda kumheshimu!”

12 Baadaye Mordekai akarudi kwenye lango la mfalme. Lakini Hamani akakimbia nyumbani, akiwa amejaa huzuni,

13 naye akamweleza Zereshi mkewe pamoja na rafiki zake wote kila kitu ambacho kimempata.

Washauri wake pamoja na Zereshi mkewe wakamwambia, “Kwa kuwa Mordekai, ambaye mbele yake umeanza kuanguka ni wa asili ya Kiyahudi, huwezi kushindana naye, kwa hakika utaanguka!”

14 Walipokuwa bado wakizungumza naye, matowashi wa mfalme wakaja na kumharakisha Hamani aende katika karamu aliyoiandaa Esta.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EST/6-79038e557bb764dad115669cd9945cfe.mp3?version_id=1627—

Esta 7

Hamani Aangikwa

1 Basi mfalme na Hamani wakaenda kula chakula pamoja na Malkia Esta,

2 walipokuwa wakinywa mvinyo katika siku ya pili, mfalme akauliza tena, “Malkia Esta, ni nini haja yako? Utapewa. Ombi lako ni nini? Hata nusu ya ufalme, utapewa.”

3 Kisha Malkia Esta akajibu, “Kama nimepata kibali kwako, Ee mfalme, tena kama inapendeza utukufu wako, nijalie maisha yangu, hii ndiyo haja yangu. Pia uokoe watu wangu, hili ndilo ombi langu.

4 Kwa kuwa mimi na watu wangu tumeuzwa kwa kuangamizwa, kuchinjwa na kuharibiwa. Kama tungalikuwa tumeuzwa tu kuwa watumwa wa kiume na wa kike, ningalinyamaza kimya, kwa sababu shida kama hii isingalitosha kumsumbua mfalme.”

5 Mfalme Ahusuero akamwuliza Malkia Esta, “Ni nani huyu? Yuko wapi mtu huyu aliyethubutu kufanya jambo kama hili?”

6 Esta akasema, “Mtesi na adui ni huyu mwovu Hamani.”

Hamani alifadhaika mbele ya mfalme na malkia.

7 Mfalme akainuka kwa ghadhabu, akaacha mvinyo wake, akaenda kwenye bustani ya jumba la kifalme. Lakini Hamani, akitambua kwamba mfalme ameshaamua hatima yake, alibaki nyuma kumsihi Malkia Esta aokoe maisha yake.

8 Mara mfalme aliporudi kutoka bustani ya jumba la kifalme na kuja kwenye ukumbi wa karamu, Hamani alikuwa akijitupa juu ya kiti mahali Esta alipokuwa akiegemea.

Mfalme akasema kwa nguvu, “Je, atamdhalilisha malkia hata huku nyumbani akiwa pamoja nami!”

Mara neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, walifunika uso wa Hamani.

9 Kisha Harbona, mmoja wa matowashi wanaomtumikia mfalme, akasema, “Mahali pa kuangika watu penye urefu wa mita ishirini na mbili pako nyumbani mwa Hamani. Alikuwa amepatengeneza kwa ajili ya Mordekai, ambaye alizungumza ili kumsaidia mfalme.”

Mfalme akasema, “Mwangikeni juu yake!”

10 Kwa hiyo wakamtundika Hamani mahali alipokuwa ameandaa kwa ajili ya Mordekai. Ndipo ghadhabu ya mfalme ikatulia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EST/7-b23ad2022149248e69d083e0c9e94d4c.mp3?version_id=1627—