Mika 1

1 Neno laBwanalilimjia Mika, Mmorashti, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu. 2 Sikia, Ee mataifa, enyi nyote, sikilizeni, Ee dunia na wote mliomo ndani yake, iliBwanaMwenyezi ashuhudie dhidi yenu, Bwana kutoka Hekalu lake takatifu. Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu 3 Tazama!Bwanaanakuja kutoka makao […]

Mika 2

Mipango Ya Mwanadamu Na Ya Mungu 1 Ole kwa wale wapangao uovu, kwa wale wafanyao shauri la hila vitandani mwao! Kunapopambazuka wanalitimiza kwa sababu uko katika uwezo wao kutekeleza. 2 Wanatamani mashamba na kuyakamata, pia nyumba na kuzichukua. Wanamlaghai mwanaume nyumba yake, mwanadamu mwenzake urithi wake. 3 Kwa hiyo,Bwanaasema: “Ninapanga maangamizi dhidi ya watu hawa, […]

Mika 3

Viongozi Na Manabii Wakemewa 1 Kisha nikasema, “Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo, enyi watawala wa nyumba ya Israeli. Je, hampaswi kujua hukumu, 2 ninyi mnaochukia mema na kupenda maovu; ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi na kuondoa nyama kwenye mifupa yao; 3 ninyi mnaokula nyama ya watu wangu, mnaowachuna ngozi na kuvunja mifupa yao vipande vipande; […]

Mika 4

Mlima Wa Bwana 1 Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu laBwanautaimarishwa na kuwa mkuu kuliko milima yote; utainuliwa juu ya vilima na mataifa yatamiminika humo. 2 Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njoni, twendeni mlimani kwaBwana, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tutembee katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno laBwanalitatoka […]

Mika 5

Mtawala Aliyeahidiwa Kutoka Bethlehemu 1 Panga majeshi yako, Ee mji wa majeshi, kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. Watampiga mtawala wa Israeli shavuni kwa fimbo. 2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, […]

Mika 6

Shauri La Bwana Dhidi Ya Israeli 1 Sikiliza asemaloBwana: “Simama, tetea shauri lako mbele ya milima; vilima na visikie lile unalotaka kusema. 2 Sikilizeni, Ee milima, mashtaka yaBwana, sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. Kwa kuwaBwanaana shauri dhidi ya watu wake; anatoa mashtaka dhidi ya Israeli. 3 “Watu wangu, nimewatendea nini? Nimewalemea kwa jinsi […]

Mika 7

Taabu Ya Israeli 1 Taabu gani hii niliyo nayo! Nimefanana na yule akusanyaye matunda ya kiangazi, aokotaye masazo baada ya kuvunwa shamba la mizabibu; hakuna kishada chenye matunda ya kula, hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani. 2 Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka katika nchi; hakuna mtu mnyofu hata mmoja aliyebaki. Watu wote wanavizia kumwaga damu, […]