2 Wafalme 20

Ugonjwa Wa Hezekia

1 Katika siku zile, Hezekia akaugua na akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea na kusema, “Hivi ndivyoBwanaasemavyo: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

2 Hezekia akaelekeza uso wake ukutani akamwombaBwanaakisema,

3 “EeBwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Hezekia akalia sana sana.

4 Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati neno laBwanalikamjia:

5 “Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hivi ndivyoBwana, Mungu wa baba yako Daudi, asemavyo: Nimeyasikia maombi yako na kuona machozi yako; nitakuponya. Katika siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda Hekaluni mwaBwana.

6 Nitaongeza miaka kumi na tano katika maisha yako. Nami nitakuokoa wewe na mji huu kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu kwa ajili yangu na kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi!’ ”

7 Kisha Isaya akasema, “Tengeneza dawa ya kubandika itokanayo na tini.” Wakafanya hivyo na kuweka kwenye jipu, naye akapona.

8 Hezekia alikuwa amemwuliza Isaya, “Kutakuwa na ishara gani kwambaBwanaataniponya mimi na kwamba nitapanda Hekaluni mwaBwanasiku ya tatu tangu leo?”

9 Isaya akajibu, “Hii ndiyo ishara yaBwanakwako kwambaBwanaatafanya kile alichoahidi: Je, kivuli kiende hatua kumi mbele, au kivuli kirudi nyuma hatua kumi?”

10 Hezekia akasema, “Ni jambo rahisi kwa kivuli kutangulia mbele hatua kumi, kuliko kukifanya kirudi nyuma hatua kumi.”

11 Ndipo nabii Isaya akamwitaBwana, nayeBwanaakakifanya kivuli kurudi nyuma hatua kumi ambazo kilikuwa kimeshuka kwenye ngazi ya Ahazi.

Wajumbe Kutoka Babeli

12 Wakati ule Merodaki-Baladani mwana wa Baladoni mfalme wa Babeli akamtumia Hezekia barua pamoja na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua kwa Hezekia.

13 Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonyesha vitu vyote vile vilivyokuwa katika ghala zake, yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu cho chote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.

14 Kisha nabii Isaya akaenda kwa Mfalme Hezekia na kumwuliza, “Hao watu wamesema nini na wametoka wapi?”

Hezekia akajibu, “Wametoka nchi ya mbali. Wametoka Babeli.”

15 Nabii akauliza, “Wameona nini katika jumba lako la kifalme?”

Hezekia akasema, “Wameona kila kitu katika jumba langu la kifalme. Hakuna kitu katika hazina yangu ambacho sikuwaonyesha.”

16 Kisha Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno laBwana:

17 Hakika wakati utakuja ambao kila kitu katika jumba lako la kifalme na vyote vile ambavyo baba zako waliweka akiba mpaka siku hii ya leo, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna cho chote kitakachobaki, asemaBwana.

18 Baadhi ya wazao wako, nyama yako mwenyewe na damu yako, ambao watazaliwa kwako, watachukuliwa, nao watakuwa matowashi ndani ya jumba la mfalme wa Babeli.”

19 Hezekia akajibu, “Neno laBwanaulilosema ni jema.” Mfalme alifikiri, “Lakini si patakuwa na amani na usalama wakati wa uhai wangu?”

20 Matukio mengine ya utawala wa Hezekia, mafanikio yake yote na jinsi alivyotengeneza bwawa na mfereji ambao ulileta maji katika mji, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

21 Hezekia akafa akazikwa pamoja na baba zake. Manase mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/20-381dbdccacaf28d65462ca64941124b5.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 21

Manase Mfalme Wa Yuda

1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka hamsini na mitano. Jina la mama yake aliitwa Hefsiba.

2 Akafanya maovu machoni paBwana, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayoBwanaaliyafukuza mbele ya Waisraeli.

3 Akajenga tena mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo baba yake Hezekia alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Baali na kutengeneza nguzo ya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya. Akasujudia na kuabudu jeshi lote la angani.

4 Akajenga madhabahu ndani ya Hekalu laBwana, ambaloBwanaalikuwa amesema, “Katika Yerusalemu nitaliweka Jina langu.”

5 Katika nyua zote mbili za Hekalu laBwana, akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani.

6 Akamtoa kafara mwanawe mwenyewe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwaBwanana kumghadhibisha.

7 Akachukua nguzo ya Ashera aliyoitengeneza na kuiweka ndani ya Hekalu, ambaloBwanaalikuwa amemwambia Daudi na Solomoni mwanawe hivi, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu, ambavyo nimevichagua kutoka katika makabila yote ya Israeli, nitaliweka Jina langu milele.

8 Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli itangetange kutoka katika nchi niliyowapa baba zao, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru na kuishika Sheria yote ambayo walipewa na Mose mtumishi wangu.”

9 Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, hivyo kwamba walifanya maovu mengi zaidi kuliko mataifa yale ambayoBwanaaliwaangamiza mbele ya Waisraeli.

10 Bwanaakasema kupitia watumishi wake manabii:

11 “Manase mfalme wa Yuda ametenda dhambi hizi za kuchukiza. Amefanya maovu mengi kuliko Waamori waliokuwepo kabla yake na ameiongoza Yuda katika dhambi kwa sanamu zake.

12 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli: Nitaleta maafa makubwa juu ya Yerusalemu na Yuda kiasi kwamba masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yatawasha.

13 Nitanyosha juu ya Yerusalemu kamba ya kupimia iliyotumika dhidi ya Samaria na timazi iliyotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu. Nitaifutilia mbali Yerusalemu kama mtu afutaye sahani, nikiifuta na kuifunikiza.

14 Nitawakataa mabaki wa urithi wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao. Watapokonywa mali zao na kutekwa nyara na adui zao wote,

15 kwa sababu wametenda uovu machoni pangu na kunighadhibisha tangu siku baba zao walipotoka Misri mpaka siku ya leo.”

16 Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, hivyo kwamba wakatenda maovu machoni paBwana.

17 Matukio mengine ya utawala wa Manase, na yote aliyoyafanya, pamoja na dhambi alizotenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

18 Manase akalala pamoja na baba zake na akazikwa katika bustani ya jumba la mfalme, katika bustani ya Uza. Naye Amoni mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Amoni Mfalme Wa Yuda

19 Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka miwili. Jina la mama yake aliitwa Meshulemethi binti Haruzi, alitoka Yotba.

20 Akatenda maovu machoni mwaBwana, kama baba yake Manase alivyofanya.

21 Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia.

22 AkamwachaBwana, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia zaBwana.

23 Maafisa wa Amoni wakafanya shauri baya dhidi yake, nao wakamwua mfalme katika jumba lake la kifalme.

24 Kisha watu wa nchi wakawaua wote waliopanga hilo shauri baya dhidi ya Mfalme Amoni, nao wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.

25 Matukio mengine ya utawala wa Amoni na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

26 Akazikwa kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza. Yosia mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/21-94863de79abd4a09d17595dced65a39d.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 22

Kitabu Cha Torati Chapatikana

1 Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi.

2 Akafanya yaliyo mema machoni paBwanana kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake, bila kugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.

3 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, Mfalme Yosia akamtuma mwandishi, Shafani mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, kwenda katika Hekalu laBwana. Akasema:

4 “Panda uende kwa Hilkia, kuhani mkuu, umwambie ahesabu zile fedha ambazo zimeletwa katika Hekalu laBwana, ambazo mabawabu wamekusanya kutoka kwa watu.

5 Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu laBwana:

6 yaani mafundi seremala, wale wajenzi na mafundi waashi. Waambie pia wanunue mbao na mawe yaliyochongwa ili kukarabati Hekalu.

7 Lakini hawahitajiki kutoa hesabu ya fedha walizokabidhiwa, kwa sababu wanafanya kwa uaminifu.”

8 Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Torati ndani ya Hekalu laBwana.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma.

9 Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu laBwanana imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.”

10 Ndipo Shafani mwandishi akampasha mfalme habari kwamba: “Hilkia kuhani amenipa kitabu hiki.” Naye Shafani akakisoma kile kitabu mbele ya mfalme.

11 Mfalme aliposikia maneno ya kile kitabu cha Torati, akararua majoho yake.

12 Akatoa amri hizi kwa Hilkia kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi na Asaia mhudumu wa mfalme:

13 “Nendeni na mkaulize kwaBwanakwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu kile kilichoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira yaBwanani kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki, hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu sisi.”

14 Hilkia kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani na Asaia wakaenda kuongea na nabii mke Hulda, ambaye alikuwa mke wa Shalumu mwana wa Tikwa, mwana wa Harhasi mtunzaji wa chumba cha mavazi. Hulda aliishi Yerusalemu, katika Mtaa wa Pili.

15 Akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyoBwana, Mungu wa Israeli: Mwambieni yule mtu aliyewatuma ninyi kwangu,

16 ‘Hivi ndivyo asemavyoBwana: Nitaleta maafa juu ya mahali hapa na watu wake, kulingana na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hicho mfalme wa Yuda alichosoma.

17 Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kunighadhibisha kwa sanamu zote zilizotengenezwa kwa mikono yao, hasira yangu itawaka dhidi ya mahali hapa nayo haiwezi kuzimwa.’

18 Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma ninyi kuulizia kwaBwana, ‘Hivi ndivyo asemavyoBwana, Mungu wa Israeli kuhusu maneno uliyoyasikia:

19 Kwa sababu moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele zaBwanauliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake, kwamba wangelaaniwa na kuachwa ukiwa, basi kwa sababu uliyararua majoho yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asemaBwana.

20 Kwa hiyo nitakukusanya wewe kwa baba zako, nawe utazikwa kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote nitakayoleta juu ya mahali hapa.’ ”

Basi wakapeleka jibu lake kwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/22-e27c297c96bde42aaf52913654b37195.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 23

Yosia Analifanya Upya Agano

1 Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.

2 Akapanda mpaka kwenye Hekalu laBwanapamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote kuanzia aliye mdogo hadi aliye mkubwa kabisa. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu laBwana.

3 Mfalme akasimama karibu na nguzo na kulifanya upya lile Agano mbele zaBwana: yaani kumfuataBwanana kuzishika amri zake, maagizo na hukumu zake kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, hivyo kuyathibitisha maneno ya hilo Agano yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki. Kisha watu wote wakajifunga wenyewe kwa kiapo katika Agano.

4 Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani mkuu, makuhani wanaomfuata kwa cheo, na mabawabu kuondoa kutoka kwenye Hekalu laBwanavyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali na Ashera na jeshi lote la mianga ya angani! Akavichoma nje ya Yerusalemu katika mashamba ya Bonde la Kidroni na kuyachukua hayo majivu mpaka Betheli.

5 Akawafukuza makuhani wa kipagani waliokuwa wameteuliwa na wafalme wa Yuda kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji ya Yuda na ile inayozunguka Yerusalemu, yaani wale waliofukiza uvumba kwa Baali, kwa jua na mwezi, kwa makundi ya nyota, na jeshi lote la angani.

6 Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka kwenye Hekalu laBwanana kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu na kuiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wabaya ambao waliitolea kafara.

7 Akabomoa pia nyumba za mahanithi wa mahali pa ibada za miungu, zilizokuwa ndani ya Hekalu laBwanana mahali wanawake walipofuma kwa ajili ya Ashera.

8 Yosia akawaleta makuhani wote waBwanakutoka miji yote ya Yuda na kupafanya mahali pa juu pa kuabudia miungu pasifae tena kufanyia hizo ibada, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji.

9 Ingawa makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu hawakuhudumu katika madhabahu yaBwanakatika Yerusalemu, walikula mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.

10 Kisha mfalme akapafanya Tofethi pasifae tena kufanyiwa hizo ibada za miungu, palipokuwa katika Bonde la Ben-Hinomu, ili mtu ye yote asiweze kupatumia kumtoa kafara mwanawe au binti yake katika moto kwa mungu Moleki.

11 Akaondoa kutoka kwenye ingilio la Hekalu laBwanawale farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa ajili ya mungu jua. Walikuwa kwenye ua karibu na chumba cha afisa aliyeitwa Nathani-Meleki. Basi Yosia akayachoma moto yale magari yaliyokuwa yamewekwa wakfu kwa mungu jua.

12 Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu laBwana. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni.

13 Mfalme pia akapaharibu mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa mashariki ya Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, pale ambapo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amejenga kwa ajili ya Ashtorethi mungu mke aliye chukizo la Wasidoni, kwa ajili ya Kemoshi yule mungu chukizo la Wamoabu, na kwa ajili ya Moleki mungu aliye chukizo la watu wa Amoni, pasifae tena kufanyia hizo ibada.

14 Yosia akapasua yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Ashera. Kisha akafunika hayo maeneo kwa mifupa ya wanadamu.

15 Hata madhabahu iliyokuwa huko Betheli, mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa pamejengwa na Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye aliwafanya Israeli watende dhambi, hata hiyo madhabahu na mahali pa juu pa kuabudia miungu alipabomoa. Alipateketeza kwa moto hapo mahali pa juu pa kuabudia miungu na kupasaga hadi pakawa vumbi na kuichoma hiyo nguzo ya Ashera pia.

16 Kisha Yosia akatazamatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa huko kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu hiyo ya Betheli ili kupafanya pasifae tena kufanyia hizo ibada za miungu. Hili lilitokea sawasawa na neno laBwanalililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya.

17 Mfalme akauliza, “Lile kaburi lenye mnara wa ukumbusho ninaloliona ni kwa ajili gani?”

Watu wa mji wakasema, “Hii ni alama ya kaburi la mtu wa Mungu ambaye alikuja kutoka Yuda, naye akanena dhidi ya hii madhabahu ya Betheli mambo yale yale uliyoifanyia leo.”

18 Akasema, “Liacheni msiliguse. Msimruhusu mtu ye yote kuiondoa mifupa yake.” Basi wakaiacha mifupa yake pamoja na ile ya yule nabii ambaye alikuwa amekuja kutoka Samaria.

19 Kama alivyokuwa amefanya huko Betheli, Yosia akabomoa na kuharibu kabisa mahali pa kuabudia miungu kwenye mahali pa juu ambapo wafalme wa Israeli walikuwa wamejenga ndani ya miji ya Samaria ambayo ilikuwa imemghadhibishaBwana, pasifae tena kwa ibada.

20 Yosia akawachinja makuhani wote wa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika madhabahu zao wenyewe na kuchoma mifupa ya wanadamu juu yake. Kisha akarudi Yerusalemu.

Yosia Aadhimisha Pasaka

21 Mfalme akatoa agizo hili kwa watu wote: “Adhimisheni Pasaka kwaBwanaMungu wenu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu hiki cha Agano.”

22 Hapakuwahi kuwapo na adhimisho jingine la Pasaka kama hilo tangu nyakati za Waamuzi walioongoza Israeli, wala katika nyakati zote za wafalme wa Israeli na wafalme wa Yuda.

23 Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia, Pasaka hii iliadhimishwa kwaBwanahuko Yerusalemu.

24 Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa wapunga pepo, wanaoabudu mizimu, sanamu za kuagulia, sanamu za kuabudiwa na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana katika Yuda na Yerusalemu. Haya aliyafanya ili kutimiza itakiwavyo kulingana na sheria iliyoandikwa ndani ya kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikikuta ndani ya Hekalu laBwana.

25 Kabla wala baada ya Mfalme Yosia hapakuwepo na mfalme mwingine ye yote ambaye alimpendaBwanakwa moyo wake wote, kwa roho yake yote na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria yote ya Mose.

26 Hata hivyo,Bwanahakuacha ghadhabu yake iliyowaka dhidi ya Yuda kwa sababu ya yale yote ambayo Manase alikuwa amefanya ili kumghadhibisha.

27 HivyoBwanaakasema, “Nitamwondoa Yuda mbele zangu kama nilivyomwondoa Israeli, nami nitaukataa Yerusalemu, mji niliouchagua na Hekalu hili, ambalo nilisema, ‘Humo Jina langu litakaa.’ ”

28 Matukio mengine ya utawala wa Yosia na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

29 Yosia alipokuwa mfalme, Farao Neko mfalme wa Misri akapanda mpaka Mto Eufrati kumsaidia mfalme wa Ashuru. Mfalme Yosia akatoka kwenda kupigana naye, lakini Neko akamkabili na kumwua huko Megido.

30 Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake ndani ya gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu na kumzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake.

Yehoahazi Mfalme Wa Yuda

31 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia kutoka Libna.

32 Akafanya maovu machoni mwaBwana, kama baba zake walivyofanya.

33 Farao Neko akamfunga katika minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili kwamba asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akaamuru kodi ya talanta 100za fedha na talanta ya dhahabukatika Yuda.

34 Farao Neko akamfanya Eliyakimu mwana wa Yosia kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia, na kulibadilisha jina la Eliyakimu kuwa Yehoiakimu. Lakini akamchukua Yehoahazi na kumpeleka Misri, naye akafia huko.

35 Yehoiakimu akamlipa Farao Neko ile fedha na dhahabu aliyodai. Ili kuweza kufanya hivyo, Yehoiakimu akatoza nchi kodi na kulipiza fedha na dhahabu kutoka kwa watu wa nchi kulingana na makadrio ya mapato yao.

Yehoiakimu Mfalme Wa Yuda

36 Yehoiakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Zebida binti Pedaya kutoka Ruma.

37 Naye akafanya maovu machoni mwaBwana, kama baba zake walivyokuwa wamefanya.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/23-51087db5fe9fa4ddeda8323be0d0a6cd.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 24

1 Wakati wa utawala wa Yehoiakimu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliishambulia nchi, naye Yehoiakimu akawa mtumwa wake kwa miaka mitatu. Lakini hatimaye akabadili mawazo yake na kuasi dhidi ya Nebukadneza.

2 Bwanaakatuma Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia ghafula. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno laBwanalililosemwa na watumishi wake manabii.

3 Hakika mambo haya yalitokea Yuda kulingana na agizo laBwana, ili kuwaondoa kutoka machoni pake kwa sababu ya dhambi za Manase na yote aliyoyafanya,

4 ikiwa ni pamoja na kumwaga damu isiyo na hatia. Kwa kuwa aliijaza Yerusalemu kwa damu isiyo na hatia naBwanahakuwa radhi kusamehe.

5 Matukio mengine ya utawala wa Yehoiakimu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

6 Yehoiakimu akalala pamoja na baba zake. Naye Yehoyakini mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

7 Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Eufrati.

Yehoyakini Mfalme Wa Yuda

8 Yehoyakini alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu.

9 Akafanya maovu machoni paBwana, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.

10 Wakati huo, maafisa wa Nebukadneza mfalme wa Babeli walikuja ili kuishambulia Yerusalemu nao wakaizunguka kwa jeshi.

11 Nebukadneza mwenyewe akaupandia mji wakati maafisa wake walipokuwa wameuzunguka kwa jeshi.

12 Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza.

Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa.

13 Kama vileBwanaalivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu laBwanana kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu laBwana.

14 Akawachukua Yerusalemu wote kwenda uhamishoni: yaani, maafisa wote na mashujaa, watu wenye ustadi na ufundi, jumla yao watu elfu kumi. Watu maskini sana ndio tu waliobaki katika nchi.

15 Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini kwenda Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu kwenda Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake na viongozi wote wa nchi.

16 Mfalme wa Babeli pia akawahamishia Babeli mashujaa elfu saba, wenye nguvu na wanaofaa kupigana vita, watu wenye ustadi na mafundi elfu moja.

17 Akamfanya Matania, ndugu wa baba yake Yehoyakini, kuwa mfalme mahali pake na akalibadilisha jina lake kuwa Sedekia.

Sedekia Mfalme wa Yuda

18 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Hamuthi binti Yeremia, kutoka Libna.

19 Akafanya maovu machoni mwaBwana, kama alivyofanya Yehoiakimu.

20 Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira yaBwanahaya yote yakatokea katika Yerusalemu na katika Yuda, na mwishoni akawasukumia mbali na uso wake.

Kuanguka Kwa Yerusalemu

Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/24-fbe193ed22d86a9e73a0483df6d0d396.mp3?version_id=1627—

2 Wafalme 25

1 Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akaenda kupigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na jeshi lake lote. Akapiga kambi nje ya mji na kuuzunguka kwa jeshi kote.

2 Mji ulizungukwa na jeshi mpaka mwaka wa kumi na moja wa Mfalme Sedekia.

3 Kufikia siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilizidi kuwa kali sana ndani ya mji, hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu.

4 Kisha ukuta wa mji ukavunjwa, jeshi lote likakimbia usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba,

5 lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatilia mfalme na kumkuta katika sehemu tambarare za Yeriko. Askari wake wote wakajitenga naye na kutawanyika,

6 naye akakamatwa. Akapelekwa kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, mahali ambapo hukumu yake ilitangazwa.

7 Wakawaua wanawe Sedekia mbele ya macho yake. Kisha wakayang’oa macho yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.

8 Katika siku ya saba ya mwezi wa tano katika mwaka wa kumi na tisa wa kutawala kwake Mfalme Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani jemadari wa jeshi la walinzi wa mfalme na afisa wa mfalme wa Babeli, wakaja Yerusalemu.

9 Akachoma moto Hekalu laBwana, jumba la kifalme, na nyumba zote za Yerusalemu. Alichoma kila jengo muhimu.

10 Jeshi lote la Wakaldayo chini ya jemadari wa jeshi la walinzi wa mfalme, wakavunja kuta zilizoizunguka Yerusalemu.

11 Nebuzaradani jemadari wa jeshi la walinzi akawapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebaki katika mji, pamoja na watu wengine waliokuwa wamebaki, na wale askari waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli.

12 Lakini yule jemadari wa jeshi akawaacha baadhi ya wale watu maskini mno wa nchi ili kutunza mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.

13 Wakaldayo wakavunja zile nguzo za shaba, vishikilio vya shaba vinavyohamishika na ile Bahari ya shaba, vile vitu ambavyo vilikuwa katika Hekalu laBwana, nao wakaichukua hiyo shaba kwenda Babeli.

14 Wakachukua pia vyungu, masepetu, mikasi ya kusawazishia utambi, vile vyombo vya udongo na vile vyombo vyote vya shaba vilivyotumika katika huduma hekaluni.

15 Yule jemadari wa jeshi la walinzi wa mfalme akachukua vile vyetezo na yale mabakuli ya kunyunyizia, vitu vyote vile vilivyokuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi au fedha.

16 Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Solomoni alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu laBwana, ilikuwa nzito kiasi kwamba haikuweza kupimika.

17 Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane. Ile taji ya shaba juu ya nguzo moja ilikuwa dhiraa tatuna ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine, pamoja na wavu wake ilifanana na hiyo.

18 Yule jemadari wa jeshi la walinzi akawachukua Seraya aliyekuwa kuhani mkuu, Sefania kuhani aliyekuwa msaidizi wake, pamoja na mabawabu watatu kama wafungwa.

19 Miongoni mwa wale ambao bado walikuwa katika mji, akamchukua afisa aliyesimamia mashujaa na washauri watano wa kifalme. Akamchukua pia mwandishi ambaye alikuwa afisa aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliokutwa ndani ya mji.

20 Nebuzaradani jemadari wa jeshi akawachukua hao wote akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.

21 Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme akaamuru wanyongwe.

Hivyo Yuda akaenda utumwani, mbali na nchi yake.

22 Nebukadneza mfalme wa Babeli akamteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, awe msimamizi wa watu aliowaacha Yuda.

23 Wakati maafisa wote wa jeshi na watu wao waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia kama mtawala, wakamjia Gedalia huko Mispa, nao ni Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao.

24 Gedalia akaapa kuwahakikishia wao na watu wao. Akasema, “Msiwaogope maafisa wa Kikaldayo. Kaeni katika nchi na mtumikieni mfalme wa Babeli, na itakuwa vyema kwenu.”

25 Hata hivyo, katika mwezi wa saba, Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, aliyekuwa wa damu ya kifalme, akaja na watu kumi na wakamwua Gedalia na watu wa Yuda, pamoja na Wakaldayo waliokuwa pamoja naye huko Mispa.

26 Katika hili, watu wote kuanzia aliye mdogo sana hadi aliye mkubwa kabisa, pamoja na maafisa wa jeshi, wakakimbilia Misri kwa kuwaogopa Wakaldayo.

Yehoyakini Anaachiwa

27 Katika mwaka wa thelathini na saba wa uhamisho wa Yehoyakini mfalme wa Yuda, katika mwaka ule ambao Evil-Merodakialikuwa mfalme wa Babeli, akamfungua Yehoyakini kutoka gerezani siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili.

28 Akazungumza naye kwa wema na akampa kiti cha heshima kilicho juu kuliko cha wale wafalme wengine waliokuwa naye huko Babeli.

29 Hivyo Yehoyakini akayavua yale mavazi yake ya kufungwa na kwa maisha yake yote, akawa anakula mezani mwa mfalme.

30 Pia siku kwa siku, mfalme akampa Yehoyakini mahitaji yake siku zote za maisha yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/25-c749dd03d84d04af0b36cf8d7ccba8b2.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 1

Adonia Ajitangaza Mwenyewe Kuwa Mfalme

1 Mfalme Daudi alipokuwa mzee umri ukiwa umesogea, hakuweza kupata joto hata walipomfunika kwa nguo.

2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Turuhusu tumtafute kijana mwanamwali bikira amhudumie mfalme na kumtunza. Anaweza kulala pembeni mwake ili bwana wetu mfalme apate joto.”

3 Kisha wakatafuta katika Israeli yote ili kumpata msichana mzuri wa sura na wakampata Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.

4 Msichana huyo alikuwa mzuri sana wa sura, akamtunza mfalme na kumhudumia, lakini mfalme hakufanya naye tendo la ndoa.

5 Basi Adonia, ambaye mama yake alikuwa Hagathi, akajigamba na kusema, “Mimi nitakuwa mfalme.” Hivyo akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, pamoja na watu hamsini watakaomtangulia wakikimbia.

6 (Baba yake hakuwa ameingilia na kumwuliza, “Kwa nini unafanya hivyo?” Alikuwa pia kijana mzuri sana wa sura, na alizaliwa baada ya Absalomu.)

7 Adonia akashauriana pamoja na Yoabu mwana wa Seruya na kuhani Abiathari, nao wakamsaidia.

8 Lakini kuhani Sadoki, Benaya mwana wa Yehoyada, Nathani nabii, Shimei, Rei na walinzi maalum wa Daudi hawakujiunga na Adonia.

9 Ndipo Adonia akatoa dhabihu ya kondoo, ng’ombe na ndama walionona kwenye Jiwe la Zohelethi karibu na En-Rogeli. Akawaalika ndugu zake wote, wana wa mfalme na wanaume wote wa Yuda waliokuwa maafisa wa kifalme,

10 lakini hakumwalika nabii Nathani, Benaya, walinzi maalum wa mfalme wala ndugu yake Solomoni.

11 Ndipo Nathani akamwuliza Bathsheba, mama yake Solomoni, “Je, hujasikia kwamba Adonia, mwana wa Hagathi, amekuwa mfalme pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili?

12 Sasa basi, acha nikushauri jinsi utakavyookoa uhai wako mwenyewe na uhai wa mwanao Solomoni.

13 Ingia kwa Mfalme Daudi na umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je hukuniapia mimi mtumishi wako: “Hakika mwanao Solomoni atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi juu ya kiti changu cha ufalme”? Kwa nini basi Adonia amekuwa mfalme?’

14 Utakapokuwa ukizungumza na mfalme, nitaingia na kuthibitisha hayo uliyoyasema.”

15 Hivyo Bathsheba akaenda kumwona mfalme chumbani mwake mahali ambapo Abishagi, Mshunami, alikuwa akimhudumia, naye mfalme alikuwa mzee sana.

16 Bathsheba akasujudu na kupiga magoti mbele ya mfalme.

Mfalme akauliza, “Ni nini hiki unachotaka?”

17 Akamwambia, “Bwana wangu, wewe mwenyewe uliniapia mimi mtumishi wako kwaBwanaMungu wako kwamba: ‘Solomoni Mwanao atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme.’

18 Lakini sasa Adonia amekuwa mfalme, nawe, bwana wangu mfalme huna habari kuhusu jambo hilo.

19 Ametoa dhabihu idadi kubwa ya ng’ombe, ndama walionona na kondoo, naye amewaalika wana wa mfalme wote, kuhani Abiathari, na Yoabu jemadari wa jeshi, lakini hakumwalika Solomoni mtumishi wako.

20 Bwana wangu mfalme, macho ya Israeli yote yanakutazama wewe wajue kutoka kwako kuwa ni nani atakayeketi katika kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake.

21 Kama sivyo, mara tu bwana wangu mfalme atakapopumzishwa pamoja na baba zake, mimi na mwanangu Solomoni tutatendewa kama wahalifu.”

22 Alipokuwa angali anazungumza na mfalme, nabii Nathani akafika.

23 Wakamwambia mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa.” Kisha akaenda mbele ya mfalme na kumsujudia hadi uso wake ukagusa ardhi.

24 Nathani akasema, “Je, bwana wangu mfalme, umetangaza kuwa Adonia atakuwa mfalme baada yako na kwamba ataketi kwenye kiti chako cha ufalme?

25 Leo ameshuka na kutoa dhabihu idadi kubwa ya ng’ombe, ndama walionona na kondoo. Amewaalika wana wote wa mfalme, jemadari wa jeshi na kuhani Abiathari. Sasa hivi, wanakula na kunywa pamoja naye wakisema, ‘Aishi maisha marefu, Mfalme Adonia!’

26 Lakini mimi mtumishi wako, kuhani Sadoki, Benaya mwana wa Yehoyada na mtumishi wako Solomoni hakutualika.

27 Je, hili ni jambo ambalo bwana wangu mfalme amelifanya pasipo kuwajulisha watumishi wake ili wapate kujua ni nani atakayeketi kwenye kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake?”

Daudi Amfanya Solomoni Kuwa Mfalme

28 Ndipo Mfalme Daudi akasema, “Mwite Bathsheba, aingie ndani.” Hivyo akaingia mbele ya mfalme na kusimama mbele yake.

29 Ndipo mfalme akaapa: “Hakika kamaBwanaaishivyo, ambaye ameniokoa kutoka katika kila taabu,

30 hakika nitatekeleza leo kile nilichokuapia kwaBwana, Mungu wa Israeli: Mwanao Solomoni atakuwa mfalme baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha ufalme baada yangu.”

31 Kisha Bathsheba akasujudu akipiga magoti mbele ya mfalme uso wake ukigusa ardhi akasema, “Bwana wangu Mfalme Daudi na aishi milele!”

32 Mfalme Daudi akasema, “Mwite kuhani Sadoki ndani, nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada.” Walipofika mbele ya mfalme,

33 akawaambia: “Wachukueni watumishi wa bwana wenu pamoja nanyi na mkamkalishe mwanangu Solomoni juu ya nyumbu wangu mwenyewe mkamtelemshe hadi Gihoni.

34 Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wamtie mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, ‘Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!’

35 Kisha mtapanda pamoja naye, atakuja na kuketi kwenye kiti changu cha ufalme na kutawala badala yangu. Nimemweka awe mtawala juu ya Israeli na Yuda.”

36 Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, “Amen!Bwana, Mungu wa bwana wangu mfalme, na aseme vivyo hivyo.

37 Kama vileBwanaalivyokuwa na bwana wangu mfalme, vivyo hivyo na awe na Solomoni kukifanya kiti chake cha utawala kuwa kikuu kuliko kile cha bwana wangu Mfalme Daudi!”

38 Hivyo kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi wakampandisha Solomoni juu ya nyumbu wa Mfalme Daudi, nao wakamsindikiza hadi Gihoni.

39 Kuhani Sadoki akachukua pembe ya mafuta kutoka kwenye hema takatifu na kumtia Solomoni mafuta. Kisha wakapiga tarumbeta na watu wote wakapaza sauti wakisema, “Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!”

40 Na watu wote wakakwea wakimfuata, wakipiga filimbi na kushangilia sana, hata ardhi ikatikisika kwa ile sauti.

41 Adonia pamoja na wageni wote waliokuwa pamoja naye wakasikia sauti hiyo walipokuwa wakimalizia karamu yao. Waliposikia sauti ya tarumbeta, Yoabu akauliza, “Nini maana ya makelele yote haya katika mji?”

42 Hata alipokuwa anasema, Yonathani mwana wa kuhani Abiathari akafika. Adonia akasema, “Ingia ndani. Mtu mstahiki kama wewe ni lazima alete habari njema.”

43 Yonathani akajibu, “La hasha! Mfalme Daudi bwana wetu amemfanya Solomoni kuwa mfalme.

44 Mfalme amemtuma pamoja naye kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi, nao wamempandisha juu ya nyumbu wa mfalme,

45 nao kuhani Sadoki na nabii Nathani wamemtia mafuta kuwa mfalme huko Gihoni. Kuanzia hapo wameendelea kushangilia na sauti zimeenea pote mjini. Hizo ndizo kelele unazosikia.

46 Zaidi ya hayo, Solomoni ameketi juu ya kiti chake cha ufalme.

47 Pia, maafisa wa kifalme wamekuja ili kumtakia heri bwana wetu Mfalme Daudi wakisema, ‘Mungu wako na alifanye jina la Solomoni kuwa mashuhuri kuliko lako na kiti chake cha ufalme kiwe na ukuu kuliko chako!’ Naye mfalme akasujudu akiabudu kitandani mwake

48 na kusema, ‘AhimidiweBwana, Mungu wa Israeli, ambaye ameruhusu macho yangu kuona mrithi juu ya kiti changu cha ufalme leo hii.’ ”

49 Katika hili, wageni wote wa Adonia wakainuka kwa mshtuko wa hofu na kutawanyika.

50 Lakini Adonia kwa kumwogopa Solomoni, akaenda na kushika pembe za madhabahu.

51 Kisha Solomoni akaambiwa, “Adonia anamwogopa Mfalme Solomoni na ameshikilia pembe za madhabahu. Anasema, ‘Mfalme Solomoni na aniapie leo kwamba hatamwua mtumishi wake kwa upanga.’ ”

52 Solomoni akajibu, “Kama akijionyesha kuwa mtu mstahiki, hakuna unywele wake utakaoanguka juu ya ardhi, lakini kama uovu ukionekana ndani yake, atakufa.”

53 Ndipo Mfalme Solomoni akawatuma watu, nao wakamshusha kutoka madhabahuni. Naye Adonia akaja akamwinamia Mfalme Solomoni, naye Solomoni akamwambia, “Nenda nyumbani kwako.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/1-b32266cda2eab3dc7b22f68d4ce05245.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 2

Maagizo Ya Daudi Kwa Solomoni

1 Siku zilipokaribia za Daudi kufa, akampa mwanawe Solomoni agizo.

2 Akasema, “Mimi ninakaribia kwenda njia ya dunia yote. Hivyo uwe hodari, jionyeshe kuwa mwanaume,

3 shika lileBwanaMungu wako analokuagiza: Enenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na po pote uendako,

4 ili kwambaBwanaaweze kunitimizia ahadi yake: ‘Kama wazao wako wakiangalia sana wanavyoishi, na kama wakienenda kwa uaminifu mbele zangu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, kamwe hutakosa kuwa na mtu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli.’

5 “Sasa wewe mwenyewe unafahamu lile Yoabu mwana wa Seruya alilonitendea, lile alilofanya kwa majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yetheri. Aliwaua, akimwaga damu yao wakati wa amani kama vile ni kwenye vita, tena akaipaka damu ile kwenye mkanda uliokuwa kiunoni mwake na viatu alivyovaa miguuni mwake.

6 Shughulika naye kwa kadiri ya hekima yako, lakini usiache kichwa chake chenye mvi kishukie kaburi kwa amani.

7 “Lakini uwaonyeshe wema wana wa Barzilai wa Gileadi na uwaruhusu wawe miongoni mwa wale walao mezani pako. Walisimama nami nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.

8 “Ukumbuke, unaye Shimei mwana wa Gera, Mbenyamini kutoka Bahurimu, ambaye alinilaani kwa laana kali siku niliyokwenda Mahanaimu. Aliposhuka kunilaki huko Yordani, nilimwapia kwaBwana: ‘Sitakuua kwa upanga!’

9 Lakini sasa, usidhani kwamba hana hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa damu.”

10 Kisha Daudi akapumzika pamoja na baba zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi.

11 Alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini, miaka saba huko Hebroni na miaka thelathini na mitatu katika Yerusalemu.

12 Kwa hiyo Solomoni akaketi katika kiti cha ufalme cha baba yake Daudi, nao utawala wake ukaimarika sana.

Kiti Cha Ufalme Cha Solomoni Chaimarishwa

13 Basi Adonia, mwana wa Hagithi, akaenda kwa Bathsheba, mama yake Solomoni. Bathsheba akamwuliza, “Je, umekuja kwa amani?”

Akajibu, “Ndiyo, kwa amani.”

14 Kisha akaongeza, “Ninalo jambo la kukuambia.”

Akajibu, “Waweza kulisema.”

15 Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwaBwana.

16 Sasa ninalo ombi moja ninalokuomba. Usinikatalie.”

Bathsheba akasema, “Waweza kuliomba.”

17 Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Solomoni, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.”

18 Bathsheba akamjibu, “Vema sana, nitazungumza na mfalme kwa ajili yako.”

19 Bathsheba alipokwenda kwa Mfalme Solomoni kuzungumza naye kwa ajili ya Adonia, mfalme alisimama kumlaki mama yake, akamwinamia na kuketi kwenye kiti chake cha ufalme. Akaamuru kiti cha ufalme kuletwa kwa ajili ya mama yake mfalme, naye akaketi mkono wake wa kuume.

20 Bathsheba akamwambia mfalme, “Ninalo ombi moja dogo la kukuomba; usinikatalie.”

Mfalme akajibu, “Omba, mama yangu; sitakukatalia.”

21 Akasema, “Mruhusu Abishagi, Mshunami, aolewe na ndugu yako Adonia.”

22 Mfalme Solomoni akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi, Mshunami, kwa ajili ya Adonia? Ungeweza pia kuomba ufalme kwa ajili yake, hata hivyo, yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, pia kuhani Abiathari na Yoabu mwana wa Seruya wapo upande wake!”

23 Mfalme Solomoni akaapa kwaBwana, akasema: “Mungu na aniulie mbali, tena bila huruma, ikiwa Adonia hatalipa kwa uhai wake kwa ajili ya ombi hili!

24 Basi sasa, hakika kamaBwanaaishivyo, yeye ambaye ameniimarisha salama kwenye kiti cha ufalme cha Daudi baba yangu naye amenipatia ukoo wa kifalme kama alivyoahidi, Adonia atauawa leo!”

25 Hivyo Mfalme Solomoni akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akampiga Adonia akafa.

26 Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku laBwanaMwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.”

27 Hivyo Solomoni akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani waBwana, akilitimiza neno laBwanaalilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.

28 Habari zilipomfikia Yoabu, ambaye alikuwa amefanya shauri baya na Adonia, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema laBwanana kushika pembe za madhabahu.

29 Mfalme Solomoni akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema laBwananaye alikuwa kando ya madhabahu. Basi Solomoni akamwagiza Benaya mwana wa Yehoyada: “Nenda ukamwue!”

30 Ndipo Benaya akaingia kwenye hema laBwanana kumwambia Yoabu, “Mfalme anasema, ‘Toka nje!’ ”

Lakini akajibu, “La! Nitafia hapa hapa.”

Benaya akamwarifu mfalme, “Hivi ndivyo Yoabu alivyonijibu.”

31 Kisha mfalme akamwamuru Benaya, “Fanya kama asemavyo. Mwue na kumzika, ili uniondolee mimi na nyumba ya baba yangu dhambi ya damu isiyokuwa na hatia ile Yoabu aliyoimwaga.

32 Bwanaatamlipiza kwa ajili ya damu aliyoimwaga, kwa sababu pasipo Daudi baba yangu kujua, aliwashambulia watu wawili na kuwaua kwa upanga. Wote wawili, Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda, walikuwa watu wazuri na wanyofu kuliko yeye.

33 Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani yaBwanamilele.”

34 Basi Benaya mwana wa Yehoyada akakwea, akampiga na kumwua Yoabu, naye akazikwa katika nchi yake mwenyewe katika jangwa.

35 Mfalme akamweka Benaya mwana wa Yehoyada juu ya jeshi kwenye nafasi ya Yoabu na kumweka kuhani Sadoki badala ya Abiathari.

36 Kisha mfalme akatuma ujumbe kwa Shimei na kumwambia, “Ujijengee nyumba huko Yerusalemu uishi huko, lakini usiende mahali pengine po pote.

37 Siku utakayoondoka kuvuka Bonde la Kidroni, uwe na hakika utakufa; damu yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe.”

38 Shimei akamjibu mfalme, “Ulilolisema ni jema. Mtumishi wako atatenda kama bwana wangu mfalme alivyosema.” Naye Shimei akakaa Yerusalemu kwa muda mrefu.

39 Lakini baada ya miaka mitatu, watumwa wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi, naye Shimei akaambiwa, “Watumwa wako wako Gathi.”

40 Kwa ajili ya hili, Shimei akatandika punda wake, akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumwa wake. Basi Shimei akaondoka na kuwarudisha watumwa wake kutoka Gathi.

41 Solomoni alipoambiwa kuwa Shimei ametoka Yerusalemu na kwenda Gathi na amekwisha kurudi,

42 mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwaBwanana kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine po pote, uwe na hakika utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’

43 Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwaBwanana kutii amri niliyokupa?”

44 Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua katika moyo wako makosa uliyomtendea baba yangu Daudi. SasaBwanaatakulipiza kwa ajili ya mabaya yako uliyotenda.

45 Lakini Mfalme Solomoni atabarikiwa, na kiti cha ufalme cha Daudi kitakuwa imara mbele zaBwanamilele.”

46 Kisha mfalme akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akatoka nje, akampiga Shimei na kumwua.

Sasa ufalme ukawa umeimarika kikamilifu mikononi mwa Solomoni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/2-04b04cb74127ecd57d457455875f8458.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 3

Solomoni Anaomba Hekima

1 Solomoni akafanya urafiki na Mfalme Farao wa Misri na kumwoa binti yake. Akamleta huyo binti katika Mji wa Daudi mpaka alipomaliza kujenga jumba lake la kifalme na Hekalu laBwana, pamoja na ukuta kuzunguka Yerusalemu.

2 Hata hivyo, watu bado walikuwa wakitoa dhabihu huko kwenye vilima, kwa sababu Hekalu lilikuwa bado halijajengwa kwa ajili ya Jina laBwana.

3 Solomoni akaonyesha upendo wake kwaBwanakwa kuenenda sawasawa na amri za Daudi baba yake, ila yeye alitoa dhabihu na kufukiza uvumba huko mahali pa juu.

4 Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu, kwa maana ndipo palipokuwa mahali maarufu zaidi, naye Solomoni akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya hiyo madhabahu.

5 Bwanaakamtokea Solomoni huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, “Omba lo lote utakalo nikupe.”

6 Solomoni akajibu, “Umemfanyia mtumishi wako baba yangu Daudi fadhili nyingi, kwa kuwa alikuwa mwaminifu kwako na mwenye haki tena mnyofu wa moyo. Nawe umemzidishia fadhili hii kuu na umempa mwana wa kuketi kwenye kiti chake cha ufalme kama ilivyo leo.

7 “Sasa, EeBwanaMungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme baada ya baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu.

8 Mtumishi wako yuko hapa miongoni mwa watu uliowachagua. Taifa kubwa, watu wengi wasioweza kuhesabika wala kutoa idadi yao.

9 Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu kutawala watu wako na kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa maana ni nani awezaye kutawala watu wako hawa walio wengi?”

10 Bwana akapendezwa kwamba Solomoni ameliomba jambo hili.

11 Basi Mungu akamwambia, “Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki,

12 nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe wala kamwe hatakuwapo baada yako.

13 Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba, yaani utajiri na heshima, ili kwamba maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme.

14 Nawe kama ukienenda katika njia zangu na kutii sheria na amri zangu kama baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.”

15 Ndipo Solomoni akaamka, akatambua kuwa alikuwa katika ndoto.

Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano laBwana, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu.

Utawala Wa Hekima

16 Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake.

17 Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami.

18 Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine ye yote katika nyumba isipokuwa sisi wawili.

19 “Wakati wa usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia.

20 Hivyo akaondoka katikati ya usiku na kumchukua mwanangu kutoka ubavuni pangu wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa nimelala. Akamweka kifuani mwake na kumweka mwanawe aliyekufa kifuani mwangu.

21 Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia sana katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyekuwa nimemzaa.”

22 Huyo mwanamke mwingine akasema, “Hapana! Mwana aliye hai ndiye wangu, aliyekufa ni wako.”

Lakini yule wa kwanza akasisitiza, “Hapana! Mwana aliyekufa ni wako, aliye hai ni wangu.” Hivi ndivyo walivyobishana mbele ya mfalme.

23 Mfalme akasema, “Huyu anasema, ‘Mwanangu ndiye aliye hai, na aliyekufa ndiye mwanao,’ maadamu yule anasema, ‘Hapana! Aliyekufa ni wako, na aliye hai ni wangu.’ ”

24 Kisha mfalme akasema, “Nileteeni upanga.” Basi wakamletea mfalme upanga.

25 Ndipo mfalme akatoa amri: “Mkate mtoto aliye hai vipande viwili; mpe huyu nusu na mwingine nusu.”

26 Mwanamke ambaye mwanawe alikuwa hai akajawa na huruma kwa ajili ya mwanawe na kumwambia mfalme, “Tafadhali, bwana wangu, mpe yeye mtoto aliye hai! Usimue!”

Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Mkate vipande viwili. Asiwe wangu au wake!”

27 Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: “Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimue; ndiye mama yake.”

28 Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/3-cbb744ac422e54270c38ab18dc0fdbe6.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 4

Maafisa Wa Solomoni Na Watawala

1 Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote.

2 Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu:

Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki;

3 Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi;

Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani;

4 Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi;

Sadoki na Abiathari: makuhani;

5 Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya;

Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme;

6 Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme;

Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha.

7 Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.

8 Majina yao ni haya:

Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu;

9 Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani;

10 Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake);

11 Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni);

12 Baana mwana wa Ahihudi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Zarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu;

13 Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba);

14 Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu;

15 Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni);

16 Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Alothi;

17 Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;

18 Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;

19 Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo.

Mahitaji Ya Solomoni Ya Kila Siku

20 Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi.

21 Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Eufrati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.

22 Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathiniza unga laini, kori sitiniza unga wa kawaida.

23 Ng’ombe kumi wa zizini, ng’ombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana.

24 Kwa kuwa Solomoni alitawala falme zote magharibi ya mto, kuanzia Tifsa hadi Gaza, naye akawa na amani pande zote.

25 Wakati wa maisha ya Solomoni Yuda na Israeli, kuanzia Dani mpaka Beer-Sheba, wakaishi salama kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake.

26 Solomoni alikuwa na mabanda 4,000ya magari ya vita, na farasi 12,000.

27 Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Solomoni na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna cho chote kilichopungua.

28 Pia walileta sehemu walizopangiwa za shayiri na majani kwa ajili ya farasi wavutao magari na farasi wengine mahali palipostahili.

Hekima Ya Solomoni

29 Mungu akampa Solomoni hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari.

30 Hekima ya Solomoni ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri.

31 Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi: kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka.

32 Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005.

33 Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki.

34 Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Solomoni, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/4-58b64b3ca7467ebf775e033f9e990b2a.mp3?version_id=1627—