2 Mambo ya nyakati 35

Mfalme Yosia Anaadhimisha Pasaka

1 Yosia akaadhimisha Pasaka kwaBwanakatika Yerusalemu, mwana-kondoo wa Pasaka akachinjwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.

2 Akawaweka makuhani kwenye wajibu wao na kuwatia moyo katika utumishi wa Hekalu laBwana.

3 Akawaambia Walawi, waliowafundisha Waisraeli wote na ambao walikuwa wamejiweka wakfu kwa ajili ya kazi yaBwana, “Liwekeni hilo Sanduku takatifu katika Hekalu lile alilojenga Solomoni mwana wa Daudi mfalme wa Israeli. Halipaswi kubebwa huko na huko mabegani mwenu. Sasa mtumikieniBwanaMungu wenu na watu wake Israeli.

4 Jiandaeni kwa kufuata jamaa zenu katika migawanyo yenu, kufuatana na maelezo yaliyoandikwa na Daudi mfalme wa Israeli na mwanawe Solomoni.

5 “Simameni mahali patakatifu kwa kufuata migawanyo ya jamaa za baba zenu kulingana na koo zenu na pawepo Walawi kwa ajili ya kila mgawanyo wa nyumba ya baba zenu.

6 Chinjeni mwana-kondoo wa Pasaka, jitakaseni, nanyi kwa niaba ya koo zenu fanyeni maandalizi, mkitenda sawasawa na neno laBwanakwa mkono wa Mose.”

7 Ndipo Yosia akawapa watu wote wana-mbuzi waliokuwepo jumla ya kondoo wapatao 30,000 kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ng’ombe 10,000, vyote hivi kutoka katika mali binafsi ya mfalme.

8 Pia maafisa wake, wakatoa kwa hiari yao wakawapa watu, makuhani na Walawi. Hilkia, Zekaria na Yehieli, waliokuwa maafisa wakuu wa Hekalu la Mungu, wakawapa makuhani sadaka za Pasaka wana-kondoo na wana-mbuzi 2,600 na mafahali 300.

9 Konania na nduguze wawili, Shemaya na Nethaneli, pamoja na Hashabia, Yeieli na Yozabadi waliokuwa viongozi wa Walawi, nao pia wakawapa Walawi wana-kondoo na wana-mbuzi 5,000 na mafahali 500, kwa ajili ya sadaka za Pasaka.

10 Huduma ilipomalizika kuandaliwa makuhani wakasimama mahali pao na Walawi katika migawanyo yao kama mfalme alivyokuwa ameamuru.

11 Wana kondoo wa Pasaka wakachinjwa, nao makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa, wakati Walawi wakiwa wanawachuna wale wanyama ngozi.

12 Wakatenga sadaka za kuteketezwa ili waweze kugawia ili migawanyo kwa kufuata jamaa za baba zao ili watoe sadaka kwaBwanakama ilivyoandikwa katika kitabu cha Mose. Wakafanya vivyo hivyo kwa wale mafahali.

13 Wakawaoka wale wanyama wa Pasaka kwenye moto kama ilivyoamuriwa, wakachemsha zile sadaka takatifu kwenye vyungu, masufuria makubwa na vikaango na kuwagawia watu wote upesi.

14 Hatimaye wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu wale makuhani, yaani, wazao wa Aroni, walikuwa wanatoa sadaka za kuteketezwa pamoja na zile sehemu zilizonona mpaka usiku. Hivyo Walawi wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani wa uzao wa Aroni.

15 Waimbaji, wazao wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagizwa na Mfalme Daudi, Asafu, Hemani na Yeduthuni mwonaji wa Mfalme. Mabawabu katika kila lango hawakuhitaji kuacha nafasi zao kwa sababu Walawi wenzao walifanya maandalizi kwa ajili yao.

16 Kwa hiyo wakati ule huduma yote yaBwanailifanyika katika kuadhimisha Pasaka, kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu yaBwanakama alivyoamuru Mfalme Yosia.

17 Waisraeli waliokuwepo wakaadhimisha Pasaka wakati huo na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa siku saba.

18 Kulikuwa hakujafanyika Pasaka kama hii katika Israeli tangu siku za nabii Samweli wala hakukuwa na mfalme ye yote wa Israeli ambaye kamwe alishaadhimisha Pasaka kama ile aliyofanya Mfalme Yosia, akiwa na makuhani, Walawi na watu wote wa Yuda na watu wa Israeli waliokuwepo huko, pamoja na watu wa Yerusalemu.

19 Pasaka iliadhimishwa katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia.

Kifo Cha Yosia

20 Baada ya haya yote, Yosia alipomaliza kulitengeneza vizuri Hekalu, Neko mfalme wa Misri, akapanda ili kupigana huko Karkemishi katika Mto Eufrati, naye Yosia akatoka kwenda kupigana naye.

21 Lakini Neko akamtumia wajumbe kusema, “Kuna ugomvi gani kati yangu mimi na wewe, Ee Mfalme wa Yuda? Si wewe ninayekushambulia wakati huu, bali ile nyumba ambayo nina vita nayo, Mungu ameniambia niharakishe, kwa hivyo acha kumpinga Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.”

22 Lakini hata hivyo, Yosia hakukubali kumwacha, bali alijibadilisha ili kupigana naye vita. Hakusikiliza yale Neko aliyokuwa amemwambia kwa agizo la Mungu bali alikwenda kupigana naye katika tambarare ya Megido.

23 Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, naye akawaambia maafisa wake, “Niondoeni, nimejeruhiwa vibaya sana.”

24 Kwa hiyo wakamshusha kutoka kwenye gari lake la farasi, wakamweka kwenye gari lingine alilokuwa nalo na kumleta Yerusalemu, ambako alifia. Akazikwa katika makaburi ya baba zake, nayo Yuda yote na Yerusalemu wakamwombolezea.

25 Nabii Yeremia akatunga maombolezo kwa ajili ya kifo chake, nao waimbaji wote, wanaume kwa wanawake, hufanya ukumbusho wa Yosia katika maombolezo hadi leo. Haya yakafanywa desturi katika Israeli nayo yameandikwa katika Maombolezo.

26 Matukio mengine ya utawala wa Yosia na matendo yake mema, kulingana na yale yaliyoandikwa katika sheria yaBwana

27 matukio yote, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/35-5eb28a8d57fe3b463b9b3dc3e4e9742e.mp3?version_id=1627—

2 Mambo ya nyakati 36

Mfalme Yehoahazi Wa Yuda

1 Watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia na kumfanya aingie mahali pa baba yake kuwa mfalme katika Yerusalemu.

2 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miezi mitatu.

3 Mfalme wa Misri akamwondoa madarakani huko Yerusalemu na akatoza Yuda kodi ya talanta 100za fedha na talanta mojaya dhahabu.

4 Mfalme wa Misri akamweka Eliyakimu, nduguye Yehoahazi, kuwa mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu na kubadili jina la Eliyakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini Neko akamchukua Yehoahazi, Nduguye Eliyakimu akampeleka Misri.

Yehoyakimu Mfalme Wa Yuda

5 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. Akafanya maovu machoni paBwanaMungu wake.

6 Nebukadneza mfalme wa Babeli akamshambulia na kumfunga kwa pingu za shaba akampeleka Babeli.

7 Nebukadneza akachukua pia vyombo kutoka katika Hekalu laBwanana kuviweka katika hekalu lakehuko Babeli.

8 Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu, machukizo aliyoyafanya na yote yaliyoonekana dhidi yake, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. Yehoyakimu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

9 Yehoyakimu alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi. Akafanya yaliyo maovu machoni paBwana.

10 Mnamo majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka katika Hekalu laBwananaye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.

Mfalme Sedekia Wa Yuda

11 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka kumi na mmoja.

12 Akafanya yaliyo maovu machoni paBwanaMungu wake wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno laBwana.

13 Pia alimwasi Mfalme Nebukadneza, ambaye alikuwa amemwapisha kwa jina la Mungu. Akashupaza shingo na akafanya moyo wake kuwa mgumu wala hakutaka kumgeukiaBwana, Mungu wa Israeli.

14 Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu laBwanaalilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu.

Kuanguka Kwa Yerusalemu

15 Bwana, Mungu wa baba zao, akawapelekea neno kupitia wajumbe wake tena na tena, kwa sababu alikuwa anawahurumia watu wake pamoja na mahali pa maskani yake.

16 Lakini waliwadhihaki wajumbe waBwanawakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake mpaka ghadhabu yaBwanaikawa kubwa dhidi ya watu wake na hakukuwa na namna ya kuituliza.

17 Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza.

18 Akavichukua kwenda Babeli vyombo vyote kutoka katika Hekalu la Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za Hekalu laBwanapamoja na hazina za mfalme na za maafisa wake.

19 Wakalitia moto Hekalu la Mungu na kuzibomoa kuta za Yerusalemu, wakachoma moto majumba yote ya kifalme na kuharibu kila kitu chake cha thamani.

20 Wale watu walionusurika kuuawa kwa upanga wakachukuliwa kwenda uhamishoni Babeli, nao wakawa watumishi wake na wa wanawe mpaka wakati wa utawala wa ufalme wa Uajemi.

21 Nchi ikaendelea kufurahia pumziko lake la Sabato, wakati wote wa kufanywa kwake ukiwa ilipumzika mpaka ile miaka sabini ilipotimia katika kutimiza neno laBwanalililonenwa na Yeremia.

Koreshi Atangaza Uhuru Kwa Waliokuwa Uhamishoni

22 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili litimie lile neno laBwanalililosemwa na nabii Yeremia,Bwanaakausukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutoa tangazo kwa maandishi katika utawala wake wote:

23 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Ye yote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, huyo mtu na apande.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/36-a1021885c5760e6e2e55b215f5fd4a01.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 1

Adamu Hadi Wana Wa Noa

1 Adamu, Sethi, Enoshi,

2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi,

3 Henoko, Methusela, Lameki, Noa.

4 Wana wa Noa:

Shemu, Hamu na Yafethi.

Wana Wa Yafethi

5 Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

6 Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

7 Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Warodanimu.

Wana Wa Hamu

8 Wana wa Hamu walikuwa:

# Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.

9 Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

10 Kushi alimzaa

Nimrodi aliyekuwa mtu shujaa katika nchi.

11 Misraimu akawazaa

Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi,

12 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.

13 Wana wa Kanaani walikuwa:

Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,

14 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

15 Wahivi, Waariki, Wasini,

16 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Wana Wa Shemu

17 Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuri, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

18 Arfaksadi akamzaa Shela,

Shela akamzaa Eberi.

19 Eberi alikuwa na wana wawili:

# Mmoja wao aliitwa Pelegikwa sababu ni katika wakati wake dunia iligawanyika, ndugu yake aliitwa Yoktani.

20 Wana wa Yoktani walikuwa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

21 Hadoramu, Uzali, Dikla,

22 Obali, Abimaeli, Sheba,

23 Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.

24 Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,

25 Eberi, Pelegi, Reu,

26 Serugi, Nahori, Tera,

27 Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).

Jamaa Ya Abrahamu

28 Abrahamu alikuwa na wana wawili:

Isaki na Ishmaeli.

Wazao Wa Hagari

29 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:

Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,

30 Mishma Duma, Masa, Hadadi, Tema,

31 Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.

Wazao Wa Ketura

32 Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:

Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.

Wana wa Yokshani walikuwa:

Sheba na Dedani.

33 Wana wa Midiani walikuwa:

Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.

Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.

Wazao Wa Sara

34 Abrahamu alikuwa baba wa Isaki.

Wana wa Isaki walikuwa:

Esau na Israeli.

Wana Wa Esau

35 Wana wa Esau walikuwa:

Elifazi, Rehueli, Yeushi, Yalamu na Kora.

36 Wana wa Elifazi walikuwa:

Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;

Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.

37 Wana wa Rehueli walikuwa:

Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu

38 Wana wa Seiri walikuwa:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.

39 Wana wa Lotani walikuwa wawili:

Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.

40 Wana wa Shobali walikuwa:

# Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

Wana wa Sibeoni walikuwa:

Aya na Ana.

41 Mwana wa Ana alikuwa:

Dishani.

Nao wana wa Dishani walikuwa:

Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

42 Wana wa Eseri walikuwa:

Bilhani, Zaavani na Akani.

Wana wa Dishani walikuwa:

Usi na Arani.

Watawala Wa Edomu

43 Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme ye yote wa Waisraeli:

Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.

44 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akaingia mahali pake kuwa mfalme.

45 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akaingia mahali pake kuwa mfalme.

46 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akaingia mahali pake kuwa mfalme, mji wake uliitwa Avithi.

47 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akaingia mahali pake kuwa mfalme.

48 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ulio karibu na Mto Eufrati, akaingia mahali pake kuwa mfalme.

49 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akaingia mahali pake kuwa mfalme.

50 Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akaingia mahali pake kuwa mfalme. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.

51 Naye Hadadi pia akafa.

Wakuu wa Edomu walikuwa:

Timna, Alva, Yethethi,

52 Oholibama, Ula, Pinoni,

53 Kenazi, Temani, Mibsari,

54 Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/1-f4c06fda4cc22e1527f752ad96ef473c.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 2

Wana Wa Israeli

1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:

Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni,

2 Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.

Yuda

Hadi Wana Wa Hesroni

3 Wana wa Yuda walikuwa:

waliozaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua: ni Eri, Onani na Shela. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni paBwanakwa hiyoBwanaalimwua.

4 Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.

5 Wana wa Peresi ni:

Hesroni na Hamuli.

6 Wana wa Zera walikuwa:

Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Daido. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.

7 Mwana wa Karmi, alikuwa:

# Akari,ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu ambavyo vilikuwa vimewekwa wakfu.

8 Mwana wa Ethani alikuwa:

Azariya.

9 Wana wa Hesroni walikuwa:

Yerameeli, Ramu na Kalebu.

Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni

10 Ramu alimzaa

Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.

11 Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi,

12 Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.

13 Yese akawazaa

# Eliyabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimei,

14 wa nne Nethaneli, wa tano Radai,

15 wa sita Osemu, na wa saba Daudi.

16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.

17 Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

Kalebu Mwana Wa Hesroni

18 Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni.

19 Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri.

20 Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.

21 Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu.

22 Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi.

23 (Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hayothi-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.

24 Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.

Yerameeli Mwana Wa Hesroni

25 Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:

Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.

26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.

27 Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:

Maasi, Yamini na Ekeri.

28 Wana wa Onamu walikuwa:

Shamai na Yada.

Wana wa Shamai walikuwa:

Nadabu na Abishuri.

29 Mke wa Abishuri aliitwa Abihali, ambaye alimzalia Abani na Molidi.

30 Wana wa Nadabu walikuwa

Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.

31 Apaimu akamzaa:

Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani.

Sheshani akamzaa Alai.

32 Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:

Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.

33 Wana wa Yonathani walikuwa:

Pelethi na Zaza.

Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.

34 Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu.

Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha.

35 Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.

36 Atai akamzaa Nathani,

Nathani akamzaa Zabadi,

37 Zabadi akamzaa Eflali,

Eflali akamzaa Obedi,

38 Obedi akamzaa Yehu,

Yehu akamzaa Azaria,

39 Azaria akamzaa Helesi,

Helesi akamzaa Eleasa,

40 Eleasa akamzaa Sismai,

Sismai akamzaa Shalumu,

41 Shalumu akamzaa Yekamia,

naye Yekamia akamzaa Elishama.

Koo Za Kalebu

42 Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:

Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.

43 Hebroni alikuwa na wana wanne:

Kora, Tapua, Rekemu na Shema.

44 Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai.

45 Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.

46 Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.

47 Wana wa Yadai walikuwa:

Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.

48 Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana.

49 Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa.

50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu.

Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa:

Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu,

51 Salma akamzaa Bethlehemu, naye Herefu akamzaa Beth-Gaderi.

52 Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:

Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi,

53 pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.

54 Wazao wa Salma walikuwa:

Bethlehemu, Wanetofathi, Waatrothi-Beth-Yoabu, nusu ya Wamenahathi, Wasori,

55 pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/2-a1dde605f23315c89d40233f2faf3c77.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 3

Wana Wa Daudi

1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:

Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli;

wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;

2 Wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;

Wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;

3 Wa tano, alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali;

wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.

4 Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita.

Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu,

5 nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu:

# mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Solomoni.

6 Pia kulikuwa na wana wengine: Ibhari, Elishua, Elifeleti,

7 Noga, Nefegi, Yafia,

8 Elishama, Eliyada na Elifeleti; wote walikuwa tisa.

9 Hawa wote walikuwa wana wa Daudi mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.

Wafalme Wa Yuda

10 Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu,

mwanawe huyo alikuwa Abiya,

mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati,

mwanawe huyo alikuwa Asa,

11 mwanawe huyo alikuwa Yehoramu,

mwanawe huyo alikuwa Ahazia,

mwanawe huyo alikuwa Yoashi,

12 mwanawe huyo alikuwa Amazia,

mwanawe huyo alikuwa Azaria,

mwanawe huyo alikuwa Yothamu,

13 mwanawe huyo alikuwa Ahazi,

mwanawe huyo alikuwa Hezekia,

mwanawe huyo alikuwa Manase,

14 mwanawe huyo alikuwa Amoni

na mwanawe huyo alikuwa Yosia.

15 Wana wa Yosia walikuwa:

Yohana ni mzaliwa wake wa kwanza,

Yehoyakimu mwanawe wa pili,

wa tatu Sedekia,

wa nne Shalumu.

16 Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni:

Yekonia mwanawe,

na Sedekia.

Ukoo Wa Kifalme Baada Ya Uhamisho

17 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka:

Shealtieli,

18 Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.

19 Wana wa Pedaya walikuwa:

Zerubabeli na Shimei.

Wana wa Zerubabeli walikuwa:

Meshulamu na Hanania.

Shelomithi alikuwa dada yao.

20 Pia walikuwepo wengine watano:

Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.

21 Wazao wa Hanania walikuwa:

Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.

22 Wazao wa Shekania:

Shemaya na wanawe:

Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.

23 Wana wa Nearia walikuwa:

Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.

24 Wana wa Elioenai walikuwa:

Hodavia, Eliyashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/3-63383f6fd4d3a50103c8a68bec68b895.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 4

Koo Nyingine Za Yuda

1 Wana wa Yuda walikuwa:

Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.

2 Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Wasorathi.

3 Hawa ndio waliokuwa wana wa Etamu:

Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi.

4 Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha.

Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu.

5 Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.

6 Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.

7 Wana wa Hela walikuwa:

Serethi, Sohari, Ethnani,

8 na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.

9 Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.”

10 Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

11 Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni.

12 Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Ir-Nahashi. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Reka.

13 Wana wa Kenazi walikuwa:

Othnieli na Seraya.

Wana wa Othnieli walikuwa:

Hathathi na Meonathai.

14 Meonathai akamzaa Ofra.

Seraya akamzaa Yoabu,

# baba wa Ge-Harashimu. Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi.

15 Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu:

Iru, Ela na Naamu.

Naye mwana wa Ela alikuwa:

Kenazi.

16 Wana wa Yahaleleli walikuwa:

Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.

17 Wana wa Ezra walikuwa:

Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Mmojawapo wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa.

18 Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa.

19 Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa:

baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi.

20 Wana wa Shimoni walikuwa:

Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni.

Wazao wa Ishi walikuwa:

Zohethi na Ben-Zohethi.

21 Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa:

Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi waliokuwa wakiishi huko Beth-Ashbea,

22 Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yoshubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.)

23 Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme.

Simeoni

24 Wazao wa Simeoni walikuwa:

Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli.

25 Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma.

26 Wazao wa Mishma walikuwa:

Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei.

27 Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda.

28 Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hazar-Shuali,

29 Bilha, Ezemu, Toladi,

30 Bethueli, Horma, Siklagi,

31 Beth-Markabothi, Hazar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi.

32 Vijiji vilivyoizunguka vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani jumla miji mitano,

33 pamoja na vijiji vyote kuizunguka hii miji hadi huko Baalathi. Haya yalikuwa makao yao, wao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao.

34 Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia,

35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.

36 Pia Elieonai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaya,

37 Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya.

38 Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao. Jamaa zao ziliongezeka sana,

39 wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao.

40 Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.

41 Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao.

42 Watu wa kabila la wa Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri.

43 Wakawaua Waamaleki waliobaki waliokuwa wamenusurika, nao wanaishi huko hadi leo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/4-6eb0fdddf0ca8f310fb8cf2047399897.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 5

Wana Wa Reubeni

1 Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli, hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa,

2 ingawa Yuda alikuwa na nguvu zaidi ya ndugu zake wote, na kwamba mtawala alitoka kwake, haki za mzaliwa wa kwanza zilikuwa za Yosefu.)

3 Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli walikuwa:

Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.

4 Wazao wa Yoeli walikuwa:

Shemaya mwanaye, Gogu mwanaye;

Shimei mwanaye,

5 Milka mwanaye,

Reaya mwanaye, Baali mwanaye,

6 na Beera mwanawe, ambaye Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alimchukua kwenda uhamishoni. Beera alikuwa kiongozi wa Wareubeni.

7 Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa kufuata koo zao kama ifuatavyo:

Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria,

8 Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni.

9 Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Eufrati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.

10 Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi.

Wana Wa Gadi

11 Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka.

12 Yoeli alikuwa ndiye mkuu wao, Shafamu alikuwa wa pili, wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani.

13 Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba:

Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi.

14 Hawa walikuwa ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yahdo, mwana wa Buzi.

15 Ahi mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa ndiye kiongozi wa jamaa yao.

16 Wagadi waliishi Gileadi, huko Bashani pamoja na vijiji vilivyoizunguka, pia katika nchi yote ya malisho ya Sharoni kote walikoenea.

17 Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.

18 Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo.

19 Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu.

20 Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea.

21 Walitwaa mifugo ya Wahagari: ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000. Pia wakateka watu 100,000,

22 na wengine wengi waliuawa kwa sababu vita vilikuwa ni vya Mungu. Nao waliendelea kuikalia nchi hiyo mpaka wakati wa uhamisho.

Nusu Ya Kabila La Manase

23 Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni.

24 Hawa ndio waliokuwa viongozi wa jamaa za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yahdieli. Walikuwa askari shujaa watu maarufu, viongozi wa jamaa zao.

25 Lakini hawakuwa waaminifu kwa Mungu wa baba zao, nao wakafanya ukahaba kwa miungu ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameyaangamiza mbele yao.

26 Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/5-7f92016b21d1f3baee614f26c685965c.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 6

Wana Wa Lawi

1 Wana wa Lawi walikuwa:

Gershoni, Kohathi na Merari.

2 Wana wa Kohathi walikuwa:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

3 Amramu alikuwa na wana:

Aroni, Mose, na Miriamu.

Aroni alikuwa na wana:

Nadabu, Abihu, Eliyazari na Ithamari.

4 Eliyazari akamzaa Finehasi,

Finehasi akamzaa Abishua,

5 Abishua akamzaa Buki,

Buki akamzaa Uzi,

6 Uzi akamzaa Zerahia,

Zerahia akamzaa Merayothi,

7 Merayothi akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

8 Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Ahimaasi,

9 Ahimaasi akamzaa Azaria,

Azaria akamzaa Yohanani,

10 Yohanani akamzaa Azaria (ndiye aliyefanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu),

11 Azaria akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

12 Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Shalumu,

13 Shalumu akamzaa Hilkia,

Hilkia akamzaa Azaria,

14 Azaria akamzaa Seraya,

Seraya akamzaa Yehosadaki.

15 Yehosadaki alihamishwa wakatiBwanaalipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.

16 Wana wa Lawi walikuwa:

Gershoni, Kohathi na Merari.

17 Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:

Libni na Shimei.

18 Wana wa Kohathi walikuwa:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

19 Wana wa Merari walikuwa:

Mahli na Mushi.

Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao:

20 Wazao wa Gershoni:

Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi,

Yahathi akamzaa Zima,

21 Zima akamzaa Yoa,

Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera,

Zera akamzaa Yeatherai.

22 Wazao wa Kohathi:

Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora,

Kora akamzaa Asiri,

23 Asiri akamzaa Elikana,

Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,

24 Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,

Urieli akamzaa Usia, Usia akamzaa Shauli.

25 Wazao wa Elikana walikuwa:

Amasia na Ahimothi,

26 Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai,

Sofai akamzaa Nahathi,

27 Nahathi akamzaa Eliyabu,

Eliyabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana,

Elikana akamzaa Samweli.

28 Wana wa Samweli walikuwa:

Yoeli mzaliwa wake wa kwanza

na Abiya mwanawe wa pili.

29 Wafuatao ndio wazao wa Merari:

Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,

Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

30 Uza akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Hagia,

Hagia akamzaa Asaia.

Waimbaji Wa Hekalu

31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba yaBwanabaada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.

32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu laBwanahuko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

33 Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:

Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:

Hemani, mpiga kinanda,

alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,

34 mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,

mwana wa Elieli, mwana wa Toa,

35 mwana wa Zufu, mwana wa Elikana,

mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,

36 mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli,

mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,

mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,

mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;

39 na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:

Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,

40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,

mwana wa Malkiya,

41 mwana wa Ethni,

mwana wa Zera, mwana wa Adaia,

42 mwana wa Ethani, mwana wa Zima,

mwana wa Shimei,

43 mwana wa Yahathi,

mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

44 Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto ni:

Elthani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi,

mwana wa Maluki,

45 mwana wa Hashabia,

mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,

46 mwana wa Amsi, mwana wa Bani,

mwana wa Shemeri,

47 mwana wa Mahli,

mwana wa Mushi, mwana wa Merari,

mwana wa Lawi.

48 Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.

49 Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.

50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:

Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,

Finehasi akamzaa Abishua,

51 Abishua akamzaa Buki,

Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Serahia,

52 Serahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

53 Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Ahimaasi.

54 Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao. (Walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka.

56 Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.

57 Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa,

58 Hileni, Debiri,

59 Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho.

60 Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.

Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.

61 Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

62 Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

63 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

64 Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho.

65 Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

66 Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.

67 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri,

68 Yokmeamu, Beth-Horoni

69 Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.

70 Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki wa miji ya Eneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.

71 Wagerishoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:

Katika nusu ya kabila la Manase:

walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.

72 Kutoka kabila la Isakari

walipokea Kedeshi, Daberathi,

73 Ramoth na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

74 Kutoka kabila la Asheri

walipokea Mashali, Abdoni,

75 Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

76 Kutoka kabila la Naftali

walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.

77 Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:

kutoka kabila la Zabuloni

walipokea Yokneamu, Karta, Rimono na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.

78 Kutoka kabila la Reubeni, ng’ambo ya Yordani mashariki ya Yeriko

walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahsa,

79 Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.

80 Na kutoka kabila la Gadi

walipokea Ramoth huko Gileadi, Mahanaimu,

81 Heshboni na Yezeri pamoja na maeneo yake ya malisho.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/6-be4a48d34bb471def64fcf4a8a0a6e97.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 7

Wana Wa Isakari

1 Wana wa Isakari walikuwa:

Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.

2 Wana wa Tola walikuwa:

Uzi, Refaia, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.

3 Mwana wa Uzi alikuwa:

Izrahia.

Wana wa Izrahia walikuwa:

Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao.

4 Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.

5 Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.

Wana Wa Benyamini

6 Wana watatu wa Benyamini walikuwa:

Bela, Bekeri na Yediaeli.

7 Wana wa Bela walikuwa:

Esboni, Uzi, Uzieli, Yerimothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.

8 Wana wa Bekeri walikuwa:

Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elieonai, Omri, Yerimothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri.

9 Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.

10 Mwana wa Yadiaeli alikuwa:

Bilhani.

Wana wa Bilhani walikuwa:

Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana. Zethani, Tarshishi na Ahishahari.

11 Hawa wana wote wa Yadiaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.

12 Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.

Wana Wa Naftali

13 Wana wa Naftali walikuwa:

Yahzieli, Guni, Yezeri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.

Wana Wa Manase

14 Wana wa Manase walikuwa:

Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi.

15 Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka.

Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.

16 Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.

17 Mwana wa Ulamu alikuwa:

Bedani.

Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase.

18 Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.

19 Wana wa Shemida walikuwa:

Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.

Wana Wa Efraimu

20 Wana wa Efraimu walikuwa:

Shuthela, ambaye alimzaa Beredi,

Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada,

Eleada akamzaa Tahathi,

21 Tahathi akamzaa Zabadi,

na Zabadi akamzaa Shuthela.

Ezeri na Eliyadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyang’anya mifugo yao.

22 Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi na jamaa zake wakaja kumfariji.

23 Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake.

24 Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliyeijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.

25 Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,

Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,

26 Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi,

Amihudi akamzaa Elishama,

27 Elishama akamzaa Nuni,

Nuni akamzaa Yoshua.

28 Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake.

29 Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.

Wana Wa Asheri

30 Wana wa Asheri walikuwa:

Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.

31 Wana wa Beria walikuwa:

Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.

32 Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.

33 Wana wa Yafleti walikuwa:

Pasaki, Bimhali na Ashvathi.

Hawa walikuwa wana wa Yafleti.

34 Wana wa Shomeri walikuwa:

Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.

35 Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa:

Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.

36 Wana wa Sofa walikuwa:

Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,

37 Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithranina Beera.

38 Wana wa Yetheri walikuwa:

Yefune, Pispa na Ara.

39 Wana wa Ula walikuwa:

Ara, Hanieli na Risia.

40 Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/7-a955d51240c25438619d34e26d9a6df2.mp3?version_id=1627—

1 Mambo ya Nyakati 8

Ukoo Wa Sauli Mbenyamini

1 Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza,

Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,

2 Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.

3 Wana wa Bela walikuwa:

Adari, Gera, Abihudi,

4 Abishua, Naamani, Ahoa,

5 Gera, Shefufani na Huramu.

6 Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:

7 Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliyewaongoza kwenda uhamishoni.

8 Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara.

9 Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yoabu, Sibia, Mesha, Malkamu,

10 Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao.

11 Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.

12 Wana wa Elpaali walikuwa:

Eberi, Mishamu, Shemedi (ambaye aliijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka),

13 na Beria na Shema, ambao walikuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.

14 Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yerimothi,

15 Zebadia, Aradi, Ederi,

16 Mikaeli, Ishpa, na Yoha.

17 Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi,

18 Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Epaali.

19 Wana wa Shimei walikuwa Yakimu, Zikri, Zabdi,

20 Elienai, Zilethai, Elieli,

21 Adaya, Beraya na Shimrathi.

22 Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli,

23 Abdoni, Zikri, Hanani,

24 Hanania, Elamu, Anthothiya,

25 Ifdeya na Penueli.

26 Wana wa Yerohamu walikuwa Shamsherai, Sheharia, Athalia,

27 Yaareshia, Eliya na Zikri.

28 Hawa wote walikuwa ni viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

29 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.

Mke wake aliitwa Maaka.

30 Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Abdoni, wakafuatia Zuri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,

31 Gedori, Ahio, Zekeri,

32 na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao katika Yerusalemu.

33 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.

34 Yonathani akamzaa:

# Merib-Baali, naye Merib-Baali akamzaa Mika.

35 Wana wa Mika walikuwa:

Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.

36 Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada aliwazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa.

37 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, Rafa akamzaa Eleasa na Aseli.

38 Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:

Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.

39 Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:

Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti.

40 Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150.

Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Benyamini.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/8-8fac8885233ff6a0f615f14f44815b0d.mp3?version_id=1627—