Hosea 1

1 Neno laBwanalililomjia Hosea mwana wa Beeri wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na wakati wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Yekoashi mfalme wa Israeli: Mke Wa Hosea Na Watoto 2 WakatiBwanaalipoanza kuzungumza kupitia Hosea,Bwanaalimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia […]

Hosea 2

1 “Waambie ndugu zako, ‘Watu wangu,’ na pia waambie dada zako, ‘Wapendwa wangu.’ Israeli Aadhibiwa Na Kurudishwa 2 “Mkemeeni mama yenu, mkemeeni, kwa maana yeye si mke wangu, nami si mume wake. Aondoe sura ya uzinzi katika uso wake na uzinzi kati ya matiti yake. 3 Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchi na kumwacha […]

Hosea 3

Upatanisho Wa Hosea Na Mkewe 1 Bwanaakaniambia, “Nenda, ukaonyeshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kamaBwanaapendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.” 2 Basi nilimnunua huyo mwanamke kwa shekeli kumi na tanoza fedha, pia kwa kiasi kama cha homeri […]

Hosea 4

Shtaka Dhidi Ya Israeli 1 Sikieni neno laBwana, enyi Waisraeli, kwa sababuBwanaanalo shtaka dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, hakuna kumjua Mungu katika nchi. 2 Kuna kulaani tu, uongo na uuaji, wizi na uzinzi, bila kuwa na mipaka, nao umwagaji damu mmoja baada ya mwingine. 3 Kwa sababu hii nchi huomboleza, […]

Hosea 5

Hukumu Dhidi Ya Israeli 1 “Sikieni hili, enyi makuhani! Iweni wasikivu, enyi Waisraeli! Sikieni, Ee nyumba ya kifalme! Hukumu hii ni dhidi yenu: Mmekuwa mtego huko Mizpa, wavu uliotandwa juu ya Tabori. 2 Waasi wamezidisha sana mauaji. Mimi nitawatiisha wote. 3 Ninajua yote kuhusu Efraimu, Israeli hukufichika kwangu. Efraimu, sasa umegeukia ukahaba, Israeli amenajisika. 4 […]

Hosea 6

Israeli Asiye Na Toba 1 “Njoni, tumrudieBwana. Ameturarua vipande vipande lakini atatuponya; ametujeruhi lakini atatufunga majeraha yetu. 2 Baada ya siku mbili atatufufua; katika siku ya tatu atatuinua, ili tuweze kuishi mbele zake. 3 TumkubaliBwana, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua […]

Hosea 7

1 kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wevi huvunja nyumba, maharamia hunyang’anya barabarani, 2 lakini hawafahamu kwamba ninakumbuka matendo yao yote mabaya. Dhambi zao zimewameza, ziko mbele zangu siku zote. 3 “Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao, wakuu wao kwa uongo wao. 4 Wote ni […]

Hosea 8

Israeli Kuvuna Kisulisuli 1 “Wekeni tarumbeta midomoni mwenu! Tai yuko juu ya nyumba yaBwana kwa sababu watu wamevunja Agano langu, wameasi dhidi ya sheria yangu. 2 Israeli ananililia, ‘Ee Mungu wetu, tunakukubali!’ 3 Lakini Israeli amekataa lile lililo jema, adui atamfuatia. 4 Wanaweka Wafalme bila idhini yangu, wamechagua wakuu bila kibali changu. Kwa fedha zao […]

Hosea 9

Adhabu Kwa Israeli 1 Usifurahie, Ee Israeli; usishangilie kama mataifa mengine. Kwa kuwa hukuwa mwaminifu kwa Mungu wako; umependa ujira wa kahaba kwenye kila sakafu ya kupuria nafaka. 2 Sakafu za kupuria nafaka na mashinikizo ya kukamulia divai havitalisha watu, divai mpya itawapungukia. 3 Hawataishi katika nchi yaBwana, Efraimu atarudi Misri na atakula chakula kilicho […]

Hosea 10

1 Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada. 2 Moyo wao ni mdanganyifu, nao sasa lazima wachukue hatia yao. Bwanaatabomoa madhabahu zao na kuharibu mawe yao ya ibada. 3 Kisha watasema, “Hatuna mfalme kwa sababu hatukumheshimuBwana. Lakini hata […]