Ayubu 1

Ayubu Na Jamaa Yake 1 Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye jina lake aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu, alimcha Mungu na kuepuka ubaya. 2 Alikuwa na wana saba na binti watatu, 3 naye alikuwa na kondoo 7,000, ngamia 3,000, jozi 500 za maksai, punda 500, tena alikuwa na idadi […]

Ayubu 2

Jaribu La Pili La Ayubu 1 Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele zaBwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake. 2 Bwanaakamwuliza Shetani, “Umetoka wapi?” Shetani akamjibuBwana“Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.” 3 Bwanaakamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Mtu ambaye hakuna mwingine duniani aliye kama yeye, […]

Ayubu 3

Hotuba Ya Kwanza Ya Ayubu 1 Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake. 2 Akasema: 3 “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, nao usiku ule iliposemekana, ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’ 4 Siku ile na iwe giza, Mungu juu na asiiangalie, nayo nuru isiiangazie. 5 Giza na kivuli […]

Ayubu 4

Elifazi Anazungumza: Ayubu Ametenda Dhambi 1 Ndipo Elifazi, Mtemani akajibu: 2 “Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe, kutakukasirisha? Lakini ni nani awezaye kujizuia asiseme? 3 Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi, jinsi ambavyo umeitia nguvu mikono iliyokuwa dhaifu. 4 Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa, umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu. 5 Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, […]

Ayubu 5

Elifazi Anaendelea 1 “Ita kama unataka, lakini ni nani atakayekujibu? Ni yupi kati ya hao watakatifu utakayemgeukia? 2 Kuweka uchungu moyoni humwua mpumbavu, nao wivu humchinja mjinga. 3 Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akistawi, lakini ghafula nyumba yake ikawa imelaaniwa. 4 Watoto wake wako mbali na usalama, hushindwa mahakamani bila mtetezi. 5 Wenye njaa huyala mavuno […]

Ayubu 6

Ayubu Anajibu: Malalamiko Yangu Ni Ya Haki 1 Kisha Ayubu akajibu: 2 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa, nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani! 3 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote, kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka. 4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, roho yangu inakunywa sumu […]

Ayubu 7

Ayubu: Mateso Yangu Hayana Mwisho 1 “Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani? Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa? 2 Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni, au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake, 3 ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili, nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku. 4 Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ […]

Ayubu 8

Bildadi Anasema: Yampasa Ayubu Atubu 1 Kisha Bildadi, Mshuhi akajibu: 2 “Hata lini wewe utasema mambo kama haya? Maneno yako ni kama upepo mkuu. 3 Je, Mungu hupotosha hukumu? Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki? 4 Watoto wako walipomtenda dhambi, aliwapa adhabu ya dhambi yao. 5 Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi, 6 ikiwa wewe […]

Ayubu 9

Hakuna Mpatanishi 1 Kisha Ayubu akajibu: 2 “Naam, najua hili ni kweli. Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? 3 Ingawa mtu angetaka kushindana naye, asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja. 4 Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. Ni nani aliyempinga naye akawa salama? 5 Aiondoa […]

Ayubu 10

Ayubu: Nayachukia Maisha Yangu 1 “Nayachukia sana haya maisha yangu; kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu. 2 Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu. 3 Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya […]