Mwanzo 32

Yakobo Ajiandaa Kukutana Na Esau 1 Yakobo pia akaondoka akaenda zake, malaika wa Mungu wakakutana naye. 2 Yakobo alipowaona, akasema, “Hii ni kambi ya Mungu!” Kwa hiyo akapaita mahali pale Mahanaimu. 3 Yakobo akatuma wajumbe kumtangulia kwa Esau ndugu yake huko Seiri, katika nchi ya Edomu. 4 Akawaagiza akisema: “Hili ndilo mtakalomwambia bwana wangu Esau: […]

Mwanzo 33

Yakobo Akutana Na Esau 1 Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike. 2 Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma. 3 Yeye mwenyewe akatangulia mbele […]

Mwanzo 34

Dina Na Washekemu 1 Basi Dina, binti wa Yakobo aliyezaliwa na Lea, akatoka nje kuwatembelea wanawake wa nchi ile. 2 Ikawa Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mtawala wa eneo lile alipomwona, akamchukua na kumnajisi. 3 Moyo wake ukavutwa sana kwa Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana na akazungumza naye kwa kumbembeleza. 4 Shekemu akamwambia baba […]

Mwanzo 35

Yakobo Arudi Betheli 1 Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.” 2 Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. 3 Kisha njoni, twende […]

Mwanzo 36

Wazao Wa Esau 1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu). 2 Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi, 3 pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi. 4 Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli, 5 […]

Mwanzo 37

Ndoto Za Yosefu 1 Yakobo akaishi Kanaani katika nchi ambayo baba yake alikuwa ameishi. 2 Zifuatazo ni habari za Yakobo. Yosefu, kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akichunga makundi ya kondoo na mbuzi pamoja na ndugu zake wa mama wengine, yaani wana wa Bilha na wana wa Zilpa wake za baba yake, naye akawa […]

Mwanzo 38

Yuda Na Tamari 1 Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake akaenda kuishi na Hira Mwadulami. 2 Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua akamwoa na akakutana naye kimwili, 3 akapata mimba akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri. 4 Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani. 5 Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu […]

Mwanzo 39

Yosefu Na Mke Wa Potifa 1 Wakati huu Yosefu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yosefu kutoka kwa Waishimaeli waliomleta Misri. 2 Bwanaalikuwa pamoja na Yosefu, naye akastawi, Yosefu akaishi nyumbani kwa bwana wake Mmisri. 3 Potifa alipoona kuwaBwanaalikuwa pamoja na Yosefu na kwambaBwanaalimfanikisha […]

Mwanzo 40

Mnyweshaji Na Mwokaji 1 Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. 2 Farao akawakasirikia hawa maafisa wake wawili, mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, 3 akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa kikosi cha ulinzi katika gereza lile lile alimofungwa Yosefu. 4 Mkuu wa kikosi […]

Mwanzo 41

Ndoto Za Farao 1 Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Nile, 2 wakati ng’ombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye manyasi. 3 Baada yao ng’ombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Nile wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. 4 Wale ng’ombe […]