Waamuzi 4

Debora

1 Baada ya Ehudi kufa, Waisraeli wakafanya tena maovu machoni paBwana.

2 HivyoBwanaakawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Jemadari wa jeshi lake alikuwa Sisera, aliyeishi huko Haroshethi-Hagoyimu.

3 Kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma yapatayo 900, naye alikuwa amewatesa Waisraeli kwa ukatili kwa muda wa miaka ishirini, Waisraeli wakamliliaBwanawakaomba msaada.

4 Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa anaamua Israeli wakati ule.

5 Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue.

6 Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, “Bwana, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume 10,000 toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori.

7 Nitamshawishi Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, pamoja na magari yake na jeshi lake, hadi Mto Kishoni na kumtia mikononi mwako.’ ”

8 Baraka akamwambia, “Ukienda pamoja nami nitakwenda, lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.”

9 Debora akamwambia, “Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini njia unayoiendea haitakupa heshima wewe, kwa kuwaBwanaatamtia Sisera mikononi mwa mwanamke.” Hivyo Debora akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi,

10 mahali ambapo Baraka aliwaita Zabuloni na Naftali. Watu 10,000 wakamfuata Baraka, naye Debora pia akaenda pamoja naye.

11 Basi Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni wengine, yaani, wazao wa Hobabu, mkwewe Mose, naye akapiga hema lake karibu na ule mti mkubwa wa mwaloni ulioko Saananimu, karibu na Kedeshi.

12 Sisera alipoambiwa kuwa Baraka mwana wa Abinoamu alikuwa amepanda Mlima Tabori,

13 Sisera akakusanya pamoja magari yake yote 600 ya chuma na watu wote waliokuwa pamoja naye, kuanzia Haroshethi-Hagoyimu mpaka Mto wa Kishoni.

14 Ndipo Debora akamwambia Baraka, “Nenda! Hii ndiyo siku ambayoBwanaamemtia Sisera mikononi mwako. Je,Bwanahakukutangulia mbele yako?” Hivyo Baraka akashuka kutoka Mlima Tabori, akifuatwa na watu 10,000.

15 Bwanaakamfadhaisha Sisera na magari yake yote, pamoja na jeshi lake lote kwa upanga mbele ya Baraka, naye Sisera akaliacha gari lake na kukimbia kwa miguu.

16 Lakini Baraka akafuatia magari pamoja na jeshi mpaka Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia.

17 Sisera, hata hivyo, akakimbia kwa miguu mpaka kwenye hema la Yaeli, mkewe Heberi, Mkeni, kwa sababu palikuwa na uhusiano wa kirafiki kati ya Yabini mfalme wa Hazori na ukoo wa Heberi, Mkeni.

18 Yaeli akaenda kumlaki Sisera na kumwambia, “Karibu, bwana wangu, karibu ingia ndani kabisa. Usiogope.” Basi Sisera akaingia ndani ya hema ya Yaeli, naye akamfunika kwa blanketi nene.

19 Akamwambia, “Nina kiu, tafadhali nipe maji ya kunywa.” Ndipo akafungua kiriba cha maziwa na kumpa akanywa, kisha akamfunika.

20 Naye Sisera akamwambia, “Simama mlangoni pa hema na mtu ye yote akija na kukuuliza, ‘Je, kuna mtu ye yote hapa?’ sema, ‘Hapana.’ ”

21 Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi, akiwa amechoka. Akakigongomea kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa.

22 Baraka akakaribia akimfuatia Sisera, Yaeli akatoka kumlaki. Akamwambia, “Njoo, nitakuonyesha mtu unayemtafuta.” Hivyo wakaingia ndani ya hema wakiwa wamefuatana na tazama Sisera alikuwa amelala humo, akiwa amekufa, na hicho kigingi cha hema kikiwa kimegongomewa kupitia paji la uso wake.

23 Basi siku ile Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani, mbele ya Israeli.

24 Nao mkono wa Waisraeli ukaendelea kuwa na nguvu zaidi na zaidi dhidi ya Yabini, mfalme wa Kanaani, mpaka wakamwangamiza.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/4-907911f3bebd3a265a18811b90486689.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 5

Wimbo Wa Debora

1 Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:

2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza,

wakati watu wanapojitoa

kwa hiari yao wenyewe:

mhimidiniBwana!

3 “Sikieni hili, enyi wafalme!

Sikilizeni, enyi watawala!

NitamwimbiaBwana, nitaimba;

kwa wimbo nitamhimidiBwana,

Mungu wa Israeli.

4 “EeBwana, ulipotoka katika Seiri,

ulipopita katika mashamba ya Edomu,

nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga,

naam, mawingu yakamwaga maji.

5 Milima ilitetemeka mbele zaBwana,

hata ule wa Sinai,

mbele zaBwana,

Mungu wa Israeli.

6 “Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi,

katika siku za Yaeli,

barabara kuu hazikuwa na watu;

wasafiri walipita njia za kando.

7 Mashujaa walikoma katika Israeli,

walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka,

nilipoinuka kama mama katika Israeli.

8 Walipochagua miungu migeni,

vita vilikuja katika malango ya mji,

hapakuonekana ngao wala mkuki

miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.

9 Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli,

pamoja na wale wanaojitoa wenyewe

kwa hiari yao miongoni mwa watu.

MhimidiniBwana!

10 “Nanyi mpandao punda weupe,

mkiketi juu ya matandiko ya thamani,

nanyi mtembeao barabarani,

fikirini

11 juu ya sauti za waimbaji

mahali pa kunyweshea maji.

Wanasimulia matendo ya haki yaBwana,

matendo ya haki ya mashujaa wake

katika Israeli.

“Ndipo watu waBwana

walipotelemka malangoni pa mji.

12 ‘Amka, amka! Debora!

Amka, amka, uimbe!

Ee Baraka! Inuka,

chukua mateka wako uliowateka,

Ee mwana wa Abinoamu.’

13 “Ndipo mabaki ya watu

wakashuka dhidi ya wenye nguvu,

watu waBwana,

wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.

14 Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki;

Benyamini akiwa miongoni

mwa watu waliokufuata.

Kutoka Makiri wakashuka viongozi,

na kutoka Zabuloni wale washikao

fimbo ya jemadari.

15 Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora;

naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka,

wakija nyuma yake kwa mbio

wakielekea bondeni.

Katika jamaa za Reubeni,

palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.

16 Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo

kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi?

Katika jamaa za Reubeni,

palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.

17 Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani.

Naye Dani, kwa nini alikaa

kwenye merikebu siku nyingi?

Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari,

akikaa kwenye ghuba zake ndogo.

18 Watu wa Zabuloni walihatirisha maisha yao,

vile vile nao watu wa Naftali.

19 “Wafalme walikuja na kufanya vita;

wafalme wa Kanaani walipigana

huko Taanaki karibu na maji ya Megido,

lakini hawakuchukua fedha wala nyara.

20 Kutoka mbinguni nyota zilipigana,

nyota kutoka katika njia zake

zilipigana na Sisera.

21 Mto wa Kishoni uliwasomba,

ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.

Songa mbele, Ee nafsi yangu,

kwa ujasiri!

22 Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo:

farasi wake wenye nguvu

huenda mbio kwa kurukaruka.

23 Malaika waBwanaakasema, ‘Merozi alaaniwe.

Walaaniwe watu wake kwa uchungu,

kwa kuwa hawakuja kumsaidiaBwana,

kumsaidiaBwanadhidi ya hao wenye nguvu.’

24 “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote,

mkewe Heberi, Mkeni,

abarikiwe kuliko wanawake wote

waishio kwenye mahema.

25 Aliomba maji, naye akampa maziwa;

kwenye bakuli la heshima

akamletea maziwa mgando.

26 Akanyoosha mkono wake

akashika kigingi cha hema,

mkono wake wa kuume

ukashika nyundo ya fundi.

Akampiga Sisera kwa nyundo,

akamponda kichwa chake,

akamvunjavunja na kumtoboa

paji lake la uso.

27 Aliinama miguuni pa Yaeli,

akaanguka; akalala hapo.

Pale alipoinama miguuni pake,

alianguka;

pale alipoinamia, ndipo alipoanguka,

akiwa amekufa.

28 “Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia;

nyuma ya dirisha alilia, akasema,

‘Mbona gari lake linachelewa kufika?

Mbona vishindo vya magari yake

vimechelewa?’

29 Wanawake wenye busara

kuliko wengine wote wakamjibu;

naam, husema moyoni mwake,

30 ‘Je, hawapati na kugawanya nyara:

msichana mmoja au wawili kwa kila mtu,

mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara,

mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa,

mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu:

yote haya kuwa nyara?’

31 “Adui zako wote na waangamie, EeBwana!

Bali wote wakupendao na wawe kama jua

lichomozavyo kwa nguvu zake.”

Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/5-54532687ea068db9b0f4449cc384bb0a.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 6

Gideoni

1 Waisraeli wakafanya tena yaliyo maovu mbele zaBwana, naye kwa miaka sabaBwanaakawatia mikononi mwa Wamidiani.

2 Mkono wa Midiani ukawa na nguvu dhidi ya Israeli na kwa ajili ya Wamidiani, Waisraeli wakajitengenezea mahali pa kujificha milimani, kwenye mapango na ngome.

3 Kila wakati Waisraeli walipopanda mazao mashambani, Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki walivamia nchi yao.

4 Wakapiga kambi katika mashamba yao na kuharibu mazao ya nchi yote hadi kufikia Gaza, wala hawakuacha kiumbe cho chote kilicho hai kwa Waisraeli, iwe kondoo au ng’ombe au punda.

5 Walipanda na mifugo yao na mahema yao, mfano wa makundi ya nzige. Ilikuwa haiwezekani kuwahesabu watu na ngamia zao; wakavamia nchi ili kuiharibu.

6 Waisraeli wakafanywa kuwa maskini sana na Wamidiani, hata Israeli wakamliliaBwanakuomba msaada.

7 Waisraeli walipomliliaBwanakwa sababu ya Wamidiani,

8 Bwanaakawapelekea nabii, ambaye aliwaambia, “Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Niliwapandisha mtoke Misri, toka nchi ya utumwa.

9 Nikawanyakua kutoka mikononi mwa Wamisri na kutoka mikononi mwa watesi wenu wote. Nikawafukuza watoke mbele yenu nami nikawapa ninyi nchi yao.

10 Nikawaambia, ‘Mimi ndimiBwanaMungu wenu; msiiabudu miungu ya Waamori, ambayo mnakaa katika nchi yao!’ Lakini ninyi hamkuitii sauti yangu.”

11 Malaika waBwanaakaja akaketi chini ya mti wa mwaloni huko Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi Mwebiezeri, ambako Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione.

12 Malaika waBwanaalipomtokea Gideoni, akamwambia, “Bwanayu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.”

13 Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kamaBwanayu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je,Bwanahakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasaBwanaametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.”

14 Bwanaakamgeukia na kusema “Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli kutoka mikononi mwa Wamidiani. Je, si mimi ninayekutuma wewe?”

15 Gideoni akauliza, “Ee Bwana wangu, nitawezaje kuwaokoa Israeli? Ukoo wangu ndio dhaifu kuliko zote katika Manase, nami ndiye mdogo wa wote katika jamaa yangu.”

16 Bwanaakamjibu, “Nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kana kwamba walikuwa ni mtu mmoja.”

17 Gideoni akajibu, “Kama basi nimepata kibali machoni pako, nipe ishara kuonyesha kweli kwamba ni wewe unayesema nami.

18 Tafadhali ninakuomba usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea sadaka yangu na kuiweka mbele yako.”

NayeBwanaakamwambia, “Nitangoja mpaka utakaporudi.”

19 Gideoni akaingia ndani ya nyumba yake na kuandaa mwana-mbuzi pamoja na kuoka mikate isiyotiwa chachu kutokana na efa mojaya unga. Akaweka nyama kwenye kikapu na mchuzi kwenye chungu, akamletea huyo malaika hapo nje chini ya mti wa mwaloni na kumpa.

20 Malaika wa Mungu akamwambia, “Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uviweke juu ya mwamba huu na umimine huo mchuzi juu yake.” Gideoni akafanya hivyo.

21 Malaika waBwanaakainyoosha fimbo iliyokuwa mkononi mwake, ncha yake ikagusa ile nyama na ile mikate isiyotiwa chachu, nao moto ukatoka kwenye mwamba ukateketeza ile nyama na ile mikate. Malaika waBwanaakatoweka kutoka machoni pake.

22 Gideoni alipotambua kuwa ni malaika waBwana, akapiga kelele kwa mshangao, akasema, “Ole wangu,BwanaMwenyezi! Kwa kuwa nimemwona malaika waBwanauso kwa uso!”

23 LakiniBwanaakamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa.”

24 Hivyo Gideoni akamjengeaBwanamadhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom. Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.

25 Usiku ule uleBwanaakamwambia, “Mchukue ng’ombe dume wa baba yako, yaani, yule wa pili mwenye miaka saba, na ubomoe ile madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate ile Ashera iliyo karibu nayo.

26 Kisha mjengeeBwanaMungu wako, madhabahu halisi, kwa taratibu zake, juu ya huu mwamba. Kwa kutumia kuni za hiyo nguzo ya Ashera uliyoikatakata, mtoe sadaka huyo dume wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa.”

27 Basi Gideoni akawachukua watumishi wake kumi na kufanya kamaBwanaalivyomwambia. Lakini kwa kuwa aliwaogopa jamaa yake na watu wa mji, akafanya haya usiku badala ya mchana.

28 Watu wa mji walipoamka asubuhi, tazama madhabahu ya Baali imebomolewa na nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwakatwa na yule ng’ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya madhabahu iliyojengwa upya!

29 Wakaulizana, “Ni nani aliyetenda mambo haya?”

Walipochunguza kwa makini, wakaambiwa, “Ni Gideoni mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda hivi.”

30 Watu wa mji wakamwambia Yoashi, “Mlete mwanao hapa. Ni lazima afe, kwa sababu amebomoa madhabahu ya Baali na kukatakata nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo.”

31 Lakini Yoashi akauambia ule umati uliokuwa umezunguka ukiwa kinyume naye, “Je, ninyi mtamtetea Baali? Mnajaribu kumwokoa? Ye yote mwenye kumpigania atauawa kufikia kesho asubuhi! Kama Baali ni mungu kweli, anaweza kujitetea mwenyewe wakati mtu anapobomoa madhabahu yake.”

32 Basi siku ile wakamwita Gideoni “Yerub-Baali,” yaani, “Baali na ashindane naye,” kwa sababu alibomoa madhabahu yake.

33 Basi Wamidiani wote, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki wakaunganisha majeshi yao, wakavuka ng’ambo ya Yordani na kupiga kambi katika Bonde la Yezreeli.

34 Ndipo Roho waBwanaakamjia Gideoni, akapiga tarumbeta, akiwaita Waabiezeri ili wamfuate.

35 Akatuma wajumbe waende katika Manase yote, akiwataka wachukue silaha na pia katika Asheri, Zabuloni na Naftali, nao wakakwea ili kukutana nao.

36 Gideoni akamwambia Mungu, “Kama utawaokoa Waisraeli kwa mkono wangu, kama ulivyoahidi:

37 tazama, nitaweka ngozi ya kondoo kwenye kiwanja cha kupuria nafaka, na kama utakuwepo umande juu ya ngozi tu, nayo ardhi yote ikiwa kavu, ndipo nitakapojua kuwa utaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.”

38 Hivyo ndivyo ilivyotokea. Gideoni akaamka asubuhi na mapema kesho yake, akaikamua ile ngozi, umande ukatoka, maji ya kujaa bakuli.

39 Kisha Gideoni akamwambiaBwana, “Usinikasirikie. Ninaomba nifanye ombi moja lingine. Niruhusu nifanye jaribio jingine moja kwa ngozi hii. Wakati huu uifanye ngozi hii kavu na ardhi yote ifunikwe na umande.”

40 Usiku ule Mungu akafanya hivyo. Ngozi ile ilikuwa kavu, nayo ardhi yote ikafunikwa na umande.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/6-2b4effce819ff9f4eabfd4b77b6bef3a.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 7

Gideoni Awashinda Wamidiani

1 Ndipo Yerub-Baali (yaani Gideoni) na lile jeshi lililokuwa pamoja naye, wakaondoka asubuhi na mapema na kupiga kambi kando ya chemchemi ya Harodi. Kambi ya Wamidiani ilikuwa kaskazini yao katika bonde karibu na kilima cha More.

2 Bwanaakamwambia Gideoni, “Jeshi lililo pamoja nawe ni kubwa sana kwa mimi kuwatia Wamidiani mikononi mwao. Ili kwamba Israeli asije akajisifu juu yangu akisema, ‘Mkono wangu ndio ulioniokoa,

3 kwa hiyo sasa tangaza jeshi lote likiwa linasikia, kwamba: Ye yote anayeogopa na kutetemeka, yeye na arudi nyumbani, aondoke katika Mlima Gileadi.’ ” Hivyo watu 22,000 walirudi, wakabaki 10,000.

4 LakiniBwanaakamwambia Gideoni, “Idadi ya jeshi bado ni kubwa. Wapeleke chini katika maji nami nitawajaribu huko kwa ajili yako. Kama nikikuambia, ‘Huyu atakwenda pamoja nawe,’ yeye atakwenda; lakini kama nikisema, ‘Huyu hatakwenda pamoja nawe,’ yeye hatakwenda.”

5 Hivyo Gideoni akalileta lile jeshi chini kwenye maji nayeBwanaakamwambia Gideoni, “Watenge upande mmoja wale wote wanywao maji kwa ulimi, kama vile mbwa anywavyo, wale wote wapigao magoti ili kunywa wakipeleka mikono yao vinywani mwao, waweke upande mwingine.”

6 Idadi ya wale waliokunywa kwa kulamba lamba walikuwa 300, lakini wengine wote katika jeshi walipiga magoti ili kunywa.

7 Bwanaakamwambia Gideoni, “Kwa hao watu 300 waliolamba maji nitawaokoa ninyi, nami nitawatia Wamidiani mkononi mwako. Waache hao watu wengine wote warudi kila mmoja nyumbani mwake.”

8 Hivyo Gideoni akawaacha wale Waisraeli wengine kila mmoja aende kwenye hema yake. Akabakia na wale 300, ambao walichukua vyakula na tarumbeta za wale wenzao.

Basi kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake bondeni.

9 Usiku ule uleBwanaakamwambia Gideoni, “Ondoka, ushuke kambini, kwa kuwa nimeitia mkononi mwako.

10 Lakini kama unaogopa kushambulia, shuka kambini pamoja na mtumishi wako Pura,

11 nawe sikiliza wanayosema. Hatimaye, utatiwa moyo kushambulia kambi.” Basi yeye na Pura mtumishi wake wakashuka na kufikia walinzi wa mbele wenye silaha waliokuwa mle kambini.

12 Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine yote ya mashariki walikaa bondeni, nao walikuwa mfano wa nzige kwa wingi wao. Ngamia zao hazikuhesabika, wingi wao ulikuwa kama mchanga wa ufuoni mwa bahari.

13 Gideoni alifika wakati huo huo kukiwa na mtu mmoja aliyekuwa anamweleza mwenzake ndoto yake, akisema, “Niliota ndoto: Tazama mkate wa shayiri ulioviringana ulianguka katika kambi moja ya Wamidiani, ukaipiga na ikaanguka nao ukaipindua juu chini na hema ikaporomoka chini.”

14 Rafiki yake akamjibu, “Habari hii si kitu kingine zaidi ya upanga wa Gideoni mwana wa Yoashi, Mwisraeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote mkononi mwake.”

15 Gideoni alipoisikia hiyo ndoto na tafsiri yake, akamwabudu Mungu. Akarudi kwenye kambi ya Israeli na kusema, “Inukeni!Bwanaamelitia jeshi la Wamidiani mikononi mwenu.”

16 Akawagawa wale watu 300 katika makundi matatu, akawakabidhi tarumbeta mikononi mwao wote na mitungi isiyokuwa na maji yenye mienge ndani yake.

17 Akawaambia, “Nitazameni, fanyeni kama nitakavyofanya, nitakapofika mwisho wa kambi mfanye kama nitakavyofanya.

18 Wakati mimi na wale walio pamoja nami wote, tutakapopiga tarumbeta zetu, ninyi nanyi pigeni tarumbeta pande zote za kambi na mpige kelele, mseme, ‘Upanga waBwanana wa Gideoni.’ ”

19 Gideoni na wale watu 100 waliokuwa pamoja naye wakafika mwisho wa kambi usiku mwanzoni mwa zamu ya kati, mara tu walipokuwa wamebadili zamu. Wakapiga zile tarumbeta zao na kuvunja ile mitungi iliyokuwa mikononi mwao.

20 Yale makundi matatu yakapiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Wakashika mienge kwa mikono yao ya kushoto na katika mikono yao ya kuume tarumbeta ili kuzipiga, wakapaza sauti zao, “Upanga waBwanana wa Gideoni!”

21 Wakasimama kila mtu mahali pake kuizunguka kambi pande zote, Wamidiani wote wakakimbia, huku wakipiga kelele.

22 Walipozipiga zile tarumbeta 300,Bwanaakafanya watu katika kambi yote kugeuziana upanga kila mmoja na mwenziwe. Jeshi likakimbia mpaka Beth-Shita kuelekea Sererahadi mpakani mwa Abel-Mehola karibu na Tabathi.

23 Watu wa Israeli wakaitwa kutoka Naftali, Asheri na Manase, wakawafuatia Wamidiani.

24 Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima vya Efraimu akisema, “Telemkeni dhidi ya Wamidiani na mkazuie vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani.”

Hivyo watu wote wa Efraimu wakakutanika pamoja na kuzingira mto wa Yordani hadi Beth-Bara.

25 Wakawakamata wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu. Wakamwulia Orebu pale penye mwamba wa Orebu, na Zeebu wakamwulia penye shinikizo la kukamulia divai la Zeebu. Wakawafuatia Wamidiani na kuleta vichwa vya Orebu na Zeebu kwa Gideoni, huko ng’ambo ya Yordani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/7-547f543df542832b22099206ba613afe.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 8

Ushindi Wa Gideoni Na Kulipiza Kisasi

1 Basi Waifraimu wakamwuliza Gideoni, “Mbona mmetutenda hivi? Kwa nini hukutuita ulipokwenda kupigana na Wamidiani?” Wakawalaumu kwa ukali sana.

2 Gideoni akawajibu, “Nilichofanya mimi ni nini kulinganisha na kile ninyi mlichofanya? Je, kuokoa masazo ya zabibu za Efraimu si bora kuliko mavuno kamili ya zabibu ya Abiezeri?

3 Mungu amewatia Orebu na Zeebu, hao viongozi wa Wamidiani, mikononi mwenu. Je, mimi niliweza kufanya nini kulinganisha na mlichofanya ninyi?” Aliposema hili, hasira yao dhidi yake ikatulia.

4 Gideoni akiwa pamoja na wale watu 300 waliofuatana naye, wakiwa wamechoka na wenye njaa lakini bado wakiwafuatia, wakafika Yordani na kuuvuka.

5 Akawaambia watu wa Sukothi, “Tafadhali lipatieni jeshi langu mikate, kwa maana wamechoka, nami ningali ninawafuatia Zeba na Salmuna, wafalme wa Midiani.”

6 Lakini maafisa wa Sukothi wakasema, “Je, mikono ya Zeba na Salmuna tayari mnayo sasa ili tuweze kulipatia jeshi lako mikate?”

7 Gideoni akajibu, “Kwa ajili ya hilo tu,Bwanaatakapowatia Zeba na Salmuna mkononi mwangu, nitaichana nyama ya miili yenu kwenye miiba ya nyikani na kwenye michongoma.”

8 Kutoka hapo alikwea mpaka Penieli na kutoa ombi lile lile, lakini nao watu wa Penieli wakamjibu kama watu wa Sukothi walivyokuwa wamemjibu.

9 Hivyo akawaambia watu wa Penieli, “Nitakaporudi baada ya kushinda, nitaubomoa mnara huu.”

10 Wakati huu Zeba na Salmuna walikuwa Karkori wakiwa na jeshi lenye watu wapatao 15,000 wale wote waliokuwa wamesalia wa mataifa ya mashariki, kwa kuwa watu wapatao 120,000 wenye panga walikuwa wameuawa.

11 Basi Gideoni akakwea kwa njia ya wasafiri mashariki ya Noba na Yogbeha na kulishambulia jeshi bila lenyewe kushuku lo lote.

12 Zeba na Salmuna, hao wafalme wawili wa Midiani, wakakimbia lakini yeye Gideoni akawafuatia na kuwakamata, akalishinda hilo jeshi lao lote.

13 Gideoni mwana wa Yoashi akarudi kutoka vitani kwa kupitia Mwinuko wa Heresi.

14 Akamkamata kijana mmoja wa Sukothi na kumwuliza maswali, naye yule kijana akamwandikia majina ya maafisa sabini wa Sukothi, ambao ni viongozi wa mji.

15 Ndipo Gideoni akaja na kuwaambia watu wa Sukothi, “Tazama, hapa wapo Zeba na Salmuna mlionisimanga kwa ajili yao mkisema, ‘Je, mikono ya Zeba na Salmuna tayari mnayo sasa ili tuweze kulipatia jeshi lako mikate?’ ”

16 Akawachukua hao viongozi wa mji na kuwafundisha watu wa Sukothi somo kwa kuwaadhibu kwa miiba na michongoma ya nyikani.

17 Pia akaubomoa mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji.

18 Kisha akawauliza Zeba na Salmuna, “Ni watu wa aina gani mliowaua huko Tabori?”

Wakajibu, “Ni watu kama wewe, kila mmoja wao akiwa na nafasi ya uana wa mfalme.”

19 Gideoni akajibu, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu hasa. Hakika kama aishivyoBwana, kama mngekuwa mmewaacha hai, mimi nisingewaua ninyi.”

20 Akamgeukia Yetheri, mwanawe mzaliwa wa kwanza, akasema, “Waue hawa!” Lakini Yetheri hakuufuta upanga wake, kwa sababu aliogopa, kwa kuwa alikuwa bado kijana mdogo tu.

21 Zeba na Salmuna wakasema, “Njoo ufanye hivyo wewe mwenyewe. ‘Alivyo mtu, ndivyo zilivyo nguvu zake.’ ” Hivyo Gideoni akatoka mbele na kuwaua, naye akayaondoa mapambo kwenye shingo za ngamia zao.

Kisibau Cha Gideoni

22 Waisraeli wakamwambia Gideoni, “Ututawale, wewe, wanao na wana wa wana wako, kwa kuwa umetuokoa kutoka mikononi mwa Wamidiani.”

23 Lakini Gideoni akawaambia, “Mimi sitatawala juu yenu, wala wanangu hawatatawala juu yenu.Bwanandiye atakayetawala juu yenu ninyi.”

24 Naye akasema, “Ninalo ombi moja, kwamba kila mmoja wenu anipatie kipuli kutoka kwenye fungu lake la nyara.” (Ilikuwa desturi ya Waishmaeli kuvaa vipuli vya dhahabu.)

25 Wakajibu, “Tutafurahi kuvitoa.” Hivyo wakatanda vazi chini na kila mwanaume akatupia juu yake pete kutoka kwenye fungu lake la nyara.

26 Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilifikia shekeli 1,700, bila kuhesabu mapambo mengine, pete za masikio na mavazi ya zambarau yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani, au mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia zao.

27 Gideoni akatengeneza kisibau kwa kutumia ile dhahabu, ambacho alikiweka katika mji wake, yaani, Ofra. Waisraeli wote wakafanya uasherati kwa kukiabudu huko, nacho kikawa mtego kwa Gideoni na jamaa yake.

28 Hivyo Midiani ikashindwa mbele ya Israeli nayo haikuinua kichwa chake tena. Wakati wa siku za uhai wa Gideoni, nchi ikafurahia amani miaka arobaini.

Kifo Cha Gideoni

29 Yerub-Baali akarudi kwenda kuishi katika nyumba yake.

30 Alikuwa na wana sabini wa kwake mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na wake wengi.

31 Suria wake, aliyekuwa anaishi huko Shekemu, pia alimzalia mwana, ambaye alimwita Abimeleki.

32 Gideoni mwana wa Yoashi akafa akiwa na umri mzuri wa uzee, na akazikwa katika kaburi la Yoashi baba yake huko Ofra ya Waabiezeri.

33 Mara tu alipokufa Gideoni, Waisraeli wakarudia hali ya uovu na kufanya uasherati kwa kuabudu Mabaali. Wakamsimamisha Baal-Berithi kuwa mungu wao na

34 wala hawakumkumbukaBwanaMungu wao, aliyewaokoa kutoka mikononi mwa adui zao wote kutoka kila upande.

35 Pia wakashindwa kuitendea mema jamaa ya Yerub-Baali (yaani Gideoni) kwa ajili ya mambo yote mema aliyokuwa amefanya kwa ajili yao.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/8-1c71e4d8db41e4b0698a5c80f0ffe2af.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 9

Abimeleki Ajaribu Kuanzisha Ufalme

1 Siku moja Abimeleki mwana wa Yerub-Baali akaenda kwa ndugu wa mama yake huko Shekemu na kuwaambia yeye na ukoo wote wa mama yake,

2 “Waulizeni watu wote wa Shekemu, ‘Lipi lililo bora kwenu: Kutawaliwa na wana wote sabini wa Yerub-Baali, au mtu mmoja peke yake?’ Kumbukeni kwamba, mimi ni mfupa wenu nyama yenu hasa.”

3 Ndugu za mama yake walipowaeleza watu wote wa Shekemu, wakaelekea kumkubali Abimeleki kwa kuwa walisema, “yeye ni ndugu yetu.”

4 Wakampa shekeli sabiniza fedha kutoka katika hekalu la Baal-Berithi, naye Abimeleki akaitumia kuajiri watu ovyo wasiojali, wakawa ndio wafuasi wake.

5 Akaenda nyumbani kwa baba yake huko Ofra, na juu ya jiwe moja wakawaua ndugu zake sabini, ambao ni wana wa Yerub-Baali. Lakini Yothamu, mwana mdogo wa wote wa Yerub-Baali, akaokoka kwa kujificha.

6 Ndipo watu wote wa Shekemu na Beth-Milo wakakusanyika pamoja chini ya mti mkubwa wa mwaloni penye nguzo iliyoko Shekemu wakamvika Abimeleki taji kuwa mfalme.

7 Yothamu alipoambiwa hayo, akapanda juu ya kilele cha mlima Gerizimu, akawapazia sauti yake akawaambia, “Nisikilizeni enyi watu wa Shekemu, ili Mungu naye apate kuwasikiliza ninyi.

8 Siku moja miti ilitoka ili kwenda kujitawazia mfalme. Ikauambia mzeituni, ‘Wewe uwe mfalme wetu.’

9 “Lakini mzeituni ukaijibu, ‘Je, niache kutoa mafuta yangu ambayo kwayo miungu na wanadamu huheshimiwa, ili nikawe juu ya miti?’

10 “Kisha miti ikauambia mtini, ‘Njoo na uwe mfalme wetu!’

11 “Lakini mtini ukaijibu, ‘Je, niache kutoa matunda yangu mazuri na matamu, ili niende nikawe juu ya miti?’

12 “Ndipo miti ikauambia mzabibu, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’

13 “Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikawe juu ya miti?’

14 “Mwishoni miti yote ikauambia mti wa miiba, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’

15 “Nao mti wa miiba ukaijibu, ‘Kama kweli mnataka niwe mfalme wenu, basi njoni mpate kupumzika chini ya kivuli changu. Lakini kama sivyo, moto na utoke kwenye mti wa miiba ukateketeze mierezi ya Lebanoni!’

16 “Basi ikiwa mmetenda kwa uaminifu na heshima kumfanya Abimeleki kuwa mfalme, na kama mmetendea vyema Yerub-Baali na jamaa yake kama ilivyostahili:

17 kwa kuwa baba yangu aliwapigania ninyi na kuhatarisha nafsi yake na kuwaokoa ninyi kutoka mikononi mwa Wamidiani

18 (lakini leo mmeasi dhidi ya jamaa ya baba yangu, na kuwaua wanawe sabini juu ya jiwe moja, nanyi mkamfanya Abimeleki mwana wa mwanamke mtumwa kuwa mfalme juu ya Shekemu, kwa kuwa yeye ni ndugu yenu),

19 nanyi kama basi mmemtendea Yerub-Baali na jamaa yake kwa heshima na uaminifu, basi Abimeleki na awe furaha yenu, nanyi mwe furaha yake pia!

20 Lakini kama sivyo, moto na utoke kwa Abimeleki na uwateketeze, ninyi watu wa Shekemu na Beth-Milo, nao moto utoke kwenu, watu wa Shekemu na Beth-Milo umteketeze Abimeleki!”

21 Ndipo Yothamu akakimbia, akatoroka akaenda Beeri, akaishi huko, kwa sababu alimwogopa ndugu yake Abimeleki.

22 Baada ya Abimeleki kutawala Israeli kwa muda wa miaka mitatu,

23 Mungu akaruhusu roho mbaya kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu, nao watu wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa hila.

24 Hili lilitokea ili ule ukatili waliotendewa hao wana sabini wa Yerub-Baali upatilizwe, na damu yao iwe juu ya Abimeleki ndugu yao aliyewaua, na pia iwe juu ya watu wa Shekemu, ambao walimsaidia kuua ndugu zake.

25 Hivyo, kutokana na uadui juu yake watu wa Shekemu wakaweka watu wa kumvizia katika vilele vya milima. Wakawanyang’anya watu wote waliopita karibu nao, nayo haya yakaarifiwa kwa Abimeleki.

26 Basi Gaali mwana wa Ebedi akaenda pamoja na ndugu zake wakaingia Shekemu, nao watu wa huko wakamtumainia yeye.

27 Wakaenda mashambani mwao kuvuna zabibu na kuzisindika hizo zabibu, wakafanya sikukuu katika hekalu la mungu wao. Wakati wakila na kunywa, wakamlaani Abimeleki.

28 Gaali mwana wa Ebedi akasema, “Abimeleki ni nani na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Je, yeye si mwana wa Yerub-Baali? Naye Zebuli si ndiye msaidizi wake? Basi watumikieni watu wa Hamori, babaye Shekemu. Kwa nini tumtumikie Abimeleki?

29 Laiti watu hawa wangekuwa chini ya amri yangu! Basi mimi ningemwondoa huyo Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, ‘Ondoa jeshi lako lote.’ ”

30 Zebuli aliyekuwa mtawala wa mji aliposikia aliyosema Gaali mwana wa Ebedi, akakasirika sana.

31 Akatuma ujumbe uende kwa Abimeleki kwa siri na kusema, “Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wamekuja Shekemu, na wanauchochea mji huu kinyume chako.

32 Sasa, basi, usiku huu wewe uondoke na watu wako ili mje kuwavizia mashambani.

33 Kisha asubuhi wakati wa kuchomoza jua, amka mapema na ujipange dhidi ya huo mji. Wakati yeye na jeshi lililo pamoja naye watakapotoka kukabiliana nanyi, mwaweza kuwatendea kwa kadiri mnavyoweza.”

34 Kwa hiyo Abimeleki pamoja na jeshi lake lote wakaondoka usiku na kujificha karibu na Shekemu wakiwa vikosi vinne.

35 Basi Gaali mwana wa Ebedi alikuwa ametoka nje akawa amesimama katika ingilio la mji wakati ule ule ambao Abimeleki na watu wake walipokuwa wanatoka sehemu zao za maficho.

36 Gaali alipowaona, akamwaambia Zebuli, “Tazama, watu wanashuka kutoka kwenye vilele vya milima!”

Zebuli akajibu, “Wewe unaona vivuli vya milima kana kwamba ni watu.”

37 Lakini Gaali akasema tena, “Tazama, watu wanashuka kutoka katikati ya nchi na kikosi kimoja kinakuja kutoka Tabur-Ezeri na kikosi kingine kutoka upande wa Elon-Meonenimu.”

38 Ndipo Zebuli akamwambia, “Kuko wapi kujivuna kwako sasa, wewe uliyesema, ‘Huyo Abimeleki ni nani hata tumtumikie?’ Hawa si wale watu uliowadharau? Toka nje sasa ukapigane nao!”

39 Basi Gaali akatoka akawaongoza watu wa Shekemu kupigana na Abimeleki.

40 Abimeleki akamfukuza, watu wengi wakajeruhiwa katika kukimbia huko, njia nzima hadi kwenye ingilio la lango.

41 Abimeleki akakaa Aruma, naye Zebuli akawafukuza Gaali na ndugu zake watoke Shekemu.

42 Kesho yake watu wa Shekemu wakatoka wakaenda mashambani, Abimeleki akaambiwa juu ya jambo hili.

43 Hivyo akawachukua watu wake, akawagawanya katika vikosi vitatu na kuwaweka waviziao huko mashambani. Alipowaona watu wanatoka kwenda nje ya mji, akainuka dhidi yao na kuwashambulia.

44 Abimeleki pamoja na vile vikosi wakaharakisha kwenda mbele kwenye nafasi, mahali pa ingilio la lango la mji. Vile vikosi viwili vikawawahi wale waliokuwa mashambani na kuwaua.

45 Siku hiyo nzima Abimeleki akazidisha mashambulizi yake dhidi ya mji hadi akawa ameuteka na kuwaua watu wa huo mji. Kisha akauangamiza mji na kusambaza chumvi juu yake.

46 Kwa kusikia jambo hili watu wote katika mnara wa Shekemu, wakaingia kwenye ngome ya hekalu la El-Berithi.

47 Abimeleki aliposikia kuwa wamekusanyika huko,

48 yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua mabegani. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Fanyeni kile mlichoona mimi nikifanya!”

49 Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome na kuitia moto ili kuwachoma wale watu wote waliokuwa ndani yake. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, karibia watu 1,000 waume kwa wake, pia wakafa.

50 Baadaye Abimeleki akaenda Thebesi na kuuzingira kwa jeshi na kuuteka.

51 Hata hivyo, ndani ya huo mji kulikuwa na mnara imara, ambako watu wote wa mji wanaume na wanawake, watu wote wa mji, walikimbilia ndani yake. Wakajifungia ndani yake na kupanda juu ya paa la mnara.

52 Abimeleki akaja kwenye ule mnara na kuushambulia, lakini alipokaribia kwenye ingilio la mnara ili kuuchoma kwa moto,

53 mwanamke mmoja akaangusha sehemu ya juu ya jiwe la kusagia juu ya kichwa cha Abimeleki, likapasua fuvu la kichwa chake.

54 Akamwita kwa haraka kijana yule aliyechukua silaha zake, na kumwambia, “Chukua upanga wako na uniue, watu wasije wakasema kwamba, ‘Mwanamke amemwua.’ ” Basi yule kijana akamchoma upanga, naye akafa.

55 Waisraeli walipoona kuwa Abimeleki amekufa, kila mtu akaenda nyumbani kwake.

56 Hivyo ndivyo Mungu alivyolipiza uovu ule ambao Abimeleki alikuwa ameutenda kwa baba yake kwa kuwaua ndugu zake sabini.

57 Mungu akawapatiliza watu wa Shekemu uovu wao juu ya vichwa vyao, na juu yao ikaja laana ya Yothamu mwana wa Yerub-Baali.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/9-0a11864ae71ad68f82ef33a30f511c7e.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 10

Tola

1 Baada ya Abimeleki, Tola mwana wa Pua mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, aliyeishi huko Shamiri, katika nchi ya vilima ya Efraimu, akainuka kuokoa Israeli.

2 Akaamua Israeli kwa miaka ishirini na mitatu. Ndipo akafa, naye akazikwa huko Shamiri.

Yairi

3 Baada yake akafuatiwa na Yairi, Mgileadi, ambaye aliamua Israeli kwa miaka ishirini na miwili.

4 Alikuwa na wana thelathini waliopanda punda thelathini. Nao walikuwa na miji thelathini iliyoko Gileadi, inayoitwa Hawoth-Yairi mpaka leo.

5 Yairi akafa, naye akazikwa huko Kamoni.

Yefta

6 Wana wa Israeli wakatenda tena maovu machoni paBwana. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni na miungu ya Wafilisti. Kwa kuwa Waisraeli walimwachaBwanawala hawakuendelea kumtumikia,

7 hivyo hasira yaBwanaikawaka dhidi ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamoni,

8 ambao waliwaonea na kuwatesa mwaka ule. Kwa miaka kumi na minane wakawatesa Waisraeli wote upande wa mashariki ya Mto Yordani katika Gileadi, nchi ya Waamoni.

9 Waamoni nao wakavuka Yordani ili kupigana na Yuda, Benyamini na nyumba ya Efraimu, nayo nyumba ya Israeli ikawa katika taabu kubwa.

10 Ndipo Waisraeli wakamliliaBwanawakasema, “Tumetenda dhambi dhidi yako, kumwacha Mungu wetu na kutumikia Mabaali.”

11 Bwanaakawaambia, “Wakati Wamisri, Waamoni, Wafilisti,

12 Wasidoni, Waamaleki na Wamaoni walipowaonea na ninyi mkanililia na kuomba msaada, je, sikuwaokoa kutoka mikononi mwao?

13 Lakini ninyi mmeniacha mimi na kutumikia miungu mingine, kwa hiyo sitawaokoa tena.

14 Nendeni mkaililie ile miungu mlioichagua. Hiyo miungu na iwaokoe mnapokuwa katika taabu!.”

15 Lakini Waisraeli wakamwambiaBwana, “Tumetenda dhambi. Ututendee lile unaloona kuwa jema kwako, lakini twakusihi utuokoe sasa.”

16 Nao wakaiondoa hiyo miungu migeni katikati yao nao wakamtumikiaBwana. Naye akahuzunika kwa sababu ya taabu ya Israeli.

17 Ndipo Waamoni wakaitwa vitani na kupiga kambi huko Gileadi, Waisraeli wakakusanyika na kupiga kambi huko Mizpa.

18 Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana wao kwa wao, “Ye yote yule atakayeanzisha mashambulizi dhidi ya Waamoni atakuwa kiongozi wa wote wakaao Gileadi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/10-5113cc20ac98462ac25381a7906f952f.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 11

1 Basi Yefta Mgileadi alikuwa mtu shujaa. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba.

2 Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamaa yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.”

3 Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika nchi ya Tobu, mahali ambako watu waasi walijiunga naye na kumfuata.

4 Baada ya muda Waamoni wakafanya vita na Israeli,

5 viongozi wa Gileadi wakaenda kumchukua Yefta katika nchi ya Tobu.

6 Wakamwambia Yefta, “Uwe jemadari wetu, ili tuweze kupigana na Waamoni.”

7 Yefta akawaambia, “Je, hamkunichukia mimi na kunifukuza katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini mnanijia sasa, wakati mna matatizo.”

8 Viongozi wa Gileadi wakamwambia, “Lakini sasa tumegeuka kukuelekea wewe, ili uende pamoja nasi kupigana na Waamoni, nawe utakuwa kiongozi wetu juu ya watu wote wa Gileadi.”

9 Yefta akawaambia, “Ikiwa mtanirudisha kwetu kupigana na Waamoni, nayeBwanaakanisaidia kuwashinda, Je, ni kweli nitakuwa kiongozi wenu?”

10 Viongozi wa Gileadi wakamjibu, “Bwanandiye shahidi yetu, kwa hakika tutafanya kama usemavyo.”

11 Basi Yefta akaenda na viongozi wa Gileadi, nao watu wakamfanya kiongozi na jemadari wao. Naye akarudia maneno yake yote mbele zaBwanahuko Mizpa.

12 Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini juu yetu, hata umekuja kushambulia nchi yetu?”

13 Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Wakati Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Arnoni mpaka Yaboki, hadi kufikia Yordani. Sasa rudisha kwa amani.”

14 Yefta akarudisha wajumbe kwa mfalme wa Waamoni,

15 kusema:

“Hili ndilo asemalo Yefta, Israeli hawakuchukua nchi ya Moabu wala ya Waamoni.

16 Lakini walipopanda kutoka Misri, Israeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu na wakafika Kadeshi.

17 Ndipo Israeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako,’ Lakini mfalme wa Edomu hakutusikia. Wakapeleka pia wajumbe kwa mfalme wa Moabu, naye akakataa. Kwa hiyo Israeli wakakaa huko Kadeshi.

18 “Baadaye wakasafiri kupitia katika jangwa wakiambaa-ambaa na hiyo nchi ya Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu na kupiga kambi upande mwingine wa Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu kwa kuwa Arnoni ilikuwa ndio mpaka wake.

19 “Kisha Israeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni mfalme wa Waamoni, aliyetawala Heshboni, na kumwambia, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako ili kufikia mahali petu.’

20 Hata hivyo, Sihoni hakuwaamini Waisraeli kupita katika nchi yake. Akaandaa jeshi lake lote na kupiga kambi huko Yahasa, nao wakapigana na Israeli.

21 “NdipoBwana, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Israeli, nao wakawashinda. Israeli wakaitwaa nchi yote ya Waamoni, waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo,

22 wakiiteka nchi yote kuanzia Arnoni mpaka Yaboki na kutoka jangwani mpaka Yordani.

23 “Basi kwa kuwaBwana, Mungu wa Israeli, amewafukuza Waamoni watoke mbele ya watu wake Israeli, wewe unayo haki gani ya kuitamalaki?

24 Je, haikupasi kuchukua kile ambacho mungu wako Kemoshi amekupa? Vivyo hivyo, cho chote kileBwanaMungu wetu alichotupa sisi, tutakimiliki.

25 Je, wewe ni bora kuliko Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu? Je, yeye alishagombana na Israeli au kupigana nao wakati wo wote?

26 Kwa maana kwa miaka 300 Israeli wameishi Heshboni na vijiji vyake, Aroeri na vijiji vyake, na katika miji yote iliyo kando ya Arnoni. Kwa nini wewe haukuichukua wakati huo?

27 Mimi sijakukosea jambo lo lote, bali wewe ndiye unayenikosea kwa kufanya vita nami. BasiBwana, aliye Mwamuzi, leo na aamue ugomvi kati ya Waisraeli na Waamoni.”

28 Hata hivyo, Mfalme wa Waamoni, hakuyajali maneno ya ujumbe wa Yefta.

29 Ndipo Roho waBwanaakaja juu ya Yefta. Akapita katikati ya Gileadi na Manase, pia akapita katika Mizpa ya Gileadi, na kutokea huko akasonga mbele kushambulia Waamoni.

30 Naye Yefta akaweka nadhiri mbele zaBwanaakisema, “Ikiwa utawatia Waamoni mikononi mwangu,

31 cho chote kile kitakachotoka katika mlango wa nyumba yangu cha kwanza ili kunilaki nirudipo kwa amani katika kuwashinda Waamoni, kitakuwa ni chaBwanana nitakitoa kuwa sadaka ya kuteketezwa.”

32 Ndipo Yefta akavuka kupigana na hao Waamoni, nayeBwanaakawatia mkononi mwake.

33 Akawapiga kwa ushindi mkubwa kuanzia Aroeri mpaka karibu na Minithi na kuendelea mpaka Abel-Keramimu, miji yote iliyopigwa ni ishirini. Basi Israeli wakawashinda Waamoni.

34 Yefta aliporudi nyumbani Mizpa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa ndiye mtoto pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine.

35 Alipomwona akararua mavazi yake akalia, “Ee! Binti yangu! Umenifanya niwe na huzuni na kunyong’onyea sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwaBwana, ambayo siwezi kuivunja.”

36 Akajibu, “Baba yangu, umetoa neno lako kwaBwana. Nitendee mimi kama vile ulivyoahidi, kwa kuwaBwanaamekupatia ushindi dhidi ya adui zako Waamoni.”

37 Naye akamwambia baba yake, “Naomba nifanyiwe jambo hili. Mimi na nipewe miezi miwili ili kuzunguka vilimani nikaulilie ubikira wangu, mimi na wenzangu.”

38 Baba yake akamwambia, “Waweza kwenda.” Naye akamwacha aende kwa miezi miwili. Hivyo akaondoka pamoja na wasichana wenzake, naye akaulilia ubikira wake huko vilimani kwa sababu asingeolewa kamwe.

39 Baada ya hiyo miezi miwili, alirejea kwa baba yake, naye baba yake akamtendea kama alivyokuwa ametoa nadhiri yake. Naye alikuwa bikira.

Nayo ikawa desturi katika Israeli,

40 kwamba kila mwaka binti za Israeli huenda kwa siku nne ili kumkumbuka huyo binti wa Yefta, Mgileadi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/11-947eb34a84206439b4e00dded81c0313.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 12

Yefta Na Efraimu

1 Watu wa Efraimu wakaita majeshi yao, wakavuka kwenda Zafoni, wakamwambia Yefta, “Kwa nini mmekwenda kupigana na Waamoni bila kutuita ili tuende pamoja nawe? Basi tutaichoma moto nyumba yako, pamoja nawe ukiwa ndani yake.”

2 Yefta akajibu, “Mimi na watu wangu tulikuwa na ugomvi mkubwa na Waamoni, hata ingawa niliwaita hamkuniokoa katika mkono wao.

3 Nilipoona kuwa hamkunipa msaada nikauhatarisha uhai wangu na nikavuka kupigana na Waamoni. NayeBwanaakanipatia ushindi dhidi yao. Sasa kwa nini mnanijia leo ili kupigana nami?”

4 Ndipo Yefta akakusanya watu wa Gileadi pamoja na kupigana na Efraimu. Wagileadi wakawashinda Efraimu, kwa kuwa Waefraimu walisema, “Ninyi Wagileadi ni watoro mliotoroka toka Efraimu na Manase.”

5 Wagileadi wakaviteka vivuko vya Yordani dhidi ya hao Waefraimu, kisha ilikuwa ye yote yule aliyenusurika katika Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao watu wa Gileadi walimwuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Kama alijibu “Hapana,”

6 walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi.’ ” Iwapo alitamka, “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumwua hapo kwenye vivuko vya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo.

7 Yefta akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa muda wa miaka sita. Basi Yefta akafa, akazikwa katika mmojawapo wa miji ya Gileadi.

Ibzani, Eloni Na Abdoni

8 Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli.

9 Alikuwa na wana thelathini na binti thelathini. Akawaoza binti zake kwa watu wengine nje ya ukoo wake, na kuwatwalia wanawe wanawake thelathini toka nje ya ukoo wake. Ibzani akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka saba.

10 Ibzani akafa, akazikwa huko Bethlehemu.

11 Baada yake Eloni, Mzabuloni, akawa mwamuzi wa Israeli, naye akawaamua kwa muda wa miaka kumi.

12 Kisha Eloni akafa, akazikwa katika Aiyaloni, katika nchi ya Zabuloni.

13 Baada yake, Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akawa mwamuzi wa Israeli.

14 Naye akazaa wana arobaini na wana wa wanawe thelathini waliopanda punda sabini. Akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka minane.

15 Ndipo Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, naye akazikwa huko Pirathoni katika Efraimu, katika nchi ya vilima ya Waamaleki.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/12-eced8fea99a75399d83399883fad5bb2.mp3?version_id=1627—

Waamuzi 13

Kuzaliwa Kwa Samsoni

1 Waisraeli wakafanya maovu tena mbele zaBwana. HivyoBwanaakawatia mikononi mwa Wafilisti kwa muda wa miaka arobaini.

2 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Sora, aliyeitwa Manoa, wa kabila la Wadani, naye alikuwa na mke ambaye alikuwa tasa na hakuwa na mtoto.

3 Malaika waBwanaakamtokea huyo mwanamke na kumwambia, “Wewe ni tasa na huna mtoto, lakini utachukua mimba na utamzaa mtoto mwanaume.

4 Lakini ujihadhari sana usinywe mvinyo wala kileo kingine cho chote, wala usile kitu cho chote kilicho najisi,

5 kwa kuwa utachukuwa mimba na utamzaa mtoto mwanaume. Wembe usipite kichwani pake, kwa kuwa huyo mwana atakuwa Mnadhiri wa Mungu, aliyewekwa wakfu kwa ajili ya Mungu tangu tumboni mwa mama yake, naye ataanza kuwakoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti.”

6 Ndipo huyo mwanamke akamwendea mumewe na kumweleza kuwa, “Mtu wa Mungu alinijia. Kule kuonekana kwake kulikuwa kama kwa malaika wa Mungu, wa kutisha sana. Sikumwuliza alikotoka wala hakuniambia jina lake.

7 Lakini aliniambia, ‘Utachukua mimba na utazaa mtoto mwanaume. Basi sasa, usinywe mvinyo wala kileo kingine cho chote wala usile kitu kilicho najisi, kwa kuwa huyo mtoto atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yake mpaka kufa kwake.’ ”

8 Ndipo Manoa akamwombaBwana, akasema: “Ee Bwana, nakusihi, huyo mtu wa Mungu uliyemtuma kwetu aje tena ili atufundishe jinsi ya kumlea huyo mwana atakayezaliwa.”

9 Mungu akamsikia Manoa, naye malaika wa Mungu akamjia tena huyo mwanamke alipokuwa shambani, lakini mumewe Manoa hakuwepo.

10 Basi yule mwanamke akaenda haraka na kumwambia mumewe, “Tazama mtu yule aliyenitokea siku ile yupo hapa!”

11 Manoa akainuka akaandamana na mkewe. Alipomfikia yule mtu akamwuliza, “Je, wewe ndiye yule uliyesema na mke wangu?”

Akasema, “Mimi ndiye.”

12 Basi Manoa akamwuliza “Wakati maneno yako yatakapotimia, masharti ya maisha ya mtoto huyu yatakuwa nini na kazi yake itakuwa ni nini?”

13 Malaika waBwanaakamjibu, “Mke wako hana budi kufanya yale yote niliyomwambia.

14 Kamwe asile kitu cho chote kitakachotoka katika mzabibu, wala asinywe mvinyo wa aina yo yote wala kileo cho chote wala asile kitu cho chote kilicho najisi. Hana budi kufanya kila kitu nilichomwagiza.”

15 Manoa akamjibu yule malaika waBwana, “Twakuomba usubiri kwanza ili tuweze kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako.”

16 Malaika waBwanaakamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula cho chote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtoleeBwanahiyo sadaka.” (Kwa kuwa Manoa hakujua kuwa alikuwa malaika waBwana.)

17 Ndipo Manoa akamwuliza yule malaika waBwana, “Jina lako ni nani, ili kwamba tuweze kukupa heshima hapo hayo uliyonena yatakapotimia?”

18 Akamjibu, “Kwa nini unauliza Jina langu? Ni Jina la ajabu.”

19 Ndipo Manoa akamchukua mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, naye akamtoleaBwanadhabihu hapo juu ya mwamba. Naye yule malaika waBwanaakafanya jambo la ajabu wakati Manoa na mkewe wakiwa wanaangalia:

20 Mwali wa moto kutoka hapo madhabahuni ulipowaka kuelekea mbinguni, malaika waBwanaakapaa ndani ya huo mwali. Manoa na mkewe, kwa kuona jambo hili, wakaanguka chini kifudifudi.

21 Malaika waBwanahakumtokea tena Manoa na mkewe. Ndipo Manoa akatambua kuwa huyo alikuwa malaika waBwana.

22 Manoa akamwambia mkewe, “Hakika tutakufa, kwa kuwa tumemwona Mungu.”

23 Lakini mkewe akamwambia, “IkiwaBwanaalikuwa amekusudia kutuua, asingelipokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya unga kutoka mikononi mwetu, wala asingelituonyesha mambo haya yote wala kututangazia mambo kama haya wakati huu.”

24 Yule mwanamke akazaa mtoto wa kiume akamwita jina lake Samsoni. Kijana akakua, nayeBwanaakambariki.

25 Roho waBwanaakaanza kumsukuma wakati alipokuwa huko Mahane-Dani, kati ya Sora na Eshtaoli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/13-e557ecacc6155f6b16ba1881e68206c8.mp3?version_id=1627—