Yoshua 3

Kuvuka Yordani

1 Yoshua na Waisraeli wote wakaondoka asubuhi na mapema kutoka Shitimu, wakaenda mpaka Mto Yordani, ambako alipiga kambi kabla ya kuvuka.

2 Baada ya siku tatu maafisa wakapita katika kambi yote,

3 wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano laBwanaMungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata.

4 Ndipo mtakapotambua njia mtakayoiendea, kwa kuwa hamjawahi kuipita kabla. Lakini msisogee karibu, bali kuwe na umbali wa dhiraa 2,000kati yenu na Sanduku.”

5 Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “Jitakaseni, kwa kuwa keshoBwanaatatenda mambo ya kushangaza katikati yenu.”

6 Yoshua akawaambia makuhani, “Liinueni Sanduku la Agano mkatangulie mbele ya watu.” Hivyo wakaliinua na kutangulia mbele yao.

7 NdipoBwanaakamwambia Yoshua, “Leo nitaanza kukutukuza machoni pa Israeli yote, ili wapate kujua kuwa niko pamoja nawe kama nilivyokuwa pamoja na Mose.

8 Uwaambie makuhani wanaochukua Sanduku la Agano, ‘Mnapofika kwenye ukingo wa maji ya Yordani, nendeni mkasimame ndani ya mto.’ ”

9 Yoshua akawaambia Waisraeli, “Njoni hapa msikilize maneno yaBwanaMungu wenu.

10 Hivi ndivyo mtakavyojua yakuwa Mungu aliye hai yupo katikati yenu na kwamba kwa hakika atawafukuza mbele yenu hao Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagirgashi, Waamori na Wayebusi.

11 Tazama, Sanduku la Agano laBwanawa dunia yote litaingia ndani ya Mto Yordani likiwa limetangulia.

12 Sasa basi, chagueni watu kumi na wawili kutoka katika makabila ya Israeli, mtu mmoja kutoka kila kabila.

13 Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku laBwana, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yatiririkayo kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”

14 Basi, watu walipovunja kambi ili kuvuka Yordani, makuhani wakiwa wamebeba Sanduku la Agano waliwatangulia.

15 Wakati huu ulikuwa wakati wa mavuno, nao Mto Yordani ulikuwa umefurika hadi kwenye kingo zake. Ilikuwa kawaida ya Yordani kufurika nyakati zote za mavuno. Mara tu makuhani wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Agano walipofika mtoni na nyayo zao kuzama ndani ya yale maji,

16 maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yalitindika yakasimama kama chuguu mbali nao, kwenye mji ulioitwa Adamu karibu na Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalikauka kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.

17 Wale makuhani waliobeba Sanduku la Agano laBwana, wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Mto Yordani, wakati Waisraeli wote wakiwa wanapita hadi taifa lile lote likaisha kuvuka mahali pakavu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/3-5397ecd5553edfe02cd68a4be02ac5c5.mp3?version_id=1627—

Yoshua 4

Ukumbusho Wa Kuvuka Mto Yordani

1 Wakati taifa lote lilipokwisha kuvuka Mto Yordani,Bwanaakamwambia Yoshua,

2 “Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja,

3 nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, pale pale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.”

4 Basi Yoshua akawaita watu kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua kutoka miongoni mwa Waisraeli, kila kabila mtu mmoja,

5 naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku laBwanaMungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli,

6 kuwa kama ishara katikati yenu. Siku zijazo, wakati watoto wenu watakapowauliza, wakisema, ‘Ni nini maana ya mawe haya?’

7 Waambieni kwamba maji ya Mto Yordani yaliyokuwa yakitiririka yalitindika mbele ya Sanduku la Agano laBwana. Wakati lilipovuka Yordani, maji ya Yordani yalitindika. Mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.”

8 Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mawili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na hesabu ya kabila za Waisraeli kamaBwanaalivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini, mahali walipoyatua chini.

9 Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mawili ambayo yalikuwa katikati ya Mto Yordani, mahali pale ambapo miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko mpaka leo.

10 Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani mpaka kila kituBwanaalichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimefanywa na watu, sawasawa na vile Mose alivyokuwa amemwamuru Yoshua! Watu wakafanya haraka kuvuka,

11 na mara tu watu wote walipokwisha kuvuka, Sanduku laBwanana makuhani wakavuka watu wakiwa wanatazama.

12 Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakavuka mbele ya Waisraeli, wakiwa wamevaa silaha, kama Mose alivyowaamuru.

13 Kiasi cha watu arobaini elfu waliojiandaa kwa vita walivuka mbele zaBwanahadi nchi tambarare za Yeriko kwa ajili ya vita.

14 Siku ileBwanaakamtukuza Yoshua mbele ya Waisraeli wote, nao wakamheshimu siku zote za maisha yake, kama vile walivyomheshimu Mose.

15 BasiBwanaakamwambia Yoshua,

16 “Waamuru hao makuhani wanaolibeba Sanduku la Ushuhuda, wapande kutoka ndani ya Mto Yordani.”

17 Kwa hiyo Yoshua akawaamuru hao makuhani akisema, “Pandeni kutoka ndani ya Mto Yordani.”

18 Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano laBwana. Mara walipoiweka miguu yao penye kingo, nje ya mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla.

19 Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza watu walipanda kutoka Yordani na kupiga kambi huko Gilgali, kwenye mpaka wa mashariki ya Yeriko.

20 Yale mawe kumi na mawili ambayo walikuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani, Yoshua akayasimamisha huko Gilgali.

21 Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’

22 Basi waambieni, ‘Israeli walivuka mahali pakavu katika Mto Yordani.’

23 Kwa maanaBwanaMungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka.BwanaMungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka.

24 Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono waBwanani wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumchaBwanaMungu wenu milele.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/4-d9f5b89c563b5a554e45754db341cecc.mp3?version_id=1627—

Yoshua 5

1 Basi wafalme wote wa Waamori magharibi ya Yordani na wafalme wote wa Kanaani waliokuwa kwenye mwambao wa bahari waliposikia jinsiBwanaalivyoukausha Mto Yordani mbele ya Waisraeli hata tulipokwisha kuvuka, mioyo yao ikayeyuka kwa hofu, wala hawakuwa na ujasiri kuwakabili Waisraeli.

Tohara Huko Gilgali

2 Wakati huoBwanaakamwambia Yoshua, “Tengeneza visu vya mawe magumu sana na uwatahiri Waisraeli.”

3 Kwa hiyo Yoshua akatengeneza visu vya mawe magumu sana na kutahiri Waisraeli huko Gibeath-Haaralothi.

4 Hii ndiyo sababu ya kufanya hivyo: Wanaume wote waliotoka Misri, wote wenye umri wa kwenda vitani, walikufa jangwani wakiwa njiani, baada ya kuondoka Misri.

5 Watu wote waliotoka Misri walikuwa wametahiriwa, lakini watu wote waliozaliwa jangwani wakiwa safarini toka Misri walikuwa hawajatahiriwa.

6 Waisraeli walitembea jangwani miaka arobaini mpaka wanaume wote wale waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakati walipoondoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakumtiiBwana. Kwa maanaBwanaalikuwa amewaapia kuwa wasingeweza kuona nchi ambayo alikuwa amewaahidi baba zao kuwapatia, nchi inayotiririka maziwa na asali.

7 Kwa hiyo akawainua wana wao baada yao na hawa ndio hao ambao Yoshua aliwatahiri. Walikuwa hawajatahiriwa bado kwa sababu walikuwa safarini.

8 Baada ya taifa lote kutahiriwa, waliendelea kukaa kambini mpaka walipokuwa wamepona.

9 Bwanaakamwambia Yoshua, “Leo nimeiondoa aibu ya Wamisri kutoka kwenu.” Basi mahali pale pakaitwa Gilgali hadi leo.

10 Jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi, wakiwa kambini huko Gilgali katika tambarare za Yeriko, Waisraeli wakaadhimisha Pasaka.

11 Siku ya pili baada ya Pasaka, katika siku ile ile, wakala mazao ya nchi, mikate isiyotiwa chachu na nafaka za kukaanga.

12 Mana ilikoma siku iliyofuata baada ya Waisraeli kula chakula kilichotoka katika nchi; hapakuwa na mana tena kwa ajili ya Waisraeli, ila mwaka huo walikula mazao ya nchi ya Kanaani.

Amiri Jeshi Wa Jeshi La Bwana

13 Basi wakati Yoshua alipokaribia Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi uliofutwa kwenye ala. Yoshua akamwendea na kumwuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?”

14 Akajibu, “La, siko upande wo wote, lakini mimi nimekujia nikiwa amiri jeshi wa jeshi laBwana.” Yoshua akaanguka kifudifudi hadi nchi, akasujudu, akamwuliza, “Je, Bwana, una ujumbe gani kwa mtumishi wako?”

15 Amiri jeshi wa jeshi laBwanaakajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/5-f82475c36c32977e1ab967abb739570b.mp3?version_id=1627—

Yoshua 6

Yeriko Yatekwa Na Kuangamizwa

1 Basi malango ya Yeriko yalifungwa kwa uthabiti kwa ajili ya Waisraeli. Hakuna mtu ye yote aliyetoka au kuingia.

2 KishaBwanaakamwambia Yoshua, “Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita.

3 Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita.

4 Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya Sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo.

5 Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.”

6 Ndipo Yoshua mwana wa Nuni akaita makuhani na kuwaambia, “Chukueni Sanduku la Agano laBwanana makuhani saba wachukue baragumu za pembe za kondoo waume mbele yake.”

7 Naye akawaagiza watu, “Songeni mbele! Mkazunguke mji, na walinzi wenye silaha watangulie mbele ya Sanduku laBwana.”

8 Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba wenye kuzibeba zile baragumu saba mbele zaBwana, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano laBwanalikawafuata.

9 Walinzi waliokuwa na silaha wakaenda mbele ya hao makuhani waliopiga hizo baragumu na hao walinzi wa nyuma waliokuwa nyuma wakafuata Sanduku. Wakati wote huu baragumu zilikuwa zikipigwa.

10 Bali Yoshua aliwaagiza watu, “Msipige kelele za vita, msipaze sauti zenu, wala kusema neno lo lote mpaka siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!”

11 Basi akalipeleka Sanduku laBwanakuzunguka huo mji, likazungushwa mara moja. Kisha watu wakarudi kambini kulala.

12 Yoshua akaamka mapema asubuhi iliyofuata na makuhani wakalichukua Sanduku laBwana.

13 Makuhani saba wakachukua zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku laBwanawakizipiga hizo baragumu. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao, walinzi waliokuwa nyuma wakalifuata Sanduku laBwana, huku makuhani wakiendelea kuzipiga hizo baragumu.

14 Siku ya pili wakazunguka mji mara moja na kurudi kambini. Wakafanya hivi kwa siku sita.

15 Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakazunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba.

16 Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipopiga baragumu kwa sauti kubwa, Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maanaBwanaamewapa mji huu!

17 Mji huu pamoja na vyote vilivyomo ndani yake utawekwa wakfu kwaBwanakwa kuangamizwa kabisa. Ila Rahabu tu, yaani yule kahaba na wote ambao wako pamoja naye nyumbani mwake ndio watakaosalimishwa, kwa sababu aliwaficha wale wapelelezi tuliowatuma.

18 Lakini mjiepushe na vitu vilivyowekwa wakfu, msije mkachukua cho chote katika hivyo, msije mkajiletea maangamizi katika maskani ya Israeli na kuiletea taabu.

19 Fedha yote na dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwaBwana, lazima viletwe katika hazina.”

20 Wakati baragumu zilipopigwa, watu walipiga kelele, kwa sauti ya baragumu, na watu kupaza sauti, ukuta ukaanguka; hivyo kila mtu akasonga mbele moja kwa moja kutokea pale alipokuwa kutokea kila upande na kuuteka mji.

21 Wakauweka mji wakfu kwaBwana, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, ng’ombe, kondoo na punda.

22 Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani kwa yule kahaba, mleteni pamoja na wote waliomo nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.”

23 Basi wale watu waliofanya upelelezi wakaenda kumleta Rahabu, baba yake na mama yake, ndugu zake na watu wote waliokuwa pamoja naye nyumbani mwake. Akaleta jamaa yake yote na kuwaweka mahali nje karibu na kambi ya Israeli.

24 Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwamo ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba yaBwana.

25 Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu yule kahaba, jamaa yake yote na wote waliokuwa wa kwake, kwa sababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko, naye anaishi miongoni mwa Waisraeli hata leo.

26 Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Alaaniwe mbele zaBwanamtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko:

“Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume

ataweka misingi yake;

kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho

ataweka malango yake.”

27 HivyoBwanaalikuwa pamoja na Yoshua, na sifa zake zikaenea katika nchi ile yote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/6-e652221fd4f29c8ada4b50863aaabe53.mp3?version_id=1627—

Yoshua 7

Dhambi Ya Akani

1 Lakini Waisraeli hawakuwa waaminifu kuhusu vile vitu vilivyowekwa wakfu, Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alivichukua baadhi ya hivyo vitu. Hasira yaBwanaikawaka dhidi ya Israeli.

2 Basi Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko waende Ai, karibu na Beth-Aveni mashariki ya Betheli, akawaambia, “Pandeni mkaipeleleze nchi.” Wakapanda wakaipeleleza Ai.

3 Waliporudi kwa Yoshua, wakasema, “Si lazima watu wote waende kupigana na Ai. Watume watu elfu mbili au tatu wakauteke huo mji. Hakuna sababu ya kuwachosha watu wote, kwa sababu huko kuna watu wachache tu.”

4 Basi wakapanda kama watu elfu tatu tu, lakini wakashambuliwa na watu wa Ai,

5 ambao waliwaua watu kama thelathini na sita miongoni mwao. Wakawafukuza Waisraeli kutoka lango la mji hadi Shebarimu, nao wakawapiga huko kwenye matelemko. Kutokana na hili mioyo ya watu ikayeyuka ikawa kama maji.

6 Ndipo Yoshua akararua mavazi yake, akapomoka kifudifudi mbele ya Sanduku laBwana, akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli wakafanya vivyo hivyo, wakatia mavumbi vichwani mwao.

7 Yoshua akasema, “EeBwanaMwenyezi, kwa nini umewavusha watu hawa ng’ambo ya Yordani ili kututia mikononi mwa Waamori watuangamize? Laiti tungeliridhika kukaa ng’ambo ile nyingine ya Yordani!

8 EeBwana, niseme nini sasa, ikiwa sasa Israeli ameshafukuzwa na adui zake?

9 Wakanaani na watu wengine wa nchi watasikia habari hii, nao watatuzunguka na kutufutilia jina letu duniani. Utafanya nini basi kwa ajili ya jina lako mwenyewe lililo kuu?”

10 Bwanaakamwambia Yoshua, “Simama! Unafanya nini hapo chini kifudifudi?

11 Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka Agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, wameiba, wamesema uongo, wameviweka pamoja na mali zao.

12 Ndiyo sababu Waisraeli hawawezi kusimama dhidi ya adui zao, wanawapa visogo na kukimbia kwa kuwa wanastahili maangamizi. Sitakuwa pamoja nanyi tena mpaka mwangamize kila kitu miongoni mwenu kilichowekwa kwa maangamizi.

13 “Nenda, ukawaweke watu wakfu. Waambie, ‘Jitakaseni mjiandae kwa kesho; kwa sababu hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli: Kwamba kitu kilichowekwa wakfu kipo katikati yenu, Ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu mpaka mtakapokiondoa.

14 “ ‘Asubuhi, mjihudhurishe kabila kwa kabila. Itakuwa kabila lile atakalolitwaaBwanalitakuja mbele ukoo kwa ukoo, ukoo ule atakaotwaaBwanautakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ile atakayoitwaaBwanaitakuja mbele mtu baada ya mtu.

15 Yule atakayekutwa na vitu vilivyowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, pamoja na vitu vyote alivyonavyo. Kwa kuwa amelivunja Agano laBwanana kufanya kitu cha aibu katika Israeli!’ ”

16 Kesho yake asubuhi na mapema Yoshua akawaamuru Israeli kuja mbele kabila kwa kabila, Yuda akatwaliwa.

17 Koo za Yuda zikaja mbele, akawatwaa Wazera. Akaamuru ukoo wa Wazera kuja mbele jamaa kwa jamaa, jamaa ya Zabdi ikatwaliwa.

18 Yoshua akaamuru watu wa jamaa ya Zabdi kuja mbele mtu baada ya mwingine, naye Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, akatwaliwa.

19 Ndipo Yoshua akamwambia Akani, “Mwanangu, umpeBwanautukufu, Mungu wa Israeli, nawe ukiri kwake. Niambie ni nini ulichotenda, wala usinifiche.”

20 Akani akamjibu, “Ni kweli! Nimetenda dhambi dhidi yaBwana, Mungu wa Israeli. Hili ndilo nililofanya:

21 Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbiliza fedha na kabari ya dhahabu uzito wake shekeli hamsini, nikavitamani nami nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.”

22 Kwa hiyo Yoshua akatuma wajumbe, nao wakapiga mbio mpaka hemani, tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, pamoja na ile fedha chini yake.

23 Wakavichukua vile vitu toka mle hemani, wakamletea Yoshua pamoja na wana wa Israeli wote, nao wakavitandaza mbele zaBwana.

24 Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, joho, kabari ya dhahabu, wanawe na binti zake, ng’ombe, punda, kondoo, hema pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori.

25 Yoshua akasema, “Kwa nini umeleta taabu hii juu yetu?Bwanaataleta taabu juu yako leo hii.”

Ndipo Waisraeli wote wakampiga Akani kwa mawe, na baada ya kuwapiga jamaa yake yote kwa mawe, wakawateketeza kwa moto.

26 Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo mpaka leo. NayeBwanaakageuka kutoka katika hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori tangu siku hiyo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/7-87ad2851a37e7a8c3b9aa6549c10bc30.mp3?version_id=1627—

Yoshua 8

Mji Wa Ai Waangamizwa

1 NdipoBwanaakamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usivunjike moyo, chukua jeshi lote la vita uende pamoja nalo kuishambulia Ai. Kwa kuwa nimeshamweka mikononi mwako huyo mfalme wa Ai, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake.

2 Utafanya Ai na mfalme wake kama ulivyofanya kwa mji wa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mnaweza kuchukua mateka yake na mifugo yake, kwa ajili yenu. Weka waviziaji upande wa nyuma ya mji.”

3 Basi Yoshua na jeshi lote wakainuka kushambulia Ai. Akachagua watu mashujaa elfu thelathini walio bora miongoni mwa wapiganaji wake, akawapeleka wakati wa usiku,

4 akiwaagiza: “Sikilizeni kwa makini. Mtavizia nyuma ya mji. Msiende mbali sana na mji. Wote iweni macho.

5 Mimi na watu walio pamoja nami, tutaukabili mji, kisha itakuwa hapo watu watakapotoka nje kupigana nasi, kama walivyofanya hapo kwanza, sisi tutawakimbia.

6 Watatufuatilia mpaka tutakapokuwa tumewavuta waende mbali na mji, kwa kuwa watasema, ‘Wanatukimbia, kama walivyofanya hapo awali.’ Hivyo tutakapowakimbia,

7 ninyi inawapasa mwinuke mtoke huko mafichoni na kuuteka mji.BwanaMungu wenu atautia mkononi mwenu.

8 Mtakapokuwa mmeuteka mji, uteketezeni kwa moto. Fanyeni kama vileBwanaalivyoamuru. Angalieni, nimewaagiza.”

9 Ndipo Yoshua akawatuma watu, nao wakaenda mahali pa kujificha, wakawa wanavizia kati ya Betheli na Ai, kuelekea upande wa magharibi wa Ai, lakini Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku huo.

10 Yoshua akaamka asubuhi na mapema siku ya pili, akawakutanisha watu wake, yeye na viongozi wa Israeli wakawa mbele ya watu kwenda Ai.

11 Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda, wakakaribia na kufika mbele ya mji. Wakapiga kambi kaskazini ya Ai, pakiwa na bonde kati yao na huo mji.

12 Yoshua alikuwa amewachukua watu wapatao elfu tano, akawaweka mafichoni kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa mji.

13 Wakawaweka askari katika maeneo yao: wale wote waliokuwa kambini wakawa kaskazini ya mji na wale waliokuwa wamejificha wakawa upande wa magharibi. Usiku huo Yoshua akaenda katika lile bonde.

14 Mfalme wa Ai alipoona jambo hili, yeye pamoja na watu wote wa mji wakatoka nje kwa haraka asubuhi na mapema, ili kukutana na Israeli katika vita mahali fulani panapotazamana na Araba. Lakini hakujua kwamba kulikuwa kumewekwa waviziaji dhidi yake nyuma ya mji.

15 Yoshua na Israeli wote wakaruhusu kurudishwa nyuma mbele yao, wakakimbia kuelekea jangwani.

16 Watu wote wa Ai wakaitwa ili kuwafuatia, nao wakavutwa kumfuatia Yoshua mbali na mji.

17 Hakuna hata mwanaume mmoja aliyebakia Ai wala Betheli ambaye hakufuatia Israeli. Wakauacha mji wazi na kuwafuatia Israeli.

18 NdipoBwanaakamwambia Yoshua, “Inua huo mkuki ulio mkononi mwako kuuelekeza Ai, kwa kuwa nitautia huo mji mkononi mwako.” Hivyo Yoshua akauelekeza mkuki wake Ai.

19 Mara tu alipofanya hivi, wale watu waliokuwa mafichoni wakaondoka upesi kutoka mahali pao na kukimbilia mbele. Wakaingia ndani ya mji, wakauteka na kuutia moto kwa haraka.

20 Watu wa Ai wakaangalia nyuma wakauona moshi wa huo mji ukielekea angani, lakini hawakuwa na nafasi ya kutoroka kwa upande wo wote, kwa kuwa wale Waisraeli waliokuwa wanawakimbia kuelekea jangwani walikuwa wamegeuka nyuma kuwakabili hao waliokuwa wakiwafuatia.

21 Basi Yoshua na Israeli wote walipoona kwamba waviziaji wameshauteka mji na moshi ulikuwa unapaa juu kutoka kwenye mji, wakawageukia watu wa Ai na kuwashambulia.

22 Wale waviziaji nao wakatoka nje ya mji dhidi yao kuwashambulia kwa nyuma, hivyo watu wa Ai wakashikiwa katikati, Waisraeli wakiwa pande zote mbili. Israeli wakawaua, bila kuwaachia ye yote aliyenusurika wala aliyetoroka.

23 Lakini wakamchukua mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua.

24 Waisraeli walipomaliza kuwaua wanaume wote wa Ai katika mashamba na jangwani walipokuwa wamewafukuzia, baada ya kila mmoja wao kuuawa kwa upanga, Waisraeli wote wakarudi Ai na kuwaua wale waliokuwa wamebakia mjini.

25 Watu kumi na mbili elfu, waume kwa wake, waliangamia siku ile, yaani watu wote wa Ai.

26 Kwa maana Yoshua hakuurudisha ule mkono wake uliokuwa ameinua mkuki hadi alipomaliza kuwaangamiza wote walioishi huko Ai.

27 Lakini Israeli wakajichukulia mifugo na nyara za mji huu, kama vileBwanaalivyokuwa amemwagiza Yoshua.

28 Kwa hiyo Yoshua akauchoma moto mji wa Ai na kuufanya kuwa rundo la kudumu la magofu, mahali pa ukiwa hadi leo.

29 Akamwangika mfalme wa Ai kwenye mti na kumwacha hapo mpaka jioni. Wakati wa jua kutua, Yoshua akawaamuru wautoe mwili wake kwenye mti na kuutupa kwenye ingilio la lango la mji. Kisha wakarundika mawe makubwa mengi juu yake, ambayo yamesalia huko mpaka leo.

Agano Linafanywa Upya Katika Mlima Ebali

30 Kisha Yoshua akajenga madhabahu yaBwana, Mungu wa Israeli, katika Mlima wa Ebali,

31 kama Mose mtumishi waBwanaalivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Mose: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtoleaBwanasadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.

32 Huko, mbele ya Waisraeli wote, Yoshua akanakili juu ya hayo mawe sheria ya Mose, aliyokuwa ameiandika.

33 Israeli wote, wageni na wazawa sawasawa, wazee wao, maafisa wao na waamuzi, walikuwa wamesimama pande zote mbili za hilo Sanduku la Agano laBwana, wakiwaelekea wale waliokuwa wamelichukua, yaani makuhani, ambao ni Walawi. Nusu ya watu walisimama mbele ya mlima wa Gerizimu na nusu yao walisimama mbele ya mlima wa Ebali, kama vile Mose mtumishi waBwanaalivyokuwa amewaagiza hapo mwanzo alipowapa maagizo ili kuwabariki watu wa Israeli.

34 Hatimaye, Yoshua akasoma maneno yote ya sheria, yaani baraka na laana, kama vile ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati.

35 Hakuna neno lo lote katika yale yote ambayo Mose alikuwa ameamuru ambalo Yoshua hakulisomea kusanyiko lote la Israeli, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, na wageni walioishi miongoni mwao.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/8-888fc29b36b2726d2a6d12efa3c361db.mp3?version_id=1627—

Yoshua 9

Udanganyifu Wa Wagibeoni

1 Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi ya Yordani waliposikia juu ya haya yote, wale waliokuwa katika nchi ya vilima, upande wa magharibi mwa vilima na katika pwani yote ya hiyo Bahari Kuu, hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi),

2 wakajiunga pamoja ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli.

3 Hata hivyo, watu wa Gibeoni waliposikia juu ya hayo yote Yoshua aliyowatendea watu wa Yeriko na Ai,

4 nao wakaamua kufanya hila: Wakaenda kama wajumbe wakiwa na punda waliobebeshwa mizigo wakiwa na magunia yaliyochakaa na vibuyu vikuukuu vya mvinyo vilivyochakaa, vyenye nyufa zilizozibwa.

5 Walivaa viatu vilivyoraruka na kushonwa na nguo kuukuu, chakula chao kilikuwa mkate uliokauka na kuingia koga.

6 Ndipo wakamwendea Yoshua kambini huko Gilgali wakamwambia yeye pamoja na watu wa Israeli, “Tumetoka katika nchi ya mbali, fanyeni mkataba nasi.”

7 Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahiti, “Lakini huenda mnakaa karibu nasi, twawezaje basi kufanya mapatano nanyi?”

8 Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.”

Yoshua akawauliza, “Ninyi ni nani, nanyi mnatoka wapi?”

9 Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu waBwanaMungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri,

10 pia yale yote aliyowatendea wafalme wawili wa Waamori mashariki ya Yordani, huyo Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani, aliyetawala huko Ashtarothi.

11 Basi wazee wetu na wale wote wanaoishi katika nchi yetu walituambia, ‘Chukueni chakula cha safari, mkakutane na watu hao na kuwaambia, “Sisi tu watumishi wenu, fanyeni mapatano nasi.” ’

12 Mkate huu ulikuwa wa moto tulipoufunga siku tulipoanza safari kuja kwenu, lakini sasa angalia jinsi ulivyokauka na kuota ukungu.

13 Viriba hivi vya mvinyo vilikuwa vipya tulipovijaza, lakini ona jinsi vilivyo na nyufa. Nguo zetu na viatu vimechakaa kwa ajili ya safari ndefu.”

14 Basi watu wa Israeli wakapokea vyakula vyao na kuvikagua bila kutaka shauri kutoka kwaBwana.

15 Ndipo Yoshua akafanya mapatano ya amani pamoja nao kuwaacha waishi, nao viongozi wa kusanyiko wakathibitisha kwa kiapo.

16 Siku ya tatu baada ya kufanya mapatano na Wagibeoni, Waisraeli wakapata habari kuwa hao watu ni jirani zao.

17 Ndipo wana wa Israeli wakasafiri na siku ya tatu wakafika kwenye miji yao ya Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-Yearimu.

18 Lakini Waisraeli hawakuwashambulia kwa kuwa viongozi wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwaBwana, Mungu wa Israeli.

Kusanyiko lote likanung’unika dhidi ya hao viongozi,

19 lakini viongozi wote wakawajibu, “Tumeshawaapia kwaBwana, Mungu wa Israeli, kwa hiyo hatuwezi kuwagusa sasa.

20 Hivi ndivyo tutakavyowafanyia: Tutawaacha waishi, ili ghadhabu isije juu yetu kwa kuvunja kiapo tulichowaapia.”

21 Wakaendelea kusema, “Waacheni waishi, lakini wawe wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii yote.” Hivyo ahadi waliyoweka viongozi ikawa hivyo.

22 Kisha Yoshua akawaita Wagibeoni na kuwaambia, “Kwa nini mmetudanganya kwa kutuambia, ‘Tunaishi mbali nanyi,’ wakati ambapo ninyi mnaishi karibu nasi?

23 Sasa mko chini ya laana: Daima mtakuwa wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.”

24 Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsiBwanaMungu wenu alivyomwamuru mtumishi wake Mose kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwafutilia mbali wakazi wake wote mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili.

25 Sasa tupo mikononi mwenu. Tufanyieni lo lote mnaloona kuwa jema na haki.”

26 Kwa hiyo Yoshua akawaokoa mikononi mwa Waisraeli, nao hawakuuawa.

27 Kuanzia siku hiyo akawafanya Wagibeoni wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii nzima na kwa ajili ya madhabahu yaBwanamahali pale ambapoBwanaangepachagua. Hivyo ndivyo walivyo mpaka hivi leo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/9-0f1cbae0ff7abb24c7b0f4ec185fa036.mp3?version_id=1627—

Yoshua 10

Jua Linasimama

1 Baada ya haya Adoni-Sedeki mfalme wa Yerusalemu alisikia kuwa Yoshua alikuwa ameteka mji wa Ai na kuuharibu kabisa, tena alikuwa ameua mfalme wake, kama alivyofanya huko Yeriko na mfalme wake, tena ya kuwa watu wa Gibeoni wamefanya mapatano ya amani na Waisraeli, tena ya kwamba walikuwa wakiishi karibu yao.

2 Yeye na watu wake wakataharuki mno kwa kuwa Gibeoni ulikuwa mji mkubwa kama mmojawapo ya miji ya kifalme; ulikuwa mkubwa kuliko Ai, nao watu wake wote walikuwa mashujaa wa vita.

3 Hivyo Adoni-Sedeki mfalme wa Yerusalemu akaomba msaada kwa Hohamu mfalme wa Hebroni, Piramu mfalme wa Yarmuthi, Yafia mfalme wa Lakishi, na Debiri mfalme wa Egloni.

4 Akawaambia, “Njoni mnisaidie kuipiga Gibeoni, kwa sababu imefanya mapatano ya amani na Yoshua pamoja na Waisraeli.”

5 Ndipo hao wafalme watano wa Waamori, ambao ni wafalme wa Yerusalemu, Hebroni, Yarmuthi, Lakishi na Egloni, wakaunganisha majeshi yao. Wakapanda na vikosi vyao vyote, nao wakajipanga dhidi ya Gibeoni na kuishambulia.

6 Nao Wagibeoni wakatuma ujumbe kwa Yoshua kwenye kambi ya Gilgali na kumwambia, “Usiwaache watumishi wako. Panda haraka uje kwetu kutuokoa! Tusaidie, kwa sababu wafalme wote wa Waamori wakaao kwenye nchi ya vilima wameunganisha majeshi yao pamoja dhidi yetu.”

7 Basi Yoshua akaondoka Gilgali pamoja na jeshi lake lote, wakiwepo watu wote mashujaa wa vita.

8 Bwanaakamwambia Yoshua, “Usiwaogope watu hao, nimewatia mkononi mwako. Hakuna ye yote atakayeweza kushindana nawe.”

9 Baada ya Yoshua kutembea usiku kucha kutoka Gilgali, Yoshua akawashambulia kwa ghafula.

10 Bwanaakawatia hofu ya ghafula na kuwafadhaisha mbele ya Waisraeli, nao wakawashinda kwa ushindi mkuu huko Gibeoni. Israeli wakawafukuza kuelekea njia iendayo Beth-Horoni wakiwaua mpaka kufikia njia iendayo Azeka hadi Makeda.

11 Walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli kwenye barabara itelemkayo kutoka Beth-Horoni hadi Azeka,Bwanaakawavumishia mawe makubwa ya mvua kutoka mbinguni, nao wengi wao wakauawa na hayo mawe kuliko wale waliouawa kwa upanga wa Waisraeli.

12 Katika siku ile ambayoBwanaaliwatia Waamori mikononi mwa Israeli, Yoshua akasema naBwanambele ya Waisraeli:

“Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni,

wewe mwezi, simama

katika Bonde la Aiyaloni.”

13 Hivyo jua likasimama kimya,

nao mwezi ukatulia,

hadi Waisraeli walipokwisha

kujipatilizia kwa adui zao,

kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari.

Jua likasimama katikati ya mbingu kimya, likachelewa kuzama muda wa siku moja nzima.

14 Haijakuwepo siku nyingine mfano wa hiyo kabla au baada, siku ambayoBwanaalimsikiliza mwanadamu. HakikaBwanaalikuwa akiwapigania Israeli.

15 Ndipo Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Waisraeli wote.

Wafalme Watano Wa Waamori Wauawa

16 Basi wale wafalme watano wakawa wamekimbia kujificha kwenye pango huko Makeda.

17 Yoshua alipoambiwa kuwa wafalme hao watano wamekutwa wakiwa wamejificha ndani ya pango huko Makeda,

18 akasema, “Vingirisheni mawe makubwa kwenye mdomo wa hilo pango, tena wekeni walinzi wa kulilinda.

19 Lakini msiwaache! Wafuatieni adui zenu, washambulieni walio nyuma, wala msiwaache wafike kwenye miji yao, kwa kuwaBwanaMungu wenu amewatia mikononi mwenu.”

20 Hivyo Yoshua pamoja na Waisraeli wakawaangamiza kabisa karibu wote, lakini wachache waliosalia ndio waliofika kwenye miji yao yenye maboma.

21 Jeshi lote likarudi salama kwa Yoshua huko kambini Makeda, hakuna ye yote aliyetoa neno kinyume cha Waisraeli.

22 Ndipo Yoshua akasema, “Haya fungueni mdomo wa pango, mniletee hao wafalme watano.”

23 Kwa hiyo wakawatoa hao wafalme watano nje ya pango: wafalme wa Yerusalemu, Hebroni, Yarmuthi, Lakishi na Egloni.

24 Baada ya kuwaleta kwa Yoshua, akawaita watu wote wa Israeli, na kuwaambia majemadari wa vita waliokwenda pamoja naye, “Njoni hapa mweke nyayo zenu juu ya shingo za hawa wafalme.” Basi wakaja wakawakanyaga shingoni.

25 Yoshua akawaambia, “Msiogope, wala msivunjike moyo. Iweni hodari na wenye moyo mkuu. Hili ndiloBwanaatakalowatendea adui zenu wote mnaokwenda kupigana nao.”

26 Ndipo Yoshua akawapiga na kuwaua wale wafalme na kuwatundika juu ya miti mitano, nao wakaachwa wananing’inia juu ya ile miti hadi jioni.

27 Wakati wa kuzama jua Yoshua akaamuru wawashushe kutoka kwenye ile miti na kuwatupa kwenye lile pango ambalo walikuwa wamejificha. Kwenye mdomo wa lile pango wakaweka mawe makubwa, ambayo yapo hadi leo.

28 Siku ile Yoshua akateka Makeda. Akamwua mfalme na kumwangamiza kila mtu aliyekuwa ndani yake kwa upanga. Hakubakiza mtu ye yote. Akamfanyia mfalme wa Makeda kama vile alivyokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.

Israeli Yaangamiza Miji Ya Kusini

29 Ndipo Yoshua akaondoka Makeda akiwa pamoja na Israeli wote mpaka mji wa Libna na kuushambulia.

30 Bwanapia akautia mji wa Libna pamoja na mfalme wake mikononi mwa Israeli. Yoshua akaangamiza ule mji na kila mtu aliyekuwa ndani yake kwa upanga. Hakubakiza huko mtu ye yote. Akamfanyia mfalme wa Libna kama alivyokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.

31 Kisha Yoshua akaondoka Libna kwenda Lakishi akiwa pamoja na Israeli wote, wakajipanga dhidi yake na kuushambulia.

32 Bwanaakautia Lakishi mikononi mwa Israeli, Yoshua akauteka siku ya pili. Yoshua akauangamiza mji na kila kilicho ndani yake kwa upanga, kama vile alivyokuwa ameufanyia mji wa Libna.

33 Wakati huo huo, Horamu mfalme wa Gezeri alikuwa amepanda ili kusaidia Lakishi, lakini Yoshua akamshinda yeye pamoja na jeshi lake, hadi alipowaangamiza wote.

34 Ndipo Yoshua akaondoka Lakishi kwenda Egloni akiwa pamoja na Israeli wote, wakajipanga dhidi yake na kuushambulia.

35 Wakauteka mji siku ile ile, wakaupiga kwa upanga na kumwangamiza kila mmoja aliyekuwa ndani yake, kama vile walivyokuwa wameufanyia Lakishi.

36 Kisha Yoshua akapanda kutoka Egloni kwenda Hebroni akiwa pamoja na Israeli wote na kuushambulia.

37 Wakauteka mji na kuupiga kwa upanga, pamoja na mfalme wake, vijiji vyake na kila mmoja aliyekuwa ndani yake. Hawakubakiza huko mtu ye yote kama vile huko Egloni, waliuangamiza kabisa pamoja na kila mmoja aliyekuwa ndani yake.

38 Ndipo Yoshua na Israeli wote wakageuka na kuushambulia Debiri.

39 Wakauteka mji, mfalme wake na vijiji vyake, na kuupiga kwa upanga. Kila mmoja aliyekuwa ndani yake wakamwangamiza kabisa. Hawakubakiza huko mtu ye yote. Wakaufanyia Debiri na mfalme wake kama vile walivyokuwa wameifanyia miji ya Libna na Hebroni na wafalme wao.

40 Hivyo Yoshua akashinda eneo hilo lote, ikiwa ni pamoja na nchi ya vilima, Negebu, sehemu ya magharibi chini ya vilima, matelemko ya milima, pamoja na wafalme wake wote. Hakubakiza humo mtu ye yote. Akaangamiza kabisa kila kitu chenye pumzi, kama vileBwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa ameamuru.

41 Yoshua akawashinda kuanzia Kadesh-Barnea hadi Gaza na kutoka eneo lote la Gosheni hadi Gibeoni.

42 Wafalme hawa wote pamoja na nchi zao Yoshua aliwashinda kwa wakati mmoja, kwa sababuBwana, Mungu wa Israeli, aliwapigania Israeli.

43 Ndipo Yoshua akarudi pamoja na Israeli wote kwenye kambi huko Gilgali.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/10-68bdea27562199370265f495a92a890d.mp3?version_id=1627—

Yoshua 11

Wafalme Wa Kaskazini Washindwa

1 Ikawa Yabini mfalme wa Hazori aliposikia habari za mambo haya, akatuma ujumbe kwa Yobabu mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu,

2 na pia kwa wafalme wa upande wa kaskazini wale waliokuwa milimani, katika Araba upande wa kusini mwa Kinerethi, nchi chini ya vilima upande wa magharibi na katika miinuko ya Nafoth-Dori upande wa magharibi;

3 kwa Wakanaani upande wa mashariki na magharibi; kwa Waamori, Wahiti, Waperizi na Wayebusi katika nchi ya vilima; na kwa Wahivi chini ya Hermoni katika nchi ya Mispa.

4 Wakaja na vikosi vyao vyote na hesabu kubwa ya magari ya kuvutwa na farasi, jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari.

5 Wafalme hao wote wakaunganisha majeshi yao na kupiga kambi pamoja penye Maji ya Meromu, ili kupigana dhidi ya Israeli.

6 Bwanaakamwambia Yoshua, “Usiwaogope, kwa sababu kesho saa kama hii nitawatia wote mikononi mwa Israeli, wakiwa wameuawa. Utakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuyachoma moto magari yao.”

7 Hivyo Yoshua pamoja na jeshi lake lote wakaja dhidi yao ghafula na kwenye maji ya Meromu kuwashambulia,

8 nayeBwanaakawatia mikononi mwa Israeli. Wakawashinda na kuwafukuza hadi Sidoni Kuu na kuwafikisha Misrefoth-Maimu, hadi Bonde la Mispa upande wa mashariki, hadi pakawa hakuna ye yote aliyebaki.

9 Yoshua akawatendea kamaBwanaalivyomwamuru. Akakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuchoma moto magari yao.

10 Wakati huo Yoshua akarudi kuuteka mji wa Hazori na kumwua mfalme wake kwa upanga. (Hazori ulikuwa mji mkuu wa falme hizo zote.)

11 Kila aliyekuwa ndani yake wakamwua kwa upanga. Wakawaangamiza kabisa, wala hawakusaza cho chote chenye pumzi na akauchoma Hazori kwa moto.

12 Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake na kuwapiga kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, kama Mose mtumishi waBwanaalivyowaagiza.

13 Lakini Israeli hawakuichoma moto hata mojawapo ya miji hiyo iliyojengwa katika vilima vya hao wafalme, isipokuwa mji wa Hazori ambao Yoshua aliuchoma moto.

14 Waisraeli wakajichukulia nyara zote na mifugo yote ya miji hii, bali waliwaua watu wote kwa upanga hadi walipowaangamiza kabisa, wala hawakumbakiza ye yote mwenye pumzi.

15 Kama vileBwanaalivyomwagiza Mose mtumishi wake, vivyo hivyo Mose alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya kama vile alivyoagizwa, akafanya yote kwa uangalifu kama vileBwanaalivyomwagiza Mose.

16 Yoshua akaiteka nchi hii yote: nchi ya vilima, Negebu yote, nchi yote ya Gosheni, nchi chini ya vilima upande wa magharibi, Araba na milima ya Israeli pamoja na nchi chini ya vilima,

17 kuanzia Mlima Halaki ambao umeinuka kuelekea Seiri hadi Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni chini ya Mlima Hermoni. Akawateka wafalme wake wote akawapiga na kuwaua.

18 Yoshua akapigana vita dhidi ya wafalme hawa wote kwa muda mrefu.

19 Hakuna ye yote katika eneo hili aliyetafuta amani na Israeli, isipokuwa hao Wahivi wa Gibeoni. Wengine wote walishindwa.

20 Kwa maana niBwanamwenyewe ambaye aliifanya mioyo yao iwe migumu ili kupigana vita dhidi ya Israeli ili kwamba apate kuwafutilia mbali, pasipo huruma, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

21 Wakati huo Yoshua akaenda kuwaangamiza Waanaki kutoka katika nchi ya vilima: kuanzia Hebroni, Debiri na Anabu, na kutoka katika nchi yote ya milima ya Yuda na kutoka katika nchi yote ya milima ya Israeli. Yoshua akawaangamiza kabisa pamoja na miji yao.

22 Hawakubaki Waanaki wo wote katika nchi ya Israeli, ila katika nchi ya Gaza, Gathi na Ashdodi.

23 Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kamaBwanaalivyokuwa amemwagiza Mose, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kama walivyogawanyika katika kabila zao.

Ndipo nchi ikawa na amani bila vita.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/11-44f48cbc598a191263d3d4c5cedd50e3.mp3?version_id=1627—

Yoshua 12

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli walikuwa wamewashinda na kutawala nchi yao upande wa mashariki ya Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

2 Sihoni mfalme wa Waamori,

ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ni pamoja na nusu ya Gileadi.

3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethihadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya matelemko ya Pisga.

4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani,

aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa Wageshuri, Wamaaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

6 Mose mtumishi waBwanana Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi waBwanaakawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi wa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ulioelekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:

8 nchi ya vilima, nchi chini ya vilima, upande wa magharibi, Araba, matelemko ya mlima, jangwa, na Negebu; watu waliokuwa wanaishi katika maeneo haya walikuwa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

9 mfalme wa Yeriko mmoja
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
10 mfalme wa Yerusalemu mmoja
mfalme wa Hebroni mmoja
11 mfalme wa Yarmuthi mmoja
mfalme wa Lakishi mmoja
12 mfalme wa Egloni mmoja
mfalme wa Gezeri mmoja
13 mfalme wa Debiri mmoja
mfalme wa Gederi mmoja
14 mfalme wa Horma mmoja
mfalme wa Aradi mmoja
15 mfalme wa Libna mmoja
mfalme wa Adulamu mmoja
16 mfalme wa Makeda mmoja
mfalme wa Betheli mmoja
17 mfalme wa Tapua mmoja
mfalme wa Heferi mmoja
18 mfalme wa Afeki mmoja
mfalme wa Lasharoni mmoja
19 mfalme wa Madoni mmoja
mfalme wa Hazori mmoja
20 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja
mfalme wa Akshafu mmoja
21 mfalme wa Taanaki mmoja
mfalme wa Megido mmoja
22 mfalme wa Kedeshi mmoja
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmoja
mfalme wa Goyimu katika Gilgali mmoja
24 mfalme wa Tirsa mmoja

wafalme jumla yao walikuwa thelathini na mmoja.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/12-5bf2afa85a57ccb197a19202e87d79aa.mp3?version_id=1627—