Mwanzo 1

Siku Sita Za Uumbaji Na Sabato 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. 2 Wakati huu Dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu, giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametanda juu ya maji. 3 Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 4 Mungu akaona ya kuwa […]

Mwanzo 2

1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo. 2 Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. 3 Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya. Adamu Na Eva […]

Mwanzo 3

Anguko La Mwanadamu 1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambaoBwanaMungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wo wote wa bustanini’?” 2 Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, […]

Mwanzo 4

Kaini Na Abeli 1 Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada waBwananimemzaa mwanaume.” 2 Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake. Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima. 3 Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwaBwana. 4 Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka […]

Mwanzo 5

Kutoka Adamu Hadi Noa 1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. 2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa akawaita “Mwanadamu.” 3 Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi. 4 Baada ya Sethi kuzaliwa, […]

Mwanzo 6

Sababu Za Gharika 1 Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao, 2 wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa ye yote miongoni mwao waliyemchagua. 3 NdipoBwanaakasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa […]

Mwanzo 7

Gharika 1 NdipoBwanaakamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. 2 Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike. 3 Pia uchukue […]

Mwanzo 8

Mwisho Wa Gharika 1 Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka. 2 Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani. 3 Maji yakaendelea […]

Mwanzo 9

Mungu Aweka Agano Na Noa 1 Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia. 2 Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. 3 Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa […]

Mwanzo 10

Mataifa Yaliyotokana Na Noa 1 Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika. Wazao Wa Yafethi 2 Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. 3 Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma. 4 Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. […]