Matendo 1

Ahadi Ya Roho Mtakatifu 1 Katika kitabu changu cha kwanza nilikuandikia mpendwa Theofilo, kuhusu mambo yote Yesu aliyofanya na kufundisha tangu mwanzo, 2 hadi siku ile alipochukuliwa kwenda mbinguni, baada ya kuwapa maelekezo kwa njia Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua. 3 Baada ya mateso yake, alijionyesha kwao na kuwathibitishia kwa njia nyingi kwamba yeye yu […]

Matendo 2

Kushuka Kwa Roho Mtakatifu 1 Ilipowadia siku ya Pentekoste, walikuwa wote mahali pamoja. 2 Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3 Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho […]

Matendo 3

Petro Amponya Mlemavu Kwa Jina La Yesu 1 Siku moja Petro na Yohana walikuwa wanapanda kwenda Hekaluni kusali yapata saa tisa alasiri. 2 Basi palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa. Alichukuliwa na kuwekwa kwenye lango la Hekalu liitwalo Zuri, kila siku ili aombe msaada kwa watu wanaoingia Hekaluni. 3 Huyu mtu akiwaona Petro […]

Matendo 4

Petro Na Yohana Mbele Ya Baraza 1 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wakisema na watu, makuhani, mkuu wa walinzi wa Hekalu na Masudakayo wakawajia wakiwa 2 wamekasirika sana kwa sababu hao mitume walikuwa wanawafundisha watu na kuhubiri kwamba katika Yesu kuna ufufuo wa wafu. 3 Wakawakamata Petro na Yohana na kuwatia gerezani mpaka kesho yake […]

Matendo 5

Anania Na Safira 1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. 2 Mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume. 3 Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na […]

Matendo 6

Saba Wachaguliwa Kuhudumia 1 Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, palitokea manung’uniko kati ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawanyo wa chakula wa kila siku. 2 Wale mitume kumi na wawili wakakusanya wanafunzi wote pamoja wakasema, “Haitakuwa vyema sisi kuacha huduma ya […]

Matendo 7

Hotuba ya Stefano 1 Ndipo Kuhani Mkuu akamwuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?” 2 Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa bado yuko Mesopotamia, kabla hajaishi Harani, 3 akamwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na kutoka kwa jamii yako uende katika nchi nitakayokuonyesha.’ 4 “Hivyo […]

Matendo 8

1 Naye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano. Kanisa Lateswa Na Kutawanyika Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria. 2 Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana. 3 Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta […]

Matendo 9

Kuongoka Kwa Sauli 1 Wakati ule ule, Sauli alikuwa bado anazidisha vitisho vya kuua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, 2 naye akamwomba Kuhani Mkuu ampe barua ya kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mtu ye yote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu. 3 Basi akiwa katika safari […]

Matendo 10

Kornelio Amwita Petro 1 Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia. 2 Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mungu daima. 3 Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa […]