Yohana 1

Neno Alifanyika Mwili 1 Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. […]

Yohana 2

Arusi Huko Kana 1 Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwako huko. 2 Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. 3 Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.” 4 Yesu akamwambia, “Mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.” 5 Mama yake […]

Yohana 3

Nikodemo Amwendea Yesu Usiku 1 Basi palikuwa na mtu mmoja Farisayo, jina lake Nikodemo, mmoja wa Baraza la Wayahudilililotawala. 2 Huyu alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye.” 3 Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, […]

Yohana 4

Yesu Azungumza Na Mwanamke Msamaria 1 Mafarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana, 2 ingawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. 3 Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya. 4 Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria. 5 Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria […]

Yohana 5

Yesu Amponya Mtu Penye Bwawa La Bethzatha 1 Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu. 2 Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa kwa Kiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwa limezungukwa na kumbi tano. 3 Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, […]

Yohana 6

Yesu Alisha Watu 5,000 1 Baada ya haya, Yesu alikwenda ng’ambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia. 2 Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa. 3 Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 4 Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. […]

Yohana 7

Kutokuamini Kwa Ndugu Zake Yesu 1 Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumwua. 2 Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. 3 Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya. 4 Mtu anayetaka kujulikana hafanyi […]

Yohana 8

Mwanamke Aliyefumaniwa Akizini 1 Lakini Yesu akaenda katika Mlima wa Mizeituni. 2 Alfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha. 3 Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote. 4 Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. 5 Katika sheria, Mose […]

Yohana 9

Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu 1 Yesu alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?” 3 Yesu akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. 4 Yanipasa […]

Yohana 10

Mchungaji Mwema 1 “Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwivi na mnyang’anyi. 2 Yeye anayeingia kwa kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo. 3 Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa […]