2 Mambo ya nyakati 5

1 Hivyo kazi yote Solomoni aliyofanya kwa ajili ya Hekalu laBwanaikamalizika, Solomoni akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu, yaani, fedha, dhahabu na vyombo vingine vyote na kuviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.

Sanduku La Agano Laletwa Hekaluni

2 Kisha Mfalme Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili kulipandisha Sanduku la Agano laBwanakutoka Sayuni, Mji wa Daudi.

3 Nao watu wote wa Israeli wakaja pamoja kwa mfalme wakati wa sikukuu katika mwezi wa saba.

4 Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamefika, Walawi wakaliinua Sanduku la Agano,

5 nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, ambao walikuwa ni Walawi walivibeba vitu hivyo,

6 naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli lililokuwa limemkusanyikia walikuwa mbele ya Sanduku, wakitoa dhabihu nyingi za kondoo na ng’ombe ambazo hazikuwezekana kuandikwa wala kuhesabiwa.

7 Kisha makuhani wakaleta Sanduku la Agano laBwanampaka mahali pake ndani ya mahali Patakatifu pa Hekalu, yaani, mahali Patakatifu pa Patakatifu na kuliweka chini ya mabawa ya wale makerubi.

8 Makerubi walitanda mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea.

9 Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zingeweza kuonekana ukiwa ndani mbele ya mahali Patakatifu, lakini siyo ukiwa nje ya mahali patakatifu, nayo hiyo mipiko ipo mpaka leo.

10 Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine cho chote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahaliBwanaalipofanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.

11 Basi makuhani wakaondoka hapo mahali patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao.

12 Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta.

13 Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuruBwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifuBwanawakisema:

“Yeye ni mwema;

upendo wake unadumu milele.”

Ndipo Hekalu laBwanalikajazwa na wingu,

14 nao makuhani hawakuweza kusimama kufanya huduma yao kwa sababu ya wingu, kwa maana utukufu waBwanaulilijaza Hekalu la Mungu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/5-1c4cf519d28ca373379f4f20da07ca96.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 6

Kuweka Hekalu Wakfu

1 Kisha Solomoni akasema, “Bwanaalisema ya kwamba angelikaa katika wingu jeusi.

2 Nimejenga Hekalu zuri kwa ajili yako, mahali pako pa kukaa milele.”

3 Wakati kusanyiko lote la Israeli likiwa limesimama huko, Mfalme Solomoni akageuka na kuwabariki.

4 Kisha akasema:

“AhimidiweBwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mkono wake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa maana alisema,

5 ‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lo lote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo kwa ajili ya Jina langu, wala sikumchagua mtu ye yote kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli.

6 Lakini sasa nimeuchagua Yerusalemu ili Jina langu lipate kuwemo humo, nami nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’

7 “Ilikuwa moyoni mwa Daudi baba yangu kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina laBwana, Mungu wa Israeli.

8 LakiniBwanaakamwambia Daudi baba yangu, ‘Kwa sababu ilikuwa moyoni mwako kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu, ulifanya vyema kuwa na jambo hili moyoni mwako.

9 Hata hivyo, sio wewe utakayenijengea Hekalu, bali mwanao, ambaye ni nyama yako na damu yako mwenyewe, yeye ndiye atakayejenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’

10 “Bwanaametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vileBwanaalivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina laBwana, Mungu wa Israeli.

11 Nimeliweka humo Sanduku la Agano, ambalo ndani yake ndimo liliko lile Agano laBwanaalilofanya na watu wa Israeli.”

Maombi Ya Solomoni Ya Kuweka Wakfu

12 Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu yaBwanamachoni pa kusanyiko lote la Israeli, naye akakunjua mikono yake.

13 Basi alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kushanyiko lote la Israeli, akanyosha mikono yake kwelekea mbinguni.

14 Akasema:

“EeBwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.

15 Umetimiza ahadi yako kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, kwa kinywa chako uliahidi na kwa mkono wako umelitimiza, kama ilivyo leo.

16 “SasaBwana, Mungu wa Israeli, mtimizie mtumishi wako Daudi baba yangu ahadi zako ulizomwahidi uliposema, ‘Kamwe hutakosa kuwa na mtu atakayeketi mbele zangu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli, kama wanao wakiangalia yote wayafanyayo kuenenda mbele zangu kama vile ulivyofanya.’

17 Sasa, EeBwana, Mungu wa Israeli, acha neno lako lile ulilomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu litimie sawasawa.

18 “Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!

19 Hata hivyo sikiliza dua ya mtumishi wako na maombi yake kwa huruma, EeBwanaMungu wangu. Sikia kilio na dua ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo.

20 Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa.

21 Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe.

22 “Mtu anapomkosea jirani yake na akatakiwa kuapa, akija na kuapa mbele ya madhabahu yako ndani ya Hekalu hili,

23 basi, sikia kutoka mbinguni na ukatende. Hukumu kati ya watumishi wako, ukimhukumu yule mwenye hatia na kuleta juu ya kichwa chake yale aliyoyatenda. Umtangazie asiye na hatia kwamba hana hatia, hivyo ukathibitishe kutokuwa na hatia kwake.

24 “Wakati watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili,

25 basi usikie kutoka mbinguni, ukasamehe dhambi ya watu wako Israeli na kuwarudisha katika nchi uliyowapa baba zao.

26 “Wakati mbingu zitakapokuwa zimefungwa kusiwe na mvua kwa sababu watu wako wametenda dhambi dhidi yako, watakapoomba kuelekea mahali hapa na kulikiri jina lako nao wakageuka kutoka katika dhambi zao kwa sababu umewaadhibu,

27 basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.

28 “Wakati njaa au tauni vikija juu ya nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wo wote, maafa ya namna yo yote au ugonjwa wo wote unaoweza kuwajia,

29 wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akijua juu ya taabu ya moyo wake mwenyewe, akainyosha mikono yake kuelekea Hekalu hili,

30 basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote),

31 ili wakuogope kwa wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.

32 “Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako kuu na mkono wako wenye nguvu ulionyoshwa, atakapokuja kuomba akikabili Hekalu hili,

33 basi na usikie kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, ukafanye lo lote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako.

34 “Wakati watu wako watakapokwenda vitani dhidi ya adui zao, po pote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwaBwanakuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako,

35 basi usikie dua na maombi yao kutoka mbinguni, ukawatetee haki yao.

36 “Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu ye yote ambaye hatendi dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwatia mikononi mwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi yake mwenyewe, mbali au karibu

37 na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya wale waliowachukua mateka na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa, tumetenda kwa uovu’;

38 kama wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako,

39 basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na ukatetee haki yao. Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako.

40 “Sasa, Mungu wangu, macho yako na yafumbuke na masikio yako yasikie maombi yaombwayo mahali hapa.

41 “Sasa inuka, EeBwanaMungu,

na uje mahali pako pa kupumzika,

wewe na Sanduku la nguvu zako.

Makuhani wako, EeBwanaMungu,

na wavikwe wokovu,

watakatifu wako na wafurahi

katika wema wako.

42 EeBwanaMungu, usimkatae

mpakwa mafuta wako.

Kumbuka upendo mkuu uliomwahidia

Daudi mtumishi wako.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/6-d58b02bea720ebf9c22c4415335c32e2.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 7

Hekalu Lawekwa Wakfu

1 Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu waBwanaukalijaza Hekalu.

2 Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu laBwanakwa sababu utukufu waBwanaulilijaza.

3 Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu waBwanaukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuruBwanawakisema,

“Yeye ni mwema;

upendo wake unadumu milele.”

4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele zaBwanaMungu.

5 Naye Mfalme Solomoni akatoa dhabihu ya ng’ombe 22,000 pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu.

6 Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vyaBwanaambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifuBwana, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.

7 Solomoni akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu laBwanana huko ndiko akatolea sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba aliyokuwa ametengeneza haikutosha kuweka sadaka hizo zote za kuteketezwa, sadaka za nafaka na za mafuta.

8 Kwa hiyo Mfalme Solomoni akaadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, akiwa pamoja na Israeli wote, kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Wadi ya Misri.

9 Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi.

10 Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Solomoni akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingiBwanaMungu aliomtendea Daudi na Solomoni na kwa ajili ya watu wake Israeli.

Bwana Mungu Amtokea Solomoni

11 Solomoni alipokuwa amemaliza kujenga Hekalu laBwanana jumba la kifalme, naye akiwa amefanikiwa kutenda yale yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kufanya katika Hekalu laBwanana katika jumba lake mwenyewe la kifalme,

12 BwanaMungu akamtokea Solomoni usiku na kumwambia:

“Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu.

13 “Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu,

14 kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.

15 Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa.

16 Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili kwamba Jina langu lipate kuwa huko milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwepo huko daima.

17 “Kwa habari yako wewe, kama ukienenda mbele zangu kama Daudi baba yako alivyoenenda na kufanya yote nikuamuruyo, nawe ukizishika amri zangu na sheria zangu,

18 Nitakifanya imara kiti chako cha enzi kama nilivyoagana na Daudi baba yako wakati niliposema, ‘Hutakosa kamwe mtu wa kutawala juu ya Israeli.’

19 “Lakini kama ukigeuka na kuyaacha maagizo na amri nilizowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu,

20 ndipo nitakapoing’oa Israeli kutoka katika nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa mataifa yote.

21 Ingawa Hekalu hili sasa ni la fahari sana, wale wote watakaopita watashangaa na kusema, ‘Kwa niniBwanaamefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’

22 Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwachaBwana, Mungu wa baba zao, ambaye aliwatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, hiyo ndiyo sababu alileta haya maafa yote juu yao.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/7-09cfd4e173b5ffc8dda972df8e82b579.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 8

Shughuli Nyingine Za Solomoni

1 Ikawa mwisho wa miaka ishirini, ambayo katika hiyo Solomoni alilijenga Hekalu laBwanana jumba lake mwenyewe la kifalme,

2 Solomoni akajenga tena vijiji vile ambavyo Hiramu alikuwa amempa, naye akawapa Waisraeli waishi humo.

3 Kisha Solomoni akaenda Hamath-Soba na kuuteka.

4 Pia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi.

5 Akajenga tena Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo,

6 pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu na miji yote kwa ajili ya magari yake ya vita na kwa ajili ya farasi wake pamoja na kila alichotaka kukijenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.

7 Watu wote waliosalia miongoni mwa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi (haya mataifa hayakuwa Waisraeli),

8 yaani, hii ni kwamba, wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawakuwa wamewaangamiza, Mfalme Solomoni akawalazimisha kufanya kazi kama ilivyo mpaka leo.

9 Lakini Solomoni hakuwafanya Waisraeli watumwa kwa ajili ya kazi yake, bali walikuwa wapiganaji, majemadari, maafisa wake, majemadari wa magari yake ya vita na waendesha magari ya vita.

10 Pia walikuwa maafisa wakuu wa Mfalme Solomoni, yaani, maafisa wakaguzi 250 waliosimamia watu.

11 Solomoni akampandisha mke wake binti wa Farao kutoka Mji wa Daudi mpaka kwenye jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku laBwanalimefika ni patakatifu.”

12 Mfalme Solomoni akamtoleaBwanadhabihu za kuteketezwa juu ya madhabahu yaBwanaambayo alikuwa ameijenga mbele ya ukumbi,

13 kulingana na mahitaji ya kila siku kwa ajili ya sadaka zilizoamriwa na Mose kwa ajili ya Sabato, Mwezi Mwandamo na sikukuu nyingine tatu za mwaka, yaani, Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma na Sikukuu ya Vibanda.

14 Kwa kushika maagizo ya Daudi baba yake, aliweka migawanyo ya makuhani kwa ajili ya kazi zao, nao Walawi kuongoza kusifu na kusaidia makuhani kufuatana na mahitaji ya kila siku. Pia akaweka mabawabu katika migawanyo kwa ajili ya malango mbalimbali, kwa sababu hili ndilo Daudi mtu wa Mungu alilokuwa ameagiza.

15 Nao hawakuziacha amri za mfalme alizoamuru makuhani au Walawi katika jambo lo lote, ikiwa ni pamoja na zile za hazina.

16 Kazi yote ya Mfalme Solomoni ilifanyika kuanzia siku msingi wa Hekalu laBwanaulipowekwa mpaka kukamilika kwake. Kwa hiyo Hekalu laBwanalikamalizika kujengwa.

17 Ndipo Solomoni akaenda Esion-Geberi na Elathi katika pwani ya Edomu.

18 Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu ambao walikuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Solomoni wakasafiri kwa njia ya bahari mpaka Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambayo walimkabidhi Mfalme Solomoni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/8-85247f1ff060ddce193564076c508ac7.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 9

Malkia Wa Sheba Amtembelea Solomoni

1 Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni na uhusiano wake na jina laBwana, huyo malkia akaja kumjaribu kwa maswali magumu. Alipofika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani, alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.

2 Solomoni akamjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lo lote lililokuwa gumu kwa mfalme asiweze kumwelezea.

3 Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Solomoni na jumba la kifalme alilokuwa amejenga,

4 chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa Solomoni alizotoa katika Hekalu laBwanaalipatwa na mshangao.

5 Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli.

6 Lakini sikuamini mambo haya mpaka nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana kuliko ile taarifa niliyoisikia.

7 Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako!

8 AhimidiweBwanaMungu wako, ambaye amependezwa sana nawe na kukuweka juu ya kiti chake cha ufalme kutawala kwa niaba yaBwanaMungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwadhibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.”

9 Naye akampa mfalme talanta 120za dhahabu, kiasi kikubwa cha vikolezi na mawe ya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa vikolezi vizuri kama vile Malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.

10 (Watumishi wa Hiramu na wa Solomoni wakaleta dhahabu kutoka Ofiri, tena wakaleta shehena kubwa ya miti ya msandali na mawe ya thamani.

11 Mfalme akatumia hiyo miti ya msandali kuwa ngazi kwa ajili ya Hekalu laBwanana kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha miti ya msandali hakikuwahi kuingizwa nchini tangu siku ile.)

12 Mfalme Solomoni akampa Malkia wa Sheba kila kitu alichohitaji na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka akarudi kwenye nchi yake mwenyewe pamoja na wafuasi wake.

Fahari Ya Solomoni

13 Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,

14 mbali na mapato mengine kutoka kwa wafanyibiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Solomoni dhahabu na fedha.

15 Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa ya dhahabu yenye uzito wa shekeli 600.

16 Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa ya uzito wa mane tatuza dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

17 Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi.

18 Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pakuwekea miguu vyote vya dhahabu. Upande wa kuume na wa kushoto wa hicho kiti palikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, pakiwa na sanamu ya simba iliyosimama kila upande.

19 Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, wawili kwenye kila ngazi, yaani, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wo wote.

20 Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Solomoni.

21 Mfalme alikuwa na meli nyingi za biasharabaharini zilizokuwa zikiandamana na meli za Hiramu. Mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wadogo na wakubwa.

22 Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia.

23 Dunia yote ikatafuta kukutana na Solomoni kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameweka katika moyo wake.

24 Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.

25 Solomoni alikuwa na mabanda 4,000 kwa ajili ya farasi na magari ya vita, farasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji ya magari ya vita na katika Yerusalemu pamoja naye.

26 Solomoni akatawala juu ya wafalme wote kuanzia Mto Eufrati mpaka kwenye nchi ya Wafilisti na kuendelea hadi mpaka wa Misri.

27 Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu na mierezi kuwa mingi kama miti ya mikuyu iliyoko chini ya vilima.

28 Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka nchi nyingine zote.

Kifo Cha Solomoni

29 Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Solomoni, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Nathani, katika unabii wa Ahiya Mshiloni na katika maono ya Ido mwonaji dhidi ya Yeroboamu mwana wa Nebati?

30 Solomoni akatawala huko Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.

31 Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/9-f8478a22f9491205cacfa6ed6c05c1f4.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 10

Israeli Wanamwasi Rehoboamu

1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wamekwenda huko kumfanya yeye kuwa mfalme.

2 Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Solomoni), akarudi kutoka Misri.

3 Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu, yeye na kusanyiko lote la Israeli wakamwendea Rehoboamu na kumwambia,

4 “Baba yako aliweka nira nzito, lakini sasa ufanye nyepesi kazi za kikatili na nira nzito baba yako aliyoweka juu yetu, nasi tutakutumikia.”

5 Rehoboamu akajibu, “Nendeni kwa muda wa siku tatu na kisha mnirudie.” Basi watu wakaenda zao.

6 Kisha Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee ambao walimtumikia Solomoni baba yake wakati wa uhai wake akawauliza, “Mnanishauri nini katika kuwajibu watu hawa?”

7 Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.”

8 Lakini Rehoboamu akakataa shauri alilopewa na wazee na akataka ushauri kwa vijana wanaume rika lake waliokuwa wakimtumikia.

9 Akawauliza, “Ninyi ushauri wenu ni nini? Tutawajibuje watu hawa wanaoniambia, ‘Ifanye nyepesi nira baba yako aliyoweka juu yetu?’ ”

10 Wale vijana wa rika lake wakamjibu, “Waambie watu hawa waliokuambia, ‘Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini ifanye nira yetu nyepesi,’ kuwa, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.

11 Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi; mimi nitawachapa kwa nge.’ ”

12 Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.”

13 Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee,

14 akafuata shauri la vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.”

15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa jambo hili lilitoka kwaBwanaili kutimiza neno ambaloBwanaalikuwa amenena kwa Yeroboamu mwana wa Nebati kupitia Ahiya Mshiloni.

16 Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme:

“Tuna fungu gani kwa Daudi?

Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese.

Nendeni kwenye mahema yenu, Ee Israeli,

angalia nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi!”

Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.

17 Lakini kwa habari ya Waisraeli waliokuwa wakiishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado.

18 Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramualiyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu.

19 Hivyo Israeli wakawa wameasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/10-600608f41618547a97ec9ee286158259.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 11

Yuda Na Benyamini Zajengwa Ngome

1 Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda na kabila la Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Solomoni.

2 Lakini neno hili laBwanalikamjia Shemaya mtu wa Mungu:

3 “Mwambie Rehoboamu mwana wa Solomoni mfalme wa Yuda na Israeli wote waliyoko Yuda na Benyamini na watu wengine wote,

4 hili ndilo asemaloBwana, ‘Usipande kwenda kupigana dhidi ya ndugu zako Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno laBwanana kurudi nyumbani, wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu kamaBwanaalivyokuwa ameagiza.

Yeroboamu Ajengea Yuda Ngome

5 Rehoboamu akaishi Yerusalemu akajenga miji yenye ngome katika Yuda:

6 Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa,

7 Beth-Suri, Soko, Adulamu,

8 Gathi, Maresha, Zifu,

9 Adoraimu, Lakishi, Azeka,

10 Sora, Aiyaloni na Hebroni. Hii ndiyo iliyokuwa miji iliyojengewa ngome katika Yuda na Benyamini.

11 Akaimarisha ulinzi wake na kuweka majemadari ndani yake, pamoja na ghala za mahitaji ya vyakula, mafuta ya zeituni na divai.

12 Akaweka ngao na mikuki katika miji na kuifanya iwe imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake.

13 Makuhani na Walawi kutoka sehemu zote za Israeli wakawa upande wake.

14 Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali zao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani waBwana.

15 Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza.

16 Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafutaBwana, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtoleaBwanadhabihu, Mungu wa baba zao.

17 Wakaimarisha ufalme wa Yuda na kumwunga mkono Rehoboamu mwana wa Solomoni miaka mitatu, wakienenda katika njia za Daudi na Solomoni katika wakati huu.

Jamaa Ya Rehoboamu

18 Rehoboamu alimwoa Mahalati ambaye alikuwa binti Yerimothi mwana wa Daudi, mamaye alikuwa Abihaili binti Eliyabu mwana wa Yese.

19 Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu.

20 Kisha akamwoa Maaka binti Absalomu, ambaye alimzalia: Abiya, Atai, Ziza na Shelomithi.

21 Rehoboamu akampenda Maaka binti Absolomu zaidi kuliko wakeze wengine na masuria wake. Kwa jumla alikuwa na wake kumi na wanane na masuria sitini, wana ishirini na wanane na binti sitini.

22 Rehoboamu akamweka Abiya mwana wa Maaka, kuwa mkuu wa wana wa mfalme miongoni mwa ndugu zake ili amfanye mfalme.

23 Akatenda kwa busara, akiwasambaza baadhi ya wanawe katika wilaya zote za Yuda na Benyamini, pamoja na miji yote yenye ngome. Akawapa mahitaji tele na kuwaoza wake wengi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/11-25efaf7862e2b12c2213d52c3e94aabf.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 12

Shishaki Ashambulia Yerusalemu

1 Baada ya nafasi ya Rehoboamu kuimarika na kuwa na nguvu, yeye na Israeli yote waliiacha sheria yaBwanaMungu.

2 Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwaBwana, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa kutawala kwa Mfalme Rehoboamu.

3 Akiwa na magari ya vita 1,200 na wapanda farasi 60,000 na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibya, Wasukii na Wakushiyaliyokuja pamoja naye kutoka Misri.

4 Akateka miji ya Yuda yenye ngome akaendelea mpaka Yerusalemu.

5 Ndipo nabii Shemaya akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda waliokuwa wamekusanyika huko Yerusalemu kwa ajili ya hofu ya Shishaki naye akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyoBwana, ‘Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo, mimi nami sasa ninawaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.’ ”

6 Viongozi wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “BwanaMungu ni mwenye haki.”

7 BwanaMungu alipoona kwamba wamejinyenyekeza, neno hili laBwanalikamjia Shemaya: “Maadamu wamejinyenyekeza, sitawaangamiza bali hivi karibuni nitawapatia wokovu. Ghadhabu yangu haitamwagwa juu ya Yerusalemu kwa kupitia Shishaki.

8 Hata hivyo, watamtumikia Shishaki ili wapate kujifunza tofauti kati ya kunitumikia mimi na kuwatumikia wafalme wa nchi nyingine.”

9 Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu laBwanana hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Solomoni alikuwa amezitengeneza.

10 Hivyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la kifalme.

11 Kila mara mfalme alipokwenda katika Hekalu laBwanawalinzi walikwenda pamoja naye wakiwa wamebeba hizo ngao na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi.

12 Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira yaBwanaikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda.

13 Mfalme Rehoboamu akajiweka imara katika Yerusalemu na akaendelea kuwa mfalme. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na saba, mji ambaoBwanaalikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili aliweke Jina lake humo. Mama yake aliitwa Naama, alikuwa Mwaamoni.

14 Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafutaBwanaMungu.

15 Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, tangu mwanzo mpaka mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwako na vita mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.

16 Rehoboamu akalala pamoja na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Abiya mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/12-6397e3bacd988c897ddc40a1b72719ba.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 13

Abiya Mfalme Wa Yuda

1 Katika mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake Mfalme Yeroboamu, Abiya akawa mfalme wa Yuda,

2 naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka, binti Urieli wa Gibeoni.

Basi kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.

3 Abiya aliingia vitani na jeshi la watu 400,000 wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu 800,000 wenye uwezo.

4 Abiya akasimama juu ya Mlima Semaraimu, katika nchi ya vilima ya Efraimu, naye akasema, “Yeroboamu na Israeli yote, nisikilizeni mimi!

5 Hamfahamu kwambaBwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi na wazao wake ufalme juu ya Israeli milele kwa Agano la chumvi?

6 Hata hivyo Yeroboamu mwana wa Nebati afisa wa Solomoni mwana wa Daudi, aliasi dhidi ya bwana wake.

7 Baadhi ya watu wasiofaa kitu, wabaya kabisa walimkusanyikia na kumpinga Rehoboamu mwana wa Solomoni alipokuwa kijana mdogo asiyekuwa na uamuzi, asiye na nguvu za kuweza kupingana nao.

8 “Hata sasa unapanga kupingana na ufalme waBwanaambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu.

9 Lakini je, hamkuwafukuza makuhani waBwana, wana wa Aroni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Ye yote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo waume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.

10 “Kwa habari yetu sisi,Bwanandiye Mungu wetu, wala hatujamwacha.

11 Makuhani wanaomtumikiaBwanani wana wa Aroni nao Walawi wakiwasaidia kila asubuhi na jioni kutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwaBwana. Huweka mikate juu ya meza safi kwa taratibu za kiibada na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Tunazishika kanuni zaBwanaMungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu.

12 Mungu yu pamoja nasi, yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi yaBwana, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.”

13 Basi Yeroboamu alikuwa ametuma jeshi kuzunguka nyuma ya Yuda ili kwamba wakati akiwa mbele ya Yuda jeshi liwavizie kwa nyuma.

14 Wakageuka na kuona kwamba wanashambuliwa pande zote mbele na nyuma. Ndipo wakamliliaBwana. Makuhani wakapiga tarumbeta zao,

15 nao watu wa Yuda wakapaza sauti ya kilio cha vita. Katika kupiga kelele za vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda.

16 Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia Israeli mikononi mwao.

17 Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli.

18 Watu wa Israeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemeaBwana, Mungu wa baba zao.

19 Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vinavyoizunguka miji hiyo.

20 Yeroboamu hakupata nguvu tena wakati wa utawala wa Abiya. NayeBwanaakampiga Yeroboamu akafa.

21 Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita.

22 Matukio mengine ya utawala wa Abiya, pamoja na mambo aliyofanya na aliyosema, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/13-1a1c230f37617988ad0eeaa6eb816e13.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 14

Asa Atawala

1 Hivyo Abiya akalala na baba zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme na katika siku zake, nchi ikawa na amani kwa miaka kumi.

2 Asa akatenda yaliyo mema na haki machoni paBwanaMungu wake.

3 Akaziondoa madhabahu za kigeni na mahali pa juu pa kuabudia miungu, akayavunja yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Maashera.

4 Akawaamuru Yuda kumtafutaBwana, Mungu wa baba zao na kutii sheria zake na amri zake.

5 Akaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu za kufukizia uvumba kwenye kila mji katika Yuda, nao ufalme ulikuwa na amani katika utawala wake.

6 Akajenga miji yenye ngome katika Yuda, wakati nchi ikiwa na amani. Hakuna mtu ye yote aliyepigana vita naye katika miaka hiyo, kwa kuwaBwanaalimstarehesha.

7 Mfalme akawaambia Yuda, “Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafutaBwanaMungu wetu, tulimtafuta naye ametupa raha kila upande.” Hivyo wakajenga na wakafanikiwa.

8 Asa alikuwa na jeshi la watu 300,000 kutoka Yuda, wenye ngao kubwa na mikuki na jeshi la watu 280,000 kutoka Benyamini, wenye ngao ndogo na pinde. Watu hawa wote walikuwa wapiganaji mashujaa.

9 Zera Mkushi akatoka kupigana dhidi yao akiwa na jeshi la watu maelfu ya maelfu na magari ya vita 300, nao wakaja mpaka Maresha.

10 Asa akatoka kumkabili, nao wakapanga vita katika Bonde la Sefatha karibu na Maresha.

11 Kisha Asa akamliliaBwanaMungu wake na kusema, “EeBwana, hakuna ye yote aliye kama wewe wa kuwasadia wasio na nguvu dhidi ya wenye nguvu. Utusaidie, EeBwana, wewe ndiwe Mungu wetu, kwa kuwa tunakutumainia wewe, nasi kwa jina lako tumekuja dhidi ya jeshi hili kubwa. EeBwana, wewe ndiwe Mungu wetu, usiwaache wanadamu wakushinde wewe.”

12 Bwanaakawapiga Wakushi mbele ya Asa na Yuda. Wakushi wakakimbia,

13 naye Asa na jeshi lake wakawafuatia mpaka Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondwapondwa mbele zaBwanana majeshi yake.

14 Watu wa Yuda wakachukua nyara nyingi sana, wakaangamiza vijiji vyote vinavyoizunguka Gerari, kwa kuwa hofu yaBwanailikuwa imewaangukia. Wakateka nyara vijiji hivi vyote, kwani kulikuwapo nyara nyingi huko.

15 Pia wakashambulia kambi za wachunga makundi ya wanyama wakachukua na kuyaswaga makundi ya kondoo, mbuzi na ngamia. Kisha wakarudi Yerusalemu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/14-e7e5474eccadc78c42f936ba1b2d035a.mp3?version_id=1627—