Yoshua 21

Miji Kwa Ajili Ya Walawi

1 Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli

2 huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwanaaliagiza kupitia Mose kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa ajili ya mifugo yetu.”

3 Hivyo kama vileBwanaalivyoagiza, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka katika urithi wao wenyewe.

4 Kura ya kwanza ikatoka kwa ajili ya Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka katika makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.

5 Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka katika koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase.

6 Wazao wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu kutoka katika koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.

7 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka katika makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

8 Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vileBwanaalivyokuwa ameagiza kupitia kwa Mose.

9 Kutoka katika makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina

10 (miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi za Walawi, kwa sababu fungu la kwanza liliwaangukia):

11 Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.)

12 Lakini mashamba na vijiji vilivyozunguka mji walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.

13 Kwa hiyo wazao wa kuhani Aroni wakapewa Hebroni (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna,

14 Yatiri, Eshtemoa,

15 Holoni, Debiri,

16 Aini, Yuta na Beth-Shemeshi; kwa jumla ilikuwa miji tisa pamoja na sehemu zake za malisho kutoka kwa makabila haya mawili.

17 Kutoka katika kabila la Benyamini wakawapa Gibeoni, Geba,

18 Anathothi na Almoni; miji yote minne pamoja na sehemu zake za malisho.

19 Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Aroni, ilikuwa jumla kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

20 Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu:

21 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri,

22 Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho; yote ilikuwa miji minne.

23 Pia kutoka kabila la Dani wakapokea Elteke, Gibethoni,

24 Aiyaloni na Gath-Rimoni; yote miji minne pamoja na sehemu zake za malisho.

25 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, wakapokea Taanaki na Gath-Rimoni; yote miji miwili pamoja na sehemu zake za malisho.

26 Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki.

27 Koo za Walawi za Wagerishoni walipewa:

kutoka katika nusu ya Manase,

Golani katika Bashani (mji wa makimbilio kwa ye yote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;

28 kutoka katika kabila la Isakari walipewa,

Kishioni, Daberathi,

29 Yermuthi na En-Ganimu, yote miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

30 kutoka kabila la Asheri walipewa,

Mishali, Abdoni,

31 Helkathi na Rehobu, yote miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

32 Kutoka katika kabila la Naftali walipewa,

Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, yote miji mitano pamoja na sehemu zake za malisho.

33 Jumla yote ya miji ya koo za Wagerishoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

34 Koo za Wamerari (waliobaki wa Walawi) walipewa:

kutoka katika kabila la Zabuloni,

Yokneamu, Karta,

35 Dimna na Nahalali, miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

36 kutoka katika kabila la Reubeni walipewa,

Bezeri, Yahazi,

37 Kedemothi na Mefaathi, miji minne pamoja na sehemu zake za malisho;

38 kutoka katika kabila la Gadi walipewa,

Ramoth katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya ye yote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu,

39 Heshboni na Yazeri, miji minne pamoja na sehemu zake za malisho.

40 Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, ambao walikuwa mabaki ya Walawi, jumla ni kumi na miwili.

41 Miji yote ya Walawi katika nchi iliyoshikwa na Waisraeli ilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho.

42 Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na sehemu ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote.

43 Kwa hiyoBwanaakawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo.

44 Bwanaakawapa raha kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao,Bwanaakawatia adui zao wote mikononi mwao.

45 Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri zaBwanakwa ajili ya nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/21-3289d313f3c32f8264ff0432930a553c.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 4 =