Yoshua 12

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli walikuwa wamewashinda na kutawala nchi yao upande wa mashariki ya Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

2 Sihoni mfalme wa Waamori,

ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ni pamoja na nusu ya Gileadi.

3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethihadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya matelemko ya Pisga.

4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani,

aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa Wageshuri, Wamaaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

6 Mose mtumishi waBwanana Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi waBwanaakawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi wa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ulioelekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:

8 nchi ya vilima, nchi chini ya vilima, upande wa magharibi, Araba, matelemko ya mlima, jangwa, na Negebu; watu waliokuwa wanaishi katika maeneo haya walikuwa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

9 mfalme wa Yeriko mmoja
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
10 mfalme wa Yerusalemu mmoja
mfalme wa Hebroni mmoja
11 mfalme wa Yarmuthi mmoja
mfalme wa Lakishi mmoja
12 mfalme wa Egloni mmoja
mfalme wa Gezeri mmoja
13 mfalme wa Debiri mmoja
mfalme wa Gederi mmoja
14 mfalme wa Horma mmoja
mfalme wa Aradi mmoja
15 mfalme wa Libna mmoja
mfalme wa Adulamu mmoja
16 mfalme wa Makeda mmoja
mfalme wa Betheli mmoja
17 mfalme wa Tapua mmoja
mfalme wa Heferi mmoja
18 mfalme wa Afeki mmoja
mfalme wa Lasharoni mmoja
19 mfalme wa Madoni mmoja
mfalme wa Hazori mmoja
20 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja
mfalme wa Akshafu mmoja
21 mfalme wa Taanaki mmoja
mfalme wa Megido mmoja
22 mfalme wa Kedeshi mmoja
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmoja
mfalme wa Goyimu katika Gilgali mmoja
24 mfalme wa Tirsa mmoja

wafalme jumla yao walikuwa thelathini na mmoja.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/12-5bf2afa85a57ccb197a19202e87d79aa.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 − 17 =