Mgawanyo Wa Nchi Magharibi Mwa Yordani
1 Basi haya ndiyo maeneo Waisraeli waliyopokea kama urithi katika nchi ya Kanaani, ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliwagawia.
2 Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.
3 Mose alikuwa amewapa yale makabila mawili na nusu urithi wao upande wa mashariki ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi miongoni mwa hao wengine,
4 kwa kuwa wana wa Yosefu walikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ng’ombe.
5 Kwa hiyo Waisraeli wakagawana ile nchi, kama vileBwanaalivyomwagiza Mose.
Kalebu Anapewa Mji Wa Hebroni
6 Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, akawaambia, “Unajua jambo ambaloBwanaalimwambia Mose mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.
7 Nilikuwa na umri wa miaka arobaini, wakati Mose mtumishi waBwana, aliponituma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza hiyo nchi. Nami nikamletea taarifa kama kulingana na nilivyosadiki moyoni.
8 Lakini wenzangu tuliopanda nao waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa hofu. Bali mimi, nilimfuataBwanaMungu wangu kwa moyo wote.
9 Hivyo siku ile Mose akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuataBwanaMungu wangu kwa moyo wote.’
10 “Sasa basi, kama vileBwanaalivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na mitano tangu wakati alipomwambia Mose jambo hili, wakati Waisraeli wakiwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo, nina umri wa miaka themanini na mitano!
11 Bado ninazo nguvu kama siku ile Mose aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule.
12 Basi nipe nchi hii ya kilima, ambayoBwanaaliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada waBwana, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”
13 Ndipo Yoshua akambariki Kalebu mwana wa Yefune, naye akampa Hebroni kuwa urithi wake.
14 Hivyo Hebroni ikawa mali ya Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandamaBwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote.
15 (Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kutokana na huyo Arba ambaye alikuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.)
Kisha nchi ikawa na amani bila vita.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/14-5c30e7dda61437aa5e4ce45651021cfa.mp3?version_id=1627—