Yoshua 16

Mgawo Kwa Ajili Ya Efraimu Na Manase

1 Mgawanyo wa Yosefu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli.

2 Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia nchi ya Waariki huko Atarothi,

3 ukatelemkia kuelekea magharibi hadi nchi ya Wayafleti mpaka sehemu ya Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.

4 Kwa hiyo Manase na Efraimu, wazao wa Yosefu, walipokea urithi wao.

5 Hii ndiyo iliyokuwa nchi ya Efraimu, ukoo kwa ukoo:

Mpaka wa urithi wao ulianzia Atarothi Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu,

6 na kuendelea mpaka baharini. Kutoka Mikmethathi upande wa kaskazini ulipinda kuelekea mashariki mpaka Taanath-Shilo, ukipitia Yanoa upande wa mashariki.

7 Kisha ulitelemkia kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara, ukagusa Yeriko na kutokea katika Mto Yordani.

8 Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Kijito cha Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo.

9 Pia ulijumuisha miji yote na vijiji vyake ambavyo vilitengwa kwa ajili ya Waefraimu ndani ya urithi wa kabila la Manase.

10 Hawakuwafukuza Wakanaani waishio Gezeri; mpaka leo Wakanaani wanaishi miongoni mwa watu wa Efraimu lakini wanatakiwa kufanya kazi ngumu za kulazimishwa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/16-706763d0d49207b997fa5a4ed8490565.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 + seventeen =