1 Wafalme 15

Abiya Mfalme Wa Yuda

1 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda,

2 naye akatawala katika Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.

3 Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwaBwanaMungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa.

4 Pamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi,BwanaMungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara.

5 Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni paBwanana hakushindwa kushika maagizo yote yaBwanasiku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.

6 Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya.

7 Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Abiya na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.

8 Naye Abiya akalala pamoja na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Asa mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Asa Mfalme Wa Yuda

9 Katika mwaka wa ishirini wa kutawala kwake Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda,

10 naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na mmoja. Jina la bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.

11 Asa akatenda yaliyo mema machoni mwaBwana, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake.

12 Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka katika nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza.

13 Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye nafasi yake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akakatakata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto kwenye Bonde la Kidroni.

14 Japokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwaBwanakikamilifu maisha yake yote.

15 Akaleta ndani ya Hekalu laBwanafedha na dhahabu, pamoja na vitu ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

16 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao.

17 Baasha mfalme wa Israeli akakwea dhidi ya Yuda na kuweka ngome Rama ili kuzuia ye yote kuingia au kutoka katika nchi ya Asa mfalme wa Yuda.

18 Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imeachwa katika hazina za Hekalu laBwanana za jumba lake mwenyewe la kifalme. Akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu, aliyekuwa akitawala Dameski.

19 “Akasema na pawepo mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nakutumia zawadi ya fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniache huru.”

20 Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na akatuma majemadari wake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote pamoja na Naftali.

21 Wakati Baasha aliposikia hili, akaacha kuijenga Rama na akaenda kuishi Tirza.

22 Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumbagua hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyoko Benyamini na Mispa pia.

23 Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda? Katika uzee wake, hata hivyo, alipata ugonjwa wa miguu.

24 Kisha Asa akalala pamoja na baba zake na kuzikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Naye Yehoshafati mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Nadabu Mfalme Wa Israeli

25 Nadabu mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Asa wa Yuda, naye akatawala Israeli kwa miaka miwili.

26 Akafanya maovu machoni paBwana, akienenda katika njia za baba yake na katika dhambi yake, ambayo alisababisha Israeli kuifanya.

27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akafanya shauri baya dhidi yake, naye akamwua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walipokuwa wameuzingira.

28 Baasha akamwua Nadabu katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, naye Baasha akaingia mahali pake kuwa mfalme.

29 Mara tu alipoanza kutawala, aliua jamaa yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu ye yote aliyekuwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno laBwanalililotolewa kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni,

30 kwa sababu ya dhambi alizokuwa amezitenda Yeroboamu na kusababisha Israeli kuzitenda, tena kwa sababu alimkasirishaBwana, Mungu wa Israeli.

31 Kwa matukio mengine ya utawala wa Nadabu na yote aliyofanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

32 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli wakati wote wa utawala wao.

Baasha Mfalme Wa Israeli

33 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme wa Israeli yote huko Tirza, naye akatawala kwa miaka ishirini na minne.

34 Akatenda maovu machoni paBwana, akienenda katika njia za Yeroboamu na dhambi yake, ambayo alikuwa amesababisha Israeli kuitenda.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/15-66d931e0f93b885b2650ee0b2505fed1.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 16

1 Ndipo neno laBwanalikamjia Yehu mwana wa Hanani dhidi ya Baasha, kusema:

2 “Nilikuinua kutoka mavumbini na kukufanya kiongozi wa watu wangu Israeli, lakini ukaenenda katika njia za Yeroboamu na kusababisha watu wangu Israeli kutenda dhambi na kunikasirisha kwa dhambi zao.

3 Basi nitamwangamiza Baasha pamoja na nyumba yake, nami nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwanawe Nebati.

4 Mbwa watawala watu wa Baasha watakaofia mjini na ndege wa angani watajilisha kwa wale watakaofia mashambani.”

5 Kwa matukio mengine ya utawala wa Baasha, aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

6 Baasha akalala na baba zake naye akazikwa huko Tirza. Naye Ela mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

7 Zaidi ya hayo, neno laBwanalikamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni paBwana, akamkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu, na pia kwa sababu aliiangamiza.

Ela Mfalme Wa Israeli

8 Katika mwaka wa ishirini na sita wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala huko Tirza kwa miaka miwili.

9 Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akafanya hila mbaya dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akilewa katika nyumba ya Arsa, mtu aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirza.

10 Zimri akaingia, akampiga na kumwua katika mwaka wa ishirini na saba wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda. Kisha Zimri akaingia mahali pake kuwa mfalme.

11 Mara tu alipoanza kutawala na kuketi juu ya kiti cha ufalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki.

12 Hivyo Zimri akaangamiza jamaa yote ya Baasha, kulingana na neno laBwanalililonenwa dhidi ya Baasha kupitia nabii Yehu:

13 kwa sababu ya dhambi zote Baasha na mwanawe Ela walizokuwa wametenda na wakasababisha Israeli kuzitenda, basi wakamkasirishaBwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.

14 Kwa matukio mengine ya utawala wa Ela, na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

Zimri Mfalme Wa Israeli

15 Katika mwaka wa ishirini na saba wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala huko Tirza siku saba. Jeshi lilikuwa limepiga kambi karibu na Gibethoni, mji wa Wafilisti.

16 Wakati Waisraeli waliokuwa kambini waliposikia kuwa Zimri alikuwa amefanya hila mbaya dhidi ya mfalme na kumwua, wakamtangaza Omri, jemadari wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli siku iyo hiyo huko kambini.

17 Ndipo Omri na Waisraeli wote pamoja naye wakaondoka Gibethoni na kuizingira Tirza.

18 Wakati Zimri alipoona kuwa mji umechukuliwa, alikwenda ndani ya ngome ya jumba la kifalme na kulichoma moto jumba la kifalme na kujiteketeza ndani yake. Kwa hiyo akafa,

19 kwa sababu ya dhambi alizofanya, akitenda maovu machoni paBwanana kuenenda katika njia za Yeroboamu na katika dhambi alizofanya na kusababisha Israeli kuzifanya.

20 Kwa matukio mengine ya utawala wa Zimri, na uasi alioutenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

Omri Mfalme Wa Israeli

21 Ndipo watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamwunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme na nusu nyingine wakamwunga mkono Omri.

22 Lakini wafuasi wa Omri wakajionyesha wenye nguvu kuliko wale wa Tibni mwana wa Ginathi. Hivyo Tibni akafa na Omri akawa mfalme.

23 Katika mwaka wa thelathini na moja wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili, sita kati ya hiyo katika Tirza.

24 Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbiliza fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.

25 Lakini Omri akatenda maovu machoni paBwanana kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia.

26 Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirishaBwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.

27 Kwa matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na vitu alivyovifanikisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

28 Omri akalala pamoja na baba zake na akazikwa huko Samaria. Ahabu mwanawe akatawala mahali pake.

Ahabu Awa Mfalme Wa Israeli

29 Katika mwaka wa thelathini na nane wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala Israeli akiwa Samaria kwa miaka ishirini na miwili.

30 Ahabu mwana wa Omri akafanya maovu zaidi machoni mwaBwanakuliko ye yote aliyewatangulia.

31 Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti wa Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu.

32 Akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali katika hekalu la Baali lile alilolijenga huko Samaria.

33 Pia Ahabu akatengeneza nguzo ya Ashera na kufanya mengi ili kumkasirishaBwana, Mungu wa Israeli, kuliko walivyofanya wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.

34 Katika wakati wa Ahabu, Hieli, Mbetheli, akaijenga upya Yeriko. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kulingana na neno laBwanaalilosema kupitia Yoshua mwana wa Nuni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/16-f4eadd4d8185d7ed343c7e87ef74a6e3.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 17

Eliya Analishwa Na Kunguru

1 Basi Eliya, Mtishbi kutoka Tishbi katika Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye ninamtumikia, hapatakuwa na umande wala mvua katika miaka hii isipokuwa kwa neno langu.”

2 Kisha neno laBwanalikamjia Eliya, kusema,

3 “Ondoka hapa, elekea upande wa mashariki ukajifiche katika Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani.

4 Utakunywa maji kutoka katika kile kijito, nami nimeagiza kunguru wakulishe huko.”

5 Hivyo akafanya kile alichoambiwa naBwana. Akaenda katika Kijito cha Kerithi, mashariki ya Yordani na akakaa huko.

6 Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji kutoka katika kile kijito.

Mjane Wa Sarepta

7 Baada ya muda, kile kijito kikakauka kwa sababu mvua haikuwa imenyesha katika nchi.

8 Kisha neno laBwanalikamjia, kusema,

9 “Ondoka, uende Sarepta ya Sidoni na ukae huko. Nimemwagiza mjane katika sehemu ile akupatie chakula.”

10 Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.”

11 Alipokuwa anakwenda kumletea, akamwita akasema, “Tafadhali niletee pia kipande cha mkate.”

12 Akamjibu, “Hakika kamaBwanaMungu wako aishivyo, sina mkate wo wote, isipokuwa konzi ya unga kwenye gudulia na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili kwamba tule, kiishe, tukafe.”

13 Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unitengenezee mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyonavyo kisha uniletee na ndipo utayarishe cho chote kwa ajili yako na mwanao.

14 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyoBwana, Mungu wa Israeli: ‘Lile gudulia la unga halitakwisha wala ile chupa ya mafuta haitakauka hadi siku ileBwanaatakapoleta mvua juu ya nchi.’ ”

15 Akaondoka na kufanya kama Eliya alivyomwambia. Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Eliya, yule mwanamke na jamaa yake.

16 Kwa kuwa lile gudulia la unga halikwisha na ile chupa ya mafuta haikukauka, sawasawa na lile neno laBwanaalilosema Eliya.

17 Baada ya muda, mwana wa yule mwanamke mwenye nyumba akaugua. Hali yake ikaendelea kuwa mbaya sana, na hatimaye akaacha kupumua.

18 Akamwambia Eliya, “Una nini dhidi yangu, ewe mtu wa Mungu? Umekuja ili kukumbushia dhambi yangu na kusababisha kifo cha mwanangu?”

19 Eliya akamjibu, “Nipe mwanao.” Eliya akampokea kutoka kifuani mwake, akambeba mpaka chumba cha juu alipokuwa anaishi, akamlaza kitandani mwake.

20 Kisha akamliliaBwana, akasema “EeBwanaMungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi pamoja naye, kwa kusababisha mwanawe kufa?”

21 Kisha akajinyoosha juu ya kijana mara tatu na kumliliaBwana, akisema, “EeBwanaMungu wangu, nakuomba roho ya huyu kijana imrudie!”

22 Bwanaakasikia kilio cha Eliya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka.

23 Eliya akamtwaa kijana na kumbeba kutoka chumbani mwake akamshusha kumpeleka kwenye nyumba. Akampa mama yake na kusema, “Tazama, mwanao yu hai!”

24 Ndipo yule mwanamke akamwambia Eliya, “Sasa ninajua kwamba wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno laBwanakutoka kinywani mwako ni kweli.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/17-23469aa3be36cb9b6f4d0d24d8a53df7.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 18

Eliya Na Obadia

1 Baada ya muda mrefu, katika mwaka wa tatu, neno laBwanalikamjia Eliya kusema, “Nenda ukajionyeshe kwa Ahabu na mimi nitanyesha mvua juu ya nchi.”

2 Kwa hiyo Eliya akaenda kujionyesha kwa Ahabu.

Wakati huu njaa ilikuwa kali sana katika Samaria,

3 naye Ahabu alikuwa amemwita Obadia ambaye alikuwa msimamizi wa jumba lake la kifalme. (Obadia alimchaBwanasana.

4 Wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii waBwana, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja na akawa anawapatia chakula na maji.)

5 Ahabu alikuwa amemwambia Obadia, “Nenda katika nchi yote kwenye vijito vyote na mabonde. Huenda tunaweza kupata majani ya kuwalisha farasi na nyumbu wapate kuishi ili tusilazimike kuwaua hata mmoja wa wanyama wetu.”

6 Kwa hiyo wakagawanya nchi waliyokusudia kutafuta majani, Ahabu akaenda upande mmoja na Obadia upande mwingine.

7 Wakati Obadia alipokuwa akitembea njiani, Eliya akakutana naye. Obadia akamtambua, akamsujudia hadi nchi na kusema, “Je, hivi kweli ni wewe, bwana wangu Eliya?”

8 Eliya akamjibu, “Ndiyo, nenda ukamwambie bwana wako Ahabu, ‘Eliya yuko hapa.’ ”

9 Obadia akamwuliza, “Ni kosa gani nimefanya, hata ukaamua kumkabidhi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu ili aniue?

10 Hakika kamaBwanaMungu wako aishivyo, hakuna taifa hata moja au ufalme ambapo bwana wangu hajamtuma mtu kukutafuta. Kila wakati taifa au ufalme walipodai kwamba haupo huko, aliwafanya waape kwamba hawakuweza kukupata.

11 Lakini sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kusema, ‘Eliya yuko hapa.’

12 Sijui ni wapi Roho waBwanaataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Kama nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua. Hata hivyo mimi mtumishi wako nimemwabuduBwanatangu ujana wangu.

13 Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini wakati Yezebeli alipokuwa akiua manabii waBwana? Niliwaficha manabii waBwanamia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, nami nikawapatia chakula na maji.

14 Nawe sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kumwambia, ‘Eliya yuko hapa.’ Yeye ataniua!”

15 Eliya akasema, “KamaBwanaMwenye Nguvu Zote aishivyo, yeye ninayemtumikia, hakika nitajionyesha kwa Ahabu leo.”

Eliya Juu Ya Mlima Karmeli

16 Basi Obadia akaenda kukutana na Ahabu na kumwambia, naye Ahabu akaenda kukutana na Eliya.

17 Alipomwona Eliya akamwambia, “Je, ni wewe, mtaabishaji wa Israeli?”

18 Eliya akamjibu, “Mimi sijaitaabisha Israeli. Lakini wewe na jamaa ya baba yako ndio mnaofanya hivyo. Mmeziacha amri zaBwanana mkafuata Mabaali.

19 Sasa waite watu kutoka Israeli yote tukutane nao juu ya Mlima Karmeli. Nawe uwalete hao manabii wa Baali mia nne na hamsini na hao manabii mia nne wa Ashera, walao chakula mezani mwa Yezebeli.”

20 Ndipo Ahabu akatuma ujumbe katika Israeli yote na kuwakusanya manabii hao juu ya mlima Karmeli.

21 Eliya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtasitasita katika mawazo mawili hadi lini? IkiwaBwanandiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.”

Lakini watu hawakusema kitu.

22 Kisha Eliya akawaambia, “Ni mimi peke yangu nabii waBwanaaliyebaki, lakini Baali ana manabii mia nne na hamsini.

23 Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na waweke juu ya kuni lakini wasiiwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni lakini sitawasha moto.

24 Kisha mliitie jina la mungu wenu, nami nitaliitia jina laBwanaMungu yule ambaye atajibu kwa moto, huyo ndiye Mungu.”

Kisha watu wote wakasema, “Hilo unalosema ni jema.”

25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na muwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.”

26 Kwa hiyo wakamchukua yule fahali waliyepewa, nao wakamwandaa.

Kisha wakaliitia jina la Baali kutoka asubuhi hadi adhuhuri, wakapiga kelele, “Ee Baali, utujibu!” Lakini hapakuwa na jibu; hakuna aliyejibu. Nao wakacheza kuizunguka madhabahu waliyoijenga.

27 Wakati wa adhuhuri, Eliya akaanza kuwadhihaki, akisema, “Pigeni kelele zaidi! Hakika yeye ni mungu! Labda amezama katika mawazo mazito, au ana shughuli nyingi, au amesafiri. Labda amelala usingizi mzito, naye ni lazima aamshwe.”

28 Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja wenyewe kwa visu na vyembe, mpaka damu ikachuruzika.

29 Adhuhuri ikapita, nao wakaendelea na utabiri wao wa kiwazimu mpaka wakati wa dhabihu ya jioni. Lakini hapakuwa na jibu, hakuna aliyejibu, hakuna aliyeangalia.

30 Kisha Eliya akawaambia watu wote, “Sogeeni karibu nami.” Watu wote wakamkaribia, naye akakarabati madhabahu yaBwana, ambayo ilikuwa imevunjwa.

31 Eliya akachukua mawe kumi na mawili, moja kwa ajili ya kila kabila la wana wa Yakobo, ambaye neno laBwanalilimjia, likisema, “Jina lako litakuwa Israeli.”

32 Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina laBwana, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu.

33 Akapanga kuni, akamkata yule fahali vipande vipande na kuvipanga juu ya kuni. Kisha akawaambia, “Jazeni mapipa manne maji na kuyamwaga juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni.”

34 Akawaambia, “Fanyeni hivyo tena.” Nao wakafanya hivyo tena.

Akaagiza, “Fanyeni kwa mara ya tatu.” Nao wakafanya hivyo kwa mara ya tatu.

35 Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki.

36 Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: “EeBwana, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.

37 Unijibu mimi, EeBwana, nijibu mimi, ili watu hawa wajue kwamba wewe, EeBwana, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena.”

38 Kisha moto waBwanaukashuka na kuiteketeza ile dhabihu, zile kuni, yale mawe, ule udongo, na pia kuramba yale maji yaliyokuwa ndani ya handaki.

39 Wakati watu wote walipoona hili, wakaanguka kifudifudi na kulia, “Bwana: yeye ndiye Mungu!Bwana: yeye ndiye Mungu!”

40 Kisha Eliya akawaamuru, “Wakamateni hao manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja atoroke!” Wakawakamata, naye Eliya akawaleta mpaka Bonde la Kishoni na kuwachinja huko.

41 Eliya akamwambia Ahabu, “Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa.”

42 Hivyo Ahabu akaondoka ili kula na kunywa. Lakini Eliya akapanda kileleni mwa Karmeli, akasujudu na akaweka kichwa chake katikati ya magoti yake.

43 Akamwambia mtumishi wake, “Nenda ukatazame kuelekea bahari.” Akaenda na kutazama.

Akasema, “Hakuna kitu cho chote huko.”

Mara saba Eliya akasema, “Nenda tena.”

44 Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, “Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini.”

Hivyo Eliya akasema, “Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ ”

45 Wakati ule ule anga likawa jeusi kwa mawingu, upepo ukainuka na mvua kubwa ikanyesha, naye Ahabu akaenda zake Yezreeli.

46 Nguvu zaBwanazikamjia Eliya, naye akajikaza viuno, akakimbia mbele ya Ahabu njia yote hadi maingilio ya Yezreeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/18-8ab90c083258fe05aca5ac0ca209a7c3.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 19

Eliya Akimbilia Horebu

1 Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Eliya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.

2 Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Hao miungu initendee hivyo na kuzidi, kama kufikia kesho wakati kama huu sitaifanya roho yako kama mmojawapo wa hao manabii.”

3 Eliya aliogopa, na akakimbia kuokoa maisha yake. Alipofika Beer-Sheba katika Yuda, akamwacha mtumishi wake huko,

4 lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa,Bwana, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.”

5 Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.

Mara malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka na ule.”

6 Akatazama pande zote, napo hapo karibu na kichwa chake palikuwepo mkate uliookwa kwenye makaa ya moto na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena.

7 Yule malaika waBwanaakaja tena mara ya pili, akamgusa akamwambia, “Inuka na ule, kwa kuwa safari ni ndefu kwako.”

8 Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini mchana na usiku mpaka akafika Horebu, mlima wa Mungu.

9 Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule.

Bwana Amtokea Eliya

Nalo neno laBwanalikamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Eliya?”

10 Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili yaBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wanaitafuta roho yangu waitoe pia.”

11 Bwanaakasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele zaBwana, kwa kuwaBwanayu karibu kupita hapo.”

Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele zaBwana, lakiniBwanahakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakiniBwanahakuwamo kwenye lile tetemeko.

12 Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakiniBwanahakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong’ona.

13 Eliya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mdomo wa pango.

Kisha ile sauti ikamwambia, “Eliya, unafanya nini hapa?”

14 Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili yaBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamekataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao wanaitafuta roho yangu waitoe.”

15 Bwanaakamwambia, “Rudi kwa njia uliyoijia, uende kwenye Jangwa la Dameski. Wakati utakapofika huko, mtie Hazaeli mafuta awe mfalme wa Aramu.

16 Pia mtie mafuta Yehu mwana wa Nimshi awe mfalme wa Israeli, na umtie Elisha mwana wa Shafati kutoka Abel-Mehola mafuta awe nabii badala yako.

17 Yehu atamwua ye yote atakayeutoroka upanga wa Hazaeli, naye Elisha atamwua ye yote atakayeutoroka upanga wa Yehu.

18 Hata sasa nimeweka akiba watu 7,000 katika Israeli, wote ambao hawajampigia Baali magoti, nao wote ambao midomo yao haijambusu.”

Wito Wa Elisha

19 Hivyo Eliya akaondoka kutoka huko na kumkuta Elisha mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliongoza ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akamrushia vazi lake.

20 Kisha Elisha akawaacha maksai wake, akamkimbilia Eliya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.”

Eliya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekutendea nini?.”

21 Basi Elisha akamwacha Eliya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Eliya, akamtumikia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/19-4f7b4d84c5c60d75b3908c03b0c643e4.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 20

Ben-Hadadi Aishambulia Samaria

1 Wakati huu, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote. Akifuatana na wafalme thelathini na wawili wakiwa na farasi na magari ya vita, akakwea kuuzingira kwa jeshi Samaria na kuishambulia.

2 Akawatuma wajumbe katika mji kwa Ahabu mfalme wa Israeli, kusema, “Hivi ndivyo asemavyo Ben-Hadadi:

3 ‘Fedha yako na dhahabu ni yangu, nao wake zako walio wazuri sana na watoto ni wangu.’ ”

4 Mfalme wa Israeli akajibu, “Iwe kama usemavyo, bwana wangu mfalme. Mimi na vyote nilivyo navyo ni mali yako.”

5 Wale wajumbe wakaja tena na kusema, “Hivi ndivyo asemavyo Ben-Hadadi: ‘Nimetuma kutaka fedha yako na dhahabu, wake zako na watoto wako.

6 Lakini kesho wakati kama huu, nitawatuma maafisa wangu kukagua jumba lako la kifalme na nyumba za maafisa wako. Watatwaa kitu unachokithamini nao watakichukua.’ ”

7 Mfalme wa Israeli akawaita wazee wote wa nchi na akawaambia, “Tazama jinsi mtu huyu anavyochokoza! Wakati alipotuma apelekewe wake zangu na watoto wangu, fedha zangu na dhahabu yangu, sikumkatalia.”

8 Wazee na watu wote wakajibu, “Usimsikilize, wala usiyakubali matakwa yake.”

9 Kwa hiyo akawajibu wajumbe wa Ben-Hadadi, “Mwambieni bwana wangu mfalme, ‘Mtumishi wako atafanya yote uliyoyadai mwanzoni, lakini dai hili la sasa siwezi kulitekeleza.’ ” Wakaondoka na kupeleka jibu kwa Ben-Hadadi.

10 Kisha Ben-Hadadi akatuma ujumbe mwingine kwa Ahabu, kusema “Miungu iniletee maafa, tena makubwa zaidi, ikiwa vumbi la Samaria litatosheleza konzi moja ya kila mtu ya wale wafuatanao nami.”

11 Mfalme wa Israeli akajibu, “Mwambieni, ‘Yule anayevaa mavazi ya vita asije akajisifu kama yule anayevua.’ ”

12 Ben-Hadadi alisikia ujumbe huu wakati ambapo yeye na wafalme walikuwa wanakunywa katika mahema yao, na akawaamuru watu wake, “Jiandaeni kushambulia.” Kwa hiyo wakajiandaa kuushambulia mji.

Ahabu Amshinda Ben-Hadadi

13 Wakati ule ule nabii akamjia Ahabu mfalme wa Israeli na kutangaza, “Hivi ndivyo asemavyoBwana: ‘Je, unaona jeshi hili kubwa? Nitalitia mkononi mwako leo, nawe ndipo utajua kwamba mimi ndimiBwana.’ ”

14 Ahabu akauliza, “Ni nani atakayefanya hili?”

Nabii akamjibu, “Hivi ndivyo asemavyoBwana: ‘Maafisa vijana majemadari wa majimbo watafanya hili.’ ”

Akauliza, “Ni nani atakayeanzisha vita?”

Nabii akamjibu, “Ni wewe.”

15 Kwa hiyo Ahabu akawaita maafisa vijana majemadari wa majimbo, wanaume 232. Kisha akawakusanya Waisraeli wote waliobaki, jumla yao 7,000.

16 Wakaondoka wakati wa adhuhuri, Ben-Hadadi na wale wafalme thelathini na wawili walioungana naye walipokuwa katika mahema yao wakilewa.

17 Maafisa vijana majemadari wa majimbo waliondoka kwanza.

Wakati huu Ben-Hadadi alikuwa amewatuma wapelelezi, ambao walileta taarifa kusema kwamba, “Askari wanasonga mbele kutoka Samaria.”

18 Akasema, “Ikiwa wamekuja kwa amani, wakamate wakiwa hai; ikiwa wamekuja kwa vita, wakamate wakiwa hai.”

19 Wale maafisa vijana majemadari wa majimbo wakatoka nje ya mji jeshi likiwa nyuma yao,

20 kila mmoja akamwua adui yake. Hii ilisababisha Waaramu kukimbia, huku Waisraeli wakiwafuatia. Lakini Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akatoroka akiwa amepanda farasi wake pamoja na baadhi ya wapanda farasi wake.

21 Mfalme wa Israeli akasonga mbele na kushinda farasi na magari ya vita na kusababisha hasara kubwa kwa Waaramu.

22 Baadaye nabii akaja kwa mfalme wa Israeli na kusema, “Jiandae vizuri ufikirie la kufanya, kwa sababu mwakani mfalme wa Aramu atakuja kukushambulia tena.”

23 Wakati ule ule, maafisa wa mfalme wa Aramu wakamshauri, wakamwambia, “Miungu yao ni miungu ya vilimani. Ndiyo sababu walikuwa na nguvu sana kutuzidi. Lakini kama tukipigana nao katika nchi tambarare, hakika tutawashinda.

24 Fanya hivi: Waondoe hao wafalme wote thelathini na wawili kutoka nafasi zao na uweke maafisa wengine mahali pao.

25 Ni lazima pia uandae jeshi jingine kama lile ulilopoteza, farasi kwa farasi, gari la vita kwa gari la vita, ili tuweze kupigana na Israeli katika nchi tambarare. Kisha kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko wao.” Akakubaliana nao naye akashughulika ipasavyo.

26 Mwaka uliofuata, majira kama hayo, Ben-Hadadi akawakusanya Waaramu mpaka Afeki kupigana dhidi ya Israeli.

27 Baada ya Waisraeli kukusanywa na kupewa mahitaji, walikwenda kukabiliana nao. Waisraeli wakapiga kambi mkabala nao kama makundi mawili madogo ya mbuzi, wakati Waaramu walienea katika nchi yote.

28 Mtu wa Mungu akaja na kumwambia mfalme wa Israeli, “Hivi ndivyoBwanaasemavyo: ‘Kwa sababu Waaramu wanafikiriBwanani Mungu wa vilimani na sio Mungu wa mabondeni, nitatia jeshi hili kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ndimiBwana.’ ”

29 Kwa siku saba walipiga kambi wakitazamana na siku ya saba vita vikaanza. Waisraeli wakawajeruhi askari wa miguu wa Waaramu 100,000 kwa siku moja.

30 Waliobaki wakatorokea katika mji wa Afeki, mahali ambapo watu 27,000 waliangukiwa na ukuta. Naye Ben-Hadadi akakimbilia mjini na kujificha kwenye chumba cha ndani.

31 Maafisa wake wakamwambia, “Tazama, tumesikia kwamba wafalme wa nyumba ya Israeli wana huruma. Twendeni kwa mfalme wa Israeli tukiwa tumevaa nguo za gunia viunoni mwetu na kamba kuzunguka vichwa vyetu. Huenda akakuacha hai.”

32 Wakiwa wamevaa nguo za gunia viunoni mwao na kamba kuzunguka vichwa vyao, walikwenda kwa mfalme wa Israeli na kusema, “Mtumishi wako Ben-Hadadi anasema: ‘Tafadhali, naomba uniache hai.’ ”

Mfalme akajibu, “Je, bado yuko hai? Yeye ni ndugu yangu.”

33 Wale watu wakalipokea jambo lile kama dalili nzuri nao wakawa wepesi kulichukua neno lake wakisema, “Ndiyo, yeye ni ndugu yako Ben-Hadadi!”

Mfalme akawaambia, “Nendeni mkamlete.” Ikawa Ben-Hadadi alipokuja, Ahabu akampandisha katika gari lake la vita.

Ben-Hadadi akajitolea, akisema,

34 “Nitairudisha ile miji ambayo baba yangu aliiteka kutoka kwa baba yako. Unaweza kuweka maeneo yako ya soko katika Dameski, kama baba yangu alivyofanya huko Samaria.”

Ahabu akasema, “Katika misingi ya mkataba, nitakuachilia huru.” Kwa hiyo akaweka mkataba naye, akamruhusu aende zake.

Nabii Amlaumu Ahabu

35 Kwa neno laBwana, mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake, “Nipige kwa silaha yako,” lakini yule mtu akakataa.

36 Kwa hiyo yule nabii akasema, “Kwa sababu hukumtiiBwana, mara tu tutakapoachana utauawa na simba.” Na baada ya yule mtu kuondoka, simba akatokea na kumwua.

37 Nabii akamkuta mtu mwingine na kumwambia, “Nipige tafadhali.” Kisha yule mtu akampiga na kumjeruhi.

38 Ndipo nabii akaenda na kusimama barabarani akimsubiri mfalme. Akajibadilisha kwa kushusha kitambaa cha kichwani mwake hadi kwenye macho.

39 Mfalme alipopita pale, yule nabii akamwita, “Mtumishi wako alikwenda vitani wakati vita vilipopamba moto, mtu mmoja akanijia na mateka akasema, ‘Mlinde mtu huyu. Kama akitoroka itakuwa uhai wako kwa uhai wake, ama vipande 3,000 vya fedha.’

40 Wakati mtumishi wako alipokuwa na shughuli nyingi hapa na pale, yule mtu akatoweka.”

Mfalme wa Israeli akasema, “Hiyo ndiyo hukumu yako. Wewe umeitaja mwenyewe.”

41 Kisha yule nabii akajifunua macho yake haraka, na mfalme wa Israeli akamtambua kama mmoja wa manabii.

42 Akamwambia mfalme, “Hivi ndivyoBwanaasemavyo: ‘Umemwacha huru mtu niliyekusudia afe. Kwa hiyo ni uhai wako kwa uhai wake, watu wako kwa watu wake.’ ”

43 Kwa uchungu na hasira, mfalme wa Israeli akaenda kwenye jumba lake la kifalme huko Samaria.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/20-3053e0ad4a24967098ad8bc5803370f7.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 21

Shamba La Mizabibu La Nabothi

1 Baada ya hayo, Nabothi, Myezreeli, alikuwa na shamba la mizabibu jirani na jumba la kifalme la Ahabu mfalme wa Samaria.

2 Ahabu akamwambia Nabothi, “Unipatie shamba lako la mizabibu nilitumie kwa bustani ya mboga, kwa kuwa liko karibu na jumba langu la kifalme. Badala yake, nitakupa shamba jingine la mizabibu zuri zaidi au, kama utapenda, nitakulipa kiasi cho chote unachoona ni thamani yake.”

3 Lakini Nabothi akajibu, “Bwanana apitishie mbali kukupa wewe urithi wa baba zangu.”

4 Basi Ahabu akaenda nyumbani, mwenye huzuni na hasira kwa sababu ya yale ambayo Nabothi, Myezreeli, alikuwa amesema, “Sitakupa urithi wa baba zangu.” Akajinyoosha juu ya kitanda akisononeka, na akakataa kula.

5 Yezebeli mke wake akaingia na akamwuliza, “Kwa nini unahuzunika hivi? Kwa nini huli chakula?”

6 Akamjibu, “Kwa sababu nilimwambia Nabothi, Myezreeli, ‘Niuzie shamba lako la mizabibu, au kama ukipenda, nitakupa shamba jingine la mizabibu badala yake.’ Lakini akasema, ‘Sitakupa shamba langu la mizabibu.’ ”

7 Yezebeli mke wake akasema, “Hivi ndivyo unavyofanya, nawe ni mfalme katika Israeli yote? Inuka na ule! Changamka. Nitakupatia shamba la mizabibu la Nabothi, Myezreeli.”

8 Kwa hiyo akaandika barua kwa jina la Ahabu akaweka muhuri wake juu ya hizo barua, akazipeleka kwa wazee na kwa watu wenye cheo walioishi katika mji pamoja na Nabothi.

9 Katika barua hizo aliandika:

“Tangazeni siku ya watu kufunga na mumketishe Nabothi mahali pa wazi miongoni mwa watu.

10 Lakini ketisheni watu wawili wabaya kabisa mkabala naye, nao washuhudie kuwa yeye amemlaani Mungu na mfalme. Kisha mtoeni nje na kumpiga kwa mawe hadi afe.”

11 Hivyo wazee na watu wenye cheo walioishi katika mji wa Nabothi wakafanya kama Yezebeli alivyoelekeza katika barua aliyowaandikia.

12 Wakatangaza mfungo na kumketisha Nabothi mahali pa wazi miongoni mwa watu.

13 Kisha watu wawili wabaya kabisa wakaja wakaketi mkabala naye, nao wakaleta mashtaka dhidi ya Nabothi mbele ya watu, wakisema, “Nabothi amemlaani Mungu na mfalme.” Kwa hiyo wakamtoa nje na kumpiga kwa mawe hadi akafa.

14 Kisha wakatuma ujumbe kwa Yezebeli, kusema, “Nabothi amepigwa mawe na amekufa.”

15 Mara tu Yezebeli aliposikia kwamba Nabothi amepigwa mawe na amekufa, akamwambia Ahabu, “Amka na uchukue lile shamba la mizabibu la Nabothi, Myezreeli, ambalo alikataa kukuuzia. Hayuko hai tena, bali amekufa.”

16 Ahabu aliposikia Nabothi amekufa, akainuka na kushuka ili kulichukua shamba la mizabibu la Nabothi.

17 Kisha neno laBwanalikamjia Eliya, Mtishbi:

18 “Shuka ukakutane na Ahabu mfalme wa Israeli, anayetawala Samaria. Sasa yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ambapo amekwenda alimiliki.

19 Umwambie, ‘Hivi ndivyoBwanaasemavyo: Je, hujamwua mtu na kuitwaa mali yake?’ Kisha umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyoBwana: Mahali ambapo mbwa walilamba damu ya Nabothi, mbwa watailamba damu yako, naam, yako wewe!’ ”

20 Ahabu akamwambia Eliya, “Kwa hiyo umenipata, wewe adui yangu!”

Akajibu, “Ndiyo, nimekupata. Kwa sababu umejiuza mwenyewe kufanya uovu mbele ya macho yaBwana.

21 ‘Nitaleta maafa juu yako. Nitaangamiza uzao wako na kukatilia mbali kutoka kwa Ahabu kila mzaliwa wa mwisho wa kiume katika Israeli, wa mtumwa au wa mtu huru.

22 Nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwana wa Nebati na ile ya Baasha mwana wa Ahia, kwa sababu umenighadhibisha kwa kuwa umesababisha Israeli kutenda dhambi.’

23 “Pia kwa habari ya YezebeliBwanaanasema, ‘Mbwa watamla Yezebeli karibu na ukuta wa Yezreeli.’

24 “Mbwa watawala wale wa nyumba ya Ahabu watakaofia mjini, nao wale watakaofia mashambani wataliwa na ndege wa angani.”

25 (Hapajapata kamwe kuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza mwenyewe kutenda uovu machoni mwaBwana, akiwa anachochewa na Yezebeli mkewe.

26 Alitenda kwa uovu sana katika kuabudu sanamu, kama wale Waamori ambaoBwanaaliowafukuza mbele ya Israeli.)

27 Ahabu aliposikia maneno haya, akararua nguo zake, akavaa nguo za gunia na kufunga. Akalala na kujifunika nguo za gunia na kwenda kwa unyenyekevu.

28 Ndipo neno laBwanalilipomjia Eliya Mtishbi kusema,

29 “Umeona jinsi Ahabu alivyojinyenyekeza mbele zangu? Kwa kuwa amejishusha mwenyewe, sitaleta maafa haya wakati akiwa hai, lakini nitayaleta juu ya nyumba yake katika siku za mwanawe.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/21-f9959196a38fb35c665b433f11f02ff6.mp3?version_id=1627—

1 Wafalme 22

Mikaya Anatabiri Dhidi Ya Ahabu

1 Kwa miaka mitatu hapakuwa na vita kati ya Aramu na Israeli.

2 Lakini katika mwaka wa tatu Yehoshafati mfalme wa Yuda akashuka kwenda kumwona mfalme wa Israeli.

3 Mfalme wa Israeli alikuwa amewaambia maafisa wake, “Je, hamjui Ramoth-Gileadi ni mali yetu na bado hatufanyi cho chote kuirudisha kwetu kutoka kwa mfalme wa Aramu?”

4 Kwa hiyo akamwuliza Yehoshafati, “Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Ramoth-Gileadi?”

Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”

5 Lakini Yehoshafati pia akamwambia mfalme wa Israeli, “Kwanza tafuta shauri laBwana.”

6 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii wanaume wapatao mia nne, akawauliza, “Je, niende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?”

Wakajibu, “Naam, nenda, kwa kuwa Bwana ataiweka Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.”

7 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii waBwanahapa ambaye tunaweza kumwulizia?”

8 Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumwuliza shauri laBwana, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lo lote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.”

Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”

9 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwita mmoja wa maafisa wake na kusema, “Mlete Mikaya mwana wa Imla mara moja.”

10 Wakiwa wamevalia majoho yao ya kifalme, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi juu ya viti vyao vya kifalme katika sakafu ya kupuria, kwenye ingilio la lango la Samaria, pamoja na manabii wote wakiwa wakitabiri mbele yao.

11 Wakati huu Zedekia mwana wa Kenaana alikuwa ametengeneza pembe za chuma na akatangaza, “Hivi ndivyoBwanaasemavyo, ‘Kwa hizi pembe utawapiga na kuwarudisha Waaramu nyuma mpaka wameangamizwa.’ ”

12 Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwaBwanaataiweka mkononi mwa mfalme.”

13 Mjumbe aliyekuwa amekwenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.”

14 Lakini Mikaya akasema, “Hakika kamaBwanaaishivyo, nitamwambia kile tuBwanaatakachoniambia.”

15 Alipofika, mfalme akamwuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?”

Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwaBwanaataiweka mkononi mwa mfalme.”

16 Mfalme akamwambia, “Je, ni mara ngapi nitakuapisha ili usiniambie kitu cho chote ila kweli tu kwa jina laBwana?”

17 Kisha Mikaya akajibu, “Niliona Israeli yote imetawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naBwanaakasema, ‘Watu hawa hawana bwana. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ”

18 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lo lote jema kunihusu, bali mabaya tu?”

19 Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno laBwana: NilimwonaBwanaameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni wamesimama kumzunguka kulia kwake na kushoto kwake.

20 NayeBwanaakasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’

“Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile.

21 Mwishoni, pepo mchafu akajitokeza, akasimama mbele zaBwanana kusema, ‘Nitamshawishi.’

22 “Bwanaakauliza, ‘Kwa njia gani?’

“Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’

“Bwanaakasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’

23 “Kwa hiyo sasaBwanaameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote.Bwanaameamuru maafa kwa ajili yako.”

24 Kisha Zedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwaBwanaalipita njia gani, alipotoka kwangu ili kusema nawe?”

25 Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapokwenda kujificha kwenye chumba cha ndani.”

26 Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni na mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme.

27 Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe cho chote ila mkate na maji mpaka nitakaporudi salama.’ ”

28 Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basiBwanahajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!”

Ahabu Anauawa Huko Ramoth-Gileadi

29 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakaenda Ramoth-Gileadi.

30 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitaingia vitani nikiwa nimejibadilisha, lakini wewe uvae majoho yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na kwenda vitani.

31 Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na ye yote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.”

32 Wakati wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati alipiga kelele,

33 wale majemadari wakaona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli, nao wakaacha kumfuatilia.

34 Lakini mtu fulani akavuta upindi pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma. Mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.”

35 Vita vikaendelea mchana kutwa, naye Mfalme Ahabu akategemezwa ndani ya gari kuelekea Waaramu. Damu kutoka kwenye jeraha lake ikachuruzika ndani ya gari na jioni yake akafa.

36 Jua lilipokuwa linazama, mbiu ikaenea katika jeshi lote: “Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake!”

37 Basi mfalme akafa na akaletwa Samaria, nao wakamzika huko.

38 Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakalamba damu yake, sawasawa na neno laBwanalilivyokuwa limesema.

39 Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahabu, pamoja na yote aliyoyafanya, jumba la kifalme alilojenga na kunakishiwa kwa pembe za ndovu, nayo miji aliyoijengea maboma, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

40 Ahabu akalala pamoja na baba zake. Naye Ahazia mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Yehoshafati Mfalme Wa Yuda

41 Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme wa Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli.

42 Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka ishirini na mitano. Jina la mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi.

43 Katika kila jambo alienenda katika njia za Asa baba yake wala hakwenda kinyume chake, akafanya yaliyo mema machoni paBwana. Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia palikuwa hapakuondolewa na watu waliendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba huko.

44 Yehoshafati pia alikuwa na amani na mfalme wa Israeli.

45 Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, mafanikio aliyokuwa nayo na uhodari wake katika vita, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?

46 Aliondolea mbali katika nchi mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu waliobaki huko hata baada ya utawala wa baba yake Asa.

47 Tangu hapo hapakuwepo na mfalme katika Edomu, naibu ndiye aliyetawala.

48 Wakati huu Yehoshafati akaunda merikebu nyingi za biasharaili kwenda Ofiri kuchukua dhahabu, lakini kamwe hazikusafiri, kwa maana zilivunjika huko Ezion-Geberi.

49 Wakati ule, Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Waache watu wangu wasafiri baharini pamoja na watu wako,” lakini Yehoshafati akakataa.

50 Kisha Yehoshafati akalala na baba zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Naye Yehoramu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Ahazia Mfalme Wa Israeli

51 Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye alitawala katika Israeli kwa miaka miwili.

52 Akafanya maovu machoni mwaBwanakwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi.

53 Alimtumikia na kumwabudu Baali na kumghadhibishaBwana, Mungu wa Israeli, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/22-3851d230159079ac1b2ab098a23a7123.mp3?version_id=1627—

2 Samweli 1

Daudi Afahamishwa Kifo Cha Sauli

1 Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alipokuwa amerudi kutoka kuwashinda Waamaleki, Daudi alikaa siku mbili huko Siklagi.

2 Siku ya tatu akaja mtu mwenye nguo zilizoraruka na mavumbi kichwani mwake kutoka kwenye kambi ya Sauli. Alipomjia Daudi, akajitupa chini ili kumpa heshima.

3 Daudi akamwuliza, “Wewe umetoka wapi?”

Akamjibu, “Nimetoroka kutoka katika kambi ya Waisraeli.”

4 Daudi akamwuliza, “Ni nini kilichotokea? Niambie.”

Akasema, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wao walianguka na kufa. Naye Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa.”

5 Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana mwanaume aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?”

6 Yule kijana mwanaume akasema, “Ilitokea nikawa juu ya Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwako huko akiwa ameegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana.

7 Alipogeuka na kuniona, akaniita, nami nikasema, ‘Je, nifanye nini?’

8 “Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’

“Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki.’

9 “Kisha akaniambia, ‘Nikaribie mimi na uniue! Niko katika maumivu makali ya kifo, lakini bado ningali hai.’

10 “Kwa hiyo nikamkaribia nikamwua, kwa sababu nilijua kwamba baada ya kuanguka hangeweza kupona. Nami nikachukua lile taji lililokuwa kichwani mwake na utepe uliokuwa mkononi mwake nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.”

11 Ndipo Daudi pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye wakazishika nguo zao na kuzirarua.

12 Wakaomboleza, wakalia pia na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli na Yonathani mwanawe, kwa ajili ya jeshi laBwanana nyumba ya Israeli, kwa sababu wameanguka kwa upanga.

13 Daudi akamwambia yule mwanaume kijana aliyemletea taarifa, “Wewe ni mwenyeji wa wapi?”

Akamjibu, “Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.”

14 Daudi akamwuliza, “Kwa nini hukuogopa kuinua mkono wako ili kumwangamiza mpakwa mafuta waBwana?”

15 Kisha Daudi akamwita mmoja wa watu wake na kumwambia, “Nenda ukamwue!” Kwa hiyo akampiga, naye akafa.

16 Kwa maana Daudi alikuwa amemwambia, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako mwenyewe. Kinywa chako mwenyewe kimeshuhudia dhidi yako uliposema, ‘Nilimwua mpakwa mafuta waBwana.’ ”

Ombolezo La Daudi Kwa Ajili Ya Sauli Na Yonathani

17 Daudi akafanya maombolezo haya kuhusu Sauli na Yonathani mwanawe,

18 naye akaagiza kwamba watu wa Yuda wafundishwe ombolezo hili la upindi (ambalo limeandikwa katika Kitabu cha Yashari):

19 “Walio fahari yako, Ee Israeli, wameuawa juu ya mahali pako palipoinuka.

Jinsi wenye nguvu walivyoanguka!

20 “Msilisimulie hili katika Gathi,

msilitangaze hili katika

barabara za Ashkeloni,

binti za Wafilisti wasije wakafurahia,

binti za hao wasiotahiriwa

wasije wakashangilia.

21 “Enyi milima ya Gilboa,

msipate umande wala mvua,

wala mashamba yazaayo sadaka ya nafaka.

Kwa maana huko ndiko ngao ya mwenye nguvu iliponajisiwa,

ngao ya Sauli haitapakwa tena mafuta.

22 Kutokana na damu ya waliouawa,

kutokana na miili ya wenye nguvu,

ule upindi wa Yonathani haukugeuka nyuma.

Upanga wa Sauli haukurudi bure.

23 “Sauli na Yonathani,

maishani walipendwa na kuneemeka,

na katika kifo hawakutengana.

Walikuwa wepesi kuliko tai,

walikuwa na nguvu kuliko simba.

24 “Enyi binti za Israeli,

lieni kwa ajili ya Sauli,

ambaye aliwavika nguo

nyekundu na maridadi,

ambaye aliremba mavazi yenu

kwa mapambo ya dhahabu.

25 “Tazama jinsi mashujaa

walivyoanguka vitani!

Yonathani ameuawa

mahali pako palipoinuka.

26 Nahuzunika kwa ajili yako,

Yonathani ndugu yangu,

kwangu ulikuwa mpendwa sana.

Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,

wa ajabu zaidi kuliko ule wa wanawake.

27 “Tazama jinsi mashujaa walivyoanguka!

Silaha za vita zimeangamia!”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2SA/1-38adc8e82f3885fc096407d8cee04f58.mp3?version_id=1627—

2 Samweli 2

Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Yuda

1 Ikawa baada ya mambo haya, Daudi akamwulizaBwana, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?”

Bwanaakasema, “Panda.”

Daudi akauliza, “Je, niende wapi?”

Bwanaakajibu, “Nenda Hebroni.”

2 Basi Daudi akakwea kwenda huko pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli.

3 Pia Daudi akawachukua watu waliokuwa pamoja naye, kila mmoja na jamaa yake, nao wakaishi huko Hebroni na miji yake.

4 Ndipo watu wa Yuda wakaja Hebroni, huko wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda.

Daudi alipoambiwa kuwa ni watu wa Yabeshi-Gileadi waliomzika Sauli,

5 akatuma wajumbe kwa watu wa Yabeshi-Gileadi kuwaambia, “Bwanaawabariki kwa kuonyesha wema huu kwa kumzika Sauli bwana wenu.

6 SasaBwanana awaonyeshe wema na uaminifu, nami pia nitawaonyesha wema ule ule kwa kuwa mmefanya jambo hili.

7 Sasa basi, iweni hodari na mashujaa, kwa maana bwana wenu Sauli amekufa, nayo nyumba ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme juu yao.”

Vita Kati Ya Nyumba Ya Daudi Na Sauli

8 Wakati huo Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Sauli, alikuwa amemchukua Ish-Boshethi mwana wa Sauli na kumleta hadi Mahanaimu.

9 Akamweka awe mfalme juu ya nchi ya Gileadi, Ashuri, Yezreeli, Efraimu, Benyamini na Israeli yote.

10 Ish-Boshethimwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi.

11 Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ilikuwa miaka saba na miezi sita.

12 Abneri mwana wa Neri, pamoja na watu wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli, wakatoka Mahanaimu kwenda Gibeoni.

13 Yaobu mwana wa Seruya na watu wa Daudi wakatoka na kukutana nao kwenye bwawa la Gideoni. Kikundi kimoja kiliketi upande mmoja wa bwawa na kikundi kingine upande wa pili.

14 Ndipo Abneri akamwambia Yoabu, “Tuwaweke baadhi ya vijana wasimame na wapigane ana kwa ana mbele yetu.”

Yoabu akasema, “Sawa, na wafanye hivyo.”

15 Kwa hiyo vijana wakasimama, wakahesabiwa: watu wa Benyamini na wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli kumi na wawili, na upande wa Daudi kumi na wawili.

16 Kisha kila mtu akakamatana na mpinzani wake kichwani na kuchomana kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.

17 Siku hiyo vita vilikuwa vikali sana, naye Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watu wa Daudi.

18 Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa.

19 Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata.

20 Abneri akaangalia nyuma na kumwuliza, “Ni wewe, Asaheli?”

Akamjibu, “Ndiyo.”

21 Ndipo Abneri akamwambia, “Geuka upande wa kulia au kushoto. Mchukue mmoja wa vijana wa kiume na umvue silaha zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfukuza.

22 Abneri akamwonya tena Asaheli akimwambia, “Acha kunifukuza! Kwa nini nikuue? Je, nitawezaje kumtazama ndugu yako Yoabu usoni?”

23 Lakini Asaheli alikataa kuacha kumfuatia, kwa hiyo Abneri akamchoma Asaheli tumboni kwa ncha butu ya mkuki wake, mkuki ukamtoboa ukatokea mgongoni mwake. Akaanguka na kufa papo hapo. Ikawa kila mtu alisimama alipofika mahali pale Asaheli alipoanguka na kufa.

24 Lakini Yoabu na Abishai walimfuata Abneri, na jua lilipokuwa linatua, wakafika kwenye kilima cha Ama, karibu na Gia kwenye njia ya kuelekea kwenye nyika ya Gibeoni.

25 Ndipo watu wa kabila la Benyamini wakakusanyika tena nyuma ya Abneri. Wakaunda kikosi na kujiimarisha juu ya kilima.

26 Abneri akamwita Yoabu, akamwambia, “Je, ni lazima upanga uendelee kuangamiza milele? Hutambui kwamba jambo hili litaishia katika uchungu? Utaacha kuwaagiza watu wako waache kuwafuatilia ndugu zao hata lini?”

27 Yoabu akajibu, “Hakika kama aishivyo Mungu, kama hukusema, hawa watu wangeendelea kuwafuatia ndugu zao mpaka asubuhi.”

28 Basi Yoabu akapiga tarumbeta, nao watu wote wakasimama, hawakuwafuata Israeli tena, wala hawakuwapiga tena.

29 Usiku ule wote Abneri na watu wake wakatembea kupitia Araba. Wakavuka Mto Yordani, wakaendelea wakipitia nchi yote ya Bithroni wakafika Mahanaimu.

30 Basi Yoabu akarudi kutoka kumfuatia Abneri, na kuwakusanya watu wake wote. Pamoja na Asaheli, watu kumi na tisa wa Daudi walikuwa wamepotea.

31 Lakini watu wa Daudi walikuwa wamewaua watu wa kabila la Benyamini 360 waliokuwa pamoja na Abneri.

32 Wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake huko Bethlehemu. Kisha Yaobu na watu wake wakatembea usiku kucha na kufika huko Hebroni wakati wa mapambazuko.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2SA/2-3c23f89d43c2a6f812f792aed3940788.mp3?version_id=1627—