Maombolezo 1

1 Tazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa, mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu! Jinsi ambavyo umekuwa kama mama mjane, ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa! Yule ambaye alikuwa malkia miongoni mwa majimbo sasa amekuwa mtumwa. 2 Kwa uchungu, hulia sana usiku, machozi yapo kwenye mashavu yake. Miongoni mwa wapenzi wake wote hakuna ye yote […]

Maombolezo 2

1 Tazama jinsi Bwana alivyomfunika Binti Sayuni kwa wingu la hasira yake! Ameitupa chini fahari ya Israeli kutoka mbinguni mpaka duniani, hakukumbuka kiti chake cha kuwekea miguu katika siku ya hasira yake. 2 Bila huruma Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo; katika ghadhabu yake amebomoa ngome za Binti Yuda. Ameuangusha ufalme wake na wakuu wake […]

Maombolezo 3

1 Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake. 2 Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru; 3 hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa. 4 Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu. 5 Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu. 6 […]

Maombolezo 4

1 Jinsi dhahabu ilivyopoteza mng’ao wake, dhahabu iliyo safi imekuwa haing’ai! Vito vya thamani vimetawanywa kwenye mwanzo wa kila barabara. 2 Jinsi wana wa Sayuni wenye thamani, ambao mwanzo uzito wa thamani yao ulikuwa wa dhahabu, sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo, kazi ya mikono ya mfinyanzi! 3 Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto […]

Maombolezo 5

1 Kumbuka, EeBwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu. 2 Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni. 3 Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane. 4 Ni lazima kununua maji tunayokunywa, kuni zetu zinaweza kupatikana tu kwa kununua. 5 Wale ambao wanatufuatilia wapo kwenye visigino vyetu, tumechoka na hakuna […]