Yoshua 6

Yeriko Yatekwa Na Kuangamizwa

1 Basi malango ya Yeriko yalifungwa kwa uthabiti kwa ajili ya Waisraeli. Hakuna mtu ye yote aliyetoka au kuingia.

2 KishaBwanaakamwambia Yoshua, “Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita.

3 Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita.

4 Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya Sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo.

5 Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.”

6 Ndipo Yoshua mwana wa Nuni akaita makuhani na kuwaambia, “Chukueni Sanduku la Agano laBwanana makuhani saba wachukue baragumu za pembe za kondoo waume mbele yake.”

7 Naye akawaagiza watu, “Songeni mbele! Mkazunguke mji, na walinzi wenye silaha watangulie mbele ya Sanduku laBwana.”

8 Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba wenye kuzibeba zile baragumu saba mbele zaBwana, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano laBwanalikawafuata.

9 Walinzi waliokuwa na silaha wakaenda mbele ya hao makuhani waliopiga hizo baragumu na hao walinzi wa nyuma waliokuwa nyuma wakafuata Sanduku. Wakati wote huu baragumu zilikuwa zikipigwa.

10 Bali Yoshua aliwaagiza watu, “Msipige kelele za vita, msipaze sauti zenu, wala kusema neno lo lote mpaka siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!”

11 Basi akalipeleka Sanduku laBwanakuzunguka huo mji, likazungushwa mara moja. Kisha watu wakarudi kambini kulala.

12 Yoshua akaamka mapema asubuhi iliyofuata na makuhani wakalichukua Sanduku laBwana.

13 Makuhani saba wakachukua zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku laBwanawakizipiga hizo baragumu. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao, walinzi waliokuwa nyuma wakalifuata Sanduku laBwana, huku makuhani wakiendelea kuzipiga hizo baragumu.

14 Siku ya pili wakazunguka mji mara moja na kurudi kambini. Wakafanya hivi kwa siku sita.

15 Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakazunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba.

16 Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipopiga baragumu kwa sauti kubwa, Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maanaBwanaamewapa mji huu!

17 Mji huu pamoja na vyote vilivyomo ndani yake utawekwa wakfu kwaBwanakwa kuangamizwa kabisa. Ila Rahabu tu, yaani yule kahaba na wote ambao wako pamoja naye nyumbani mwake ndio watakaosalimishwa, kwa sababu aliwaficha wale wapelelezi tuliowatuma.

18 Lakini mjiepushe na vitu vilivyowekwa wakfu, msije mkachukua cho chote katika hivyo, msije mkajiletea maangamizi katika maskani ya Israeli na kuiletea taabu.

19 Fedha yote na dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwaBwana, lazima viletwe katika hazina.”

20 Wakati baragumu zilipopigwa, watu walipiga kelele, kwa sauti ya baragumu, na watu kupaza sauti, ukuta ukaanguka; hivyo kila mtu akasonga mbele moja kwa moja kutokea pale alipokuwa kutokea kila upande na kuuteka mji.

21 Wakauweka mji wakfu kwaBwana, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, ng’ombe, kondoo na punda.

22 Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani kwa yule kahaba, mleteni pamoja na wote waliomo nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.”

23 Basi wale watu waliofanya upelelezi wakaenda kumleta Rahabu, baba yake na mama yake, ndugu zake na watu wote waliokuwa pamoja naye nyumbani mwake. Akaleta jamaa yake yote na kuwaweka mahali nje karibu na kambi ya Israeli.

24 Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwamo ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba yaBwana.

25 Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu yule kahaba, jamaa yake yote na wote waliokuwa wa kwake, kwa sababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko, naye anaishi miongoni mwa Waisraeli hata leo.

26 Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Alaaniwe mbele zaBwanamtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko:

“Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume

ataweka misingi yake;

kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho

ataweka malango yake.”

27 HivyoBwanaalikuwa pamoja na Yoshua, na sifa zake zikaenea katika nchi ile yote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOS/6-e652221fd4f29c8ada4b50863aaabe53.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 − five =