2 Mambo ya nyakati 15

Asa Afanya Matengenezo

1 Roho waBwanaakamjia Azaria mwana wa Obedi.

2 Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini.Bwanayu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi.

3 Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria.

4 Lakini katika taabu yao walimrudiaBwana, Mungu wa Israeli na kumtafuta, naye akaonekana kwao.

5 Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa ye yote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa.

6 Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina.

7 Lakini kwa habari yenu ninyi, iweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.”

8 Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Obedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka katika miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu yaBwanailiyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu laBwana.

9 Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwambaBwanaMungu wake alikuwa pamoja naye.

10 Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Asa.

11 Wakati huo wakamtoleaBwanadhabihu za ng’ombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka katika zile nyara walizoteka.

12 Wakafanya agano kumtafutaBwana, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote.

13 Wale wote ambao hawangemtafutaBwana, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke.

14 WakamwapiaBwanakwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu.

15 Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyoBwanaakawastarehesha pande zote.

16 Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake asiwe mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza kichakani nguzo ya chukizo ya Ashera. Asa akaikata ile nguzo akaiangusha, akaivunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.

17 Ingawa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, Asa akauweka moyo wake wote kwaBwanakikamilifu siku zote za maisha yake.

18 Akaleta katika Hekalu la Mungu fedha, dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

19 Hapakuwepo vita tena mpaka mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/15-04520e161cb1855d8372f266d5f43653.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 16

Miaka Ya Mwisho Ya Mfalme Asa

1 Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwa Asa, Mfalme Baasha wa Israeli akaishambulia Yuda na kuujengea ngome mji wa Rama ili kumzuia ye yote asitoke wala kuingia katika nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.

2 Ndipo Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka katika hazina ya Hekalu laBwanana kutoka katika jumba lake mwenyewe la kifalme na kumpelekea Ben-Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye alikuwa anatawala huko Dameski.

3 Akasema, “Pawepo na makubaliano kati yangu na wewe, kama yalivyokuwako kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, ninakupelekea fedha na dhahabu. Basi vunja makubaliano yako na Mfalme Baasha wa Israeli ili aweze kujiondoa huku kwangu.”

4 Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Wakashinda Iyoni, Dani, Abel-Maimu na miji yote ya hazina ya Naftali.

5 Baasha aliposikia jambo hili, akasimamisha kujenga Rama na kuacha kazi yake.

6 Ndipo Mfalme Asa akawaleta watu wote wa Yuda, nao wakachukua mawe na miti ambayo Baasha alikuwa anavitumia huko Rama. Kwa vitu hivyo akajenga Geba na Mizpa.

7 Ikawa wakati huo mwonaji Hanani akamjia Mfalme Asa wa Yuda na kumwambia: “Kwa sababu ulimtegemea mfalme wa Aramu nawe hukumtegemeaBwanaMungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limeponyoka mkononi mwako.

8 Je, hukumbuki lililotendeka kwa Wakushi na Walibya, hawakuwa jeshi lenye nguvu na magari mengi ya vita na wapanda farasi? Hata hivyo, ulipomtegemeaBwanayeye aliwatia mkononi mwako.

9 Kwa kuwa macho yaBwanahukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.”

10 Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.

11 Matukio ya utawala wa Asa, kuanzia mwanzo mpaka mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.

12 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwaBwanabali kwa matabibu tu.

13 Ndipo katika mwaka wa arobaini na moja wa kutawala kwake Asa, akafa na kulala na baba zake.

14 Nao wakamzika katika kaburi lile alilokuwa amelichonga kwa ajili yake mwenyewe katika Mji wa Daudi. Wakamzika kwa jeneza lililowekwa vikolezi na mchanganyiko wa manukato ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa kwa utaalamu wa mtengeneza marashi, nao wakawasha moto mkubwa kwa heshima yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/16-b5e4d38dff0ca430fc83a88e91b8ff29.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 17

Yehoshafati Mfalme Wa Yuda

1 Yehoshafati mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme na akajiimarisha dhidi ya Israeli.

2 Akaweka jeshi katika miji yote ya Yuda yenye ngome na kuweka askari walinzi katika Yuda na katika miji ya Efraimu ile ambayo baba yake Asa alikuwa ameiteka.

3 BwanaMungu alikuwa na Yehoshafati kwa sababu katika miaka yake ya mwanzoni alienenda katika njia za Daudi baba yake. Hakutafuta Mabaali

4 bali alimtafuta Mungu wa baba yake na kuzifuata amri zake badala ya kufuata desturi za watu wa Israeli.

5 Kwa hiyoBwanaakauimarisha ufalme chini ya uongozi wake, nao Yuda wote wakamletea Yehoshafati zawadi, hivyo akawa na utajiri mwingi na heshima.

6 Moyo wake ukawa hodari katika njia zaBwanana zaidi ya yote, akaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu na nguzo za Maashera katika Yuda.

7 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake akatuma maafisa wake ambao ni: Ben-Haili, Obadia, Zekaria, Nethaneli na Mikaya ili kufundisha katika miji ya Yuda.

8 Pamoja nao walikuwepo Walawi fulani nao ni: Shemaya, Nethania, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adonia, Tobia, Tob-Adonia, pamoja nao walikuwapo makuhani Elishama na Yehoramu.

9 Wakafundisha Yuda yote, wakiwa wamechukua Kitabu cha Torati yaBwanawakazunguka miji yote ya Yuda na kufundisha watu.

10 Hofu yaBwanaikawa juu ya falme zote za nchi zilizozunguka Yuda, hivyo hawakufanya vita na Yehoshafati.

11 Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi na fedha kama ushuru, nao Waarabu wakamletea mifugo: Kondoo waume 7,700 na mbuzi 7,700.

12 Yehoshafati akaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi, akajenga ngome na miji ya hazina katika Yuda

13 na akawa na wingi mkubwa wa vitu katika miji ya Yuda. Pia aliweka askari wa vita wenye uzoefu huko Yerusalemu.

14 Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo:

Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu:

Jemadari Adna akiwa na askari wa vita 300,000;

15 aliyefuata ni jemadari Yehonathani, akiwa na askari 280,000 walio tayari kwa vita;

16 aliyefuata ni Amasia mwana wa Zikri, ambaye alijitolea kwa ajili ya kazi yaBwana, akiwa na askari 200,000.

17 Kutoka Benyamini:

Eliyada, askari shujaa akiwa na watu 200,000 wenye silaha za nyuta na ngao;

18 aliyefuata ni Yehozabadi, akiwa na askari 180,000 wenye silaha za vita.

19 Hawa ndio watu waliomtumikia mfalme huko Yerusalemu, mbali na hawa mfalme aliweka askari katika miji yenye ngome katika Yuda yote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/17-1e7667768d42c049d8396cd8b2c2020a.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 18

Mikaya Atoa Unabii Dhidi Ya Ahabu

1 Basi, Yehoshafati alikuwa na mali nyingi sana na heshima. Naye akafanya urafiki na Ahabu kwa mwanawe kumwoa binti wa Ahabu.

2 Baada ya miaka kadhaa akashuka kumtembelea Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja ng’ombe na kondoo wengi kwa ajili yake na watu aliokuwa amefuatana nao. Kisha Ahabu akamshawishi Yehoshafati kukwea pamoja naye ili kuishambulia Ramoth-Gileadi.

3 Ahabu mfalme wa Israeli akamwuliza Yehoshafati mfalme wa Yuda, “Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Ramoth-Gileadi?”

Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako. Tutakuwa pamoja nawe vitani.”

4 Lakini Mfalme Yehoshafati pia akamwambia mfalme wa Israeli, “Kwanza tafuta shauri laBwana.”

5 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii wanaume wapatao 400, akawauliza, “Je, niende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?”

Wakajibu, “Naam, nenda kwa kuwaBwanaataitiya Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.”

6 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii waBwanahapa ambaye tunaweza kumwuliza?”

7 Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumwuliza shauri laBwana, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lo lote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.”

Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”

8 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwita mmoja wa maafisa wake na kusema, “Mlete Mikaya mwana wa Imla mara moja.”

9 Wakiwa wamevalia majoho yao ya kifalme, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi juu ya viti vyao vya kifalme katika sakafu ya kupuria, kwenye ingilio la lango la Samaria, pamoja na manabii wote wakiwa wakitabiri mbele yao.

10 Wakati huu Zedekia mwana wa Kenaana alikuwa ametengeneza pembe za chuma na akatangaza, “Hivi ndivyoBwanaasemavyo, ‘Kwa hizi pembe utawapiga na kuwarudisha Waaramu nyuma mpaka wameangamizwa.’ ”

11 Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwaBwanaataitia mkononi mwa mfalme.”

12 Mjumbe aliyekuwa amekwenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.”

13 Lakini Mikaya akasema, “Hakika kamaBwanaaishivyo, nitamwambia kile tuBwanaatakachoniambia.”

14 Alipofika, mfalme akamwuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?”

Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwaBwanaatawatia mkononi mwa mfalme.”

15 Mfalme akamwambia, “Je, ni mara ngapi nitakuapisha ili usiniambie kitu cho chote ila kweli tu kwa jina laBwana?”

16 Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, nayeBwanaakasema, ‘Watu hawa hawana bwana. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ”

17 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lo lote jema kunihusu bali mabaya tu?”

18 Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno laBwana: NilimwonaBwanaameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka kulia kwake na kushoto kwake.

19 NayeBwanaakasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’

“Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile.

20 Mwishoni, roho akajitokeza, akasimama mbele zaBwanana kusema, ‘Nitamshawishi.’

“Bwanaakauliza, ‘Kwa njia gani?’

21 “Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’

“Bwanaakasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’

22 “Kwa hiyo sasaBwanaameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote.Bwanaameamuru maafa kwa ajili yako.”

23 Kisha Zedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwaBwanaalipita njia gani, alipotoka kwangu ili kusema nawe?”

24 Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapokwenda kujificha kwenye chumba cha ndani.”

25 Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni na mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme.

26 Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe cho chote ila mkate na maji mpaka nitakaporudi salama.’ ”

27 Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basiBwanahajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!”

Ahabu Anauawa Huko Ramoth-Gileadi

28 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakaenda Ramoth-Gileadi.

29 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitaingia vitani nikiwa nimejibadilisha, lakini wewe uvae majoho yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na kwenda vitani.

30 Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na mtu ye yote, mdogo wala mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.”

31 Wakati wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele,

32 wale majemadari wakaona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli nao wakaacha kumfuatilia.

33 Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma, mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.”

34 Vita vikaendelea mchana kutwa naye Mfalme Ahabu akategemezwa ndani ya gari kuelekea Waaramu. Damu kutoka kwenye jeraha lake ikachuruzika ndani ya gari na jioni yake akafa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/18-04ee92994ad35d860ec7046f7d9faa79.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 19

Mwonaji Yehu Amkemea Yehoshafati

1 Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu.

2 Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukiaBwana? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu yaBwanaiko juu yako.

3 Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.”

Yehoshafati Aweka Waamuzi

4 Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza watu wakamrudiaBwana, Mungu wa baba zao.

5 Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma.

6 Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mtendayo, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili yaBwanaambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu.

7 Basi sasa hofu yaBwanana iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwaBwanaMungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo wala rushwa.”

8 Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili yaBwanana kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu.

9 Akawapa maagizo haya: “Ni lazima mtumike kwa uaminifu na kwa moyo wote katika kicho chaBwana.

10 Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wale waishio katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine yahusuyo sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasitende dhambi dhidi yaBwana, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.

11 “Amaria Kuhani Mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lo lote linalomhusuBwananaye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kuhusiana na jambo lo lote la mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, nayeBwanaatakuwa pamoja na wale watendao vyema.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/19-738292e7d347d9b4cb4a35538b39fdae.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 20

1 Ikawa baada ya jambo hili, Wamoabu na Waamoni, pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja ili wapigane vita na Yehoshafati.

2 Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako toka Edomu na ng’ambo ya Bahari. Tayari wako Hasason-Tamari” (ndio En-Gedi).

3 Yehoshafati akaogopa, akaazimu kumtafutaBwana, akatangaza kwa Yuda wote kufunga.

4 Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwaBwana. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafutaBwana.

5 Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu katika Hekalu laBwana, mbele ya ua mpya,

6 akasema:

“EeBwana, Mungu wa baba zetu, si wewe ndiwe uliye Mungu mbinguni? Si wewe ndiwe utawalaye juu ya falme zote za mataifa? Uweza na nguvu viko mkononi mwako, wala hakuna ye yote awezaye kushindana nawe.

7 Je, si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Abrahamu, rafiki yako, hata milele?

8 Wameishi ndani yake na humo wamekujengea mahali patakatifu kwa ajili ya Jina lako, wakisema:

9 ‘Kama maafa yakitujia, ikiwa ni upanga, hukumu, tauni, au njaa, tutasimama mbele zako, mbele ya Hekalu hili ambalo limeitwa kwa Jina lako na kukulilia katika shida yetu, nawe utatusikia na kutuokoa.’

10 “Lakini sasa hawa watu wa kutoka Amoni, Moabu na Mlima Seiri, ambao hukuwaruhusu Israeli wazivamie nchi zao wakati walipotoka Misri, hivyo wakageukia mbali nao na hawakuwaangamiza,

11 tazama jinsi wanavyotulipa kwa kuja kututupa nje ya milki uliyotupa sisi kuwa urithi.

12 Ee Mungu wetu, je, wewe hutawahukumu? Kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa linalokuja kutushambulia. Sisi hatujui la kufanya, bali macho yetu yanakutazama wewe.”

13 Watu wa Yuda pamoja na wake zao, watoto wao na wadogo wao wakasimama mbele zaBwana.

14 Ndipo Roho waBwanaakaja juu ya mtu mmoja jina lake Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, Mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi mzao wa Asafu alipokuwa amesimama katika kusanyiko.

15 Akasema: “Sikilizeni, enyi Yuda wote nanyi nyote mkaao Yerusalemu, nawe Mfalme Yehoshafati! Hili ndiloBwanaasemalo kwenu, ‘Msiogope wala msifadhaike kwa sababu ya jeshi hili kubwa. Kwa maana vita hivi si vyenu, bali ni vya Mungu.

16 Kesho shukeni kukabiliana nao. Wanakwea kwa kupandia Genge la Sisi, nanyi mtawakuta mwisho wa bonde, kabla ya Jangwa la Yerueli.

17 Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovuBwanaatakaowapatia, Enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, nayeBwanaatakuwa pamoja nanyi.’ ”

18 Yehoshafati akainama na kusujudu uso wake hadi chini, nao watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakaanguka chini ili kuabudu mbele zaBwana.

19 Ndipo baadhi ya Walawi kutoka kwa Wakohathi na kwa wana wa Kora wakasimama na kumsifuBwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.

20 Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, nanyi watu wa Yerusalemu! MwamininiBwanaMungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.

21 Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbiaBwanana kumsifu katika uzuri wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema:

“MshukuruniBwana

kwa kuwa upendo wake wadumu milele.”

22 Walipoanza kuimba na kusifu,Bwanaakaweka waviziao dhidi ya watu wa Amoni, Moabu na wale wa Mlima Seiri waliokuwa wamekuja kuishambulia Yuda, nao wakashindwa.

23 Watu wa Amoni na Moabu wakawainukia watu wa Mlima Seiri ili kuwaua na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kumaliza kuwachinja watu wa Seiri, wakasaidia kuangamizana wao kwa wao.

24 Yuda walipofika katika mnara wa ulinzi wa jangwani, wakaliangalia lile jeshi kubwa, wakaona ni maiti tupu zimetapakaa ardhini, wala hakuna ye yote aliyenusurika.

25 Hivyo Yehoshafati na watu wake wakaenda kujitwalia nyara kutoka kwao, nao wakakuta humo wingi wa mifugo, mali, nguo na vitu vya thamani, ambavyo vilikuwa vingi zaidi ya vile walivyoweza kuchukua. Wakakusanya nyara kwa siku tatu kwa sababu zilikuwa nyingi mno.

26 Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Berakakwa maana huko ndiko walikomsifuBwana. Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka mpaka leo.

27 Kisha watu wote wa Yuda na Yerusalemu, wakiongozwa na Yehoshafati, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kwa kuwaBwanaalikuwa amewasababisha wafurahi juu ya adui zao.

28 Wakaingia Yerusalemu na kwenda hekaluni mwaBwanawakiwa na vinubi, zeze na tarumbeta.

29 Hofu ya Mungu ikazipata falme zote za nchi waliposikia jinsiBwanaalivyokuwa amepigana dhidi ya adui za Israeli.

30 Ufalme wa Yehoshafati ukawa na amani, kwa kuwa Mungu wake alikuwa amemstarehesha pande zote.

Mwisho Wa Utawala Wa Yehoshafati

31 Hivyo Yehoshafati akatawala Yuda. Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka ishirini na mitano. Mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi.

32 Akaiendea njia ya Asa baba yake wala hakuiacha, akifanya yaliyo mema machoni paBwanaMungu.

33 Lakini hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia miungu hapakuondolewa, nao watu wakawa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa, Mungu wa baba zao.

34 Matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Yehu mwana wa Hanani, ambazo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.

35 Hatimaye Yehoshafati mfalme wa Yuda akafanya urafiki na Ahazia mfalme wa Israeli ambaye alifanya maovu sana.

36 Akaungana naye kutengeneza meli nyingi za kwenda Tarshishi, nazo zilitengenezwa huko Esion-Geberi.

37 Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii dhidi ya Yehoshafati, akasema, “Kwa kuwa umeungana na Ahazia,Bwanaataangamiza vile mlivyotengeneza.” Zile meli zikavunjika na hazikuweza kung’oa nanga ili kwenda Tarshishi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/20-e6d8d078101cbc0df9cf616f0775a5a1.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 21

Yehoramu Atawala

1 Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi, mwanawe Yehoramu akaingia mahali pa baba yake kuwa mfalme.

2 Ndugu zake Yehoramu, wana wa Yehoshafati walikuwa: Azaria, Yehieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli na Shefatia. Hawa wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli.

3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali ufalme akampa Yehoramu kwa sababu alikuwa mwanawe mzaliwa wa kwanza.

4 Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli.

5 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane.

6 Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli, kama ilivyokuwa imefanya nyumba ya Ahabu, kwa sababu alioa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni paBwana.

7 Hata hivyo, kwa sababu ya Agano ambaloBwanaalikuwa amefanya na Daudi,Bwanahakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi, Mungu alikuwa ameahidi kumpa Daudi taa, yeye na wazao wake milele.

8 Wakati wa Yehoramu, Edomu iliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe.

9 Hivyo Yehoramu akaenda huko pamoja na maafisa wake na magari yake yote ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake yote ya vita, lakini akaondoka akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu.

10 Hadi leo Edomu imeasi Yuda.

Libna nao wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwachaBwana, Mungu wa baba zake.

11 Alikuwa pia ametengeneza mahali pa juu pa kuabudia miungu katika vilima vya Yuda na akawa amewasababisha watu wa Yerusalemu kufanya uzinzi na akawa amewapotosha watu wa Yuda.

12 Yehoramu akapokea barua kutoka kwa nabii Eliya iliyosema:

“Hili ndiloBwana, Mungu wa Daudi baba yako, asemalo: ‘Hukuenenda katika njia za Yehoshafati baba yako au za Asa mfalme wa Yuda.

13 Lakini umeenenda katika njia za wafalme wa Israeli, nawe umewaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu kuzini, kama vile nyumba ya Ahabu ilivyofanya. Pia umewaua ndugu zako mwenyewe, watu wa nyumbani mwa baba yako, watu waliokuwa bora kuliko wewe.

14 Hivyo basiBwanayu karibu kuwapiga watu wako, wanao, wake zako na kila kitu kilicho chako, kwa pigo zito.

15 Wewe mwenyewe utaugua sana kwa ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu, hadi ugonjwa utakaposababisha matumbo yako kutoka nje.’ ”

16 Bwanaakaamsha chuki ya Wafilisti na ya Waarabu walioishi karibu na Wakushi dhidi ya Yehoramu.

17 Wakaishambulia Yuda, wakaivamia na kuchukua mali zote zilizopatikana katika jumba la mfalme pamoja na wanawe na wake zake. Hakubakiziwa mwana ye yote isipokuwa Ahazia aliyekuwa mdogo wa wote.

18 Baada ya mambo haya yote,Bwanaakampiga Yehoramu kwa ugonjwa usioponyeka wa matumbo.

19 Ikawa baada ya muda, mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatoka nje kwa sababu ya ugonjwa, naye akafa katika maumivu makali sana. Watu wake hawakuwasha moto kwa heshima yake, kama walivyokuwa wamewafanyia baba zake.

20 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka minane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu ye yote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/21-fb2fb28b48a6df986161112880fff558.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 22

Ahazia Mfalme Wa Yuda

1 Watu wa Yerusalemu wakamfanya Ahazia, mdogo wa wote wa wana wa Yerohamu, kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwa sababu washambuliaji wa ghafula waliokuwa wameingia kambini pamoja na Waarabu, walikuwa wamewaua wana wakubwa wote wa Yehoramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akaanza kutawala.

2 Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia mjukuu wa kike wa Omri.

3 Ahazia naye akaziendea njia za nyumba ya Ahabu kwa sababu mama yake alikuwa mshauri wake katika kutenda maovu.

4 Akafanya yaliyo maovu machoni paBwanakama walivyokuwa wamefanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa baada ya kufa kwa baba yake nyumba ya Ahabu ndio waliokuwa washauri wake, kwa uangamivu wake.

5 Pia akafuata shauri lao alipokwenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu,

6 hivyo akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyokuwa ameyapata huko Ramoth, kwenye vita vyake na Hazaeli mfalme wa Aramu.

Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda, akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.

7 Mungu alikuwa ameamuru kwamba kuanguka kwa Ahazia kungetokea atakapokwenda kumwona Yoramu. Ahazia alipowasili, wakatoka pamoja na Yoramu ili kwenda kukutana na Yehu mwana wa Nimshi, ambayeBwanaalikuwa amemtia mafuta kuangamiza nyumba ya Ahabu.

8 Yehu alipokuwa anatekeleza hukumu juu ya nyumba ya Ahabu, akawakuta wakuu wa Yuda na wana wa jamaa ya Ahazia waliokuwa wanamhudumia Ahazia, naye akawaua.

9 Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamwua. Wakamzika kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafutaBwanakwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme.

Athalia na Yoashi

10 Athalia mamaye Ahazia alipoona kuwa mwanawe amekufa, akaondoka akawaua wazao wote wa kifalme wa nyumba ya Yuda.

11 Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia na kumwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa wanakaribia kuuawa. Akamweka yeye pamoja na yaya wake kwenye chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, mkewe Kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha mtoto ili Athalia asimwue.

12 Akawa pamoja nao akiwa amefichwa katika Hekalu la Mungu kwa muda wa miaka sita wakati Athalia alipokuwa anatawala nchi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/22-9535bc86352f36317895a9b0cead91a8.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 23

Uasi Dhidi Ya Athalia

1 Katika mwaka wa saba Yehoyada akaonyesha nguvu zake. Akafanya agano na majemadari wa vikosi vya mamia: Azaria mwana wa Yehoramu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya na Elishafati mwana wa Zikri.

2 Wakazunguka katika Yuda yote na kukusanya Walawi na viongozi wa jamaa za Israeli kutoka katika miji yote. Walipofika Yerusalemu,

3 kusanyiko lote likafanya agano na mfalme kwenye Hekalu la Mungu.

Yehoyada akawaambia, “Mwana wa mfalme atatawala, kamaBwanaalivyoahidi kuhusu wazao wa Daudi.

4 Basi hili ndilo liwapasalo kufanya: Theluthi ya makuhani wenu na Walawi ambao watakuwa kwenye zamu siku ya Sabato watalinda milangoni,

5 theluthi watalinda jumba la kifalme, theluthi nyingine watalinda Lango la Msingi. Watu wengine wote itawapasa wawe ndani ya nyua za Hekalu laBwana.

6 Hakuna ruhusa mtu ye yote kuingia Hekaluni mwaBwanaisipokuwa makuhani na Walawi walioko kwenye zamu. Wao wanaweza kuingia kwa sababu ni watakatifu, lakini watu wengine wote itawapasa kuangalia kile kilichoamriwa naBwana.

7 Walawi watajipanga kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha zake mkononi. Mtu mwingine ye yote aingiaye Hekaluni lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme po pote aendapo.”

8 Walawi na watu wote wa Yuda wakafanya vile vile kama Kuhani Yehoyada alivyoagiza. Kila mmoja akachukua watu wake, wale waliokuwa wakienda kwenye zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakitoka kwenye zamu, kwa sababu Kuhani Yehoyada hakuruhusu kikosi cho chote kiondoke.

9 Kisha akawapa majemadari wa vikosi vya mamia mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa mali ya Mfalme Daudi na ambazo zilikuwa ndani ya Hekalu la Mungu.

10 Akawapanga walinzi kumzunguka mfalme, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi. Wakakaa kwenye mduara kuanzia upande wa kusini hadi upande wa kaskazini wa Hekalu wakiizunguka madhabahu yote.

11 Yehoyada na wanawe wakamtoa nje Yoashi mwana wa mfalme nao wakamvika taji wakampa nakala ya Agano na kumtangaza kuwa mfalme. Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, nao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”

12 Athalia aliposikia kelele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akawaendea watu katika Hekalu laBwana.

13 Athalia akaangalia, tazama alikuwepo mfalme akiwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta na waimbaji wakiwa na vyombo vya uimbaji, walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kupiga kelele, akisema, “Uhaini! Uhaini!”

14 Kuhani Yehoyada akawatoa nje majemadari wa vikosi vya mia, waliokuwa viongozi wa jeshi na kuwaambia: “Mtoeni nje kati ya safu na mkamwue kwa upanga ye yote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Msimwulie ndani ya Hekalu laBwana.”

15 Kwa hiyo wakamkamata alipofika kwenye ingilio la Lango la Farasi katika viwanja vya jumba la kifalme wakamwulia hapo.

16 Kisha Yehoyada akafanya agano kwamba yeye na watu wote pamoja na mfalme watakuwa watu waBwana.

17 Kisha watu wote wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu pamoja na sanamu na kumwua Matani kuhani wa Baali mbele ya hizo madhabahu.

18 Kisha Kuhani Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu laBwanamikononi mwa makuhani, waliokuwa Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa zaBwanakama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, kwa kushangilia na kuimba kama Daudi alivyokuwa ameagiza.

19 Pia akawaweka mabawabu kwenye malango ya Hekalu laBwanaili kwamba kwa vyo vyote asije akaingia mtu ye yote aliye najisi.

20 Akawachukua majemadari wa mamia, watu waheshimiwa, viongozi wa watu pamoja na watu wote wa nchi na kumteremsha mfalme kutoka hekaluni mwaBwana. Wakaingia kwenye jumba la kifalme kwa kupitia Lango la Juu na kumkalisha mfalme kwenye kiti cha enzi cha ufalme,

21 nao watu wote wa nchi wakafurahi. Mji ukatulia kwa sababu Athalia alikuwa ameuawa kwa upanga.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/23-b6936cf294b110a947eb1843261e8c10.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 24

Yoashi Akarabati Hekalu

1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia aliyekuwa ametoka Beer-Sheba.

2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni paBwanamiaka yote ya Yehoyada kuhani.

3 Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike.

4 Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu laBwana.

5 Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi.

6 Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada Kuhani Mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Mose mtumishi waBwanapamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema ya Ushuhuda?”

7 Kwa kuwa wana wa yule mwanamke mwovu Athalia, walikuwa wamevunja na kuingia katika Hekalu la Mungu, nao wakawa wamevitumia hata vile vitu vilivyowekwa wakfu kwaBwanakwa mabaali.

8 Kwa amri ya mfalme, likatengenezwa kasha, nalo likawekwa nje kwenye lango la Hekalu laBwana.

9 Tangazo likatolewa katika Yuda na Yerusalemu kwamba inapasa wamleteeBwanakodi ile ambayo Mose, mtumishi waBwanaalikuwa amewaagiza Israeli huko jangwani.

10 Maafisa wote na watu wote wakaleta michango yao kwa furaha, wakaweka kwenye kasha mpaka likajaa.

11 Ikawa kila wakati kasha lilipoletwa ndani na Walawi kwa maafisa wa mfalme na kuona kwamba kuna kiasi kikubwa cha fedha, mwandishi wa mfalme na afisa wa Kuhani Mkuu walikuwa wanakuja na kumimina, kisha kulirudisha mahali pake. Walifanya hivi mara kwa mara, nao wakakusanya fedha nyingi sana.

12 Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu laBwana. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu laBwana, pia wafanya kazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu laBwana.

13 Watu walioshughulika na kazi walikuwa wenye bidii, nayo kazi ya kukarabati ikaendelea vizuri mikononi mwao. Wakalitengeneza upya Hekalu laBwanalikarudi katika hali yake ya awali na kuliimarisha.

14 Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu laBwana: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada alipokuwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu laBwana.

15 Basi Yehoyada alikuwa mzee aliyeshiba siku wakati alipokufa. Alikufa akiwa na umri wa miaka 130.

16 Wakamzika pamoja na wafalme katika Mji wa Daudi, kwa sababu ya mema aliyokuwa ametenda katika Israeli kwa ajili ya Mungu na Hekalu lake.

Uovu Wa Yoashi

17 Baada ya kifo cha Yehoyada, wakuu wa Yuda walikuja kumpa mfalme heshima, naye akawasikiliza.

18 Wakaacha Hekalu laBwana, Mungu wa baba zao, wakaabudu nguzo za maashera na sanamu. Kwa sababu ya kosa lao, hasira ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu.

19 IngawaBwanaaliwatuma manabii wawarudishe watu kwake na ingawa waliwaonya, hawakuwasikiliza.

20 Ndipo Roho waBwanaakaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri zaBwana? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwachaBwana, yeye naye amewaacha ninyi.’ ”

21 Lakini wakafanya shauri baya juu yake na kwa amri ya mfalme wakampiga kwa mawe mpaka akafa katika ukumbi wa Hekalu laBwana.

22 Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria ila alimwua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “Bwanana alione hili na alipize kisasi.”

23 Mwishoni mwa ule mwaka, jeshi la Waaramu likaja dhidi ya Yoashi, likavamia Yuda na Yerusalemu na kuwaua viongozi wote wa watu. Wakapeleka nyara zao zote kwa mfalme wao huko Dameski.

24 Ingawa jeshi la Waaramu lilikuwa limekuja na watu wachache tu,Bwanaakatia mikononi mwao jeshi kubwa kuliko lao. Kwa sababu Yuda walikuwa wamemwachaBwana, Mungu wa baba zao, hukumu ilitekelezwa juu ya Yoashi.

25 Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakafanya hila dhidi yake kwa sababu alikuwa amemwua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamwulia kitandani mwake. Hivyo akafa na wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.

26 Wale waliofanya hila mbaya dhidi yake walikuwa Zabadi, mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, Yehozabadi, mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabi.

27 Kwa habari za wanawe, unabii mwingi kumhusu na kumbukumbu za kutengenezwa upya kwa Hekalu la Mungu, zimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme. Amazia mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/24-a1cf888b463e80b8736a814ed1081f27.mp3?version_id=1627—