Nehemiah 1

Maombi Ya Nehemia 1 Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia: # Katika mwezi wa Kisleukatika mwaka wa ishirini, wakati nikiwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani, 2 Hanani, mmoja wa ndugu zangu, alikuja kutoka Yuda akiwa na watu wengine, nami nikawauliza kuhusu mabaki ya Wayahudi walionusurika kwenda uhamishoni na pia kuhusu Yerusalemu. 3 Wakaniambia, […]

Nehemiah 2

Artashasta Amtuma Nehemia Yerusalemu 1 Katika mwezi wa Nisanimwaka wa ishirini wa kutawala kwake Mfalme Artashasta, wakati divai ilipoletwa kwa ajili yake, niliichukua na kumpa mfalme. Sikuwahi kuonekana mwenye huzuni mbele yake kabla ya hapo. 2 Basi mfalme akaniuliza, “Kwa nini uso wako unaonekana una huzuni wakati wewe si mgonjwa? Jambo hili si kitu kingine […]

Nehemiah 3

Wajenzi Wa Ukuta 1 Eliyashibu Kuhani Mkuu na makuhani wenzake walikwenda kufanya kazi na kulijenga upya Lango la Kondoo. Waliliweka wakfu na kuweka milango mahali pake, wakajenga hadi kufikia Mnara wa Mia Moja, ambao waliuweka wakfu hadi Mnara wa Hananeli. 2 Watu wa Yeriko wakajenga sehemu zilizopakana nao, Zahuri mwana wa Imri aliendelea kujenga karibu […]

Nehemiah 4

Upinzani Wakati Wa Ujenzi 1 Sanbalati aliposikia kwamba tulikuwa tunajenga upya ukuta, alikasirika na akawa na uchungu sana. Aliwadhihaki Wayahudi, 2 mbele ya rafiki zake na jeshi la Samaria, akisema, “Hawa Wayahudi wanyonge wanafanya nini? Je, wataweza kuurudishia ukuta wao? Je, watatoa dhabihu? Je, wataweza kumaliza kuujenga kwa siku moja? Je, wataweza kufufua mawe kutoka […]

Nehemiah 5

Nehemia Anawasaidia Maskini 1 Wakati huu watu na wake zao wakalia kilio kikuu dhidi ya ndugu zao Wayahudi. 2 Baadhi yao walikuwa wakisema, “Sisi na wana wetu na binti zetu tu wengi, ili tuweze kula na kuishi, ni lazima tupate nafaka.” 3 Wengine walikuwa wakisema, “Tunaweka rehani mashamba yetu, mashamba ya mizabibu na nyumba zetu […]

Nehemiah 6

Upinzani Zaidi Wakati Wa Ujenzi 1 Habari zilipofika kwa Sanbalati, Tobia, Geshemu Mwarabu na adui zetu wengine kwamba nimejenga tena ukuta na hakuna nafasi iliyobakia ndani mwake, ingawa mpaka wakati huo sikuwa nimeweka milango kwenye malango, 2 Sanbalati na Geshemu wakanipelekea ujumbe huu: “Njoo, tukutane katika mojawapo ya vijiji katika nchi tambarare ya Ono.” Lakini […]

Nehemiah 7

1 Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na kuweka milango, waliteuliwa mabawabu wa lango, waimbaji na Walawi. 2 Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3 Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Wakati […]

Nehemiah 8

1 watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja kwenye uwanja mbele ya Lango la Maji. Wakamwambia Ezra mwandishi alete kitabu cha sheria ya Mose, ambachoBwanaaliamuru kwa ajili ya Israeli. 2 Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba kuhani Ezra akaleta Sheria mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwemo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu. 3 […]

Nehemiah 9

Waisraeli Waungama Dhambi Zao 1 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi ule ule, Waisraeli walikusanyika pamoja, wakifunga na kuvaa nguo za gunia na kujipaka mavumbi vichwani mwao. 2 Wale wa uzao wa Israeli walijitenga na wageni wote. Wakasimama mahali pao na kuungama dhambi zao na uovu wa baba zao. 3 Wakasimama pale walipokuwa, […]

Nehemiah 10

1 Wale waliotia muhuri walikuwa: Nehemia mtawala, mwana wa Hakalia. Sedekia, 2 Seraya, Azaria, Yeremia, 3 Pashuri, Amaria, Malkiya, 4 Hatushi, Shebania, Maluki, 5 Harimu, Meremothi, Obadia, 6 Danieli, Ginethoni, Baruki, 7 Meshulamu, Abiya, Miyamini, 8 Maazia, Bilgai na Shemaya. Hawa ndio waliokuwa makuhani. 9 Walawi: Yeshua mwana wa Azania, Binui wana wa Henadadi, Kadmieli, […]