Ezekieli 1

Viumbe Hai Na Utukufu Wa Bwana 1 Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, wakati nilipokuwa miongoni mwa hao waliokuwa uhamishoni kando ya Mto Kebari, mbingu zilifunguka nami nikaona maono ya Mungu. 2 Katika siku ya tano ya mwezi, ilikuwa mwaka wa tano wa kuhamishwa kwa Mfalme Yehayakini, 3 neno […]

Ezekieli 2

Wito Wa Ezekieli 1 Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” 2 Alipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami. 3 Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo. 4 Watu ambao ninakutuma kwao ni wapotovu na wakaidi. Waambie, […]

Ezekieli 3

1 Naye akaniambia, “Mwanadamu, kula kile kilichoko mbele yako, kula huu ukurasa wa kitabu, kisha uende ukaseme na nyumba ya Israeli.” 2 Ndipo nikafungua kinywa changu, naye akanilisha ule ukurasa wa kitabu. 3 Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula ukurasa huu wa kitabu ninaokupa ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu. 4 […]

Ezekieli 4

Kuzingirwa Kwa Yerusalemu Kwaonyeshwa Kwa Mfano 1 “Mwanadamu, sasa chukua tofali, uliweke mbele yako na uchore juu yake ramani ya mji wa Yerusalemu. 2 Kisha uuzingire: Simamisha askari dhidi yake kuuzunguka, uzunguke kwa majeshi, weka kambi dhidi yake pande zote pamoja na magogo ya kubomolea boma vitani. 3 Kisha chukua bamba la chuma, ukalisimamishe liwe […]

Ezekieli 5

Upanga Dhidi Ya Yerusalemu 1 “Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo. 2 Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine […]

Ezekieli 6

Unabii Dhidi Ya Milima Ya Israeli 1 Neno laBwanalikanijia kusema, 2 “Mwanadamu, elekeza uso wako kukabili milima ya Israeli, utabiri dhidi yake 3 na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno laBwanaMwenyezi. Hili ndiloBwanaMwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia […]

Ezekieli 7

Mwisho Umewadia 1 Neno laBwanalikanijia kusema: 2 “Mwanadamu, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kwa nchi ya Israeli: Mwisho! Mwisho umekuja juu ya pembe nne za nchi. 3 Sasa mwisho umekuja juu yenu nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza. 4 Sitawaonea huruma wala […]

Ezekieli 8

Ibada Ya Sanamu Hekaluni 1 Katika siku ya tano ya mwezi wa sita mwaka wa sita, baada ya kupelekwa uhamishoni nilipokuwa nimeketi katika nyumba yangu na wazee wa Yuda walikuwa wameketi mbele yangu, mkono waBwanaMwenyezi ulikuja juu yangu. 2 Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana […]

Ezekieli 9

Waabudu Sanamu Wauawa 1 Kisha nikamsikia akiita kwa sauti kubwa akisema, “Walete wasimamizi wa mji hapa, kila mmoja akiwa na silaha mkononi mwake.” 2 Nami nikaona watu sita wakija toka upande wa lango la juu, linalotazama kaskazini kila mmoja na silaha za kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao alikuwepo mtu aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani safi, […]

Ezekieli 10

Utukufu Unaondoka Hekaluni 1 Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu kilichofanana na kiti cha enzi cha yakuti samawati. 2 Bwanaakamwambia mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani, “Ingia katikati ya yale Magurudumu yaliyo chini ya makerubi. Ukaijaze mikono yako makaa ya mawe ya moto kutoka […]