Amosi 1

1 Maneno ya Amosi, mmoja wa wachunga wanyama wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda na Yeroboamu mwana wa Yoashi alipokuwa mfalme wa Israeli. 2 Alisema: “Bwanaananguruma toka Sayuni, pia ananguruma kutoka Yerusalemu; malisho ya wachunga wanyama yanakauka, kilele cha Karmeli kinanyauka.” Hukumu […]

Amosi 2

1 Hili ndilo asemaloBwana: “Kwa dhambi tatu za Moabu, hata kwa dhambi nne, sitazuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu, ikawa kama chokaa. 2 Nitatuma moto juu ya Moabu ambao utateketeza ngome ya Keriothi. Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa katikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta. 3 Nitamwangamiza mtawala […]

Amosi 3

Mashahidi Waitwa Dhidi Ya Israeli 1 Sikilizeni neno hiliBwanaalilosema dhidi yenu, Enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri: 2 “Ni ninyi tu niliowachagua kati ya jamaa zote za dunia, kwa hiyo nitawaadhibu kwa ajili ya dhambi zenu zote.” 3 Je, watu wawili hutembea pamoja wasipokubaliana kufanya hivyo? 4 Je, simba hunguruma […]

Amosi 4

Israeli Hajarudi Kwa Mungu 1 Sikilizeni neno hili, ninyi ng’ombe wa Bashani mlioko juu ya Mlima Samaria, ninyi wanawake mnaowaonea maskini na kuwagandamiza wahitaji na kuwaambia wanaume wenu, “Tuleteeni vinywaji!” 2 BwanaMwenyezi ameapa kwa utakatifu wake: “Hakika wakati utakuja mtakapochukuliwa na kulabu, na wanaosalia kwa ndoana za samaki. 3 Nanyi mtakwenda moja kwa moja kupitia […]

Amosi 5

Maombolezo Na Wito Wa Toba 1 Sikia neno hili, Ee nyumba ya Israeli, ombolezo hili ninalifanya kuwahusu ninyi: 2 “Bikira Israeli ameanguka, kamwe hatainuka tena, ameachwa pweke katika nchi yake, hakuna ye yote wa kumwinua.” 3 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: “Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani, mia moja tu watarudi; wakati mji […]

Amosi 6

Ole Kwa Wanaoridhika 1 Ole wenu ninyi mnaostarehe na kuridhika katika Sayuni, na ninyi mnaojisikia salama juu ya Mlima Samaria, ninyi watu mashuhuri wa taifa lililoendelea kuliko mataifa mengine, ambao watu wa Israeli wanawategemea! 2 Nendeni Kalne mkaone kutoka huko; mwende hadi Hamathi iliyo kuu, kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti. Je, wao ni bora […]

Amosi 7

Maono Ya Kwanza: Nzige 1 Hili ndilo alilonionyeshaBwanaMwenyezi katika maono: Alikuwa anaandaa makundi ya nzige baada ya kuvunwa fungu la mfalme na wakati ule tu mimea ya pili ilipokuwa ikichipua. 2 Wakati nzige walipokuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “BwanaMwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!” 3 […]

Amosi 8

Maono Ya Nne: Kikapu Cha Matunda Yaliyoiva 1 Hili ndilo alilonionyeshaBwanaMwenyezi katika maono: kikapu cha matunda yaliyoiva. 2 Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” NdipoBwanaakaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli, sitawahurumia zaidi.” 3 BwanaMwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi sana; itatupwa kila mahali! Kimya!” […]

Amosi 9

Israeli Kuangamizwa 1 Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: “Piga juu ya nguzo ili vizingiti vitikisike. Viangushe juu ya vichwa vya watu wote, na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. Hakuna awaye yote atakayekimbia, hakuna atakayetoroka. 2 Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu, kutoka huko mkono wangu utawatoa. Wajapopanda juu hadi kwenye […]