Malaki 1

1 Ujumbe: Neno laBwanakwa Israeli kupitia kwa Malaki. Yakobo Alipendwa, Esau Alichukiwa 2 Bwanaasema, “Nimewapenda ninyi.” “Lakini ninyi mnauliza, ‘Wewe umetupendaje?’ ” Bwanaasema, “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo, 3 lakini nikamchukia Esau, nami nimeifanya milima yake kuwa ukiwa na urithi wake nimewapa mbweha wa jangwani.” 4 Edomu anaweza kusema, “Ingawa […]

Malaki 2

Onyo Kwa Makuhani 1 “Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, Enyi makuhani. 2 Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote. 3 “Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka […]

Malaki 3

1 “Angalieni, nitamtuma mjumbe wangu, atakayeiandaa njia mbele yangu. Ndipo ghafula Bwana mnayemtafuta atakuja hekaluni mwake. Mjumbe wa Agano, ambaye mnamwonea shauku, atakuja,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. 2 Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye […]

Malaki 4

Siku Ya Bwana 1 “Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. 2 Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake. Nanyi mtatoka nje na […]