Waebrania 1

Mwana Ni Mkuu Kuliko Malaika 1 Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, 2 lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kwa yeye aliuumba ulimwengu. 3 Mwana ni mng’ao wa utukufu wa […]

Waebrania 2

Wokovu Mkuu 1 Kwa hiyo, imetupasa kuwa waangalifu sana kuhusu kile tulichosikia, ili tusije tukakiacha. 2 Kwa kuwa ujumbe ulionenwa na malaika ulikuwa imara na kila uasi na kutokutii kulipata adhabu ya haki, 3 je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana, kisha ulithibitishwa kwetu na […]

Waebrania 3

Yesu Ni Mkuu Kuliko Mose 1 Kwa hiyo ndugu watakatifu, mnaoshiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu. 2 Alikuwa mwaminifu kwa yeye aliyemweka, kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu. 3 Yesu ameonekana anastahili heshima kubwa kuliko Mose, kama vile mjenzi wa nyumba alivyo wa heshima […]

Waebrania 4

Pumziko Lile Mungu Aliloahidi 1 Kwa hiyo, kwa kuwa bado ahadi ya kuingia rahani iko wazi, tujihadhari ili hata mmoja wenu asije akaikosa. 2 Kwa maana sisi pia tumesikia Injili iliyohubiriwa kwetu, kama nao walivyosikia, lakini ujumbe ule waliousikia haukuwa na maana kwao, kwa sababu wale waliousikia hawakuuchanganya na imani. 3 Sasa sisi ambao tumeamini […]

Waebrania 5

1 Kwa maana kila Kuhani Mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi. 2 Kwa kuwa yeye mwenyewe ni dhaifu, aweza kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na kupotoka. 3 Hii ndiyo sababu inampasa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na […]

Waebrania 6

Hatari Ya Kuanguka 1 Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Kristo na tusonge mbele ili tufikie utimilifu, si kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, yaani, 2 mafundisho kuhusu aina za ubatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. 3 Mungu […]

Waebrania 7

Kuhani Melkizedeki 1 Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na Kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana, aliyekutana na Abrahamu akirudi katika kuwashinda hao wafalme, naye Melkizedeki akambariki, 2 ambaye Abrahamu alimpa sehemu ya kumiya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake “mfalme wa haki”; pia “mfalme wa Salemu,” maana yake “mfalme wa […]

Waebrania 8

Kuhani Mkuu Wa Agano Jipya 1 Basi jambo tunalotaka kulisema ni hili: Tunaye Kuhani Mkuu ambaye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 yeye ahudumuye katika patakatifu, pa hema la kweli lililowekwa na Bwana, wala si mwanadamu. 3 Kila Kuhani Mkuu huwekwa ili atoe sadaka na dhabihu. Vivyo hivyo ilikuwa […]

Waebrania 9

Ibada Katika Hema La Kidunia 1 Basi Agano lile la kwanza lilikuwa na kanuni zake za kuabudu na pia patakatifu pake pa kidunia. 2 Hema lilitengenezwa, katika sehemu yake ya kwanza kulikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa wakfu, hii sehemu iliitwa Mahali Patakatifu. 3 Nyuma ya pazia la pili, palikuwa na sehemu […]

Waebrania 10

Dhabihu Ya Kristo Ni Mara Moja Tu 1 Kwa maana Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka, kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu. 2 Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo […]