Mgawo Kwa Simeoni
1 Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya nchi ya Yuda.
2 Ulijumuisha:
Beer-Sheba (au Sheba), Molada,
3 Hasar-Shuali, Bala na Esemu,
4 Eltoladi, Bethuli, Horma,
5 Siklagi, Beth-Markabothi, Hazar-Susa,
6 Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.
7 Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani, hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake,
8 pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii mpaka Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni ukoo kwa ukoo.
9 Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka katika fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya nchi ya Yuda.
Mgawo Kwa Wazabuloni
10 Nayo kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, ukoo kwa ukoo:
Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi.
11 Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea mpaka kijito cha maji karibu na Yokneamu.
12 Ukageuka mashariki kuanzia Saridi kuelekea maawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori na kwenda hadi Daberathi kupanda Jafia.
13 Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea.
14 Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli.
15 Miji mingine ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.
16 Miji hii na vijiji vyake vilikuwa ndio urithi wa Zabuloni, ukoo kwa ukoo.
Mgawo Kwa Isakari
17 Kura ya nne ikamwangukia Isakari, ukoo kwa ukoo.
18 Nchi yao ilijumuisha:
Yezreeli, Kesulothi, Shunemu,
19 Hafaraimu, Shioni, Anaharathi,
20 Rabithi, Kishioni, Ebesi,
21 Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi.
22 Mpaka ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Mto Yordani. Hii ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
23 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, ukoo kwa ukoo.
Mgawo Kwa Asheri
24 Kura ya tano iliangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.
25 Nchi yao ilijumuisha:
Miji ya Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu,
26 Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.
27 Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.
28 Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.
29 Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika nchi ya Akzibu,
30 Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
31 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.
Mgawo Kwa Naftali
32 Kura ya sita iliangukia kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo:
33 Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mti mkubwa ulio katika Sananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu na kuishia katika Mto Yordani.
34 Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.
35 Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi,
36 Adama, Rama, Hazori,
37 Kedeshi, Edrei, na En-Hasori,
38 Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.
39 Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo.
Mgawo Kwa Dani
40 Kura ya saba iliangukia kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.
41 Nchi ya urithi wao ilijumuisha:
Sora, Eshtaoli, Ir-Shemeshi,
42 Shaalabini, Aiyaloni, Ithla,
43 Eloni, Timna, Ekroni,
44 Elteke, Gibethoni, Baalathi,
45 Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni,
46 Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.
47 (Lakini Wadani walipata shida kuimiliki nchi yao, kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)
48 Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.
Mgawo Kwa Yoshua
49 Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao,
50 kama vileBwanaalivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Seraulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.
51 Hizo ndizo nchi ambazo Eleazari kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli walizigawanya kwa kura huko Shilo mbele zaBwanapenye ingilio la Hema la Kukutania. Nao wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/19-a382a1f74d5d00631596cca7fbf30244.mp3?version_id=1627—