Mithali 1

Utangulizi: Kusudi Na Kiini 1 Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli: 2 Kwa kupata hekima na nidhamu, kwa kufahamu maneno ya busara, 3 kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea, 4 huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana, 5 wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu […]

Mithali 2

Faida Za Hekima 1 Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, 2 kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, 3 na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu, 4 na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, 5 ndipo utakapoelewa kumchaBwana na […]

Mithali 3

Faida Nyingine Za Hekima 1 Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, 2 kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio. 3 Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako. 4 Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na […]

Mithali 4

Hekima Ni Bora Kupita Vitu Vyote 1 Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu, sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu. 2 Ninawapa mafundisho ya maana, kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. 3 Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu, ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu, 4 baba alinifundisha akisema, “Yashike maneno yangu yote kwa […]

Mithali 5

Onyo Dhidi Ya Uzinzi 1 Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, 2 ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa. 3 Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta, 4 lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama […]

Mithali 6

Maonyo Dhidi Ya Upumbavu 1 Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako, ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi kwa ajili ya mwingine, 2 kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako, 3 basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: Nenda ukajinyenyekeshe kwake, msihi jirani yako! 4 […]

Mithali 7

Onyo Dhidi Ya Mwanamke Mzinzi 1 Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. 2 Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. 3 Yafunge katika vidole vyako, yaandike katika kibao cha moyo wako. 4 Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako; 5 watakuepusha na […]

Mithali 8

Wito Wa Hekima 1 Je, hekima haiti? Je, ufahamu hapazi sauti? 2 Juu ya miinuko karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo, 3 kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema: 4 “Ni ninyi wanaume, ninaowaita, ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote. 5 Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili, ninyi […]

Mithali 9

Makaribisho Ya Hekima Na Ya Upumbavu 1 Hekima amejenga nyumba yake, amechonga nguzo zake saba. 2 Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake. 3 Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji. 4 Anawaambia wale wasio na maamuzi, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa! 5 […]

Mithali 10

Mithali Za Solomoni 1 Mithali za Solomoni: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. 2 Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. 3 Bwanahawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. 4 Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono […]