Zaburi 1

Furaha Ya Kweli 1 Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi au kuketi katika baraza la wenye mizaha. 2 Bali huifurahia sheria yaBwana, naye huitafakari hiyo sheria mchana na usiku. 3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda […]

Zaburi 2

Mfalme Aliyechaguliwa Na Mungu 1 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na mataifa kula njama bure? 2 Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi yaBwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. 3 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” 4 Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. 5 Kisha huwakemea katika hasira […]

Zaburi 3

Sala Ya Asubuhi Ya Kuomba Msaada (Zaburi Ya Daudi Alipomkimbia Absalomu) 1 EeBwana, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu! 2 Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” 3 Lakini wewe, EeBwana, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. 4 NinamliliaBwanakwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka katika mlima […]

Zaburi 4

Sala Ya Jioni Ya Kuomba Msaada (Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Muziki. Zaburi Ya Daudi) 1 Unijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Unipumzishe katika shida zangu, nirehemu, usikie ombi langu. 2 Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu mpaka lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo mpaka lini? 3 Fahamuni hakika […]

Zaburi 5

Sala Kwa Ajili Ya Ulinzi Wakati Wa Hatari (Kwa Mwimbishaji: Kwa Filimbi. Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. 2 Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba. 3 Asubuhi, unasikia sauti yangu, EeBwana; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa […]

Zaburi 6

Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu (Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Muziki. Mtindo Wa Sheminithi # . Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. 2 UnirehemuBwana, kwa maana nimedhoofika; EeBwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali. 3 Nafsi yangu ina uchungu mwingi. […]

Zaburi 7

Sala Ya Mtu Anayedhulumiwa (Ombolezo La Daudi Kwa Mungu Kwa Sababu Ya Kushi, Mbenyamini) 1 EeBwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia, 2 la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande asiwepo wa kuniokoa. 3 EeBwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu, 4 au ikiwa nimetenda […]

Zaburi 8

Utukufu Wa Mungu Na Heshima Ya Mwanadamu (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu. 2 Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeweka sifa, kwa sababu ya watesi wako, kuwanyamazisha adui na mlipiza kisasi. 3 Nikiziangalia mbingu […]

Zaburi 9

Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Muth-Labeni # . Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. 2 Nitafurahi na kushangilia katika wewe, nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. 3 Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako. […]

Zaburi 10

Sala Kwa Ajili Ya Haki 1 Kwa nini, EeBwana, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida? 2 Katika kiburi chake mtu mwovu humtesa mtu aliye maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. 3 Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukanaBwana. 4 Katika kiburi chake mtu mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote […]