Ezra 1

Koreshi Asaidia Watu Kurudi Kutoka Uhamishoni 1 Katika mwaka wa kwanza wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kutimiza neno laBwanalililosemwa na Yeremia,Bwanaaliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote na kuliweka katika maandishi: 2 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: “ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani […]

Ezra 2

Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni 1 Basi hawa ndio watu wa jimbo, waliotoka uhamishoni ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirejea Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya watu wa Israeli […]

Ezra 3

Madhabahu Yajengwa Tena 1 Mwezi wa saba ulipowadia baada ya Waisraeli kukaa katika miji yao, watu wote walikusanyika huko Yerusalemu kama mtu mmoja. 2 Yeshua mwana wa Yosadaki na makuhani wenzake, Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na wenzake walianza kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli ili kumtolea dhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto juu […]

Ezra 4

Upinzani Kuhusu Ujenzi Mpya 1 Adui za Yuda na Benyamini waliposikia kwamba watu waliorudi kutoka uhamishoni wanajenga Hekalu kwa ajili yaBwana, Mungu wa Israeli, 2 wakamjia Zerubabeli na viongozi wa jamaa, nao wakasema, “Turuhusuni tuwasaidie kujenga, kwa sababu sisi tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi na tumekuwa tukimtolea dhabihu tangu wakati wa Esar-hadoni mfalme wa Ashuru, […]

Ezra 5

Barua Ya Tatenai Kwa Dario 1 Ndipo nabii Hagai na nabii Zekaria mzao wa Ido, wakawatolea unabii Wayahudi waliokuwa Yuda na Yerusalemu kwa jina la Mungu wa Israeli, aliyekuwa pamoja nao. 2 Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli na Yeshua mwana wa Yosadaki wakaanza kujenga tena nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Nao manabii wa Mungu walikuwa […]

Ezra 6

Amri Ya Dario 1 Kisha Mfalme Dario alitoa amri, nao wakafanya uchunguzi katika kumbukumbu zilizohifadhiwa katika hazina huko Babeli. 2 Karatasi moja ndefu ya maandishi ilipatikana huko Ekbatana katika jimbo la Umedi. Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa humo: Kumbukumbu: 3 Katika mwaka wa kwanza wa kutawala Mfalme Koreshi, mfalme alitoa amri kuhusu Hekalu la Mungu katika […]

Ezra 7

Ezra Awasili Yerusalemu 1 Baada ya mambo haya, wakati wa utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Ezra mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia, 2 mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu, 3 mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi, 4 mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa […]

Ezra 8

Orodha Ya Viongozi Wa Jamaa Waliorudi Na Ezra 1 Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta: 2 wa wazao wa Finehasi, alikuwa Gershoni; wa wazao wa Ithamari, alikuwa Danieli; wa wazao wa Daudi, alikuwa Hatushi 3 wa wazao wa Shekania; wa […]

Ezra 9

Maombi Ya Ezra Kuhusu Kuoa Wake Wa Kigeni 1 Baada ya mambo haya kutendeka, viongozi walinijia na kusema, “Watu wa Israeli, wakiwemo makuhani na Walawi, hawakujitenga na majirani zao katika kufanya machukizo, kama yale ya Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Waamoni, Wamoabi, Wamisri na Waamori. 2 Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake […]

Ezra 10

Toba Ya Watu 1 Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana. 2 Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake […]