Yoshua 15

Mgawo Kwa Yuda

1 Mgawo kwa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo, ulishuka kufikia nchi ya Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.

2 Mpaka wao wa kusini ulianzia kwenye ghuba iliyoko kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi,

3 ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni ukapanda hadi Adari na ukapinda hadi Karka.

4 Kisha ukaendelea mpaka Azmoni na kuunganika na Mto wa Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini.

5 Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi hadi mahali Mto Yordani unapoingilia.

Mpaka wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia,

6 ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.

7 Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Ahori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na matelemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.

8 Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mtelemko wa kusini wa mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini ya Bonde la Warefai.

9 Kutoka juu ya kilima mpaka ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kutelemka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu).

10 Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri ukafuatia mtelemko wa kaskazini wa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna.

11 Ukaelekea hadi kwenye mtelemko wa kaskazini wa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabneeli. Mpaka ukaishia baharini.

12 Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu.

Hii ndiyo iliyokuwa mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao.

Nchi Aliyopewa Kalebu

13 Kwa kufuata maagizo yaBwanakwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa Anaki).

14 Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki.

15 Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu waishio Debiri (jina la Debiri hapo kwanza iliitwa Kiriath-Seferi).

16 Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.”

17 Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake aolewe naye.

18 Siku moja baada ya yule mwanamke kuolewa na Othnieli, alimsihi amwombe Kalebu baba yake shamba. Aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamwuliza, “Wataka nikufanyie nini?”

19 Akamjibu, “Nifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa shamba lililoko huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa Aksa binti yake chemchemi za juu na za chini.

Miji Ya Yuda

20 Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo:

21 Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa:

Kabseeli, Ederi, Yaguri,

22 Kina, Dimona, Adada,

23 Kedeshi, Hazori, Ithnani,

24 Zifu, Telemu, Bealothi,

25 Hazor-Hadata, Kerioth-Hesroni (yaani Hazori),

26 Amamu, Shema, Molada,

27 Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti,

28 Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia,

29 Baala, Iyimu, Esemu,

30 Eltoladi, Kesili, Horma,

31 Siklagi, Madmana, Sansana,

32 Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.

33 Upande wa magharibi chini ya vilima:

Eshtaoli, Sora, Ashna,

34 Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu,

35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,

36 Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.

37 Senani, Hadasha, Migdal-Gadi,

38 Dileani, Mispa, Yoktheeli,

39 Lakishi, Boskathi, Egloni,

40 Kaboni, Lahmasi, Kitlishi,

41 Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake.

42 Libna, Etheri, Ashani,

43 Yifta, Ashna, Nesibu,

44 Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake.

45 Ekroni, pamoja na viunga vyake na vijiji vyake;

46 magharibi ya Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake;

47 Ashdodi, miji yake na vijiji vyake na Gaza viunga vyake na vijiji vyake, hadi kufikia Mto wa Misri na Pwani ya Bahari Kuu.

48 Katika nchi ya vilima:

Shamiri, Yatiri, Soko,

49 Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri),

50 Anabu, Eshtamoa, Animu,

51 Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake.

52 Arabu, Duma, Ashani,

53 Yanimu, Beth-Tapua, Afeka,

54 Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake.

55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,

56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,

57 Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake.

58 Halhuli, Beth-Zuri, Gedori,

59 Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake.

60 Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake.

61 Huko jangwani:

Beth-Araba, Midini, Sekaka,

62 Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake.

63 Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, ambao walikuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/15-fbac4cf1d47ad803a8f9eb62b5644fee.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 − 18 =