Marko 1

Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji 1 Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele yako, yeye atakayeitengeneza njia yako”: 3 “sauti ya mtu aliaye nyikani. ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake.’ ” 4 Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa […]

Marko 2

Yesu Amponya Mtu Aliyepooza 1 Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba amerudi nyumbani. 2 Hivyo watu wengi wakakusanyika kiasi kwamba hapakubaki nafasi yo yote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno. 3 Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. 4 Kwa kuwa walikuwa hawawezi kumfikisha kwa […]

Marko 3

Yesu Amponya Mtu Mwenye Mkono Uliopooza 1 Yesu akaingia tena ndani ya sinagogi na huko palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza. 2 Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. 3 Yesu akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele.” 4 Kisha Yesu akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku […]

Marko 4

Mfano Wa Mpanzi 1 Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umemkusanyikia na kumzunguka ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo. 2 Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema: 3 “Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. 4 Alipokuwa akipanda, mbegu […]

Marko 5

Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo 1 Wakafika upande wa pili wa bahari wakaingia katika nchi ya Wagerasi. 2 Yesu alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini akakutana naye. 3 Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo, 4 kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa kwa minyororo […]

Marko 6

Nabii Hana Heshima Kwao 1 Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake. 2 Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia wakashangaa. Wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! […]

Marko 7

Kilicho Safi Na Kilicho Najisi 1 Mafarisayo na baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu wakakusanyika mbele ya Yesu. 2 Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani, bila kunawa kama ilivyotakiwa na sheria ya dini ya Wayahudi. 3 Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa […]

Marko 8

Yesu Alisha Watu 4,000 1 Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, 2 “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula. 3 Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao […]

Marko 9

1 Yesu akaendelea kuwaambia, “Amin, amin nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija katika nguvu.” Yesu Ageuka Sura 2 Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. 3 Mavazi yake yakawa […]

Marko 10

Mafundisho Kuhusu Talaka 1 Yesu akaondoka huko akavuka Mto wa Yordani, akaenda sehemu ya Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukamjia tena na kama ilivyokuwa desturi yake akawafundisha. 2 Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumwuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?” 3 Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru nini?” 4 Wakajibu, “Mose aliruhusu kwamba […]