Luka 1

1 Kwa kuwa, watu wengi wamekaa ili kuandika habari za mambo yaliyotukia katikati yetu, 2 kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale ambao walikuwa mashahidi walioona na watumishi wa Bwana, 3 mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo ewe mtukufu Theofilo, 4 ili upate kujua ukweli […]

Luka 2

Kuzaliwa Kwa Yesu 1 Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. 2 (Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alipokuwa mtawala wa Shamu). 3 Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa. 4 Hivyo Yosefu akapanda kutoka mji wa Nazareti ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji […]

Luka 3

Yohana Mbatizaji Aanza Kuhubiri 1 Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, 2 Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, ndipo neno la Mungu […]

Luka 4

Yesu Ajaribiwa Na Shetani 1 Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani, 2 mahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula cho chote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa. 3 Ibilisi akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili […]

Luka 5

Kuitwa Kwa Wanafunzi Wa Kwanza 1 Siku moja Yesu alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti, watu wengi wakiwa wanasongana kumzunguka ili wapate kusikia neno la Mungu, 2 akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, zikiwa zimeachwa hapo na wavuvi waliokuwa wanaosha nyavu zao. 3 Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba […]

Luka 6

Bwana Wa Sabato 1 Ikawa siku moja ya Sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake. 2 Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya mambo ambayo ni kinyume na sheria siku ya Sabato?” 3 Yesu akawajibu, “Je, ninyi hamkusoma jinsi alivyofanya […]

Luka 7

Yesu Amponya Mtumishi Wa Jemadari 1 Baada ya Yesu kumaliza kusema haya yote watu wakiwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu. 2 Mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu ya kufa. 3 Jemadari huyo aliposikia habari za Yesu, aliwatuma wazee wa Kiyahudi kwake, wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo jemadari. […]

Luka 8

Mfano Wa Mpanzi 1 Baada ya haya Yesu alikwenda akawa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walikuwa pamoja naye, 2 pia baadhi ya wanawake waliokuwa wametolewa pepo wachafu na kuponywa magonjwa miongoni mwao alikuwepo Maria Magdalene, aliyetolewa pepo wachafu saba, 3 Yoana mkewe […]

Luka 9

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili 1 Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2 kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3 Akawaagiza akisema, “Msichukue cho chote safarini, wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala […]

Luka 10

Yesu Awatuma Wale Sabini Na Wawili 1 Baada ya hayo, Yesu akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda yeye mwenyewe. 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, awapeleke watenda kazi katika shamba lake. 3 Haya! nendeni. Ninawatuma […]