1 Mambo ya Nyakati 16

Sanduku Lawekwa Ndani Ya Hema

1 Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili hiyo, wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.

2 Baada ya Daudi kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina laBwana.

3 Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, maandazi ya tende na maandazi ya zabibu kavu.

4 Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku laBwanakufanya maombi, kumshukuru na kumsifuBwana, Mungu wa Israeli:

5 Asafu ndiye aliyekuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliyabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio ambao wangepiga zeze na vinubi, Asafu angelipiga matoazi,

6 nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio ambao wangelipiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.

Zaburi Ya Daudi Ya Shukrani

7 Siku ile kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwaBwana:

8 MshukuruniBwana, liitieni jina lake,

wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

9 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,

waambieni matendo yake yote ya ajabu.

10 Utukufu kwa jina lake takatifu,

mioyo ya wale wamtafutaoBwanana ifurahi.

11 MtafuteniBwanana nguvu zake,

utafuteni uso wake siku zote.

12 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,

miujiza yake na hukumu alizozitamka.

13 Ee wazao wa Israeli mtumishi wake,

Ee wana wa Yakobo, wateule wake.

14 Yeye ndiyeBwanaMungu wetu,

hukumu zake zimo duniani pote.

15 Hulikumbuka Agano lake milele,

neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,

16 Agano alilolifanya na Abrahamu,

kiapo alichomwapia Isaki.

17 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,

kwa Israeli kuwa Agano la milele:

18 “Wewe nitakupa nchi ya Kanaani

kuwa sehemu utakayoirithi.”

19 Walipokuwa wachache kwa idadi,

wachache sana na wageni ndani yake,

20 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,

kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.

21 Hakuruhusu mtu ye yote awaonee,

kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema,

22 “Msiwaguse masiyawangu,

msiwadhuru manabii wangu.”

23 MwimbieniBwanadunia yote;

tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

24 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

25 Kwa kuwaBwanani mkuu,

mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote,

yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

26 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,

lakiniBwanaaliziumba mbingu.

27 Fahari na enzi viko mbele yake,

nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

28 MpeniBwana, enyi jamaa za mataifa,

mpeniBwanautukufu na nguvu,

29 mpeniBwanautukufu

unaostahili jina lake.

Leteni sadaka na mje katika nyua zake;

mwabuduniBwanakatika uzuri

wa utakatifu wake,

30 Dunia yote na itetemeke mbele zake.

Ulimwengu ameuweka imara;

hauwezi kusogezwa.

31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;

katikati ya mataifa semeni,

“Bwanaanatawala.”

32 Bahari na ivume na vyote vilivyomo ndani yake;

mashamba na yashangilie,

na vyote vilivyomo ndani yake.

33 Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha,

itaimba mbele zaBwana

kwa maana anakuja kuihukumu dunia.

34 MshukuruniBwanakwa kuwa ni Mwema,

upendo wake wadumu milele.

35 Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe;

utukusanye tena kutoka katika mataifa,

ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,

na kujisifu katika sifa zako.”

36 AtukuzweBwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Nao watu wote wakasema, “Amen,” na, “MsifuniBwana.”

37 Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano laBwanaili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku.

38 Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.

39 Daudi akamwacha Sadoki, kuhani, pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada yaBwanakatika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni

40 ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwaBwanakwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria yaBwanaambayo alikuwa amempa Israeli.

41 Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpaBwanashukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”

42 Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.

43 Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/16-157fff63e48fccd5acea57599db47d28.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

9 − one =