Esta 1

Malkia Vashti Aondolewa 1 Hili ndilo lililotokea wakati wa utawala wa Mfalme Ahusuero ambaye alitawala juu ya majimbo mia na ishirini na saba tangu Bara Hindi mpaka Kushi. 2 Wakati huo Mfalme Ahusuero alipotawala katika kiti chake cha enzi kilikuwa katika ngome ya mji wa Shushani, 3 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake, alifanya […]

Esta 2

Esta Afanywa Malkia 1 Baadaye, wakati hasira ya Mfalme Ahusuero ilipokuwa imetulia, alimkumbuka Vashti na kile alichokuwa amekifanya na alilokuwa ameamuru juu yake. 2 Kisha watumishi waliomhudumia mfalme walipendekeza, “Na ufanyike utafiti kwa ajili ya wanawali mabikira wazuri wa sura kwa ajili ya mfalme. 3 Mfalme na ateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake […]

Esta 3

Hila Ya Hamani Kuwaangamiza Wayahudi 1 Baada ya matukio haya, Mfalme Ahusuero alimheshimu Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akampandisha na kumpa kiti chake cha heshima cha juu sana kuliko wakuu wengine wote. 2 Maafisa wote wa kifalme waliokaa langoni mwa mfalme walipiga magoti na kumpa Hamani heshima, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru hili kuhusu Hamani. […]

Esta 4

Mordekai Amshawishi Esta Kusaidia 1 Wakati Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini, akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu. 2 Alikwenda akasimama nje ya lango la mfalme, kwa sababu hakuna ye yote aliyeruhusiwa kuingia akiwa amevaa nguo za magunia. 3 Katika kila jimbo ambapo […]

Esta 5

Ombi La Esta Kwa Mfalme 1 Siku ya tatu Esta alivaa mavazi yake ya kimalkia, naye akasimama katika ua wa ndani wa jumba la mfalme, mbele ya ukumbi wa mfalme. Naye mfalme alikuwa akiketi katika kiti chake cha kifalme katika ukumbi, akielekea langoni. 2 Alipomwona Malkia Esta amesimama uani alipendezwa naye, akamnyoshea fimbo ya utawala […]

Esta 6

Mordekai Anapewa Heshima 1 Usiku ule mfalme hakupata usingizi, hivyo akaagiza aletewe kitabu cha kumbukumbu za matukio ya utawala wake, asomewe. 2 Kitabu hicho kilikutwa na kumbukumbu kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumwua Mfalme Ahusuero. 3 Mfalme akauliza, “Je, ni […]

Esta 7

Hamani Aangikwa 1 Basi mfalme na Hamani wakaenda kula chakula pamoja na Malkia Esta, 2 walipokuwa wakinywa mvinyo katika siku ya pili, mfalme akauliza tena, “Malkia Esta, ni nini haja yako? Utapewa. Ombi lako ni nini? Hata nusu ya ufalme, utapewa.” 3 Kisha Malkia Esta akajibu, “Kama nimepata kibali kwako, Ee mfalme, tena kama inapendeza […]

Esta 8

Amri Ya Mfalme Kuhusu Wayahudi 1 Siku ile ile Mfalme Ahusuero akampa Malkia Esta shamba la Hamani, adui wa Wayahudi. Naye Mordekai akaja mbele ya mfalme, kwa kuwa Esta alikuwa amesema jinsi anavyohusiana naye. 2 Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang’anya Hamani, akampa Mordekai naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la […]

Esta 9

Ushindi Wa Wayahudi 1 Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia. 2 Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahusuero […]

Esta 10

Ukuu Wa Mordekai 1 Mfalme Ahusuero alitoza ushuru katika ufalme wake wote hadi kwenye miambao yake ya mbali. 2 Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Umedi na Uajemi? 3 Mordekai Myahudi alikuwa wa […]