1 Petro 1

Salamu 1 Petro, mtume wa Yesu Kristo: Kwa wateule wa Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia. 2 Ninawaandikia ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kwa kazi ya utakaso wa Roho, katika utii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo: Neema iwe nanyi na […]

1 Petro 2

Jiwe Lililo Hai Na Watu Waliochaguliwa 1 Kwa hiyo, wekeni mbali nanyi uovu wote na udanganyifu wote, unafiki, wivu na masingizio ya kila namna. 2 Kama watoto wachanga, waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya kiroho yasiyochanganywa na kitu kingine cho chote, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu, 3 ikiwa kweli mmeonja ya kwamba Bwana ni mwema. […]

1 Petro 3

Mafundisho Kwa Wake Na Waume 1 Kadhalika enyi wake, watiini waume zenu, ili kama wako wasioamini lile neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno, 2 kwa kuuona utakatifu na uchaji wa Mungu katika maisha yenu. 3 Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na […]

1 Petro 4

Kuishi Kwa Ajili Ya Mungu 1 Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni nia iyo hiyo kwa maana mtu aliyekwisha kuteswa katika mwili ameachana na dhambi. 2 Matokeo yake, maisha yake yaliyobaki ya kuishi hapa duniani, haishi tena kwa kufuata tamaa mbaya za wanadamu, bali anaishi kwa kufuata mapenzi ya […]

1 Petro 5

Kulichunga Kundi La Mungu 1 Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa, 2 lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe, si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika. […]