Nehemiah 8

1 watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja kwenye uwanja mbele ya Lango la Maji. Wakamwambia Ezra mwandishi alete kitabu cha sheria ya Mose, ambachoBwanaaliamuru kwa ajili ya Israeli.

2 Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba kuhani Ezra akaleta Sheria mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwemo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.

3 Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko mpaka adhuhuri akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Sheria.

4 Mwandishi Ezra akasimama juu ya jukwaa la miti lililojengwa kwa kusudi hilo. Karibu naye upande wa kuume alisimama Matithia, Shema, Anaya, Uria, Hilkia na Maaseya. Upande wake wa kushoto walikuwepo Pedaya, Mishaeli, Malkiya, Hashumu, Hashbadani, Zekaria na Meshulamu.

5 Ezra akakifungua kile kitabu. Watu wote waliweza kumwona kwa sababu alikuwa amesimama juu zaidi, naye alipokifungua watu wote wakasimama.

6 Ezra akamsifuBwana, Mungu mkuu, nao watu wote wakainua mikono yao na kuitikia, “Amen! Amen!” Kisha wakasujudu na kumwabuduBwanahali nyuso zao zikigusa ardhi.

7 Wakati wakiwa wamesimama pale walawi wafuatao walikuwa wakiwaelewesha watu ile sheria: Yeshua, Bani, Sherebia, Jamini, Akubu, Shabethai, Hodai, Maaseya, Kelita, Azaria, Yozabadi, Hanani na Pelaya.

8 Walisoma kutoka katika kile Kitabu cha Sheria ya Mungu, wakiifafanua na kuwapa maelezo ili watu waweze kufahamu kile kilichokuwa kikisomwa.

9 Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Sheria. Ndipo Nehemia Tirshatha, Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, “Siku hii ni takatifu kwaBwanaMungu wenu. Msiomboleze wala msilie.”

10 Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana cho chote cha kula. Siku hii ni takatifu kwaBwana. Msihuzunike, kwa kuwa furaha yaBwanani nguvu zenu.”

11 Walawi wakawatuliza watu wote wakisema, “Iweni watulivu, kwa kuwa hii ni siku takatifu. Msihuzunike.”

12 Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa na kuwapelekea watu sehemu ya chakula na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa wamefahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa.

13 Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa mbari zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Sheria.

14 Wakakuta imeandikwa katika ile Sheria, ambayoBwanaaliiamuru kupitia kwa Mose kwamba Waisraeli wanapaswa kukaa katika vibanda wakati wa sikukuu ya mwezi wa saba

15 na kwamba wanapaswa kutangaza neno hili na kulieneza katika miji yao na katika Yerusalemu wakisema: “Enendeni katika nchi ya mlima na kuleta matawi kutoka miti ya mizeituni, mizeituni mwitu, mihadasi, mitende na miti ya kivuli, ili kutengeneza vibanda,” kama ilivyoandikwa.

16 Basi watu wakaenda na kuleta matawi nao wakajijengea vibanda juu ya paa za nyumba zao, katika nyua zao, katika nyua za nyumba ya Mungu na katika uwanja karibu na Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu.

17 Jamii yote ya watu waliorudi kutoka utumwani wakajenga vibanda na kuishi ndani yake. Tangu wakati wa Yoshua mwana wa Nuni mpaka siku ile, Waisraeli hawakuwahi kuiadhimisha namna hii kama hivi. Furaha yao ilikuwa kubwa sana.

18 Siku baada ya siku, kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho, Ezra alisoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Sheria ya Mungu. Wakaadhimisha sikukuu ile kwa siku saba na katika siku ya nane, kwa kufuatana na maagizo, kulikuwa na kusanyiko maalum.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NEH/8-e97364f016c37ffeccd1c00d2f62fb16.mp3?version_id=1627—

Nehemiah 9

Waisraeli Waungama Dhambi Zao

1 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi ule ule, Waisraeli walikusanyika pamoja, wakifunga na kuvaa nguo za gunia na kujipaka mavumbi vichwani mwao.

2 Wale wa uzao wa Israeli walijitenga na wageni wote. Wakasimama mahali pao na kuungama dhambi zao na uovu wa baba zao.

3 Wakasimama pale walipokuwa, wakasoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Sheria yaBwanaMungu wao kwa muda wa robo siku, wakatumia robo nyingine kwa kuungama na kumwabuduBwanaMungu wao.

4 Walawi wafuatao walikuwa wamesimama kwenye ngazi: Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebania, Buni, Sherebia, Bani na Kenani. Hawa walimliliaBwanaMungu wao kwa sauti kubwa.

5 Nao Walawi Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabnea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakasema: “Simameni mumsifuBwanaMungu wenu, yeye ambaye ni Mungu tangu milele hata milele.”

“Libarikiwe jina lake tukufu, litukuzwe juu ya baraka zote na sifa.

6 Wewe peke yako ndiweBwana. Uliumba mbingu, hata mbingu za mbingu, nalo jeshi lote la angani, dunia na vyote vilivyo ndani yake, bahari na vyote vilivyomo ndani yake. Huvipa vitu vyote uhai, nalo jeshi la mbinguni linakuabudu wewe.

7 “Wewe niBwanaMungu uliyemchagua Abramu na kumtoa kutoka Uri ya Wakaldayo, nawe ukamwita Abrahamu.

8 Uliona kuwa moyo wake ni mwaminifu kwako, nawe ukafanya Agano naye kuwapa wazao wake nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgashi. Umetimiza ahadi yako kwa sababu wewe ni mwenye haki.

9 “Uliona mateso ya baba zetu huko Misri, ukasikia kilio chao huko Bahari ya Shamu.

10 Ulituma ishara za miujiza na maajabu dhidi ya Farao, dhidi ya maafisa wake wote na watu wote wa nchi yake, kwa kuwa ulifahamu jinsi Wamisri walivyowafanyia ufidhuli. Ukajifanyia jina linalodumu hadi leo.

11 Ukagawa bahari mbele yao, ili waweze kupita ndani yake penye nchi kavu, lakini uliwatupa Wamisri waliowafuatilia katika vilindi, kama jiwe kwenye maji mengi.

12 Mchana uliwaongoza kwa nguzo ya wingu na usiku kwa nguzo ya moto kuwamulikia njia iliyowapasa kuiendea.

13 “Ulishuka katika Mlima Sinai, ukanena nao kutoka mbinguni. Ukawapa masharti na sheria zile ambazo ni za kweli na haki, pia amri na maagizo mazuri.

14 Ukawafahamisha Sabato yako takatifu na ukawapa amri, maagizo na sheria kupitia mtumishi wako Mose.

15 Katika njaa yao uliwapa mkate kutoka mbinguni na katika kiu yao uliwatolea maji kutoka kwenye mwamba. Ukawaambia waingie na kuimiliki nchi ambayo ulikuwa umeapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa.

16 “Lakini wao, baba zetu, wakawa na kiburi na shingo ngumu, nao hawakutii maagizo yako.

17 Wakakataa kusikiliza na kushindwa kukumbuka miujiza uliyoifanya miongoni mwao. Wakawa na shingo ngumu na katika uasi wao wakamchagua kiongozi ili warudi kwenye utumwa wao. Lakini wewe ni Mungu mwenye kusamehe, mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo. Kwa hiyo hukuwaacha,

18 hata wakati walipojitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu na kusema, ‘Huyu ni mungu wenu, aliyewapandisha kutoka nchi ya Misri,’ au wakati walipofanya makufuru makubwa.

19 “Kwa sababu ya huruma zako kuu hukuwaacha jangwani. Wakati wa mchana ile nguzo ya wingu haikukoma kuwaongoza katika njia yao, wala nguzo ya moto haikuacha kuwamulikia usiku njia iliyowapasa kuiendea.

20 Ukawapa Roho wako mwema ili kuwafundisha. Hukuwanyima mana yako vinywani mwao, nawe ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao.

21 Kwa miaka arobaini uliwatunza jangwani, hawakukosa cho chote, nguo zao hazikuchakaa wala miguu yao haikuvimba.

22 “Ukawapa falme na mataifa, ukiwagawia hata mipaka ya mbali. Wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani.

23 Ukawafanya wana wao kuwa wengi kama nyota za angani, nawe ukawaleta katika nchi ambayo uliwaambia baba zao kuingia na kuimiliki.

24 Wana wao wakaingia na kuimiliki nchi. Ukawatiisha Wakanaani mbele yao, walioishi katika nchi, ukawatia Wakanaani mikononi mwao, pamoja na wafalme wao na watu wa nchi, wawafanyie kama wapendavyo.

25 Wakateka miji yenye ngome na nchi yenye rutuba, wakamiliki nyumba zilizojazwa na vitu vizuri vya kila aina, visima vilivyochimbwa tayari, mashamba ya mizabibu, mashamba ya mizeituni na miti yenye matunda kwa wingi. Wakala wakashiba nao wakanawiri sana, wakajifurahisha katika wema wako mwingi.

26 “Lakini hawakukutii nao wakaasi dhidi yako, wakatupa sheria zako nyuma yao. Wakawaua manabii wako, waliowaonya ili wakurudie, wakafanya makufuru makubwa.

27 Hivyo ukawatia mikononi mwa adui zao, ambao waliwatesa. Lakini walipoteswa wakakulilia wewe. Kutoka mbinguni uliwasikia, nawe kwa huruma zako kuu ukawapa waokozi, waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.

28 “Lakini mara walipokuwa na raha, wakafanya maovu tena machoni pako. Kisha ukawaacha mikononi mwa adui zao nao wakawatawala. Walipokulilia tena, ukasikia kutoka mbinguni na kwa huruma zako ukawaokoa kila mara.

29 “Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza.

30 Kwa miaka mingi ulikuwa mvumilivu kwao. Kwa njia ya Roho wako ukawaonya kupitia manabii wako. Hata hivyo hawakujali, basi ukawatia mikononi mwa mataifa jirani.

31 Lakini kwa rehema zako kuu hukuwakomesha wala kuwaacha, kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na rehema.

32 “Basi sasa, Ee Mungu wetu, uliye mkuu, mwenye nguvu na Mungu wa kuogofya, mwenye kushika Agano lake la upendo, usiache taabu hizi zote zionekane ni kitu kidogo mbele za macho yako, taabu hizi zilizotupata, juu ya wafalme wetu na viongozi, juu ya makuhani wetu na manabii, juu ya baba zetu na watu wako wote, tangu siku za wafalme wa Ashuru hadi leo.

33 Katika hayo yote yaliyotupata, umekuwa mwenye haki, umetenda kwa uaminifu, wakati sisi tumetenda mabaya.

34 Wafalme wetu, viongozi wetu, makuhani wetu na baba zetu hawakufuata sheria yako, hawakuzingatia amri zako wala maonyo uliyowapa.

35 Hata walipokuwa wangali katika ufalme wao, wakiufurahia wema wako mkuu katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa, hawakukutumikia wala kugeuka kutoka katika njia zao mbaya.

36 “Lakini tazama, leo sisi ni watumwa, watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu ili wapate kula matunda yake na vitu vingine vizuri inayozalisha.

37 Kwa sababu ya dhambi zetu, mavuno yake mengi huenda kwa wafalme uliowaweka watutawale. Wanatawala juu ya miili yetu na mifugo yetu kama wapendavyo. Tuko katika dhiki kuu.

Mapatano Ya Watu

38 “Kwa sababu ya haya yote, tunajifunga katika mapatano, maandishi, pamoja na viongozi wetu, Walawi wetu na makuhani wetu wakitia mihuri yao.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NEH/9-dd44841dcd571e56b7d99745957c7815.mp3?version_id=1627—

Nehemiah 10

1 Wale waliotia muhuri walikuwa:

Nehemia mtawala, mwana wa Hakalia.

Sedekia,

2 Seraya, Azaria, Yeremia,

3 Pashuri, Amaria, Malkiya,

4 Hatushi, Shebania, Maluki,

5 Harimu, Meremothi, Obadia,

6 Danieli, Ginethoni, Baruki,

7 Meshulamu, Abiya, Miyamini,

8 Maazia, Bilgai na Shemaya.

Hawa ndio waliokuwa makuhani.

9 Walawi:

Yeshua mwana wa Azania, Binui wana wa Henadadi, Kadmieli,

10 na wenzao: Shebania,

Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani,

11 Mika, Rehobu, Hashabia,

12 Zakuri, Sherebia, Shebania,

13 Hodia, Bani na Beninu.

14 Viongozi wa watu:

Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani,

15 Buni, Azgadi, Bebai,

16 Adoniya, Bigwai, Adini,

17 Ateri, Hezekia, Azuri,

18 Hodia, Hashumu, Bezai,

19 Harifu, Anathothi, Nebai,

20 Magpiashi, Meshulamu, Heziri,

21 Meshezabeli, Sadoki, Yadua,

22 Pelatia, Hanani, Anaia,

23 Hoshea, Hanania, Hashubu,

24 Haloheshi, Pilha, Shobeki,

25 Rehumu, Hashabna, Maaseya,

26 Ahia, Hanani, Anani,

27 Maluki, Harimu na Baana.

28 “Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Sheria ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao na binti zao wote waliokuwa na uwezo wa kufahamu,

29 basi hawa wote wakajiunga na ndugu zao na wakuu wao, wakajifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Sheria ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Mose mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria zaBwana, Bwana wetu.

30 “Tunaahidi kutowaoza binti zetu kwa watu wanaotuzunguka, wala kuwaoza wana wetu binti zao.

31 “Wakati mataifa jirani waletapo bidhaa zao au nafaka kuuza siku ya Sabato, hatutazinunua toka kwao siku ya Sabato wala siku nyingine yo yote takatifu. Kila mwaka wa saba tutaacha kuilima ardhi na tutafuta madeni yote.

32 “Tunakubali wajibu wa kutimiza amri za kutoa theluthi ya shekelikila mwaka kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu:

33 Kwa ajili ya mikate Mitakatifu, kwa ajili ya sadaka za kawaida za nafaka na sadaka za kuteketezwa, kwa ajili ya sadaka za siku za Sabato, Sikukuu za Mwandamo wa Mwezi na sikukuu nyingine zilizoamuriwa, kwa ajili ya sadaka takatifu, kwa ajili ya sadaka za dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na kwa ajili ya kazi zote za nyumba ya Mungu wetu.

34 “Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu yaBwanaMungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Sheria.

35 “Pia tunachukua wajibu wa kuleta malimbuko ya mazao yetu na matunda ya kwanza ya kila mti wa matunda katika nyumba yaBwanakila mwaka.

36 “Kama pia ilivyoandikwa katika Sheria, tutawaleta wazaliwa wetu wa kwanza wa kiume na wa mifugo yetu yaani wa ng’ombe wetu na wa makundi yetu ya kondoo na mbuzi katika nyumba ya Mungu wetu, kwa ajili ya makuhani wanaohudumu huko.

37 “Zaidi ya hayo, tutaleta katika ghala za nyumba ya Mungu wetu, kwa makuhani, vyakula vya kwanza vya mashamba yetu, sadaka zetu za nafaka, matunda ya miti yetu yote, divai yetu mpya na mafuta. Nasi tutaleta zaka za mazao yetu kwa Walawi, kwa kuwa Walawi ndio ambao hukusanya zaka katika miji yote tunakofanya kazi.

38 Kuhani atokanaye na uzao wa Aroni atashirikiana na Walawi wakati wapokeapo zaka, nao Walawi itawapasa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu katika ghala za hazina.

39 Watu wa Israeli, pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala mahali vifaa vya mahali patakatifu vihifadhiwapo na wanapokaa makuhani wanaohudumu, mabawabu na waimbaji.

“Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NEH/10-0831f1a86ba195edaaff4e475f6c009e.mp3?version_id=1627—

Nehemiah 11

Wakazi Wapya Wa Yerusalemu

1 Basi, viongozi wa watu waliokaa Yerusalemu na watu wengine, walipiga kura mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, wengine tisa waliobaki ilikuwa wakae katika miji yao wenyewe.

2 Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu.

3 Hawa ndio viongozi wa majimbo waliokuja kuishi Yerusalemu (baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi, Wanethini, na wazao wa watumishi wa Solomoni waliendelea kuishi katika miji ya Yuda, kila mmoja katika milki yake mwenyewe katika miji mbalimbali,

4 ambapo watu wengine kutoka Yuda na Benyamini waliishi Yerusalemu).

Kutoka wazao wa Yuda:

Athaya mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mzao wa Peresi.

5 Naye Maaseya mwana wa Baruki, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, mzao wa Mshelani.

6 Wazao wa Peresi walioishi Yerusalemu walikuwa 468, watu wenye uwezo.

7 Kutoka wazao wa Benyamini:

Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseya, mwana wa Ithieli, mwana wa Yeshaya

8 na wafuasi wake, Gabai na Salai watu 928.

9 Yoeli mwana wa Zikri alikuwa afisa wao mkuu, naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa msimamizi juu ya Mtaa wa Pili katika mji.

10 Kutoka makuhani:

Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini,

11 Seraya mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Meraiothi, mwana wa Ahitubu, msimamizi katika nyumba ya Mungu,

12 pamoja na wenzao 822 waliofanya kazi hekaluni. Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amzi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya,

13 na wenzao, waliokuwa viongozi wa jamaa walikuwa watu 242. Amashsai mwana wa Azareli, mwana wa Ahzai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri,

14 na wenzao waliokuwa wenye uwezo walikuwa watu 128. Afisa wao mkuu alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.

15 Kutoka Walawi:

Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni;

16 Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu;

17 Matania mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mwana wa Asafu, kiongozi aliyeongoza kutoa shukrani na maombi; Bakbukia aliyekuwa msaidizi wake kati ya wenzake; na Abda mwana wa Shamua, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.

18 Jumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.

19 Mabawabu:

Akubu, Talmoni na wenzao, waliolinda malango, walikuwa watu 172.

20 Waisraeli waliosalia, pamoja na makuhani na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda, kila mmoja katika urithi wa baba yake.

21 Wanethini waliishi katika kilima cha Ofeli. Ziha na Gishpa walikuwa wasimamizi wao.

22 Afisa mkuu wa Walawi huko Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika. Uzi alikuwa mmoja wa wazao wa Asafu, waliokuwa waimbaji wenye kuwajibika kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu.

23 Waimbaji walikuwa chini ya amri za mfalme ambazo pia ziliratibu shughuli zao za kila siku.

24 Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu.

25 Kuhusu vijiji na mashamba yake, baadhi ya watu wa Yuda waliishi Kiriath-Arba na makazi yaliyokizunguka, katika Diboni na makazi yake, katika Yekabzeeli na vijiji vyake,

26 katika Yeshua, katika Molada, katika Beth-Peleti,

27 katika Hazar-Shuali, katika Beer-Sheba na makazi yake,

28 katika Ziklagi, katika Mekona na makazi yake,

29 katika En-Rimoni, katika Sora, katika Yarmuthi,

30 Zanoa, Adulamu na vijiji vyazo, katika Lakishi na mashamba yake, katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba mpaka Bonde la Hinomu.

31 Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake,

32 katika Anathothi, Nobu na Anania,

33 katika Hazori, Rama na Gitaimu,

34 katika Hadidi, Zeboimu na Nebalati,

35 katika Lodi, Ono na katika Bonde la Mafundi.

36 Baadhi ya makundi ya Walawi wa Yuda waliishi huko Benyamini.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NEH/11-f95714bc5b0dcdd2fc55b771d8e7daf6.mp3?version_id=1627—

Nehemiah 12

Makuhani Na Walawi Waliorudi Na Zerubabeli

1 Hawa wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua:

Seraya, Yeremia, Ezra,

2 Amaria, Maluki, Hatushi,

3 Shekania, Rehumu, Meremothi,

4 Ido, Ginethoni, Abiya,

5 Miyamini, Moadia, Bilga,

6 Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,

7 Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya.

Hawa walikuwa viongozi wa makuhani na wenzao wakati wa Yeshua.

8 Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani.

9 Bakbukia na Uni, wenzao, walisimama mkabala nao wakati wa ibada.

10 Yeshua alikuwa baba wa Yoiakimu, Yoiakimu alikuwa baba wa Eliyashibu, Eliyashibu alikuwa baba wa Yoyada,

11 Yoyada alikuwa baba wa Yonathani, na Yonathani alikuwa baba wa Yadua.

12 Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani:

wa jamaa ya Seraya, Meraya;

wa Yeremia, Hamania;

13 wa jamaa ya Ezra, Meshulamu;

wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;

14 wa jamaa ya Maluki, Yonathani;

wa jamaa ya Shekania, Yusufu;

15 wa jamaa ya Harimu, Helkai;

16 wa jamaa ya Ido, Zekaria;

wa jamaa ya Ginethoni, Meshulamu;

17 wa jamaa ya Abia, Zikri;

wa jamaa ya Miyamini na ya Maazia, Piltai;

18 wa jamaa ya Bilgai, Shamua;

wa jamaa ya Shemaya, Yehonathani;

19 wa jamaa ya Yoyaribu, Matenai;

wa jamaa ya Yedaya, Uzi;

20 wa jamaa ya Salu, Kalai;

wajamaa ya Amoki, Eberi;

21 wa jamaa ya Hilkia, Hashabia;

wa jamaa ya Yedaya, Nethaneli.

22 Wakuu wa jamaa za Walawi katika siku za Eliyashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua, pia wale jamaa za makuhani, waliandikishwa wakati wa utawala wa Dario, Mwajemi.

23 Wakuu wa jamaa miongoni mwa wazao wa Lawi hadi wakati wa Yohanani mwana wa Eliyashibu waliandikishwa katika kitabu cha kumbukumbu.

24 Viongozi wa Walawi walikuwa: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli na wenzao, waliosimama mkabala nao kusifu na kushukuru, sehemu moja ikipokezana na nyingine kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu.

25 Mabawabu waliokuwa wakilinda kwenye malango ya ghala ni: Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni na Akubu.

26 Walihudumu siku za Yoakimu mwana wa Yeshua, mwana wa Yozadaki, na katika siku za mtawala Nehemia na za Ezra kuhani na mwandishi.

Kuwekwa Wakfu Ukuta Wa Yerusalemu

27 Wakati wa kuwekwa wakfu ukuta wa Yerusalemu, Walawi walitafutwa huko walikokuwa wakiishi, nao wakaletwa Yerusalemu kuadhimisha kwa shangwe huko kuweka wakfu kwa nyimbo za shukrani na kwa uimbaji kwa kutumia matoazi, vinubi na zeze.

28 Pia waimbaji walikusanywa pamoja kutoka maeneo yanayozunguka Yerusalemu, kutoka vijiji vya Wanetofathi,

29 kutoka Beth-Gilgali, kutoka eneo la Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kuzunguka Yerusalemu.

30 Wakati makuhani na Walawi walipokuwa wamekwisha kujitakasa kwa kufuatana na desturi, waliwatakasa watu, malango na ukuta.

31 Niliwaagiza viongozi wa Yuda wapande juu ya ukuta. Pia niliagiza makundi mawili makubwa ya waimbaji waimbe nyimbo za kumshukuru Mungu. Moja lipande juu ya ukuta upande wa kuume, kuelekea Lango la Samadi.

32 Hoshaya na nusu ya viongozi wa Yuda wakawafuata,

33 pamoja na Azaria, Ezra, Meshulamu,

34 Yuda, Benyamini, Shemaya, Yeremia,

35 pamoja na baadhi ya makuhani wenye tarumbeta, pia walikuwa na Zekaria mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu,

36 pamoja na wenzao, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda na Hanani wakiwa na vyombo vya uimbaji, kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu. Mwandishi Ezra aliongoza maandamano.

37 Kwenye Lango la Chemchemi waliendelea moja kwa moja mpaka kwenye ngazi za Mji wa Daudi kwenye mwinuko wa ukuta na kupitia juu ya nyumba ya Daudi mpaka kwenye Lango la Maji upande wa mashariki.

38 Kundi la pili la waimbaji lilielekea upande wa kushoto. Niliwafuata juu ya ukuta, pamoja na nusu ya watu nyuma ya mnara wa Tanuru mpaka kwenye Ukuta Mpana,

39 juu ya Lango la Efraimu, Lango la Yeshana, Lango la Samaki, Mnara wa Hananeli na Mnara wa Mia, mpaka kwenye lango la Kondoo. Walipofika kwenye Lango la Ulinzi wakasimama.

40 Kisha yale makundi mawili ya waimbaji yaliyoshukuru yalichukua nafasi zao katika nyumba ya Mungu, nami pia, pamoja na nusu ya maafisa,

41 pamoja na makuhani wafuatao: Eliyakimu, Maaseya, Miniamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania wakiwa na tarumbeta zao,

42 pia Maaseya, Shemaya, Eleazari, Uzi, Yehohanani, Malkiya, Elamu na Ezeri. Makundi haya yaliimba chini ya uongozi wa Yezrahia.

43 Siku hiyo watu walitoa dhabihu nyingi, walishangilia kwa sababu Mungu aliwapa furaha kuu. Wanawake na watoto walishangilia pia. Sauti ya kushangilia huko Yerusalemu iliweza kusikika mbali sana.

44 Wakati huo watu walichaguliwa kuwa wasimamizi wa vyumba vya ghala kwa ajili ya matoleo, malimbuko na zaka. Kutoka kwenye yale mashamba yaliyozunguka miji walipaswa walete kwenye ghala mafungu kama sheria ilivyoamuru kwa ajili ya makuhani na Walawi, kwa kuwa Yuda alifurahishwa na huduma ya makuhani na Walawi.

45 Walifanya ibada ya Mungu wao na ibada ya utakaso, waimbaji na walinzi wa lango walifanya hivyo pia, kufuatana na amri za Daudi na Solomoni mwanawe.

46 Kwa muda mrefu uliopita, katika siku za Daudi na Asafu, walikuwepo viongozi wa waimbaji na wa nyimbo za sifa na za kumshukuru Mungu.

47 Kwa hiyo katika siku za Zerubabeli na za Nehemia, Israeli wote walitoa mafungu kila siku kwa ajili ya waimbaji na mabawabu. Pia walitenga fungu kwa ajili ya Walawi wengine, nao Walawi walitenga fungu kwa ajili ya wazao wa Aroni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NEH/12-66d363585c6d3fe335271bf2ee34be25.mp3?version_id=1627—

Nehemiah 13

Nehemia Afanya Matengenezo Ya Mwisho

1 Katika siku hiyo kitabu cha Mose kilisomwa kwa sauti kuu na watu wote wakasikia. Humo ilionekana imeandikwa kwamba hakuna Mwamori wala Mmoabi atakayeruhusiwa katika kusanyiko la watu wa Mungu,

2 kwa sababu hawakuwalaki Waisraeli kwa chakula na maji, badala yake walimwajiri Balaamu kuwalaani (lakini hata hivyo Mungu wetu aligeuza laana kuwa baraka).

3 Watu waliposikia sheria hii, waliwatenga watu wote wasio Waisraeli waliokuwa wa uzao wa kigeni.

4 Kabla ya hili, kuhani Eliyashibu alikuwa amewekwa kuwa msimamizi wa vyumba vya ghala ya nyumba ya Mungu wetu. Alikuwa na uhusiano wa karibu na Tobia,

5 naye alikuwa amempa Tobia chumba kikubwa ambacho mwanzo kilikuwa kikitumika kuweka sadaka za nafaka, uvumba na vyombo vya Hekalu, pamoja na zaka za nafaka, divai mpya na mafuta waliyoagizwa Waisraeli kwa ajili ya Walawi, waimbaji na mabawabu wa Lango, pamoja na matoleo kwa makuhani.

6 Lakini wakati haya yote yalipokuwa yakitendeka, sikuwa Yerusalemu, kwa kuwa katika mwaka wa thelathini na mbili wa kutawala Artashasta mfalme wa Babeli nilikuwa nimerudi kwa mfalme. Baadaye nilimwomba ruhusa,

7 nirudi Yerusalemu. Hapo niligundua jambo la uovu alilofanya Eliyashibu kwa kumpa Tobia chumba katika nyua za nyumba ya Mungu.

8 Nilikasirika sana na nilivitupa nje vyombo vyote vya Tobia.

9 Nilitoa amri kutakasa vyumba, kisha nilivirudisha vifaa vya nyumba ya Mungu, pamoja na sadaka za nafaka na uvumba.

10 Pia niligundua kuwa mafungu yaliyopangwa kupewa Walawi hawakuwa wamepewa, pia Walawi wote na waimbaji waliowajibika kwa huduma walikuwa wamerudi katika mashamba yao.

11 Basi niliwakemea maafisa na kuwauliza, “Kwa nini nyumba ya Mungu imepuuzwa?” Kisha niliwaita pamoja na kuwaweka kwenye nafasi zao.

12 Yuda wote walileta zaka za nafaka, divai mpya na mafuta kwenye ghala.

13 Nikamweka kuhani Shelemia, mwandishi Sadoki na Mlawi aliyeitwa Pedaya kuwa wasimamizi wa ghala na kumfanya Hanani mwana wa Zakuri, mwana wa Matania, kuwa msaidizi wao, kwa sababu watu hawa walionekana kuwa waaminifu. Walipewa wajibu wa kugawa mahitaji kwa ndugu zao.

14 Ee Mungu wangu, unikumbuke kwa hili, wala usifute kile nilichokifanya kwa uaminifu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu na kwa ajili ya huduma yake.

15 Siku hizo nikaona watu katika Yuda wakikanyaga mashinikizo ya divai siku ya Sabato na kuleta nafaka wakiwapakiza punda, pamoja na divai, zabibu, tini na aina nyingine za mizigo. Nao walikuwa wakileta haya yote Yerusalemu siku ya Sabato. Kwa hiyo niliwaonya dhidi ya kuuza vyakula siku hiyo.

16 Watu kutoka Tiro waliokuwa wakiishi Yerusalemu walileta samaki na aina nyingi za bidhaa na kuziuza Yerusalemu siku ya Sabato kwa watu wa Yuda.

17 Niliwakemea wakuu wa Yuda na kuwaambia, “Ni uovu gani huu mnaofanya kuinajisi siku ya Sabato?

18 Je, baba zenu hawakufanya mambo ya jinsi hii hata kumsababisha Mungu wetu kuleta maafa haya yote juu yetu na juu ya mji huu? Sasa bado mnazidi kuchochea ghadhabu yake dhidi ya Israeli kwa kuinajisi Sabato.”

19 Wakati vivuli vya jioni vilipoangukia juu ya malango ya Yerusalemu kabla ya Sabato, niliamuru milango ifungwe na isifunguliwe mpaka Sabato iishe. Nikawaweka baadhi ya watu wangu mwenyewe kwenye malango ili kwamba pasiwepo mzigo utakaoingizwa ndani siku ya Sabato.

20 Mara moja au mbili wachuuzi na wauzaji wa bidhaa za aina zote walilala usiku nje ya mji wa Yerusalemu.

21 Lakini niliwaonya na kuwaambia, “Kwa nini mnalala karibu na ukuta? Kama mkifanya hivi tena, nitawaadhibu.” Kuanzia wakati ule hawakuja tena siku ya Sabato.

22 Kisha nikawaamuru Walawi kujitakasa na kwenda kulinda malango ili kutunza Sabato iwe takatifu.

Ee Mungu wangu, unikumbuke kwa ajili ya hili pia, nawe unionyeshe wema wako sawasawa na upendo wako mkuu.

23 Zaidi ya hayo, niliona watu wa Yuda waliokuwa wameoa wanawake kutoka Ashdodi, Amoni na Moabu.

24 Nusu ya watoto wao walizungumza lugha ya Kiashidodi au lugha ya watu wengine, hawakuweza kuzungumza Kiyahudi.

25 Niliwakemea na kuwalaani. Niliwapiga baadhi ya watu na kung’oa nywele zao. Niliwaapisha kwa jina la Mungu na kusema: “Msiwaoze binti zenu kwa wana wao, wala binti zao wasiolewe na wana wenu wala ninyi wenyewe.

26 Je, Solomoni hakutenda dhambi kwa sababu ya wanawake wa namna hiyo? Miongoni mwa mataifa mengi hapakuwepo mfalme kama yeye. Alipendwa na Mungu wake. Naye Mungu alimweka kuwa mfalme juu ya Israeli yote, hata hivyo wanawake wa mataifa mengine walimfanya hata yeye atende dhambi.

27 Je, tulazimike sasa kusikia kwamba ninyi pia mmefanya uovu huu mkubwa na kutokuwa waaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni?”

28 Mmoja wa wana wa Yoyada mwana wa Eliashibu Kuhani Mkuu alikuwa mkwewe Sanbalati Mhoroni. Nami nilimfukuza mbele yangu.

29 Ee Mungu wangu, uwakumbuke, kwa sababu wamenajisi ukuhani na agano la kikuhani na la Walawi.

30 Kwa hiyo niliwatakasa makuhani na Walawi kutokana na cho chote kilichokuwa cha kigeni, na kuwapa wajibu, kila mmoja katika kazi yake.

31 Pia nilihakikisha kwamba matoleo ya kuni yaliletwa kwa wakati unaopaswa na malimbuko kwa wakati wake.

Ee Mungu wangu, unikumbuke, unitendee mema.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NEH/13-64e882dd6740d1962afcb87f89876d45.mp3?version_id=1627—

Ezra 1

Koreshi Asaidia Watu Kurudi Kutoka Uhamishoni

1 Katika mwaka wa kwanza wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kutimiza neno laBwanalililosemwa na Yeremia,Bwanaaliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote na kuliweka katika maandishi:

2 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda.

3 Ye yote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu laBwana, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko huko Yerusalemu.

4 Nao watu wa mahali po pote wale walionusurika wanapoishi sasa, watu hao wampe fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, mbali na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ”

5 Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba yaBwanahuko Yerusalemu.

6 Majirani zao wote wakawasaidia vyombo vya fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, pia na zawadi za thamani, pamoja na sadaka zote za hiari.

7 Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu laBwana, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalua la mungu wake.

8 Koreshi mfalme wa Uajemi akavitoa kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, aliyevihesabu mbele ya Sheshbaza mkuu wa Yuda.

9 Hii ilikuwa ndio orodha ya vifaa:

masinia ya dhahabu yalikuwa 30
masinia ya fedha yalikuwa 1,000
vyetezo vya fedha vilikuwa 29
10 mabakuli ya dhahabu yalikuwa 30
mabakuli ya fedha yanayofanana yalikuwa 410
vifaa vingine vilikuwa 1,000.

11 Kwa ujumla, kulikuweko na vyombo 5,400 vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZR/1-0dc481afe6e1fa96d3f5bae426bc45ec.mp3?version_id=1627—

Ezra 2

Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni

1 Basi hawa ndio watu wa jimbo, waliotoka uhamishoni ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirejea Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,

2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):

Orodha ya watu wa Israeli ilikuwa:

3 wazao wa Paroshi 2,172
4 wa Shefatia 372
5 wa Ara 775
6 wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812
7 wa Elamu 1,254
8 wa Zatu 945
9 wa Zaka 760
10 wa Bani 642
11 wa Bebai 623
12 wa Azgadi 1,222
13 wa Adonikamu 666
14 wa Bigwai 2,056
15 wa Adini 454
16 wa Ateri (kwa Hezekia) 98
17 wa Besai 323
18 wa Yora 112
19 wa Hashumu 223
20 wa Gibari 95
21 watu wa Bethlehemu 123
22 wa Netofa 56
23 wa Anathothi 128
24 wa Azmawethi 42
25 wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
26 wa Rama na Geba 621
27 wa Mikmashi 122
28 wa Betheli na Ai 223
29 wa Nebo 52
30 wa Magbishi 156
31 wa Elamu ile ingine 1,254
32 wa Harimu 320
33 wa Lodi, Hadidi na Ono 725
34 wa Yeriko 345
35 wa Senaa 3,630

36 Makuhani:

wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
37 wa Imeri 1,052
38 wa Pashuri 1,247
39 wa Harimu 1,017

40 Walawi:

Wazao wa Yeshua na Kadmieli (wa jamaa ya Hodavia) 74

41 Waimbaji:

Wazao wa Asafu 128

42 Mabawabu wa lango la Hekalu:

Wazao waShalumu, Ateri, Talmoni,Akubu, Hatita na Shobai 139

43 Wanethini:

wazao wa

Siha, Hasufa, tabaothi,

44 Kerosi, Siaha, Padoni,

45 Lebana, Hagaba, Akubu,

46 Hagabu, Shalmai, Hanani,

47 Gideli, Gahari, Reaya,

48 Resini, Nekoda, Gazamu,

49 Uza, Pasea, Besai,

50 Asna, Meunimu, Nefusimu,

51 Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

52 Basluthi, Mehida, Harsha,

53 Barkosi, Sisera, Tema,

54 Nesia na Hatifa.

55 Wazao wa watumishi wa Solomoni:

wazao wa

Sotai, Hasaferethi, Peruda,

56 Yaala, Darkoni, Gideli,

57 Shefatia, Hatili,

Pokereth-Hasebaimu na Ami.

58 Wanethini nawazao wa watumishiwa Solomoni 392

59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuonyesha ya kuwa jamaa zao zilitokana na uzao wa Israeli:

60 Wazao waDelaya, Tobia na Nekoda 652

61 Kutoka miongoni mwa makuhani:

Wazao wa

Hobaya, Hakosi, Barzilai (ambaye alikuwa ameoa binti wa Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo.)

62 Hawa walitafuta orodha ya jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kwenye kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.

63 Mtawala aliwaagiza wasile chakula cho chote kitakatifu mpaka awepo kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.

64 Kundi lote lilikuwa na watu 42,360;

65 pamoja na hao kulikuwapo na watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwapo waimbaji wanaume na wanawake 200.

66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,

67 ngamia 435 na punda 6,720.

68 Walipofika kwenye nyumba yaBwanahuko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika lile eneo lake.

69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000za dhahabu, mane 5,000za fedha na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hii.

70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na Wanethini waliishi mijini mwao, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi kwenye miji yao.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZR/2-286d7b4ee7229a577ba3596e7fd918a7.mp3?version_id=1627—

Ezra 3

Madhabahu Yajengwa Tena

1 Mwezi wa saba ulipowadia baada ya Waisraeli kukaa katika miji yao, watu wote walikusanyika huko Yerusalemu kama mtu mmoja.

2 Yeshua mwana wa Yosadaki na makuhani wenzake, Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na wenzake walianza kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli ili kumtolea dhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto juu yake, kulingana na ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose mtu wa Mungu.

3 Ingawa waliwaogopa watu waliowazunguka, walijenga madhabahu juu ya ule msingi wake, wakamtoleaBwanadhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto juu yake za asubuhi na za jioni.

4 Kisha kulingana na kile kilichoandikwa, wakaiadhimisha Sikukuu ya Vibanda wakitoa idadi ya sadaka za kuteketezwa kama ilivyohitajika kila siku sawasawa na ilivyoagizwa.

5 Baada ya hayo, walitoa sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za Mwezi Mwandamo na dhabihu zote za sikukuu takatifu zaBwanazilizoamuriwa, pamoja na zile sadaka za hiari zilizotolewa kwaBwana.

6 Ingawa bado msingi wa Hekalu laBwanaulikuwa haujawekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwaBwanatangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.

Kujenga Upya Hekalu

7 Kisha watu wakawapa mafundi wa uashi na useremala fedha, wakawapa watu wa Sidoni na Tiro vyakula, vinywaji na mafuta ili waweze kuleta magogo ya mierezi kwa njia ya bahari kutoka Lebanoni hadi Yafa, kama alivyoagiza Koreshi mfalme wa Uajemi.

8 Katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kufika kwenye nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zao wengine (makuhani, Walawi na wote waliorejea Yerusalemu kutoka uhamishoni) walianza kazi, wakiteua Walawi wenye umri kuanzia miaka ishirini au zaidi kusimamia ujenzi wa nyumba yaBwana.

9 Yeshua na wanawe pamoja na ndugu zake, Kadmieli na wanawe (wazao wa Hodavia), wana wa Henadadi na wana wao na ndugu zao, Walawi wote walijiunga pamoja kusimamia wale waliofanya kazi katika nyumba ya Mungu.

10 Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu laBwana, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumtukuzaBwana, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli.

11 Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwaBwanahivi:

“Yeye ni mwema;

upendo wake kwa Israeli

wadumu milele.”

Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwaBwana, kwa sababu msingi wa nyumba yaBwanaulikuwa umewekwa.

12 Lakini wengi wa makuhani wazee, Walawi na viongozi wa jamaa ambao walikuwa wameona Hekalu la mwanzoni, walilia kwa sauti wakati walipoona msingi wa Hekalu hili ukiwekwa, huku wengine wengi wakipiga kelele kwa furaha.

13 Hakuna mtu ambaye angeweza kutofautisha sauti hizo za furaha na za kilio, kwa sababu watu walipiga kelele sana. Nayo hiyo sauti ikasikika mbali.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZR/3-20fb248e7db5a0564f8cfd340916147d.mp3?version_id=1627—

Ezra 4

Upinzani Kuhusu Ujenzi Mpya

1 Adui za Yuda na Benyamini waliposikia kwamba watu waliorudi kutoka uhamishoni wanajenga Hekalu kwa ajili yaBwana, Mungu wa Israeli,

2 wakamjia Zerubabeli na viongozi wa jamaa, nao wakasema, “Turuhusuni tuwasaidie kujenga, kwa sababu sisi tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi na tumekuwa tukimtolea dhabihu tangu wakati wa Esar-hadoni mfalme wa Ashuru, aliyetuleta hapa.”

3 Lakini Zerubabeli, Yeshua na viongozi wengine wa jamaa ya Israeli wakawajibu, “Ninyi hamna sehemu nasi katika kujenga Hekalu la Mungu wetu. Sisi peke yetu tutajenga Hekalu kwa ajili yaBwana, Mungu wa Israeli, kama Mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi alivyotuagiza.”

4 Ndipo watu waliowazunguka wakajipanga kuwakatisha tamaa watu wa Yuda na kuwafanya waogope walipokuwa wakiendelea na ujenzi.

5 Wakaajiri washauri kuwapinga katika kazi yao, nao wakaipinga mipango yao wakati wote wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi hadi wakati wa utawala wa Dario mfalme wa Uajemi.

Upinzani Mwingine Chini Ya Ahusuero Na Artashasta

6 Mnamo mwanzo wa utawala wa Ahusuero, hao adui waliandika mashtaka dhidi ya watu wa Yuda na Yerusalemu.

7 Pia katika siku za utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli pamoja na wenzao waliandika barua kwa Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa mwandiko wa Kiaramu na katika lugha ya Kiaramu.

8 Rehumu afisa msimamizi na mwandishi Shimshai waliandika barua kwa Mfalme Artashasta dhidi ya watu wa Yerusalemu kama ifuatavyo:

9 Rehumu afisa msimamizi na mwandishi Shimshai, pamoja na wenzao, yaani mahakimu na maafisa walio juu ya watu kuanzia Tripoli, Uajemi, Ereki na Babeli, Waelami wa Shushani,

10 na watu wengine ambao mheshimiwa Asur-Banipalialiwahamisha na kuwakalisha katika mji wa Samaria na mahali pengine Ng’ambo ya Mto Eufrati.

11 (Hii ndiyo nakala ya barua waliyompelekea.)

Kwa Mfalme Artashasta,

Kutoka kwa watumishi wako, watu wa Ng’ambo ya Mto Eufrati:

12 Yapasa Mfalme ajue kuwa Wayahudi waliopanda kuja kwetu kutoka kwenu, wamekwenda Yerusalemu nao wanaujenga upya ule mji wa uasi na wa uovu. Wanajenga upya kuta na kukarabati misingi yake.

13 Zaidi ya hayo, mfalme yampasa ajue kwamba kama mji huu ukijengwa na kuta zake zikafanywa upya, hakutakuwa na ulipaji wa kodi wala ada au ushuru, hivyo hazina ya kifalme itaathirika.

14 Sisi sasa kwa kuwa tunawajibika kwa jumba la kifalme na kwamba siyo sawasawa kwetu kuona mfalme akidharauliwa, basi tunatuma ujumbe huu kumtaarifu mfalme,

15 ili kwamba ufanyike uchunguzi kwenye kumbukumbu ya maandishi ya waliokutangulia. Katika kumbukumbu hizi utagundua kwamba mji huu ni wa maasi, unaowataabisha wafalme na majimbo, ni mahali pa maasi tangu zamani. Ndiyo maana mji huu uliharibiwa.

16 Tunamjulisha mfalme kwamba kama mji huu ukijengwa na kuta zake zikifanywa upya, hutabakiwa na cho chote Ng’ambo ya Mto Eufrati.

17 Mfalme alirudisha jibu hili:

Kwa Rehumu, afisa msimamizi, mwandishi Shimshai na wenzenu wote wanaoishi katika Samaria na penginepo Ng’ambo ya Mto Eufrati:

Salaam.

18 Barua mliyotutumia imesomwa na kutafsiriwa mbele yangu.

19 Nilitoa amri na uchunguzi ukafanyika na imegundulika kwamba mji huu una historia ndefu ya maasi dhidi ya wafalme na pamekuwa mahali pa maasi na uchochezi.

20 Yerusalemu umepata kuwa na wafalme wenye nguvu wakitawala nchi yote iliyo Ng’ambo ya Mto Eufrati, wakitoza kodi, ada na ushuru huko.

21 Kwa hiyo toeni amri kwa watu hawa wasimamishe ujenzi, ili kwamba mji huu usiendelee kujengwa hadi nitakapoagiza.

22 Mwe waangalifu msipuuze jambo hili. Kwa nini kuruhusu tishio hili kuendelea na kusababisha hasara kwa ufalme?

23 Mara waliposomewa nakala ya barua ya Mfalme Artashasta, Rehumu na Shimshai aliyekuwa mwandishi na wenzao, walikwenda mara moja kwa Wayahudi huko Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu kusimamisha ujenzi.

24 Hivyo kazi ya ujenzi wa nyumba ya Mungu huko Yerusalemu ikasimamishwa kabisa hadi mwaka wa pili wa utawala wa Dario mfalme wa Uajemi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZR/4-f793384efa402637b5ca37ea965b08d5.mp3?version_id=1627—