Isaya 1

1 Maono kuhusu Yuda na Yerusalemu ambayo Isaya mwana wa Amozi aliyaona wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda. Taifa Asi 2 Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia! Kwa maanaBwanaamesema: “Nimewalisha watoto na kuwalea, lakini wameniasi mimi. 3 Ng’ombe anamjua bwana wake, naye punda anajua hori la mmiliki wake, lakini […]

Isaya 2

Mlima Wa Bwana 1 Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu: 2 Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu laBwanautaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima, utainuliwa juu kupita vilima na mataifa yote yatamiminika huko. 3 Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njoni na tuupande mlima waBwana, kwenye nyumba ya Mungu wa […]

Isaya 3

Hukumu Juu Ya Yerusalemu Na Yuda. 1 Tazama sasa, Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote, yu karibu kuwaondolea Yerusalemu na Yuda upatikanaji wa mahitaji na misaada, upatikanaji wote wa chakula na maji, 2 shujaa na mtu wa vita, mwamuzi na nabii, mwaguzi na mzee, 3 jemadari wa kikosi cha watu hamsini na mtu mwenye cheo, mshauri, fundi stadi […]

Isaya 4

1 Katika siku ile wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe na kuvaa nguo zetu wenyewe, ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako. Utuondolee aibu yetu!” Tawi La Bwana 2 Katika siku ile Tawi laBwanalitakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika. […]

Isaya 5

Wimbo Wa Shamba La Mizabibu 1 Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye kuhusu shamba lake la mizabibu: Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu kwenye kilima chenye rutuba. 2 Alililima na kuondoa mawe na akaliotesha mizabibu bora sana. Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia. Kisha akatazamia kupata […]

Isaya 6

Agizo Kwa Isaya 1 Katika mwaka ule Mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza Hekalu. 2 Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili […]

Isaya 7

Ishara Ya Imanueli 1 Wakati Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, Mfalme Resini wa Aramuna Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli walipanda kupigana dhidi ya Yerusalemu, lakini hawakuweza kuushinda. 2 Wakati huu nyumba ya Daudi iliambiwa, “Aramu wameungana na Efraimu.” Kwa hiyo moyo wa Ahazi na ya watu wake […]

Isaya 8

Ashuru, Chombo Cha Bwana 1 Bwanaakaniambia, “Chukua gombo kubwa uandike juu yake kwa kalamu ya kawaida. Maher-Shalal-Hash-Bazi. 2 Nami nitawaita kuhani Uria na Zekaria mwana wa Yeberekia kama mashahidi wangu waaminifu.” 3 Kisha nikaenda kwa nabii mke, naye akapata mimba akazaa mwana. KishaBwanaakaniambia, “Mwite huyo mtoto Maher-Shalal-Hash-Bazi. 4 Kabla mtoto hajaweza kusema, ‘Baba yangu’ au […]

Isaya 9

Kwa Ajili Yetu Mtoto Amezaliwa 1 Hata hivyo, hapatakuwepo huzuni zaidi kwa wale waliokuwa katika dhiki. Wakati uliopita aliidhili nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini katika siku zijazo ataiheshimu Galilaya ya Mataifa, karibu na njia ya bahari, kando ya Yordani: 2 Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya […]

Isaya 10

1 Ole wao wawekao sheria zisizo za haki, kwa wale watoao amri za kuonea, 2 kuwanyima maskini haki zao na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa, kuwafanya wajane mawindo yao na kuwanyang’anya yatima. 3 Mtafanya nini siku ya kutoa hesabu, wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali? Mtamkimbilia nani awape msaada? Mtaacha wapi mali zenu? 4 Hakutasalia […]