1 Mambo ya Nyakati 11

Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Israeli

1 Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako.

2 Wakati wote uliopita, hata wakati Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, nayeBwanaMungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”

3 Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele zaBwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa naBwanaalivyoahidi kupitia kwa Samweli.

Daudi Ashinda Yerusalemu

4 Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi, ambao ndio waliokuwa wanaishi humo

5 wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

6 Daudi alikuwa amesema, “Ye yote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya, akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.

7 Daudi akafanya maskani yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi.

8 Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu.

9 Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababuBwanaMwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.

Mashujaa Wa Daudi

10 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote, wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kamaBwanaalivyoahidi.

11 Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi:

Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.

12 Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu.

13 Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walipokusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti.

14 Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. NayeBwanaakawapa ushindi mkubwa.

15 Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikosi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi kwenye Bonde la Warefai.

16 Wakati ule Daudi alikuwa katika ngome na askari walinzi wa Wafilisti walikuwa katika mji wa Bethlehemu.

17 Daudi alitamani maji akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!”

18 Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwenye hicho kisima kilichoko nje ya lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala ya kuyanywa akayamimina mbele zaBwana.

19 Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa.

Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

20 Abishai, nduguye Yoabu alikuwa mkuu wa wale Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, hivyo akawa maarufu kama wale Watatu.

21 Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

22 Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli, aliyefanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua watu wawili mashujaa wa Moabu. Pia aliingia shimoni siku ya theluji na kumwua simba.

23 Alimwua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyang’anya Mmisri mkuki wake na kumwua nao.

24 Mambo kama hayo ya ujasiri ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, yeye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.

25 Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa kundi la walinzi wake.

26 Wale watu mashujaa walikuwa:

Asaheli nduguye Yoabu,

Ehanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,

27 Shamothi, Mharori,

Helesi, Mpeloni,

28 Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa,

Abiezeri kutoka Anathothi,

29 Sibekai, Mhushathi,

Ilai, Mwahohi,

30 Maharai, Mnetofathi,

Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,

31 Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini,

Benaya, Mpirathoni,

32 Hurai kutoka mabonde ya Gaashi,

Abieli, Mwairibathi,

33 Azmawethi, Mbaharumi,

Eliyahba, Mshaalboni,

34 wana wa Hashemu, Mgiloni,

Yonathani mwana wa Shagee, Mharari,

35 Ahiamu mwana wa Sakari, Mharari,

Elifale mwana wa Uri,

36 Heferi, Mmekerathi,

Ahia, Mpeloni,

37 Hezro, Mkarmeli,

Naarai mwana wa Ezbai.

38 Yoeli nduguye Nathani,

Mibhari mwana wa Hagri,

39 Seleki, Mwamoni,

Naharai, Mbeorothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,

40 Ira, Muithiri,

Garebu, Muithiri,

41 Uria, Mhiti,

Zabadi mwana wa Ahlai,

42 Adina mwana wa Shiza, Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini,

43 Hanani mwana wa Maaka,

Yoshafati, Mmithni,

44 Uzia, Mwashterathi,

Shama na Yeieli wana wa Hothamu, Mwaroeri,

45 Yediaeli mwana wa Shimri,

nduguye Yoha, Mtizi,

46 Elieli, Mmahawi,

Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu,

Ithma, Mmoabi,

47 Elieli, na Obedi na Yaasieli, Mmesobai.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/11-3761b931983b4e0a41b3d8fda616b2cd.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − 4 =