1 Mambo ya Nyakati 10

Sauli Ajiua 1 Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, wengi wakauawa katika mlima Gilboa. 2 Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua wanawe Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. 3 Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi. 4 Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome, la sivyo hawa watu […]