Kutoka 1

Waisraeli Waonewa 1 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli ambao walikwenda Misri na Yakobo, kila mmoja akiwa pamoja na jamaa yake: 2 Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda; 3 Isakari, Zabuloni na Benyamini; 4 Dani na Naftali; Gadi na Asheri. 5 Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yosefu alikuwa tayari yuko Misri. 6 Basi […]

Kutoka 2

Kuzaliwa Kwa Mose 1 Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, 2 naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 3 Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha matete, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete […]

Kutoka 3

Mose Na Kichaka Kinachowaka Moto 1 Basi Mose alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Mose akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu. 2 Huko malaika waBwanaakamtokea Mose katika mwali wa moto kutoka katika kichaka. Mose akaona hilo, ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei. 3 Ndipo […]

Kutoka 4

Ishara Za Mose 1 Mose akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwanahakukutokea’?” 2 NdipoBwanaakamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?” Akajibu, “Fimbo.” 3 Bwanaakasema, “Itupe chini.” Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4 KishaBwanaakamwambia, “Nyosha mkono wako uikamate mkiani.” Basi Mose akanyosha mkono akamkamata yule nyoka, nayo ikabadilika tena kuwa […]

Kutoka 5

Matofali Bila Nyasi 1 Baadaye Mose na Aroni wakaenda kwa Farao, wakamwambia, “Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli: ‘Waruhusu watu wangu waende, ili waweze kunifanyia sikukuu huko jangwani.’ ” 2 Farao akasema, “HuyoBwanani nani, hata nimtii na kuruhusu Israeli uende? Simjui huyoBwanawala sitawaruhusu Israeli waende.” 3 Ndipo Mose na Aroni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana […]

Kutoka 6

1 KishaBwanaakamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.” 2 Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimiBwana. 3 Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi, ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. 4 […]

Kutoka 7

1 KishaBwanaakamwambia Mose, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa Farao, naye Aroni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako. 2 Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Aroni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake. 3 Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hata ingawa nitazidisha ishara na maajabu katika Misri, 4 hatawasikiliza. Kisha nitaupeleka […]

Kutoka 8

1 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. 2 Kama ukikataa kuwaruhusu kuondoka, basi nitaipiga nchi yako yote kwa kuwaletea vyura. 3 Mto Nile utafurika vyura. Watakuja kwenye jumba lako la kifalme na katika chumba chako cha kulala na kitandani mwako, katika nyumba za maafisa wako […]

Kutoka 9

Pigo La Tano: Vifo Vya Mifugo 1 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndiloBwana, Mungu wa Waebrania asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.” 2 Kama ukikataa kuwaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia, 3 mkono waBwanautaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ng’ombe wako, kondoo na mbuzi. 4 LakiniBwanaataweka […]

Kutoka 10

Pigo La Nane: Nzige 1 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake kuwa mgumu na mioyo ya maafisa wake ili kwamba nipate kutenda ishara hizi zangu za ajabu miongoni mwao 2 ili upate kuwaeleza watoto wako na wajukuu wako jinsi nilivyowatendea Wamisri kwa ukali na jinsi nilivyofanya ishara zangu miongoni mwao, nanyi […]