Obadia 1

1 Maono ya Obadia. Hili ndilo asemaloBwanaMwenyezi kuhusu Edomu: Tumesikia ujumbe kutoka kwaBwana: Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema, “Inukeni, na twendeni tukapigane vita dhidi ya Edomu.” 2 “Angalieni, nitawafanya wadogo miongoni mwa mataifa, mtadharauliwa kabisa. 3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wewe unayeishi kwenye nyufa za miamba na kufanya makao yako juu, wewe unayejiambia mwenyewe, […]