3 Yohana 1

Salamu 1 Mzee: Kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Gayo Anasifiwa Kwa Ajili Ya Ukarimu Wake 2 Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli. […]