Wafalme Wa Kaskazini Washindwa 1 Ikawa Yabini mfalme wa Hazori aliposikia habari za mambo haya, akatuma ujumbe kwa Yobabu mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu, 2 na pia kwa wafalme wa upande wa kaskazini wale waliokuwa milimani, katika Araba upande wa kusini mwa Kinerethi, nchi chini ya vilima […]
Category Archives: Yoshua
Yoshua 12
Orodha Ya Wafalme Walioshindwa 1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli walikuwa wamewashinda na kutawala nchi yao upande wa mashariki ya Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba: 2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa […]
Yoshua 13
Sehemu Za Kanaani Ambazo Hazijatwaliwa 1 Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana,Bwanaakamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa. 2 “Haya ndiyo maeneo ambayo bado hayajatekwa: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: 3 Eneo hili linaanzia Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea […]
Yoshua 14
Mgawanyo Wa Nchi Magharibi Mwa Yordani 1 Basi haya ndiyo maeneo Waisraeli waliyopokea kama urithi katika nchi ya Kanaani, ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliwagawia. 2 Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kamaBwanaalivyomwagiza Mose. 3 Mose alikuwa amewapa yale makabila […]
Yoshua 15
Mgawo Kwa Yuda 1 Mgawo kwa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo, ulishuka kufikia nchi ya Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini. 2 Mpaka wao wa kusini ulianzia kwenye ghuba iliyoko kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi, 3 ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini ukaenda hadi kusini mwa […]
Yoshua 16
Mgawo Kwa Ajili Ya Efraimu Na Manase 1 Mgawanyo wa Yosefu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli. 2 Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia nchi ya Waariki huko Atarothi, 3 ukatelemkia kuelekea magharibi hadi nchi ya Wayafleti […]
Yoshua 17
Mgawo Wa Nusu Nyingine Ya Manase Upande Wa Magharibi 1 Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu. 2 Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa […]
Yoshua 18
Mgawanyo Wa Nchi Iliyobaki 1 Kusanyiko lote la Waisraeli likakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema ya Mkutano. Nchi ikawa chini ya utawala wao, 2 lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao. 3 Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayoBwana, Mungu wa baba zenu, amewapa? […]
Yoshua 19
Mgawo Kwa Simeoni 1 Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya nchi ya Yuda. 2 Ulijumuisha: Beer-Sheba (au Sheba), Molada, 3 Hasar-Shuali, Bala na Esemu, 4 Eltoladi, Bethuli, Horma, 5 Siklagi, Beth-Markabothi, Hazar-Susa, 6 Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. […]
Yoshua 20
Miji Ya Makimbilio 1 NdipoBwanaakamwambia Yoshua, 2 “Waambie Waisraeli, watenge miji ya kukimbilia, kama nilivyokuamuru kupitia Mose, 3 ili mtu ye yote atakayemwua mtu kwa bahati mbaya na pasipokukusudia aweze kukimbilia huko na kujiepusha na mlipiza kisasi cha damu. 4 “Anapokimbilia mojawapo ya miji hii, atasimama kwenye maingilio ya lango la mji na kueleza wazee […]