Danieli 1

Mafunzo Ya Danieli Huko Babeli 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja akazingira Yerusalemu kwa jeshi. 2 Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza pamoja na baadhi ya vyombo kutoka katika Hekalu la Mungu. Hivi akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko […]

Danieli 2

Ndoto Ya Nebukadneza 1 Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto, akili yake ikasumbuka na hakuweza kulala. 2 Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme, 3 akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua nami nataka nijue maana yake.” 4 Ndipo wanajimu […]

Danieli 3

Sanamu Ya Dhahabu Na Moto Mkali 1 Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitinina upana wake dhiraa sita, akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la nchi ya Babeli. 2 Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo […]

Danieli 4

Ndoto Ya Nebukadneza Ya Mti 1 Mfalme Nebukadneza, Kwa kabila za watu, mataifa na watu wa kila lugha, wanaoishi katika ulimwengu wote: Amani na mafanikio yawe kwenu! 2 Ni furaha yangu kuwaambia kuhusu ishara ya miujiza na maajabu ambayo Mungu Aliye Juu Sana amenifanyia. 3 Tazama jinsi ishara zake zilivyo kuu, jinsi maajabu yake yalivyo […]

Danieli 5

Maandishi Ukutani 1 Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao. 2 Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake […]

Danieli 6

Danieli Katika Tundu La Simba 1 Ilimpendeza Dario kuteua wakuu 120 kutawala katika ufalme wake wote, 2 pamoja na wasimamizi watatu juu yao, ambao mmoja wao alikuwa Danieli. Wakuu walitoa hesabu kwa hao wasimamizi ili mfalme asipate hasara. 3 Basi Danieli alijidhihirisha mwenyewe, miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee hata mfalme […]

Danieli 7

Ndoto Ya Danieli Ya Wanyama Wanne 1 Katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita katika akili yake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake. 2 Danieli akasema: “Katika maono yangu usiku nilitazama, mbele yangu kulikuwepo na upepo kutoka pande nne za mbinguni […]

Danieli 8

Maono Ya Danieli Ya Kondoo Dume Na Beberu 1 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Mfalme Belshaza, mimi Danieli, nilipata maono, baada ya maono ambayo yalikuwa yamenitokea. 2 Katika maono yangu mimi nilijiona nikiwa ndani ya ngome ya Shushani katika jimbo la Elamu, katika maono nilikuwa kando ya Mto Ulai. 3 Nikatazama juu, hapo […]

Danieli 9

Maombi Ya Danieli 1 Katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake Dario mwana wa Ahusuero (mzaliwa wa Umedi) ambaye alifanywa mtawala juu ya ufalme wa Babeli, 2 katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, mimi Danieli, nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno laBwanaalilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini. 3 […]

Danieli 10

Maono Ya Danieli Kuhusu Mtu 1 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono. 2 Wakati huo, mimi Danieli, nikaomboleza kwa majuma matatu. 3 Sikula chakula kizuri, nyama wala divai havikugusa midomo […]