2 Wafalme 10

Jamii Ya Ahabu Yauawa

1 Wakati huu katika Samaria walikuwepo wana sabini wa nyumba ya Ahabu. Kwa hiyo Yehu akaandika barua na kuzituma Samaria kwa: Maafisa wa Yezreeli, kwa wazee na kwa walezi wa watoto wa Ahabu. Akasema,

2 “Mara tu barua hii itakapokufikia, kwa kuwa wana wa bwana wako wapo pamoja nawe, nawe una magari ya vita na farasi, mji wenye ngome na silaha,

3 mchague mwenye uwezo zaidi kati ya wana wa bwana wako na umweke juu ya kiti cha enzi cha baba yake. Kisha upigane kwa ajili ya nyumba ya bwana wako.”

4 Lakini wakaogopa sana na kusema, “Ikiwa wafalme wawili hawakuweza kupambana na Yehu, sisi tutawezaje?”

5 Basi msimamizi wa jumba la kifalme, mtawala wa mji, wazee na walezi wakatuma ujumbe huu kwa Yehu: “Sisi tu watumishi wako na tutafanya kila kitu utakachosema. Hatutamteuwa mtu ye yote kuwa mfalme, wewe fanya uonalo kuwa ni bora.”

6 Kisha Yehu akawaandikia barua ya pili, akisema, “Ikiwa ninyi mko upande wangu na mtanitii mimi, twaeni vichwa vya wana wa bwana wenu na mnijie huku Yezreeli kesho wakati kama huu.”

Wakati huo wana sabini wa kifalme, walikuwa wakiishi pamoja na viongozi wa mji wa Samaria, ambao walikuwa wakiwalea.

7 Hiyo barua ilipowafikia, watu hawa wakawachukuwa wale wana sabini wa mfalme na kuwachinja wote. Wakaweka vichwa vyao ndani ya makapu na kumpelekea Yehu huko Yezreeli.

8 Mjumbe alipofika, akamwambia Yehu, “Wameleta vichwa vya wana wa mfalme.”

Ndipo Yehu akaagiza, “Viwekeni katika marundo mawili katika ingilio la lango la mji mpaka asubuhi.”

9 Asubuhi yake, Yehu akatoka nje. Akasimama mbele ya watu wote na akasema, “Hamna hatia. Ni mimi niliyefanya shauri baya dhidi ya bwana wangu na kumwua, lakini ni nani aliyewaua wote hawa?

10 Fahamuni basi kwamba, hakuna neno ambaloBwanaamesema dhidi ya nyumba ya Ahabu ambalo halitatimia.Bwanaamefanya lile aliloahidi kupitia mtumishi wake Eliya.”

11 Hivyo Yehu akaua kila mtu huko Yezreeli aliyekuwa amebaki wa nyumba ya Ahabu, ikiwa ni pamoja na wakuu wake, rafiki zake wa karibu na makuhani wake, hakuacha ye yote anusurike.

12 Kisha Yehu akaondoka kuelekea Samaria. Alipokuwa njiani karibu na nyumba ya kukatia manyoya ya kondoo, yaani, Beth-Ekedi ya wachunga kondoo,

13 Yehu akakutana na watu wa jamaa ya Ahazia mfalme wa Yuda akauliza, “Ninyi ni nani?”

Wao wakasema, “Sisi ni jamaa ya Ahazia, nasi tumeshuka kuwasalimu jamaa ya mfalme na ya mama malkia.”

14 Yehu akaagiza, “Wakamateni wakiwa hai!” Kwa hiyo wakawachukua wakiwa hai, watu arobaini na wawili, na kuwachinja kando ya kisima cha Beth-Ekedi. Hakuacha ye yote anusurike.

15 Baada ya kuondoka hapo, alimkuta Yehonadabu mwana wa Rekabu, aliyekuwa akienda kumlaki. Yehu akamsalimu na kusema, “Je, moyo wako ni mnyofu kwangu kama moyo wangu ulivyo kwako?”

Yehonadabu akajibu, “Ndiyo.”

Yehu akasema, “Kama ndivyo, nipe mkono wako.” Yeye akampa mkono, naye Yehu akampandisha kwenye gari lake la vita.

16 Yehu akasema, “Twende pamoja ukaone wivu wangu kwa ajili yaBwana.” Hivyo wakasafiri pamoja kwenye gari lake.

17 Yehu alipofika Samaria, akawaua wale wote waliokuwa wamesalia wa jamaa ya Ahabu, akawaangamiza, sawasawa na neno laBwanaalilosema kwa kupitia Eliya.

Watumishi Wa Baali Wauawa

18 Kisha Yehu akawaleta watu wote pamoja na kuwaambia, “Ahabu alimtumikia Baali kidogo, Yehu atamtumikia zaidi.

19 Sasa waiteni manabii wote wa Baali, watumishi wake wote na makuhani wake wote. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja atakayekosekana, kwa sababu ninakwenda kutoa kafara kubwa sana kwa Baali. Ye yote atakayeshindwa kuja hataendelea kuishi.” Lakini Yehu alifanya hivyo kwa hila ili apate kuwaangamiza watumishi wote wa Baali.

20 Yehu akasema, “Itisheni kusanyiko kwa heshima ya Baali.” Basi wakatangaza jambo hilo.

21 Kisha akapeleka ujumbe katika Israeli yote na watumishi wote wa Baali wakaja, hakuna hata mmoja ambaye hakufika. Wakasongana ndani ya hekalu la Baali mpaka likajaa tangu mwanzo hadi mwisho wake.

22 Naye Yehu akamwambia yule aliyekuwa mtunza chumba cha mavazi, “Leta majoho kwa ajili ya watumishi wote wa Baali.” Basi akawaletea majoho.

23 Kisha Yehu na Yehonadabu mwana wa Rekabu wakaingia ndani ya hekalu la Baali. Yehu akawaambia watumishi wa Baali, “Tazameni kila mahali mhakikishe kwamba hakuna hata mtumishi mmoja waBwanaaliye hapa pamoja nanyi, wawe ni watumishi wa Baali tu.”

24 Kwa hiyo wakaingia ndani ili kutoa kafara na sadaka ya kuteketezwa. Wakati huu, Yehu alikuwa amewaweka watu wake themanini akiwa amewapa onyo kwamba, “Ikiwa mmoja wenu atamwachia mtu ye yote ninayemweka mikononi mwake atoroke, itakuwa uhai wako kwa uhai wake.”

25 Mara baada ya Yehu kutoa sadaka ya kuteketezwa akawaamuru walinzi na maafisa: “Ingieni ndani, waueni; asitoroke hata mmoja.” Basi wakawakatakata kwa upanga. Walinzi na maafisa wakazitupa zile maiti nje na kisha wakaingia mahali pa ndani pa kuabudia miungu katika hekalu la Baali.

26 Wakaileta ile nguzo ya kuabudiwa nje ya hekalu la Baali na wakaichoma moto.

27 Wakabomoa ile nguzo ya kuabudiwa ya Baali pamoja na hekalu la Baali, nao watu wakapafanya kuwa choo hadi leo.

28 Kwa hiyo Yehu akaangamiza kuabudiwa kwa Baali katika Israeli.

29 Hata hivyo, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, yaani, kuabudu ndama za dhahabu huko Betheli ya Dani.

30 Bwanaakamwambia Yehu, “Kwa kuwa umefanya vyema kwa kutimiza yaliyo sawa machoni pangu na umetenda kwa nyumba ya Ahabu yale yote niliyokuwa nimekusudia kutenda, wazao wako wataketi juu ya kiti cha enzi cha Israeli hadi kizazi cha nne.”

31 Lakini Yehu hakuwa mwangalifu kushika sheria zaBwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda.

32 Katika siku hizo,Bwanaakaanza kupunguza ukubwa wa Israeli. Hazaeli akawashinda Waisraeli sehemu zote za nchi yao

33 mashariki ya Yordani katika nchi yote ya Gileadi (eneo la Gadi, Reubeni na Manase), kutoka Aroeri karibu na Bonde la Arnoni kupitia Gileadi hadi Bashani.

34 Kwa matukio mengine ya utawala wa Yehu, yote aliyofanya na mafanikio yake yote, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

35 Yehu akalala pamoja na baba zake naye akazikwa huko Samaria. Naye Yehoahazi mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme badala yake.

36 Muda Yehu aliotawala juu ya Israeli huko Samaria ilikuwa miaka ishirini na minane.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/10-39c42e8055d8fe053eeeace2fb8aa4a6.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 11

Athalia Na Yoashi

1 Wakati Athalia mamaye Ahazia alipoona kwamba mwanawe amekufa, akainuka na kuiangamiza jamaa yote ya kifalme.

2 Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu ambaye ni dada yake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa kifalme, ambao walikuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala na kumficha humo ili Athalia asimwone; kwa hiyo hakuuawa.

3 Alibaki amefichwa pamoja na yaya wake kwenye Hekalu laBwanakwa miaka sita wakati Athalia alipokuwa akitawala nchi.

4 Katika mwaka wa saba Yehoyada kuhani akaamuru waletwe wakuu wa vikundi vya mamia wa Wakarina walinzi, nao wakaletwa kwake kwenye Hekalu laBwana. Akafanya agano nao na kuwaapisha katika Hekalu laBwana. Ndipo akawaonyesha mwana wa mfalme.

5 Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaokwenda zamu siku ya Sabato, theluthi yenu itakuwa ikilinda jumba la kifalme,

6 theluthi nyingine italinda Lango la Suri, na theluthi nyingine italinda lango lililo nyuma ya walinzi, ambao hupeana zamu kulinda Hekalu;

7 nanyi ambao mko katika makundi mengine mawili ambao kwa kawaida hupumzika Sabato, wote mtalinda Hekalu kwa ajili ya mfalme.

8 Jipangeni kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi mwake. Ye yote anayesogelea safu yenu ya askari ni lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme po pote aendako.”

9 Majemadari wa vikosi vya mamia wakafanya sawasawa kama alivyoagiza kuhani Yehoyada. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakienda zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa katika mapumziko, nao wakaja kwa kuhani Yehoyada.

10 Ndipo akawapa wale majemadari mikuki na ngao zilizokuwa mali ya Mfalme Daudi na zile zilizokuwa ndani ya Hekalu laBwana.

11 Wale walinzi, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi mwake, wakajipanga kumzunguka mfalme, karibu na madhabahu na Hekalu, kuanzia upande wa kusini hadi upande wa kaskazini mwa Hekalu.

12 Yehoyada akamtoa mwana wa mfalme na kumvika taji, akampa nakala ya agano na kumtangaza kuwa mfalme. Wakamtia mafuta, nao watu wakapiga makofi na kupaza sauti wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”

13 Athalia aliposikia kelele iliyofanywa na walinzi pamoja na watu, akawaendea watu pale penye Hekalu laBwana.

14 Akaangalia na tazama alikuwako mfalme, akiwa amesimama karibu na nguzo, kama ilivyokuwa desturi. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa pembeni mwa mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wakifurahi na kupiga tarumbeta. Kisha Athalia akararua majoho yake na kupiga kelele, “Uhaini! Uhaini!”

15 Kuhani Yehoyada akawaagiza majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa wasimamizi wa jeshi, “Mleteni huyo Athalia nje katikati ya safu, na mtieni upanga mtu ye yote atakayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Hatauawa ndani ya Hekalu laBwana.”

16 Basi wakamkamata Athalia na alipofika mahali ambapo farasi huingilia katika viwanja vya jumba la mfalme, wakamwulia hapo.

17 Ndipo Yehoyada akafanya Agano kati yaBwanana mfalme na watu kwamba watakuwa watu waBwana. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu.

18 Watu wote wa nchi wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunja madhabahu zote na sanamu vipande vipande na kumwua Matani kuhani wa Baali mbele ya hiyo madhabahu.

Kisha Yehoyada kuhani akawaweka walinzi kwenye Hekalu laBwana.

19 Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamshusha mfalme kutoka katika Hekalu laBwanana kwenda kwenye jumba la kifalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi,

20 nao watu wote wa nchi wakafurahi. Mji ukatulia, kwa sababu Athalia alikuwa ameuawa kwa upanga huko kwenye jumba la kifalme.

21 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba wakati alipoanza kutawala.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/11-529a000ba40df9fc04897c306afddbef.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 12

Yoashi Anakarabati Hekalu

1 Katika mwaka wa saba wa kutawala kwake Yehu, Yoashi alianza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka arobaini. Jina la mama yake aliitwa Sibia, kutoka Beer-Sheba.

2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu miaka yote ambayo Yehoyada kuhani alikuwa akimwelekeza.

3 Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa, watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.

4 Yoashi akawaambia makuhani, “Kusanyeni fedha zote ambazo zitaletwa kama sadaka takatifu kwenye Hekalu laBwana, yaani, fedha zilizokusanywa kama kodi, fedha zilizopokelewa kutokana na nadhiri za watu binafsi na fedha zilizoletwa kwa hiari hekaluni.

5 Kila kuhani na apokee fedha kutoka kwa mmoja wa watunza hazina, nazo zitumike kukarabati uharibifu wo wote unaoonekana katika Hekalu.”

6 Lakini ikawa kufikia mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Mfalme Yoashi, makuhani walikuwa bado hawajalikarabati Hekalu.

7 Kwa hiyo Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na makuhani wengine na akawauliza, “Kwa nini hamtengenezi uharibifu uliofanyika hekaluni? Msichukue fedha zaidi kutoka kwa watunza hazina wenu kwa ajili ya matumizi yenu, lakini kuanzia sasa ni lazima fedha yote itumike kwa ajili ya kukarabati Hekalu.”

8 Makuhani wakakubali kuwa hawatakusanya tena fedha kutoka kwa watu na kwamba hawatakarabati Hekalu wenyewe.

9 Yehoyada kuhani akachukua kisanduku na akatoboa tundu kwenye kifuniko chake. Akakiweka kando ya madhabahu upande wa kulia unapoingia hekaluni mwaBwana. Makuhani waliolinda ingilio wakaweka ndani ya kisanduku fedha zote ambazo zililetwa katika Hekalu laBwana.

10 Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa jumba la kifalme na Kuhani Mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu laBwanana kuziweka katika mifuko.

11 Wakiisha kuthibitisha kiasi cha hizo fedha, waliwapa watu walioteuliwa kusimamia kazi katika Hekalu. Kwa fedha hizo, wakawalipa wale watu waliofanya kazi katika Hekalu laBwana: yaani, maseremala na wajenzi,

12 waashi na wakata mawe. Walinunua mbao na mawe ya kuchongwa kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu laBwana, na kulipia gharama nyingine zote za kulitengeneza.

13 Fedha zilizoletwa kwenye Hekalu hazikutumiwa kutengenezea masinia ya fedha, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, tarumbeta wala vyombo vingine vyo vyote vya dhahabu au fedha kwa ajili ya Hekalu laBwana;

14 zililipwa kwa wafanyakazi, ambao walizitumia kwa kukarabati Hekalu.

15 Wao hawakudai kupewa hesabu ya fedha kutoka kwa wale waliowapa ili kuwalipa wafanyakazi, kwa sababu walifanya kwa uaminifu wote.

16 Fedha zilizopatikana kutokana na sadaka za hatia na sadaka za dhambi hazikuletwa katika Hekalu laBwana; zilikuwa mali ya makuhani.

17 Wakati huu Hazaeli mfalme wa Aramu akapanda kuishambulia Gathi na akaiteka. Kisha akageuka ili kuishambulia Yerusalemu.

18 Lakini Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vyombo vyote vitakatifu vilivyowekwa wakfu na baba zake, yaani Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia wafalme wa Yuda, zawadi ambazo yeye mwenyewe alikuwa ameziweka wakfu pamoja na dhahabu yote iliyokutwa katika hazina za Hekalu laBwanana katika jumba la kifalme, akazipeleka kwa Hazaeli mfalme wa Aramu, ambaye hatimaye aliondoka Yerusalemu.

19 Kwa matukio mengine ya utawala wa Yoashi na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

20 Maafisa wake wakafanya shauri baya dhidi yake, nao wakamwua huko Beth-Milo, kwenye barabara itelemkayo kuelekea Sila.

21 Maafisa waliomwua walikuwa Yozabadi mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri. Akafa na akazikwa pamoja na baba zake katika Mji wa Daudi. Naye Amazia mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/12-0bf3d5d4bc12bdb60a8e0c4ae1a28110.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 13

Yehoahazi Mfalme Wa Israeli

1 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa kutawala kwake Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoahazi mwana wa Yehu alianza kutawala Israeli katika Samaria, naye akatawala miaka kumi na saba.

2 Akafanya maovu machoni paBwanakwa kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda na wala hakuziacha.

3 Kwa hiyo hasira yaBwanaikawaka dhidi ya Israeli na kwa muda mrefu akawaweka chini ya utawala wa Hazaeli mfalme wa Aramu na Ben-Hadadi mwanawe.

4 Ndipo Yehoahazi akamsihiBwanarehema, nayeBwanaakamsikiliza, kwa maana aliona jinsi mfalme wa Aramu alivyokuwa akiwatesa Israeli vikali.

5 Bwanaakamtoa mwokozi kwa ajili ya Israeli, nao wakaokoka kutoka kwenye mamlaka ya Aramu. Hivyo Waisraeli wakaishi katika nyumba zao wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali.

6 Lakini hawakuziacha dhambi za nyumba ya Yeroboamu, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, bali wakaendelea kuzitenda. Nguzo ya Ashera pia iliendelea kusimama katika Samaria.

7 Hapakubaki kitu cho chote katika jeshi la Yehoahazi isipokuwa wapanda farasi hamsini, magari kumi ya vita na askari wa miguu 10,000, kwa kuwa mfalme wa Aramu alikuwa amewaangamiza hao wengine na kuwafanya kama mavumbi wakati wa kupura nafaka.

8 Matukio mengine ya utawala wa Yehoahazi yote aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

9 Yehoahazi akalala pamoja na baba zake na akazikwa huko Samaria. Naye Yehoashimwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Yehoashi Mfalme Wa Israeli

10 Katika mwaka wa thelathini na saba wa kutawala kwake Yoashi mfalme wa Yuda, Yehoashi mwana wa Yehoahazi alianza kutawala Israeli huko Samaria, naye akatawala miaka kumi na sita.

11 Alifanya maovu machoni paBwanana hakuacha dhambi yo yote kati ya zile za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, aliendelea kuzitenda.

12 Na kwa matukio mengine ya utawala wa Yehoashi, yote aliyoyafanya na mafanikio yake, pamoja na vita yake dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

13 Yehoashi akalala pamoja na baba zake, akazikwa Samaria pamoja na wafalme wa Israeli. Yeroboamu akaingia mahali pake kuwa mfalme.

14 Wakati huu, Elisha alikuwa anaumwa na ugonjwa ambao baadaye ulimwua. Yehoashi mfalme wa Israeli akashuka kwenda kumwona na kumlilia. Akalia, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!”

15 Elisha akasema, “Leta upinde na baadhi ya mishale,” naye mfalme akafanya hivyo.

16 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Shika upinde mikononi mwako.” Alipokwisha kuichukua, Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme.

17 Elisha akasema, “Fungua dirisha la mashariki,” naye akalifungua. Elisha akasema, “Piga mshale!” Naye akapiga mshale. Elisha akasema, “Mshale wa ushindi waBwana, mshale wa ushindi juu ya Aramu! Utawaangamiza kabisa Waaramu katika Afeki.”

18 Kisha akasema, “Chukua mishale,” naye mfalme akaichukua. Elisha akamwambia, “Piga ardhi kwa hiyo mishale.” Akaipiga mara tatu, halafu akaacha.

19 Mtu wa Mungu akamkasirikia na akasema, “Ungepiga chini mara tano au sita, ndipo ungeishinda Aramu na kuiangamiza kabisa. Lakini sasa utaishinda mara tatu tu.”

20 Elisha akafa, nao wakamzika.

Vikosi vya Wamoabu vilikuwa vinashambulia nchi kwa vita kila mwaka wakati wa vuli.

21 Ikawa Waisraeli fulani walipokuwa wanamzika mtu, ghafula wakaona kikosi cha washambuliaji, basi wakaitupa ile maiti ya yule mtu ndani ya kaburi la Elisha. Wakati ile maiti ilipogusa mifupa ya Elisha, yule mtu akafufuka na kusimama kwa miguu yake.

22 Hazaeli mfalme wa Aramu aliwatesa Israeli wakati wote wa utawala wa Yehoahazi.

23 LakiniBwanaakawarehemu na akawahurumia, akaonyesha kujishughulisha nao kwa sababu ya Agano lake na Abrahamu, Isaki na Yakobo. Hadi leo, hajawaangamiza wala kuwafukuza mbele zake.

24 Hazaeli mfalme wa Shamu akafa, naye Ben-Hadadi mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

25 Kisha Yehoashi mwana wa Yehoahazi akateka tena kutoka kwa Ben-Hadadi mwana wa Hazaeli ile miji aliyokuwa ameitwaa kwa vita kutoka kwa baba yake Yehoahazi. Yehoashi alimshinda mara tatu, hivyo akaweza kuiteka tena ile miji ya Waisraeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/13-b2368dcc40dc50ce7c8abe8529489db3.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 14

Amazia Mfalme Wa Yuda

1 Katika mwaka wa pili wa kutawala kwake Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda alianza kutawala.

2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipokuwa mfalme, naye akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na tisa. Jina la mama yake aliitwa Yehoadani, kutoka Yerusalemu.

3 Akatenda yaliyo mema machoni paBwana, lakini sio kama Daudi baba yake alivyokuwa amefanya. Katika kila kitu alifuata mfano wa Yoashi baba yake.

4 Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia miungu hapakuondolewa; watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.

5 Baada ya ufalme kuwa imara mikononi mwake, aliwaua wale maafisa waliomwua Mfalme Yoashi baba yake.

6 Hata hivyo, hakuwaua wana wa wale wauaji, sawasawa na ilivyoandikwa katika kitabu cha Sheria ya Mose ambakoBwanaaliagiza akisema, “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”

7 Yeye ndiye aliyewashinda Waedomu 10,000 katika Bonde la Chumvi na akauteka Sela katika vita akauita Yokitheeli, jina ambalo mji huo unalo hadi leo.

8 Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli, akisema, “Njoo, tuonane uso kwa uso.”

9 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akamjibu Amazia mfalme wa Yuda, akisema: “Mbaruti ulioko Lebanoni uliutumia ujumbe mwerezi ulioko Lebanoni, ‘Mtoe binti yako aolewe na mwanangu.’ Kisha mnyama wa mwituni katika Lebanoni akaja na kuukanyaga ule mbaruti chini ya nyayo zake.

10 Hakika umeishinda Edomu na sasa unajivuna. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani! Kwa nini unachokoza nawe usababishe anguko lako mwenyewe na lile la Yuda pia?”

11 Hata hivyo, Amazia hakusikia, hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akashambulia, yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth-Shemeshi katika Yuda.

12 Yuda ikashindwa na Israeli na kila mtu akakimbilia nyumbani kwake.

13 Yehoashi mfalme wa Israeli akamkamata Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-Shemeshi. Kisha Yehoashi akaenda Yerusalemu na kuvunja ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi Lango la Kwenye Pembe, kisehemu chenye urefu wa kama dhiraa 400.

14 Akachukua dhahabu yote na fedha na vyombo vyote vilivyopatikana ndani ya Hekalu laBwanana katika hazina zote za jumba la mfalme. Akachukua pia mateka na kurudi Samaria.

15 Matukio mengine ya utawala wa Yehoashi, aliyoyafanya na mafanikio yake, pamoja na vita vyake dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

16 Yehoashi akalala pamoja na baba zake na akazikwa Samaria pamoja na wafalme wa Israeli, naye Yeroboamu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

17 Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda aliishi miaka kumi na mitano baada ya kifo cha Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli.

18 Matukio mengine ya utawala wa Amazia, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

19 Wakafanya shauri baya dhidi ya Amazia huko Yerusalemu, naye akakimbilia Lakishi, lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi nao wakamwua huko.

20 Akarudishwa kwa farasi na akazikwa huko Yerusalemu pamoja na baba zake, katika Mji wa Daudi.

21 Kisha watu wote wa Yuda wakamchukua Azariaaliyekuwa na umri wa miaka kumi na sita na kumfanya mfalme mahali pa baba yake Amazia.

22 Yeye ndiye aliyeijenga tena Elathi na kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala pamoja na baba zake.

Yeroboamu Wa Pili Mfalme Wa Israeli

23 Katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yehoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala huko Samaria, naye akatawala kwa miaka arobaini na mmoja.

24 Akafanya maovu machoni paBwanana hakuacha dhambi hata moja ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda.

25 Yeye ndiye aliyerudishia mipaka ya Israeli kuanzia Lebo-Hamathi hadi Bahari ya Araba, sawasawa na neno laBwana, Mungu wa Israeli, lililosemwa kupitia mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii kutoka Gath-Heferi.

26 Bwanaalikuwa ameona jinsi kila mmoja katika Israeli, awe mtumwa au aliye huru alivyoteseka kwa uchungu; hapakuwepo na ye yote wa kuwasaidia.

27 Kwa kuwaBwanaalikuwa hajasema kuwa atafuta jina la Israeli chini ya mbingu, akawaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.

28 Kwa matukio mengine ya utawala wa Yeroboamu, yote aliyoyafanya na mafanikio yake ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na jinsi alivyorudisha Dameski na Hamathi kwa Israeli, ambayo ilikuwa mali ya Yaudi, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

29 Yeroboamu akalala pamoja na baba zake, wafalme wa Israeli. Naye Zekaria mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/14-7629f10205fbb5f2b98752a2a7631875.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 15

Azaria Mfalme Wa Yuda

1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa kutawala kwake Yeroboamu mfalme wa Israeli Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala.

2 Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili. Jina la mama yake aliitwa Yekolia kutoka Yerusalemu.

3 Akatenda yaliyo mema machoni paBwana, kama Amazia baba yake alivyofanya.

4 Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia miungu hapakuondolewa; watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.

5 Bwanaakampiga mfalme kwa ukoma mpaka siku aliyokufa, naye aliishi katika nyumba iliyotengwa peke yake. Yothamu mwana wa mfalme akawa msimamizi wa jumba la kifalme na akawatawala watu wa nchi.

6 Matukio mengine ya utawala wa Azaria na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

7 Azaria akalala pamoja na baba zake naye akazikwa karibu nao katika Mji wa Daudi, na Yothamu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Zekaria Mfalme Wa Israeli

8 Katika mwaka wa thelathini na nane wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, naye akatawala miezi sita.

9 Akafanya maovu machoni paBwana, kama baba zake walivyofanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.

10 Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya shauri baya dhidi ya Zekaria. Akamshambulia mbele ya watu, akamwua na kuingia mahali pake kuwa mfalme.

11 Matukio mengine ya utawala wa Zekaria yameandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli.

12 Kwa hiyo neno laBwanalililonenwa kwa Yehu likatimia kwamba, “Uzao wako utaketi juu ya kiti cha enzi cha Israeli mpaka kizazi cha nne.”

Shalumu Mfalme Wa Israeli

13 Shalumu mwana wa Yabeshi akawa mfalme katika mwaka wa thelathini na tisa wa Uzia mfalme wa Yuda, naye akatawala katika Samaria kwa mwezi mmoja.

14 Kisha Menahemu mwana wa Gadi akaenda kutoka Tirza mpaka Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana Yabeshi huko Samaria, akamwua na kuingia mahali pake kuwa mfalme.

15 Matukio mengine ya utawala wa Shalumu na mauaji aliyoyafanya, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli.

16 Wakati ule, akianzia Tirza, Menahemu akashambulia Tifsa na kila mtu ndani yake na wale waliokuwa jirani kwa sababu walikataa kufungua malango yao. Akaiangamiza Tifsa yote na kuwapasua matumbo wanawake wote wenye mimba.

Menahemu Mfalme Wa Israeli

17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akawa mfalme wa Israeli na alitawala huko Samaria kwa miaka kumi.

18 Akatenda maovu machoni paBwana. Katika wakati wa utawala wake wote hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.

19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaishambulia Israeli. Menahemu mfalme wa Israeli akampa talanta 1,000 za fedhaili amsaidie na kumwezesha katika utawala wake.

20 Menahemu akatoza fedha hizi kwa nguvu kutoka kwa Israeli. Kila mtu tajiri alilazimika kuchanga shekeli hamsini za fedhaambazo alipewa mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akajiondoa na hakuendelea kuikalia nchi.

21 Matukio mengine ya utawala wa Menahemu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

22 Menahemu akalala pamoja na baba zake. Naye Pekahia mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Pekahia Mfalme Wa Israeli

23 Katika mwaka wa hamsini wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, akatawala miaka miwili.

24 Pekahia akafanya uovu machoni paBwana. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.

25 Mmoja wa maafisa wake wakuu, Peka mwana wa Remalia, akafanya shauri baya dhidi yake. Akachukua watu hamsini wa Gileadi pamoja naye, akamwua Pekahia, pamoja na Argobu na Aria, katika ngome ya jumba la kifalme huko Samaria. Kwa hiyo Peka akamwua Pekahia, naye akaingia mahali pake kuwa mfalme.

26 Matukio mengine ya utawala wa Pekahia na yote aliyoyafanya yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli.

Peka Mfalme Wa Israeli

27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, naye alitawala miaka ishirini.

28 Akafanya maovu machoni paBwana. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.

29 Wakati wa utawala wa Peka mfalme wa Israeli, Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alikuja na kuiteka Iyoni, Abeli-Beth-Maaka, Yanoa, Kedeshi na Hazori. Akateka miji ya Gileadi na Galilaya, pamoja na nchi yote ya Naftali na kuwahamishia watu wote Ashuru.

30 Kisha Hoshea mwana wa Ela akafanya shauri baya dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akamshambulia na kumwua, kisha akaingia mahali pake kuwa mfalme katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.

31 Matukio mengine ya utawala wa Peka na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

Yothamu Mfalme Wa Yuda

32 Katika mwaka wa pili wa kutawala kwake Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala.

33 Alikuwa na miaka ishirini na mitano wakati alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Jina la mama yake aliitwa Yerusha binti Zadoki.

34 Akafanya yaliyo mema machoni paBwana, kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya.

35 Hata hivyo, mahali pa juu hapakuondolewa; watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu laBwana.

36 Matukio mengine ya utawala wa Yothamu na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

37 (Katika siku hizoBwanaakaanza kuwatuma Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia dhidi ya Yuda.)

38 Yothamu akalala na baba zake na akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi, mji wa baba zake. Naye Ahazi mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/15-0c8f39f460884ddfc1a8935f6bc23374.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 16

Ahazi Mfalme Wa Yuda

1 Katika mwaka wa kumi na saba wa kutawala kwake Peka mwana wa Remalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala.

2 Ahazi alikuwa na miaka ishirini alipoanza kutawala kama mfalme, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo sawa mbele ya macho yaBwana, Mungu wake.

3 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli na hata kumtoa mwanawe kafara katika moto, akafuata njia za machukizo za mataifa ambayoBwanaalikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli.

4 Akatoa kafara na kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu, juu ya vilele vya vilima, na chini ya kila mti uliotanda.

5 Kisha Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli wakaondoka kwenda kupigana dhidi ya Yerusalemu na kumzunguka Ahazi kwa jeshi, lakini hawakuweza kumshinda.

6 Wakati ule, Resini mfalme wa Aramu akaurudisha Elathi kwa Aramu kwa kuwafukuza watu wa Yuda. Kisha Waedomu wakahamia Elathi nao wanaishi huko mpaka leo.

7 Ahazi akatuma wajumbe kumwambia Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru kwamba, “Mimi ni mtumishi na mtumwa wako. Njoo na uniokoe kutoka mkononi mwa mfalme wa Aramu na wa mfalme wa Israeli ambao wananishambulia.”

8 Naye Ahazi akachukua fedha na dhahabu zilizopatikana ndani ya Hekalu laBwanana katika hazina ya jumba la kifalme na kuzituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.

9 Mfalme wa Ashuru akamwitikia kwa kushambulia Dameski na kuiteka. Akawahamishia wenyeji wake huko Kiri, na kumwua Resini.

10 Kisha Mfalme Ahazi akaenda Dameski kukutana na Tiglath-Pileseri wa Ashuru. Akaiona madhabahu huko Dameski na akamtumia Uria kuhani mchoro wa hiyo madhabahu, pamoja na maelezo yakiwa ya mpango kamili kwa ajili ya ujenzi wake.

11 Kwa hiyo Uria kuhani akajenga madhabahu kulingana na mipango yote ambayo Mfalme Ahazi alikuwa ameituma kutoka Dameski na kumaliza ujenzi kabla ya kurudi Mfalme Ahazi.

12 Mfalme aliporudi kutoka Dameski na kuiona hiyo madhabahu, aliisogelea na kutoa sadaka juu yake.

13 Akatoa sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka, akamimina sadaka ya kinywaji na kunyunyizia damu ya sadaka zake za amani juu ya hiyo madhabahu.

14 Mfalme Ahazi akaiondoa ile madhabahu ya zamani ya shaba kutoka hapo mbele ya Hekalu laBwana, iliyokuwa imesimama kati ya ingilio la Hekalu na hiyo madhabahu mpya, naye akaiweka upande wa kaskazini mwa hiyo madhabahu mpya.

15 Ndipo Mfalme Ahazi akatoa amri zifuatazo kwa kuhani, Uria: “Juu ya hiyo madhabahu kubwa mpya, utoe sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa na sadaka ya jioni ya nafaka, sadaka ya mfalme ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, sadaka za kuteketezwa za watu wote wa nchi, pamoja na sadaka yao ya nafaka na sadaka yao ya kinywaji. Unyunyize juu ya hiyo madhabahu damu yote ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu. Lakini mimi nitatumia hiyo madhabahu ya zamani ya shaba kwa ajili ya kutafuta uongozi.”

16 Naye Uria, kuhani, akafanya sawasawa kama Mfalme Ahazi alivyoagiza.

17 Mfalme Ahazi akaondoa mbao za pembeni na kuondoa masinia kwenye vile vishikilio vinavyohamishika. Akaondoa ile Bahari kutoka kwenye mafahali wa shaba walioishikilia na kuiweka kwenye kitako cha jiwe.

18 Kwa ajili ya mfalme wa Ashuru akaliondoa pia pazia la Sabato lililokuwa limewekwa ndani ya Hekalu na akafuata ile njia ya kifalme ya kuingia kwenye Hekalu laBwana.

19 Matukio mengine ya utawala wa Ahazi na yale aliyoyafanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

20 Ahazia akalala pamoja na baba zake naye akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Hezekia mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/16-e340f60562e2b8a0145fb1aae103b7f1.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 17

Hoshea, Mfalme Wa Mwisho Katika Israeli

1 Katika mwaka wa kumi na mbili wa kutawala kwake Ahazi mfalme wa Yuda, Hoshea mwana wa Ela akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, akatawala kwa miaka tisa.

2 Akafanya maovu machoni paBwana, lakini si kama wafalme wengine wa Israeli waliomtangulia.

3 Mfalme Shalmanesa wa Ashuru akainuka dhidi ya Mfalme Hoshea, ambaye hapo mbeleni alikuwa mtumwa wake na kumlipa ushuru.

4 Lakini mfalme wa Ashuru akagundua kuwa Hoshea alikuwa msaliti, kwa kuwa alikuwa ametuma wajumbe kwa So mfalme wa Misri, naye hakuendelea kulipa ushuru kwa mfalme wa Ashuru tena kama alivyokuwa anafanya kila mwaka. Kwa hiyo Shalmanesa akamkamata na kumtia gerezani.

5 Mfalme wa Ashuru akaishambulia nchi yote, akapigana dhidi ya Samaria na kuizunguka kwa majeshi miaka mitatu.

6 Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, mfalme wa Ashuru akaiteka Samaria na kuwahamishia Waisraeli huko Ashuru. Akawaweka huko Hala, Gozani karibu na Mto Habori, na katika miji ya Wamedi.

Israeli Inakwenda Uhamishoni Kwa Sababu Ya Dhambi

7 Yote haya yalitokea kwa sababu Waisraeli walikuwa wametenda dhambi dhidi yaBwanaMungu wao, ambaye alikuwa amewapandisha kutoka Misri akiwatoa chini ya utawala wa nguvu wa Farao mfalme wa Misri. Waliabudu miungu mingine

8 na kufuata desturi za mataifa ambayoBwanaalikuwa ameyafukuza mbele yao, pamoja na desturi ambazo wafalme wa Israeli walizileta.

9 Waisraeli wakafanya vitu kwa siri dhidi yaBwanaMungu wao, ambavyo havikuwa sawa. Kuanzia kwenye mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye maboma walijijengea wenyewe mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji yao yote.

10 Wakaweka mawe ya kuabudiwa na nguzo za Ashera juu ya kila kilima kirefu na chini ya kila mti uliotanda.

11 Wakafukiza uvumba kila mahali palipoinuka, kama walivyofanya yale mataifa ambayoBwanaalikuwa ameyafukuza mbele yao. Wakafanya mambo maovu ambayo yalimghadhibishaBwana.

12 Wakaabudu sanamu, ingawaBwanaalikuwa amesema, “Msifanye mambo haya.”

13 Bwanaakawaonya Israeli na Yuda kupitia kwa manabii na waonaji wake wote: “Acheni njia zenu mbaya. Zishikeni amri na maagizo yangu, sawasawa na sheria yangu yote niliyowaagiza baba zenu kuitii ambayo niliileta kwenu kupitia kwa watumishi wangu manabii.”

14 Lakini hawakusikiliza, walikuwa na shingo ngumu kama baba zao, ambao hawakumtegemeaBwanaMungu wao.

15 Walizikataa amri zake na Agano alilokuwa amelifanya na baba zao na maonyo aliyokuwa amewapa. Wakafuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai. Wakayaigiza mataifa yaliyowazunguka, ingawaBwanaalikuwa amewaonya akiwaambia, “Msifanye kama wanavyofanya,” nao wakafanya mambo ambayoBwanaalikuwa amewakataza wasifanye.

16 Wakayaacha maagizo yote yaBwanaMungu wao na kujitengenezea sanamu mbili walizozisubu katika sura ya ndama na nguzo ya Ashera. Wakasujudia mianga yote ya angani, wakamtumikia Baali.

17 Wakawatoa kafara wana wao na mabinti zao katika moto. Wakafanya uaguzi na uchawi, nao wakajiuza wenyewe katika kutenda uovu machoni paBwana, wakamghadhibisha.

18 BasiBwanaakawakasirikia sana Israeli na kuwaondoa kwenye uwepo wake. Ni kabila la Yuda tu ndilo lililobaki;

19 hata hivyo nao hawakuzishika amri zaBwanaMungu wao. Wakafuata desturi ambazo Israeli alikuwa amezileta.

20 Kwa hiyoBwanaaliwakataa watu wote wa Israeli; akawatesa na kuwaachia katika mikono ya wateka nyara hadi alipowaondoa kutoka kwenye uwepo wake.

21 Alipokwisha kuwatenga Israeli mbali na nyumba ya Daudi, wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nebati kuwa mfalme wao. Yeroboamu akawashawishi Israeli waache kumfuataBwanana akawasababisha kutenda dhambi kuu.

22 Nao Israeli wakadumu katika dhambi zote za Yeroboamu mwana wa Nebati, hawakuziacha

23 hadiBwanaalipowaondoa kutoka kwenye uwepo wake, kama vile alivyokuwa ameonya kupitia watumishi wake wote manabii. Hivyo watu wa Israeli wakaondolewa kutoka katika nchi yao kwenda uhamishoni Ashuru, nao wako huko mpaka sasa.

Samaria Inakaliwa Tena

24 Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria badala ya Waisraeli. Wakaimiliki Samaria na kuishi katika miji yake.

25 Wakati walipoanza kuishi humo, hawakumwabuduBwana, kwa hiyo akatuma simba miongoni mwao, wakawaua baadhi ya watu.

26 Habari ikapelekwa kwa mfalme wa Ashuru, kusema: “Watu uliowahamisha na kuwaweka katika miji ya Samaria hawajui kile Mungu wa nchi hiyo anachokitaka. Ametuma simba miongoni mwao, ambao wanawaua, kwa sababu watu hawajui anachokitaka.”

27 Ndipo mfalme wa Ashuru akaamuru hivi: “Mtwae mmoja wa makuhani uliowachukua mateka kutoka Samaria ili arudi kuishi humo na awafundishe watu kile ambacho Mungu wa nchi anataka.”

28 Basi mmoja wa makuhani ambaye alikuwa amepelekwa uhamishoni kutoka Samaria akaja kuishi Betheli na kuwafundisha jinsi ya kumwabuduBwana.

29 Hata hivyo, kila kikundi cha taifa lililoletwa Samaria kilitengeneza miungu yao wenyewe katika miji kadhaa mahali walipoishi, nao wakaiweka mahali pa ibada za miungu ambapo watu wa Samaria walikuwa wametengeneza katika mahali pa juu.

30 Watu kutoka Babeli wakamtengeneza Sukoth-Benothi kuwa mungu wao, watu kutoka Kutha wakamtengeneza Nergali na watu kutoka Hamathi wakamtengeneza Ashima;

31 Waavi wakamtengeneza Nibhazi na Tartaki, Wasefarvi wakachoma watoto wao kama kafara kwa Adrameleki na Anameleki miungu ya Sefarvaimu.

32 WalimwabuduBwana, lakini pia waliteua aina zote za watu wao ili kuwawakilisha kama makuhani katika mahali pa kuabudia miungu kwenye mahali pa juu pa ibada za miungu.

33 WalimwabuduBwana, lakini pia waliitumikia miungu yao kulingana na desturi za mataifa walikotoka.

34 Mpaka leo wanashikilia desturi zao za zamani. HawamwabuduBwanawala kuzishika hukumu na maagizo, sheria na amri ambazoBwanaaliwapa uzao wa Yakobo, ambaye alimwita Israeli.

35 WakatiBwanaalipofanya Agano na Waisraeli aliwaamuru akisema: “Msiiabudu miungu mingine yo yote wala kuisujudia, wala kuitumikia wala kuitolea dhabihu.

36 Bali imewapasa kumwabuduBwanaaliyewapandisha kutoka Misri kwa uwezo wake mkuu na kwa mkono wake ulionyooshwa. Kwake yeye mtasujudu na kwake yeye mtatoa dhabihu.

37 Imewapasa daima kuwa waangalifu kutunza hukumu na maagizo, sheria na amri alizowaandikia. Msiabudu miungu mingine.

38 Msisahau Agano nililofanya nanyi, wala msiabudu miungu mingine.

39 Bali, mtamwabuduBwanaMungu wenu, kwani yeye ndiye atakayewakomboa kutoka mikononi mwa adui zenu wote.”

40 Hata hivyo hawakusikiliza, lakini waliendelea na desturi zao za awali.

41 Hata wakati watu hawa walipokuwa wanamwabuduBwana, walikuwa bado wakitumikia sanamu zao. Mpaka leo watoto wao na watoto wa watoto wao wanaendelea kufanya kama baba zao walivyofanya.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/17-b2924ce8e896f80c28dd7a70830a9003.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 18

Hezekia Mfalme Wa Yuda

1 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi mfalme wa Yuda alianza kutawala.

2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Jina la mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria.

3 Akafanya yaliyo mema machoni paBwana, kama Daudi baba yake alivyofanya.

4 Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Mose aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo wana wa Israeli walikuwa wanaifukizia uvumba (nayo ilikuwa ikiitwa Nehushtani).

5 Hezekia aliweka tumaini lake kwaBwana, Mungu wa Israeli. Hapakuwepo na mfalme mwingine wa kufanana naye miongoni mwa wafalme wa Yuda, kabla yake au baada yake.

6 Alishikamana naBwanakwa bidii wala hakuacha kumfuata; alishika amri ambazoBwanaalikuwa amempa Mose.

7 NayeBwanaalikuwa pamoja naye, akafanikiwa katika kila alichokifanya. Aliasi dhidi ya mfalme wa Ashuru na wala hakumtumikia.

8 Kuanzia mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye ngome, aliwashinda Wafilisti, hadi kufikia Gaza na himaya yake yote.

9 Mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela kutawala Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru alikwenda kuishambulia Samaria na kuuzunguka kwa majeshi.

10 Baada ya miaka mitatu Waashuru wakautwaa. Kwa hiyo Samaria ulitekwa katika mwaka wa sita wa utawala wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa kutawala kwake Hoshea mfalme wa Israeli.

11 Mfalme wa Ashuru akawahamishia Waisraeli huko Ashuru na akawaweka Hala, Gozani karibu na Mto Habori, na katika miji ya Wamedi.

12 Hili lilitokea kwa sababu walikuwa hawakumtiiBwanaMungu wao, lakini walikuwa wamevunja Agano lake, yale yote ambayo Mose mtumishi waBwanaaliwaamuru. Hawakuzisikiliza amri wala kuzitimiza.

13 Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda iliyozungushiwa ngome na kuitwaa.

14 Basi Hezekia mfalme wa Yuda akamtumia ujumbe mfalme wa Ashuru huko Lakishi akisema: “Nimefanya makosa. Ondoka katika nchi yangu, nami nitakulipa cho chote unachokitaka kwangu.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia mfalme wa Yuda talanta 300za fedha na talanta thelathiniza dhahabu.

15 Basi Hezekia akampa fedha yote iliyopatikana ndani ya Hekalu laBwanana katika hazina ya jumba la kifalme.

16 Wakati huu Hezekia mfalme wa Yuda akabandua dhahabu yote iliyokuwa imefunika milango na miimo ya Hekalu laBwana, akampa mfalme wa Ashuru.

Senakeribu Anaitishia Yerusalemu

17 Mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wake mkuu, na afisa wake mkuu, na jemadari wa jeshi lake pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi mpaka kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Wakaja mpaka Yerusalemu na kusimama kando ya mfereji unaopeleka maji katika Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.

18 Wakaagiza mfalme aitwe; Eliyakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, na Shebna mwandishi, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wa kumbukumbu, nao wakawaendea.

19 Yule jemadari wa jeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia:

“ ‘Hivi ndivyo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru asemavyo: Ni wapi unapoweka hilo tumaini lako?

20 Unasema unazo mbinu na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Ni nani unayemtegemea hata kuasi dhidi yangu?

21 Tazama, sasa unategemea Misri, ile fimbo ya mwanzi iliyopasuka, ambayo huuchoma mkono wa mtu na kumjeruhi kama akiuegemea. Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri kwa ye yote anayemtegemea.

22 Nawe kama ukiniambia, “TunamtumainiBwanaMungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akisema kwa Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu hii katika Yerusalemu”?

23 “ ‘Njoni sasa, mfanye majadiliano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi elfu mbili, kama unaweza kuwapata wapanda farasi elfu mbili!

24 Wewe na hilo jeshi lako dogo utawezaje kumzuia hata afisa mmoja wa kundi dogo na dhaifu la jeshi la bwana wangu, ijapo unaitegemea Misri kwa magari ya vita na wapanda farasi?

25 Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza mahali hapa pasipo neno kutoka kwaBwana?Bwanamwenyewe ndiye aliyeniambia niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’ ”

26 Kisha Eliyakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa Kiaramu, kwa kuwa tunakielewa vizuri. Usiseme nasi kwa Kiebrania wakati hao watu walio juu ya ukuta wanasikia.”

27 Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioko ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mikojo yao wenyewe?”

28 Kisha yule jemadari wa jeshi akasimama na kuita kwa Kiebrania: “Sikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru!

29 Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa mkononi mwangu.

30 Msimkubali Hezekia awashawishi kumtumainiBwanakwa kuwaambia, ‘HakikaBwanaatatuokoa; mji huu hautaangukia mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’

31 “Msimsikilize Hezekia. Hivi ndivyo asemavyo mfalme wa Ashuru: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwenye mzabibu wake mwenyewe na kwenye mtini wake na kunywa maji kutoka kwenye kisima chake mwenyewe,

32 mpaka nitakapokuja na kuwapeleka kwenye nchi iliyo kama hii ya kwenu, nchi yenye nafaka na divai mpya, nchi ya mikate na mashamba ya mizabibu, nchi ya mizeituni na asali. Chagueni uzima na sio mauti!

“Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa anawapotosha wakati anaposema, ‘Bwanaatatuokoa.’

33 Je, yuko mungu wa taifa lo lote aliyeiokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru?

34 Iko wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena na Iva? Je, imeweza kuiokoa Samaria kutoka mkononi mwangu?

35 Je, ni nani kati ya miungu yote ya nchi hizi ameweza kuokoa nchi yake kutoka kwangu? Itawezekanaje basi,Bwanaaiokoe Yerusalemu mkononi mwangu?”

36 Lakini wale watu wakakaa kimya hawakujibu lo lote, kwa sababu Mfalme Hezekia alikuwa amewaamuru, “Msimjibu lo lote.”

37 Kisha Eliyakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna mwandishi na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wa kumbukumbu wakamwendea Mfalme Hezekia, wakiwa wamerarua nguo zao, wakamwambia yale waliyoambiwa na yule jemadari wa jeshi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/18-bcb5f8868b1befd6b62ad5091abcc6cd.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 19

Hezekia Autafuta Msaada Wa Bwana

1 Wakati Mfalme Hezekia aliposikia haya, akararua nguo zake na kuvaa nguo ya gunia, naye akaenda katika Hekalu laBwana.

2 Akamtuma Eliyakimu msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna mwandishi na makuhani viongozi, wote wakiwa wamevaa nguo ya gunia, waende kwa nabii Isaya mwana wa Amozi.

3 Wakamwambia, “Hivi ndivyo asemavyo Hezekia: Siku hii ni siku ya huzuni, kukemewa na fedheha, kama vile wakati watoto wanapofikia hatua ya kuzaliwa lakini hakuna nguvu ya kuwazaa.

4 Inawezekana kuwaBwanaMungu wako atasikia maneno yote ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai na kwamba atamkemea kwa maneno ambayoBwanaMungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wanaishi.”

5 Maafisa wa Mfalme Hezekia walipofika kwa Isaya,

6 Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hivi ndivyo asemavyoBwana: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenikufuru mimi.

7 Sikia! Ninakwenda kuweka roho ndani yake ambayo wakati atakaposikia habari fulani, atarudi kwenye nchi yake mwenyewe na huko nitahakikisha ameanguka kwa upanga.’ ”

8 Yule jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alijiondoa na kumkuta mfalme akipigana dhidi ya Libna.

9 Mfalme Senakeribu alipokea taarifa kwamba Tirhaka, Mkushi mfalme wa Misri, ametoka ili kupigana dhidi yake. Basi akatuma tena wajumbe kwa Hezekia wakiwa na neno hili:

10 “Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda: Usiruhusu huyo Mungu unayemtumaini akudanganye wakati anaposema, ‘Yerusalemu haitatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’

11 Hakika umesikia yale ambayo wafalme wa Ashuru wamefanya kwa nchi zote, walivyoziangamiza kabisa. Je, unafikiri wewe utaokoka?

12 Je, miungu ya mataifa ambayo yaliangamizwa na baba zangu iliweza kuwaokoa, yaani: miungu ya Gozani, Harani, Resefu na watu wa Edeni ambao walikuwa Telasari?

13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa mji wa Sefarvaimu, au wa Hena au Iva?”

Maombi Ya Hezekia

14 Hezekia akapokea barua kutoka kwa wajumbe naye akaisoma. Kisha akapanda kwenda katika Hekalu laBwanana kuikunjua mbele zaBwana.

15 Naye Hezekia akamwombaBwanaakisema: “EeBwana, Mungu wa Israeli, uliyeketi kwenye kiti chako cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako, ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe ndiye uliyeumba mbingu na dunia.

16 Tega sikio, EeBwana, usikie; fungua macho yako, EeBwana, uone; sikiliza maneno ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

17 “Ni kweli, EeBwana, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya na nchi zao.

18 Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiangamiza, kwa kuwa haikuwa miungu bali ni miti na mawe tu, iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

19 Sasa basi, EeBwanaMungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili kwamba falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, EeBwana, ndiwe Mungu.”

Isaya Anatoa Unabii Kuanguka Kwa Senakeribu

20 Kisha Isaya mwana wa Amozi akatuma ujumbe kwa Hezekia kusema: “Hivi ndivyo asemavyoBwana, Mungu wa Israeli: Nimesikia maombi yako kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru.

21 Hili ndilo neno ambaloBwanaamelisema dhidi yake:

“ ‘Bikira Binti Sayuni

anakudharau wewe na kukudhihaki.

Binti Yerusalemu

anatikisa kichwa chake unapokimbia.

22 Unafikiri ni nani uliyemtukana na kumkufuru?

Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake

na kumwinulia macho yako kwa kiburi?

Ni dhidi ya yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!

23 Kupitia kwa wajumbe wako

umelundika matukano juu ya Bwana.

Nawe umesema,

“Kwa magari yangu mengi ya vita,

nimepanda juu ya vilele vya milima,

vilele vya juu sana katika Lebanoni.

Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu,

misunobari yake mizuri;

nimefikia sehemu zake zilizo mbali sana,

misitu yake iliyo mizuri sana.

24 Nimechimba visima katika nchi za kigeni

na kunywa maji yake.

Kwa nyayo za miguu yangu

nimekausha chemchemi zote za Misri.”

25 “ ‘Je, hujasikia?

Zamani sana niliamuru hili.

Siku za kale nilipanga hili;

sasa nimelifanya litokee,

kwamba umegeuza miji yenye ngome

kuwa lundo la mawe.

26 Watu wake, wakiwa wameishiwa nguvu,

wamevunjika moyo na wameaibishwa.

Wamekuwa kama mimea katika shamba,

kama machipukizi mabichi mororo,

kama majani yanayochipua kwenye paa la nyumba,

yaliyokauka kabla hayajakua.

27 “ ‘Lakini mimi ninajua ukaapo,

kuingia kwako na kutoka kwako

na jinsi unavyonighadhabikia.

28 Kwa sababu unaghadhabika dhidi yangu

na kiburi chako kimefika masikioni mwangu,

nitaweka ndoana yangu puani mwako

na lijamu yangu kinywani mwako

nami nitakufanya urudi

kwa njia ile uliyoijia.’

29 “Hii itakuwa ishara kwako, Ee Hezekia:

“Mwaka huu, utakula kile kinachoota chenyewe

na mwaka wa pili, utakula maotea yake.

Lakini katika mwaka wa tatu panda na uvune,

panda mashamba ya mizabibu

na kula matunda yake.

30 Kwa mara nyingine tena wale waliobaki wa nyumba ya Yuda

watatia mizizi chini na kuzaa matunda juu.

31 Kwa maana kutoka Yerusalemu watakuja mabaki,

na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika.

Wivu waBwanaMwenye Nguvu Zote ndio utakaotimiliza hili.

32 “Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyoBwanakuhusu mfalme wa Ashuru:

“Hataingia katika mji huu

wala kupiga mshale hapa.

Hatakuja mbele yake akiwa na ngao,

wala kuweka jeshi kuuzunguka.

33 Kwa njia ile aliyojia, atarudi;

hataingia katika mji huu,

asemaBwana.

34 Nitaulinda mji huu na kuuokoa,

kwa ajili yangu na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.”

35 Usiku ule, malaika waBwanaakatokea na kuwaua watu 185,000 katika kambi ya Waashuru. Askari waliosalia walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!

36 Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.

37 Siku moja, wakati alipokuwa anaabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamwua kwa upanga, nao wakatoroka kwenda katika nchi ya Ararati. Esar-Hadoni mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/19-27bb3072b84e788ebf4961ce6459df60.mp3?version_id=1627—